Choveki, Tuambie ilikuwa lini hiyo?.
Kama nilivyosema miaka ya TANU/CCM yaani late 70's hadi mwanzoni mwa 80's.
Katika miiko ya TANU ilikuwa ni marufuku kwa kiongozi wa serikali kuwa pia mfanyabiashara. Walikuwa wanaweza kuwa wakulima lakini sio wafanyabiashara.
Sasa ukiwa mkulima hivyo vitu utapeleka wapi kama siyo kuviuza. Na kama nilivyosema hawa walikuwa wafugaji/wakulima. Na nimeeleza hivyo baada ya wachangiaji kusema ati wakati wa JKN viongozi walikuwa hawaruhusiwi kufuga hata kuku (si ndiyo ukulima huo??)
Of course hiyo haina maana kama baba ni kiongozi basi mama naye alizuiwa kabisa kufanya biashara yoyote. Ulikuwa unaweza kufanya lakini pia jua ilikuwa lazima usalama wa taifa na watu wengine wa maadili wakupitie mara nyingi kujua umepataje hizo mali.
Kama nilivyosema awali, katika familia mojawapo baba na mama wote walikuwa kwenye system!, Baba General Manager wa SU na mama Mkuu wa mkoa/ wilaya (sikumbuki vizuri)-
Ila tetesi ni kuwa baba (mume) alikuwa mwanafunzi wa JKN kule tabora- hivyo alikuwa anagateway na vitu vingi tu, na ndo maana waote walipewa post)
Hilo liliwafanya wengi waliokuwa na pesa za ziada kutokuziweka kwenye asset yoyote kwa kuogopa kuulizwa kazipataje
Nakubaliana nawe, hususan wale waliokuwa na pesa za wizi au dhuluma. Ila wapo wale wachache ambao for some reason pia waliweza ku-gate away withit, na wale walioukuwa na bahati ya kuwa recyled eg: fuatilia mifano ya GAPEX, Kampuni za ushirika za mikoa/wilaya, Tanzania Elimu Supplies, Mawasilaino ya anga nk.
Mimi ni mpenzi na muumini wa mwalimu lakini pia naelewa hayo mambo yalikuwa yanatokea. Nikiangalia ufisadi wa sasa, wala simlaumu mwalimu kwa hilo
Hilo hata mimi nimeliona, na mwalimu yeye siyo wa kulamiwa, ila ninachotaka kusema ni kuwa hata enzi zake kulikuwa na makosa na kuna victims pia wa makosa yake
Labda alichokosea Mwalimu ni kutokuwatengenezea pension viongozi wa siasa sawa na wafanyakazi wengine wa serikali
Kwanini viongozi wa siasa tu, mimi nasema pensheni ni kwa kila mtz anayefikisha miaka fulani, mfano 65, siyo chosen few!
Tatizo lingine la TZ ni hii pride ambayo wasomi wanakuwa nayo hata pale ambapo hawana kitu. Naamini watu kama akina Mgonja au huyu Mwafongo kuna kazi nyingi sana wanaweza kufanya hata kwasasa, ni kuamua kujishusha na kukubali kazi zilizopo ambazo wana uwezo nazo.
Ndiyo maana baadhi yetu tumehoji jinsi ambavyo Ben Mkapa anavyolaumiwa ati hajamsaidia huyu bwana!, Au kwanini mbunge wake hamsaidii, Je mimi mzee wangu kijijini amkimbilie nani? Wengi wamesema huyu anaweza kufundisha shule nying tu je kwanini hafanyi hivyo?
Hata sasa bado serikali inaweza kutenga japo pesa chache kuwasaidia hawa ndugu zetu ambao walifanya kazi kwa uaminifu wote na sasa wanahangaika.
Pesa zitengwe kwa watanzania wote watakapoozeeka, kwani mimi bado naamini asilimia 99 ya waTz ni waaminifu, na ni wengi uzeeni wanahangaika.
Tukishindwa kuwasaidia na badala yake kuwacheka, itakuwa ngumu sana kumshawishi mtu awe mwadilifu, watu wataona afadhali wawe mafisadi lakini wajihakikishie maisha bora uzeeni
Kucheka mzee yeyote ni utovu mkubwa wa nidhamu na ukosefu wa maadili, ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa taifa la kesho wanakuwa na maadili tunayoweza kuringia.
Hapa JF tuna watu wa magazeti, kama huyu mzee bado ana uwezo wake, msaidieni japo apate kibarua cha miezi kwenye hiyo sector ya habari.
Nakubaliana nawe, ila wengi tumesema kuwa kuna kitu ambacho kimefichika hapo, hatuwezi kutoa maamuzi ya maana mpaka tupate picha kamili, na nakubaliana na kumsaidia ila wazee ni wengi wa kusaidiwa na ndiyo maana unatakiwa uwe mkakati wa taifa na siyo wana JF tu, kwa waTz wote siyo waliofanya kazi state house au serikalini tu.