Mkapa kuwa mgeni rasmi leo katika mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha st. Johns hapa Dodoma

Mkapa kuwa mgeni rasmi leo katika mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha st. Johns hapa Dodoma

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Leo hii raisi mstaafu,Benjamini Mkapa,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ktk mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha st. Johns hapa Dodoma maeneo ya Kikuyu.Maandaliza yanakwenda vizuri na sherehe inatarajiwa kuanza saa 8 mchana huu.

Hapa wengine cha msingi, ni kutaka tu kusikia leo anakuja na kauli gani kwa wahitimu wa chuo kikuu hiki na wa vyuo vingine kwa ujumla.Bila shaka atakuja na kauli za kisiasa kuhusu soko la ajira kwa wahitimu wa vyuo mbali mbali nchini.

Ngoja tumsubiri atasema nini.
 
Kama ningekuwa mhitimu, nisingehudhuria hayo mahafali. Liwalo na liwe, but sio kumsikiliza muhasisi wa UFISADI
 
Hakuna jipya hapo,,,yale yale marudio ya kila siku isitoshe ataongea kama mtua ambaye yupo nje ya serikali.
 
Hakuna jipya hapo,,,yale yale marudio ya kila siku isitoshe taongea kama mtua ambaye yupo nje yam serikali.
Mkuu labda atarudia ile kauli yake kuwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.
 
Awahutubie njia ya kuliibia hili taifa kama alivyofanya yeye.....na sasa anapeta.
 
Huku ni kukidhalilisha chuo. A man in a list of shame kaalikwa kwa heshima na taadhima
 
namkubali saana mzee wa uwazi na ukweli. alikuwa anatufundisha na kutuongoza akiwa rais na alikuwa na hotuba zenye mvuto, na hata sasa kila anapopata nafasi ya kuzungumza anatoa maneno ya busara saana. kwa mara ya mwisho nilimsikiliza kwa makini pale nkrumah hall, kwenye kigoda cha mwl.
 
Back
Top Bottom