Wakati kuna madai kuwa Mkapa analalamikia kuchafuliwa na baadhi ya wanamtandao wa mwaka 2005, Jaji Warioba amekuwa akitishiwa kupelekwa mahakamani, jambo ambalo linadaiwa kulenga kumchafua.
Vilevile Warioba amekuwa akidaiwa kumuunga mkono Dk. Salim katika kinyanganyiro cha mwaka 2005; na mwaka jana alihusishwa na kuunga mkono maazimio ya kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere yaliyotaka rais achukue maamuzi mazito kurejesha heshima ya taifa.
Naye, Dk. Salim amekuwa majeruhi mkuu wa mtandao wa Kikwete. Katika kinyanganyiro cha urais mwaka 2005, ambapo alitwishwa zigo la tuhuma za kuwa mwarabu na kushiriki mauaji ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.
Kwa upande mwingine, Malecela anadaiwa kuchafuliwa wakati wa kampeni za kura za maoni jimboni mwake, kitu ambacho inadaiwa pia kiliandaliwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama.
Phillip Mangula ni mhanga wa siasa za mtandao. Alitupwa nje mara baada ya Kikwete kuingia madarakani na baadaye kushindiliwa wakati wa kugombea uenyekiti wa mkoa ambapo alishindwa na diwani.
Kudondoka kwa Mangula kulifuatia Kikwete kukabidhiwa mikoba ya uenyekiti na mtangulizi wake, Benjamin Mkapa. Duru za gazeti hili zinamnukuu Kikwete akisema, Leo hii usiku, Mangula si katibu mkuu tena wa CCM.
Mangula aliibuka wiki iliyopita mjini Njombe kwenye mkutano wa kampeni za rais na kunukuliwa akisema amefurahishwa na uamuzi wa Kikwete wa kufanya Njombe kuwa mkoa.