Ufanisi wa kiutendaji wa Mkapa hakuna anayeweza kuutiliashaka, kwa kiasi kikubwa ni Rais ambaye naweza kusema ni mzuri kuliko wote ambao Tanzania iliwahi kuwapata, (this is debatable). Alikoitoa nchi na alipoifikisha wakati anaondoka anapaswa kushukuruwa sana. Hata jumuiya ya kimataifa (ndani na nje ya Afrika na kwa watanzania wenye akili) wanatambua wazi kuwa Ben alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wapya wa Afrika wenye kuletea matumaini. Aliweza kudhibiti mfumuko wa bei, aliweza kutoa leadership ambayo sasa haipo tena, alijaribu kuleta heshima kwenye Ikulu ya Tanzania ambayo iliezuliwa na Mwinyi, na kuondoa uswahiliswahili serikalini, at least Tanzania ikaonekana tena kuwa ni nchi, na sio kama genge la wajinga.
Lakini baada ya kusema haya inabidi tukubali ukweli kuwa yeye kama kiongozi mkuu wa nchi, alikalia kimya mambo mengi ambayo ninahakika yeye mwenyewe aliyajua kuwa ni uhalifu na wizi, ambayo ni kinyume na maadili ya Chama chake na conscience yake binafsi, na kinyume na kiapo alichotoa wakati anachukua urais mara mbili, kinyume na dini yake, na kinyume na aliyosema kuwa napaginaia, na baya zaidi alitumia vibaya cheo chake kujinufaisha (sio kuiba japo sina hakika). Haya yote na mengine mengi ambayo siwezi kuyasema na mengine ambayo siyafahamu yanamfanya asiwe kwenye kundi la watu waadilifu, he is equally liable kama mafisadi wengine.
NI kweli mimi ni-admirer wa Ben and i will keep on being so, lakini mazuri aliyotufanyia hayawezi kumfanya awe immune kwa ujinga aliousimamia, ambao angeweza kuusimamisha alipokuwa na uwezo kama Rais wa nchi na mwenyekiti wa Chama. Ni sawa na kusema mtu anakaa pembeni anaangalia jambazi linaua na anaweza kabisa kulishimamisha, halafu anasema mimi sikuhusika na uuaji huo, that is madness. Unless there is something we do not know! Ben is in for it and he must speak out, kwanini ametufanya hivyo.
The guy is more smart than many in the administration now, kwa hiyo kauli yake inaweza kuwa na mawili, kwanza inawezekana kabisa akisema tu watu wakakaa kimya na kuacha kupiga domo anajua sana kujenga hoja na kuzitetea hata kama ni za uongo, au anaweza kumwaga sumu ambayo ita-i palaralyze kabisa CCM na serikali. Inategemeana tumejiandaa kwa lipi!