Tetesi: Mkapa Anahusika na Sakata la Mchanga

Mkapa na wa awamu ya nne... wale wote waliohusika ketengeneza huo mkataba.
Kinacho fanya hii ishu kuwa ngumu ni mkataba.. kumfukuza wazir haisaidii coz kama mkataba ni ule ule nchi itaendelea kutekeleza according to mkataba.. means hata wazir ajae atakapo pewa kiti, kama mkataba ni ule ule naye hatafanya kitu
 
hayo yatafanyika ccm ikiwa madarakani au?? we unaota njozi ya mchana. sisi wazalendo wa kweli tunamuunga mkono magufuli si kwa sababu tunampenda la. ni kwasababu anarahisisha kifo cha ccm. ili sasa madai yetu ya katiba mpya yapate nguvu mpya
 
Watanzania tunamjua Mh. Mkapa kwa 100%. Tuna mwachia MUNGU na Mkombozi wetu Mh. Magufuli. Roho inauma sana.

Huu ndiyo ujinga tuliyonayo , kila kitu tumuachia Mungu, Kwanini tunampa kazi MUNGU Wakati mambo mengine tunaweza kuyashughulikia sisi wenyewe? Ujinga GANI Huu wa kumwachia Mungu kila kitu, Wakati MUNGU ametupa kila kitu cha kujitetea kwa watu waonevu na wenye ubinafsi kama Mkapa? Huu ni Uwoga ama kukosa akili? Watanzania wote tuungane pamoja bila ya kujali chama tupambane na hawa mabepari wa kiafrika wanaojiita ati Viongozi wetu.
 
Mrema alishangazwa sana na aina ya kinyago walicho mzawadia Benjamin Mkapa...

....Mbona kinyago kizito sana...

Ile ilikuwa taktrima kwa kukubali kuingia nao mkataba ambao walijua watapiga hii nchi kwa muda mrefu
Samahani unatuumiza sana, bado tuna machungu sana. Kwa TZ maneno matupu hayavunji mfupa. Ila kwa Magufuli yanawezekana.
 
hayo yatafanyika ccm ikiwa madarakani au?? we unaota njozi ya mchana. sisi wazalendo wa kweli tunamuunga mkono magufuli si kwa sababu tunampenda la. ni kwasababu anarahisisha kifo cha ccm. ili sasa madai yetu ya katiba mpya yapate nguvu mpya
Jamani, tusizungumze kuhusu siasa, tujikite kwenye hatma ya Taifa.
 
Sasa haya yote mbona kama yanasemwa na Raia tu huku wenye mamlaka wamekaa kimya
au hawaoni na kusikia yowe la wananchi,,....??
 
Samahani unatuumiza sana, bado tuna machungu sana. Kwa TZ maneno matupu hayavunji mfupa. Ila kwa Magufuli yanawezekana.
Hata mimi sifurahii, Nchi his watt wamekuwa illiterate kwa muda mrefu...Rais ana kinga ya kuto shtakiwa....

Kwa hiyo hii kelee ya Mkapa na Kikwete itaishia hewani...
 
Nakuunga mkono Mkuu.
 
ccm wote wanahusika huwezi kuchambua mmoja mmoja, na mkuu aliahidi kuwalinda ila anaumiza wengine sasa.. angebadili mawazo ataifishe mali za wote waliomtangulia kufidia hii hasara.
 
Sasa hapo si ataanza kufukua MAKABURI ambayo aliishajiapiza kuwa hawezi kufanya hiyo project kwa sababu atashindwa kuyafukia? Hapa ndipo huwa naipendea Bongo - tuna vituko, mihemko, pupa, ukariri wa ngonjera, vichwa vya samaki kama rais mstaafu wa Znz, Karume, alivyowahi kusema, kulazimisha kiki, nk, kwa kifupi katika komedi za kisisa tusipimwe.
 
Hata mimi sifurahii, Nchi his watt wamekuwa illiterate kwa muda mrefu...Rais ana kinga ya kuto shtakiwa....

Kwa hiyo hii kelee ya Mkapa na Kikwete itaishia hewani...
Muhimu sio kuwahukumu, bali sisi kujikwamua na pia kuwa na viongozi wazalendo kwa muda wote.
 
Mbona hata rais wa sasa alishiriki kubariki mikataba hii kama sehemu ya serikali zilizopita?

Mbona rais wa sasa kaachia hizi habari ziendelee kwa mwaka mmoja na nusu tangu awe rais?
 
Hapa KATIBA YETU iwe reviewed tu ili rais akitoka madarakani ashitakiwe kabisa. Binafsi marais waliopita ndo wametufika hapa tulipo
 
Hata mimi sifurahii, Nchi his watt wamekuwa illiterate kwa muda mrefu...Rais ana kinga ya kuto shtakiwa....

Kwa hiyo hii kelee ya Mkapa na Kikwete itaishia hewani...
KAMA LENGO NI KUFUKUA MAKABURI, WAFUATAO WAFANYIWE UCHUNGUZI NA KUCHUKULIWA HATUA KUHUSU SAGA HILI LA KUIBIWA MADINI:

MARAIS - BENJAMIN MKAPA NA JAKAYA MRISHO KIKWETE

MAWAZIRI - JAKAYA MRISHO KIKWETE, IBRAHIM MSABAHA, MAOKOLA MAJOGO, DANIEL YONA, KARAMAGI, SIMBACHAWENE NA MUHONGO

KATIBU MKUU - PATRICK RUTABANZIBWA, MAREHEMU MWAKAPUGI, JAIRO, MASWI, CHAMBO NA NTALIKWA.

MAKAMISHNA - MWAKALUKWA, NYELO, KAFUMU, MASANJA, NA SAMAJE.

WANASHERIA - SALOME MAKANGE NA MEDARD KALEMANI.

NIONAVYO MIMI UCHUNGUZI HUO NA MATOKEO YAKE YATAKWAMISHA KABISA SAFARI YETU YA KUPATA MAPATO TUNAYOYALENGA. NI KAZI NGUMU SANA KUWAPATA HAO KWA KUWA SHERIA NA MIKATABA ILIYOPO INAWALINDA KISHERIA. SULUHISHO - JPM AANZIE HAPA KWA KUWEKA MFUMO MZURI WA KUDHIBITI MAPATO YA SERIKALI ILI TUONE MATOKEO YAKE. UNAWEZA KUKOMAA KUSHUGHULIKIA WATU KAMA WEZI KUMBE BAADHI YAO WALITIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO. UKAWEKA WATU NA MFUMO WAKO NA MATOKEO YAKE MAPATO YAKASHUKA KULIKO HATA YA WALE UNAOWAITA WEZI. TAHADHALI NI MUHIMU. ALWAYS MAAMUZI SAHIHI NI KUTOANGALIA ULIPOANGUKIA, BALI KUSIMAMA NA KUSONGA MBELE. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kuna kahuzuni kana nijia kuwa baba wa taifa asingeweza kuishi ndani ya hili lindi la wezi wenye tamaa na mali ambazo hawatazikwa nazo!!
Unakufa unaacha ma billions yakazi gani kwa faida gani huku watoto wadogo wakiangamia kwa kukosa madawa huku hayo ma billions uliyo yaweka kwenye bank za wezi wa magharibi yaki baki huko na kupotelea hko!!!
 
Kwa katiba uliyonayo Rais mstaafu utamtiaje hatiani? Acheni porojo, lilieni rasimu ya Warioba irudishwe, hili ndiyo suluhisho.
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…