Mkanganyiko wa matamko (Wizara na Polisi) kuhusu kung’olewa viti na fujo za Uwanja wa Mkapa

Mkanganyiko wa matamko (Wizara na Polisi) kuhusu kung’olewa viti na fujo za Uwanja wa Mkapa

Huu uwanja si uko ktk matengenezo na ulitengewa 31 billion katika bajeti iliyopita,na mpk sasa imekarabatiwa sehemu ya pitch na kukimbilia,jukwaani pamoja na viti vyake bado hakujaguswa....sasa hizo hela zikilipwa zitaenda kununua vipi tena?
Walipe
 
Wakuu,

Fujo zilizoibuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba SC na CS Sfaxien zimeibua mkanganyiko kuhusu uwajibikaji.

Jeshi la Polisi lilibainisha kuwa mashabiki wa CS Sfaxien walihusika moja kwa moja kung’oa viti 256 na kuanzisha vurugu baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa kuongeza dakika saba za nyongeza, zilizoiwezesha Simba SC kupata goli la ushindi.
View attachment 3177861
Hata hivyo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Waziri Prof. Palamagamba Kabudi imeelekeza Simba SC na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kubeba gharama za uharibifu huo.
View attachment 3177862
Hatua hii imeibua maswali kwani haijaeleza wazi uhusiano wa Simba SC na vitendo vya uharibifu vilivyofanywa na mashabiki wa timu pinzani na iweje matamko yapishane?

Pia, Soma:

Simba yatakiwa kulipa gharama viti kung'olewa kwa Mkapa

Jeshi la Polisi latoa tamko baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti Uwanja wa Taifa

Mara nyingi tumekuwa tukisikia na kushuhudia mikutano au mikusanyiko ya vyama vya siasa ikizuiliwa kufanyika kwa kuwepo kwa viashiria vya fujo au uvunjifu wa amani ambao hugunduliwa mapema sana na police (watu wa intelijensia),

Je hili la fujo na kuharibu viti vya uwanja hawakuweza kuliona mapema? Au intelijensia yao iko katika mambo fulani fulani tu.
 
Back
Top Bottom