Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu,
Fujo zilizoibuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba SC na CS Sfaxien zimeibua mkanganyiko kuhusu uwajibikaji.
Jeshi la Polisi lilibainisha kuwa mashabiki wa CS Sfaxien walihusika moja kwa moja kung’oa viti 256 na kuanzisha vurugu baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa kuongeza dakika saba za nyongeza, zilizoiwezesha Simba SC kupata goli la ushindi.
Hata hivyo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Waziri Prof. Palamagamba Kabudi imeelekeza Simba SC na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kubeba gharama za uharibifu huo.
Hatua hii imeibua maswali kwani haijaeleza wazi uhusiano wa Simba SC na vitendo vya uharibifu vilivyofanywa na mashabiki wa timu pinzani na iweje matamko yapishane?
Pia, Soma:
• Simba yatakiwa kulipa gharama viti kung'olewa kwa Mkapa
• Jeshi la Polisi latoa tamko baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti Uwanja wa Taifa