Leo hii raisi mstaafu,Benjamini Mkapa,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ktk mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha st. Johns hapa Dodoma maeneo ya Kikuyu.Maandaliza yanakwenda vizuri na sherehe inatarajiwa kuanza saa 8 mchana huu.
Hapa wengine cha msingi, ni kutaka tu kusikia leo anakuja na kauli gani kwa wahitimu wa chuo kikuu hiki na wa vyuo vingine kwa ujumla.Bila shaka atakuja na kauli za kisiasa kuhusu soko la ajira kwa wahitimu wa vyuo mbali mbali nchini.
namkubali saana mzee wa uwazi na ukweli. alikuwa anatufundisha na kutuongoza akiwa rais na alikuwa na hotuba zenye mvuto, na hata sasa kila anapopata nafasi ya kuzungumza anatoa maneno ya busara saana. kwa mara ya mwisho nilimsikiliza kwa makini pale nkrumah hall, kwenye kigoda cha mwl.