JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kwa mujibu wa kifungu namba 4 (1) ya Sheria ya Mtoto inaeleza Mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka kumi na nane (18)
Lakini Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 katika kifungu cha 13 kinaruhusu Mtoto wa kike kuozwa akiwa na umri wa miaka 14.
Hivyo Sheria hizi mbili zinakinzana na kusababisha harakati za kulinda ustawi wa Mtoto wa Kike kuzorota
Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa Msichana akiwa na umri wa chini ya miaka 18 anakuwa hajapevuka kiakili au kukomaa sawa sawa via vyake vya uzazi.
Upvote
0