Mkapa alia na serikali mbili (2)

kwa hali ilivyo katika bunge la katiba ningeshauri kama hoja ya serikali tatu itapita watakaounga mkono wakati wa kampeni wapeperushe bendera ya Tanganyika kwa upande wa bara na ya Zanzibar kwa upande wa Unguja na pemba
 
Huyu Mzee Mkapa ni fake! Alikataa mapendekezo ya Tume moja ya mabadiliko ya Katiba (white paper) aliyoiunda na kumfedhehesha sana yule Jaji ambaye alikuwa Mwenyekiti (jina nimelisahau)! Badala yake alikubali kipengere cha ushindi wa Rais kwa kutumia kigezo cha "simple majority"!
 
Hana credibility ya kutoa maoni ya hivi. Ni katika uongozi wake tulishuhudia uzembe mkubwa kwenye kushughulikia kero za muungano. Ni yeye aliyeamuru kuuawa kwa mamia ya Wapemba mwaka 2001. Bora hata aongee Kikwete kuliko huyu dikteta...
Mkuu kama ulikuwa kichwani mwangu, unafiki ndiyo sndiyo unaowasumbua hawa magamba, unataka kuonesha ushirikiano na watu uliyo wasababishia vifo na "ukimbizi"?
 
Kinacho msumbua huyu Mkapa ni ubabe na kudhani yeye ndiyo anaakili kuliko Watanzania wote...muda wake wa kuiongoza nchi hii uliisha kitambo na tuliona madudu aliyo fanya sasa akae kimya na wengine watumie kipindi chao...tatizo la hawa viongozi wetu mafisadi wanaanza kujifanya wazalendo baada ya kuwa wameisha tafuna nchi vya kutosha sasa wanarudi kwa gia ya uzalendo baada ya kugundu watu hawawahitaji tena!
 
Mimi kiukweli nashangaa sana hawa wanaolilia huu muungano na wakati watu wanaitaka nchi yao.pia kwa uwezo wa viongozi wetu hii nchi ni kubwa mno ndo maana hata utendaji unakuwa mgumu.
 
Tunataka tanganyika, ccm acheni kushabikia ushoga wa muungano wa asp na tanu
 
You can bring a dead man to life, iwejeufananishe mtu na nchi ,Tanganyika can exist again.
 
Mods huu uzi mlio weka hapa wa hammy-d sio wangu naomba murudishe uzi wangu nilio andika leo kwenye hiyo heading ya WATANGANYIKA KUPATA TANGANYIKA YAO KUNA DHAMBI WAKATI WAZANZIBAR WANA ZANZIBAR YAO?tafadhali sana mlicho weka hapo ni kama kuhujumu mawazo yangu na kuninyima haki yakujieleza maana sio mara ya kwanza kunifanyia hivyo.naomba nitendewe haki kama kanuni za jf zinavyojieleza ahasante
 
ccm wote ni wale wale wazee wa serikali mbili.jamani si muwaache zanzibar na nchi yao?kuna nini hapo mpaka muwang'ang'anie??? ccm mmetuchosha na mambo yenu hayo
 

Judge Kisanga
 
Tunataka U-Taganyika wetu ujulikane rasmi, na siyo ubaki ndani ya nafsi na kwenye vitabu vya ki-historia, Muungano ulikuwa ni wa nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar), Wa-Tanganyika tukakubali kuukana U-Tanganyika na kujiita wa-Tanzania lakini wenzetu wameungángánia U-zanzibari mpaka hii leo wanajiita wao Wazanzibari kwa miaka 50 ndani ya TANU baadae CCM (Chukua Chako Mapema) lakin haijatunufaisha kwa lolote zaidi ya kutengeneza U-falme (Kurithishana madaraka) ndani ya nchi yetu
 

TATIZO SIYO MKAPA....TATIZO NI UMILIKI WA HOJA HII UNA ORIGIN YA CCM? Kama haina hata awe nani si rahisi kuondoa mfumo uliopo kwa nadharia na dhana za uhuru wa maoni..
 

Kama sikosei ilikuwa tume ya jaji Kisanga mkuu
 

yaelekea wewe hujawajua mods wa JF, in short ndo wako hivyo, mara nyingi watu wamekuwa wakilalamika lkn wapi. Kuna members (majina kapuni) humu wanaabudiwa kupita maelezo
 
Naona tubaki na serikali mbili ila matatizo yaliyopo tukabiliane nayo kwanza. Kama migogoro iliyopo tu hatujaitatua kwanini tutengeneze matatizo mapya? Au tunahisi yatakuwa mepesi mno? Kukimbia migogoro sio njia ya kuyatatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…