Mkanganyiko wa kuteua viongozi watakaosimamia dira ya taifa

Mkanganyiko wa kuteua viongozi watakaosimamia dira ya taifa

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Uongozi naouzungumzia hapa ni ule wa ngazi ya taifa katika kuwapeleka watu kwenye makusudio yao ama malengo yao. kiuchumi,kijamii,afya na nyanja zote za maendeleo.

Binafsi nimekuwa nikiona kuwepo kwa mkanganyiko katika kuteua viongozi, hii ni kutokana na watu kukosa elimu ya namna yakuteua watu sahihi katika nafasi sahihi!.
Bila kurukaruka uongozi ni kipaji na sio kila kiongozi anaweza kuongoza kila sehemu!, kuna mtu anaweza kuongoza mfumo ambao umeshaundwa na kuna mtu anaweza kuongoza kuunda mfumo!.

Nimechunguza nimegundua watu wengi katika kuteua viongozi haswa wakisiasa hufuata hisia!, aidha kwasababu wanatoka chama kimoja,rika,kabila,kanda,undugu n.k lakini nadhiria nzima yakuteua kiongozi sahihi huwa haingalii hilo kwani kiongozi sahihi anatakiwa ajue anachokiongoza,maarifa yakuongoza,nia yakuongoza, ajue kutofautisha hisia na akili na wapi avitumie vyote hivyo!, dira ya anaowaongoza na atawaongoza vipi kufikia hio dira.

Kiongozi akiweza kupatikana na akiwa na sifa hizo bila shaka hakutakuwa na doa ama dosari la uchaguzi wenu!.

Imekuwepo imani ya watu kuamini kuwa watu waliofanikiwa kiuchumi basi wanaweza kuwaongoza pia kitaifa katika kufikia malengo yao!, kwenye hilo naweka big "NO".
Watu waliofanikiwa kiuchumi mara nyingi atafanya awezalo kuhakikisha anakuwa kiuchumi pasipo kuangalia anamkanyaga nani!. Hawa watu nguvu yao kubwa huangazia katika kujitangaza,kumiliki nakutengeneza jina. Mambo yakuangalia atainufaishaje nchi,mkoa au kata sio kariba yao. Hawa zaidi wanafaa kuongoza katika ngazi za kiuchumi tu na si siasa!.

Moja kati ya kosa ambalo tumelifanya nchi yetu ni kushindwa kuwa na watu wazuri wanaoweza kufanya uchaguzi mzuri wa viongozi!, huku tukijificha kwenye kichaka cha demokrasia ambacho nacho tunakikanyaga!.. Nchi tumeiacha kwa wafanyabiashara wakiwa nyuma ya migongo ya wanasiasa ambao hawana nguvu kimaamuzi!.

Kuna maamuzi yanafanyika kuwanufaisha wao haijalishi hali ya wengi ipo katika namna gani!, hata pale kunapohitajika maamuzi ya hekima na hali basi yanafanyika maamuzi yakinamba kwa upande wao!.

Hivi viumbe ni visumbufu pale masirahi yao yakishikwa na wanaweza kufanya chochote mfano katika awamu ya tano waliisumbua serikali katika swala zima la sukari.
Ilifikia hatua walificha hadi fedha mpaka serikali kutishia kuunda fedha mpya!.

Unaweza kuona labda naikandia nchi yangu tu lakini jaribu kuangalia hata nchi ya marekani baada ya trump kuwekwa madarakani, mfanyabiashara huyu amekuwa akiisumbua dunia kiuchumi kiasi kwamba hata nchi yake imeanza kupata madhira!.

Pasipo kumuangalia mtu yoyote machoni uongozi katika ngazi ya kusimamia mambo yote nyeti anayotakiwa kuyapata binadamu, basi uchaguzi hautakiwi kuchezewa katika namna yoyote na uwiano katika madaraka ni lazima uwepo ili kuweka uwiano katika ngazi zote!.

Alie huru kufanya biashara na afanye,siasa na afanye, shughuli za kidini na afanye ila kwa uwiano uliostahiki. Rai yangu kwa raia wenzangu tusipofunguka sisi hatutaweza kuifungua hii nchi bado kutakuwa na matabaka hata kwa zile huduma ambazo ni haki yako kuzipata katika nchi!.

Uongozi ni swala nyeti halipaswi kuletewa mzaha maana linagusa maisha yako na kizazi chako.
 
Well said mkuu, kuna wajinga wanasema eti wenye elimu hawakuwasaidia kwahiyo sasa wanajaribu wasiojitambua waone kama watapata matokeo chanya kama sio ujinga uliokithiri ni nini?
 
Well said mkuu, kuna wajinga wanasema eti wenye elimu hawakuwasaidia kwahiyo sasa wanajaribu wasiojitambua waone kama watapata matokeo chanya kama sio ujinga uliokithiri ni nini?
Huo ni uzumbukuku..
Kwenye njaa, hisia hufuata harufu ya chakula.
Hayo ndio matatizo yanayotakiwa yatatuliwe na hiyo ndio sifa ya kiongozi
 
Back
Top Bottom