Sasa hao wanaozaa kabla ya kufika miaka 18 hua hawafanyi tendo la ndoa?Unaruhusiwa kumuoa akiwa na miaka 14 ila haurusiwi kufanya naye tendo la ndoa mpaka afikishe miaka 18, kabla ya umri huo ukifanya naye sex utafunguliwa kesi ya ubakaji japo ni mke wako halali wa ndoa
Hiyo sheria ya mtoto ni ya mwaka gani? Ukinzani huo lazima utakuwa unatokana na kukosa umakini kwa waandaa miswada na wapitisha sheria. Pia kutokushirikisha wanachi walio wengi kwenye utungaji wa sera na sheria.
Kwa mujibu wa kifungu namba 4 (1) ya Sheria ya Mtoto inaeleza Mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka kumi na nane (18)
Lakini Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 katika kifungu cha 13 kinaruhusu Mtoto wa kike kuozwa akiwa na umri wa miaka 14.
Hivyo Sheria hizi mbili zinakinzana na kusababisha harakati za kulinda ustawi wa Mtoto wa Kike kuzorota
Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa Msichana akiwa na umri wa chini ya miaka 18 anakuwa hajapevuka kiakili au kukomaa sawa sawa via vyake vya uzazi.
Hapa suala nafikiri ni ubebaji mimba na kujifungua, na sio tendo la ndoa.Sasa hao wanaozaa kabla ya kufika miaka 18 hua hawafanyi tendo la ndoa?
Ni wangapi wapo jela kwa hilo?
Sheria hii ni tata
Mbona haisemi kuhusu wavulana