Elections 2010 Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete

Elections 2010 Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete

These bunch of thives, let them avoid one another!!!
 
Sera za JK za kuwatumia wenzie kwa manufaa yake sasa zimemfika vilivyo. Pia kauli zake kampeni za uraisi ni suala la kifamilia limechochea kabisa. Hivi tunahitaji ushahidi gani mwingine wa ziada?

Wakati kuna madai kuwa Mkapa analalamikia kuchafuliwa na baadhi ya wanamtandao wa mwaka 2005, Jaji Warioba amekuwa akitishiwa kupelekwa mahakamani, jambo ambalo linadaiwa kulenga kumchafua.
Vilevile Warioba amekuwa akidaiwa kumuunga mkono Dk. Salim katika kinyang’anyiro cha mwaka 2005; na mwaka jana alihusishwa na kuunga mkono maazimio ya kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere yaliyotaka rais achukue maamuzi mazito kurejesha heshima ya taifa.
Naye, Dk. Salim amekuwa majeruhi mkuu wa mtandao wa Kikwete. Katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2005, ambapo alitwishwa zigo la tuhuma za kuwa mwarabu na kushiriki mauaji ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.
Kwa upande mwingine, Malecela anadaiwa kuchafuliwa wakati wa kampeni za kura za maoni jimboni mwake, kitu ambacho inadaiwa pia kiliandaliwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama.
Phillip Mangula ni mhanga wa siasa za mtandao. Alitupwa nje mara baada ya Kikwete kuingia madarakani na baadaye kushindiliwa wakati wa kugombea uenyekiti wa mkoa ambapo alishindwa na diwani.
Kudondoka kwa Mangula kulifuatia Kikwete kukabidhiwa mikoba ya uenyekiti na mtangulizi wake, Benjamin Mkapa. Duru za gazeti hili zinamnukuu Kikwete akisema, “Leo hii usiku, Mangula si katibu mkuu tena wa CCM.”
Mangula aliibuka wiki iliyopita mjini Njombe kwenye mkutano wa kampeni za rais na kunukuliwa akisema amefurahishwa na uamuzi wa Kikwete wa kufanya Njombe kuwa mkoa.
 
Kubenea Mwana wa Mwanahalisi, historia yako inafahamika. Mimi nadhani, kama kweli hayo ndio yaliyotokea ndani ya CCM, basi wazee wamtose waziwazi tu, wajipange waongee na wenyeviti wa mikoa wa chama ambao asilimia kubwa ni wazee kama wao, kisha wambwage chini Komredi wao. Au la, watangaze kuhamia CHADEMA.
 
duh! mwaka huu tutazichapa! mporomoko wote huu wa maadili na ulafi watu bado wanang'ania ikulu! sikio la kufa halisikii dawa
 
Back
Top Bottom