Mkao huu umenikumbusha mbali;

Mkao huu umenikumbusha mbali;

[h=3]NIMEUKUMBUKA MKAO HUU:- KUKAA PAMOJA FAMILIA NZIMA KWA KUJUMUIKA KULA!![/h]

Picha hii imenikumbusha enzi zile miaka arobaini na saba familia nzima inajumuika pamoja na kushika chakula iwe cha asubuhi, mchana au jioni. Hakika hii ilikuwa safi sana. Ila hapa naona watatu wanatumia vijiko na mmoja anatumia mkono... Halafu unajua kitu kimoja ukishazoea kula chakula mkiwa wengi huwa kinanoga sana kuliko kula peke yako...je wewe nawe umekumbuka nin? IJUMAA

Shurti kwa sinia au beseni, kama na wana ndugu hakuna noma lakini kwenye shughuli mhhhhhh! Niliwahi kwenda kwenye msiba mmoja basi ilipofika wakati wa pilau tukakaa na babu mmoja ambaye sijui alikuwa na njaa kali au uroho tu wa pilau basi udenda ukawa unamchuruzika ndani ya sinia Ewwwwwww yuck! 🙁 nilipoona hivyo tu niliondoa majeshi yangu haraka sana na hamu yote ya kula ikapotea
 
Tulipaka mafuta fulani ya mgando sijui ndio rays????ukipaka mwili wote unabaki na vitu vinameremeta!teh teh teh...........Kupiga picha mpaka uende studio tena za kutafuta!
Yale mafuta yalikuwa yanaitwa ''shanti'' ya orange hivi mkebe wake mrefu yana harufu kaliii
 
Back
Top Bottom