Tetesi: Mkapa Anahusika na Sakata la Mchanga

Hayo yote bure kama katiba haitabadilishwa na hii mambo ya kuwa na kinga ya kutoshitakiwa ni bure!
 
Kwani huyo Magufuli hakuwepo serikali ya Mkapa? Hakuwepo kwenye cabinet?
 
Alikuwa anasaka kitumbua
Na kitumbua kakipata mwezi wa ngapi sasa? Kama hili muhimu na kila siku tulikuwa tunapigwa, 2015 kawa rais mwishoni (tunapigwa tu), 2016 nzima yeye rais (tunapigwa tu), 2017 karibu nusu sasa yeye rais (tunapigwa tu) ndo anaamka.

Hili jambo alilijua tangu utawala wa Mkapa. Kuna video kaliongelea.

Na yeye alilipitisha. Kama Waziri.

Kaliachia mwaka mmoja na nusu akiwa rais.

Kwa nini?
 
Waprove hilo.kwamba sisi ndio tunaongoza kuliko.migodi yote duniani kwa kutoa dhahabu..
..wataanzia wapi ni uongo mtupu
 
Benjamin William Mkapa ndiye aliyeuza mali zetu kwa wazungu
 

Watanzania lazima wademand MARAIS wa zamani waliifanya makosa kama haya washitakiwe. Benjamini Mkapa Ali wait a Watanzania marofa kwa kuwa anajuwa hatujui chochote, waogamna kiingereza chake cha kikoloni cha kunyamazisha Watanzania. Aliposhika madaraka akamudharau hata Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere, kwa UCHUNGU na majonzi makubwa akauza banki ya taifa kinyume na matako ya Baba wa taifa kwa jeuri. Mpaka leo tunamuheshimu kwa mabaya na wizi wote huu kweli Watanzania tuko gizani.

Soma familia ya Nyerere inanyomuzania Mkapa.

Google Groupes
 
Rais angekuwa anaitakia mema hii nchi,angeipitisha katiba ya Warioba.
Hawa wakina mkapa ma wezi wengine wangeshughulikiwa vizuri.
 
Kwenye mchanga wa madini Serikali ya CCM inastahili kuwajibika kwa watanzania kwa kuwaingiza wananchi wake kwenye mikataba mibovu iliyoliingza taifa kwenye hasara kubwa. Lazma CCM ibebe lawama hizi kwa kushindwa kuisimamia nchi. Na mikataba minhine yote ya kimataifa iwekwe wazi ili wananchi wajionee nchi yao ilivyotafunwa kwa miaka 50 na ushee.
 

Issue hapo wote wafukuliwe MAKABURI yao haya yeye afukue ya kwake ,kama anataka kuwa msafi aanze kurejsha vyote alivyokwapua,kuanzia zile Bilioni nane,vile vihoteli alivyojengewa kule,aombe radhi watanzania,na yule jamaa yake RC wa Dar naye achukuliwe hatua za kinidhamu,maana panapofuka moshi,moto utakuja.

Bila hivyo hili sakata ni sinema itakayoishia na kufukuza vimende na kuacha mipanya.
 
Alikuwa kalala kimyaa leo ndio anajifanya ameamka.
Halafu Watanzania wanasherehekea maigizo haya hata bilankuhoji mswali ya msingi kabisa.

Kama kweli tumepigwa, Magufuli yukobresponsibke tangu akiwa Waziri.

Na yuko responsibke zaidi kwa kila siku aliyokuwa rais mpaka aliposimamisha.
 
Mrema alikuwepo jana ikulu wakawasiliana na raisi
hizi harakati za mikataba mibovu ya madini alianzisha mrema na tundu lissu miaka ya tisini mwishoni
 

Story hii ni ya majonzi makubwa, kawaida Viongozi wanaopigania haki kwa wote tunawapuuza wanakosa support mpaka wanaishiwa na NGUVU. Tunawashangilia Viongozi wezi, wenye ubinafsi ni kama tumezibwa masikini na tumefunikwa macho. Nakubaliana na wewe Mkapa ni jeuri na mwenye zarau. Zarau alimuuonyesha hata baba wa Taifa Nyerere. Nyerere alifariki akiwa na majonzi makubwa ya vitendo vilivyofanywa na Mkapa. Mkapa ni mmoja wa maadui number 1 ya Watanzania.
 
Naunga mkono hoja makaburi lazima yafukuliwe ili twende sawa. Hii mikataba toka enzi za BWM. Barrick ikiitwa Placerdome enzi hizo. Hawa wakina malima wote viburi wamevipatia wizara ya madini.

Raisi kusikia uchungu na kulalamika haitotisaidia sana lazima wahusika waliotupeleka hapa wawajibishwe. Alihojiwa Kamishna wa Takukuru akasema Jinai haiozi na ufisadi hauozi utakuja siku itashitakiwa tuu.

Yupo askofu wa jimbo la kusini wa Anglicana aliuliza swali la mwisho pale ukumbini Je waliotufikisha hapa huko nyuma watashughulikiwa??
 

Mrema alishangazwa sana na aina ya kinyago walicho mzawadia Benjamin Mkapa...

....Mbona kinyago kizito sana...

Ile ilikuwa taktrima kwa kukubali kuingia nao mkataba ambao walijua watapiga hii nchi kwa muda mrefu
 

Sio chama kibebe lawama, Viongozi waliokuwepo wakati huo. Kuna watu ndani ya CCM hawakukubaliana na mikataba hii ikiwa pamoja na baba wa Taifa Nyerere, lakini Watu kama Mkapa waliposhika madaraka wakaifanya Tanzania kama Mali yao binafsi. Hawakumdikiliza mtu yeyote. Mtanzania mmoja ama kumi wakifanya vibaya haiwezekani kuwalaumu Watanzania wote. Aliyegundua wizi Huu ni Rais ambaye ametoka kwenye chama cha CCM. Huu ni Wakati wa kuungana Watanzania wote bila ya kujali chama. Kwa sauti moja ikiwezekana Watu kama Mkapa tuwaone mahakani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…