Mkanganyiko wa Wanandoa Uliopelekea Umauti na Makovu ya Kudumu

Mkanganyiko wa Wanandoa Uliopelekea Umauti na Makovu ya Kudumu

Kindred Spirit

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
457
Reaction score
666
Tukio hili lilitokea China ndani ya hifadhi ya wanyama pori huko Beijing.

Wanandoa na mama mkwe (mama wa mke) walikuwa ndani ya hifadhi mke aliposhuka kuelekea upande wa dereva alikokuwa amekaa mumewe. Inadaiwa alikuwa anasubiri mumewe ahamie kwenye siti ya abiria ili yeye aendeshe. Punde kidogo mke akavamiwa na tiger kama CCTV footage inavyoonesha.

Ilichukua takribani sekunde 11 kwa mume kupisha siti, hata wakati mke anavamiwa jamaa alikuwa bado yuko kwenye kiti cha dereva (check video). Hapo ni ndani ya hifadhi ya wanyama hatari, like seriously?

Jamaa hakuwa na courage ya kumsaidia mkewe, angalia anavyohangaika na gari hadi mama mkwe wake anashuka jamaa bado hajajiongeza kumsaidia mkewe. Mama mkwe aliuawa na 🐅 mwingine aliyekuwa karibu, mke alijeruhiwa vibaya, ila jamaa hakupata hata jeraha.

Wanandoa hawa walijaribu kudai fidia. Mamlaka ya hifadhi ilisema wote walisaini fomu iliyowataka wasitoke nje ya gari wakiwa ndani ya hifadhi. So why jamaa aliruhusu mkewe ashuke kati kati ya hatari?.

Mke anadai alikuwa anajisikia vibaya, alishuka ili ajaribu kutapika. But video haioneshi kama alikuwa katika hali hiyo. Walilipwa kiasi kidogo na mamlaka ya hifadhi kuwasaidia gharama za mazishi na matibabu, kama sehemu ya moral support tu, lakini hawakushinda kesi yao ya madai.

Wanandoa walikiri kusaini fomu lakini wakadai hawakujua kwanini waliambiwa washishuke ndani ya hialfadhi. Yaani walitaka hifadhi iseme usishuke ndani ya hifadhi "ili kuepuka hatari ya kuvamiwa na wanyama". Duh

Inadaiwa mke alitofautiana na mumewe kuhusu namna anavyoendesha gari, akataka ampishe aendeshe yeye. May be why jamaa alikuwa bado anadelay kukubaliana na maamuzi. But mke wako yuko nje eneo hatari hata hujiongezi jamani?

Kati ya wawili waliohusika na shambulio, angalau mmoja aliuliwa na wasimamizi wa hifadhi.

Hapa wote walikuwa na makosa, ila mke ndo atajutia zaidi maisha yake yote kwa kumpoteza mama yake mzazi kwa maamuzi ya kinjinga kama haya.


 
Back
Top Bottom