Mkapa to miss Sullivan Summit

Mkapa to miss Sullivan Summit

Mtanzania,
kwi kwi kwi unataka akale wapi? Polisi? tena sasa hivi ukimuuliza ufisadi wa Mkapa ni mkali kweli kweli
 
Huko Arusha kuna wajanja kuliko yeyem anajua kuwa hata akienda hatoambulia kitu (just jocjing) lakini on a serious note, inabidi tuanze kupatwa na wasi wasi jinsi mzee Mkapa, tuliyemtegemea kama mtu wa kutoa mwongozo kwenye masuala makubwa, anavyo jitahidi kukwepa national functions. Anaweza kuwa na commitment nyingi huko nje ya nchi, lakini kwa mtu kama yeye, ambaye tulimwamini kutuongoza kwa miaka 10, nadhani viongozi wa sasa wanapaswa kupta ushauri mkubwa kutoka kwake, anapokwepa, hatutendei haki watanzania
 
kama kuna hizi accusations zoooote kuhusu mkapa, nani aliyefungua kesi na kumshitaki ?? NONE ! that makes those people accusing him the waropokaji !
 
Tufahamishe tafadhali ni "facts" gani hizo zinazokufanya uamini kwamba tuhuma zote za ufisadi dhidi ya Mkapa (kuanzia kuanzisha kampuni ya biashara ANBEN Ikulu, hisa kwenye Bank M hadi kutaifisha mgodi wa Kiwira) zote ni uwongo (na zinatokana na chuki binafsi ya baadhi ya watu aliowanyima vyeo wakati wa urais wake?)
Lazima niwe clear hapa, sijasema kwamba siamini kuwa hajafanya hivyo ila sina facts zinazonizibitishia kuwa amefanya hivyo na alikiuka sheria zilizopo. Siwezi nikasikiliza magazeti au midomo ya watu. Kama kuna utofauti wa kutafsiri sheri basi apelekwe mahakamani ambako ndicho chombo kinachotafsiri sheria.
Umeandika sentensi chache zenye mambo mengi. Hakuna chombo kilichozibitisha kuwa hiyo kampuni ni ya Mkapa hata kama yake siijui sheria inayomkataza rais kuanzisha kampuni akiwa Ikulu labda ndugu yangu uniambie. Wanahisa wa Bank M walishatajwa kama aliyowataja alidanganya chombo kinachotakiwa kutoa hiyo orodha kifanye hivyo tuone kama yumo. Na ya kiwira ninakosa udhibitisho kwamba jina lake limo kwenye watu wanaomiliki hiyo kampuni iliyobinafsishiwa. Mimi sikatai kwamba kuna matatizo katika haya mambo lakini we have to fight on the right direction, mimi sidhani kama kuna tatizo kama rais akianzisha kampuni ila lazima afuate sheria zilizopo kama raia mwingine yoyote.
 
kama kuna hizi accusations zoooote kuhusu mkapa, nani aliyefungua kesi na kumshitaki ?? NONE ! that makes those people accusing him the waropokaji !
Nakuunga mkono Kada kwa hili, mimi nadhani wapeleke uropokaji wao mahakamani.
 
Kwenye website ya hawa jamaa wa ICF - http://www-usa.investmentclimatefacility.org/
kuna maelezo ya Mkapa kama yafuatavyo:

Message from ICF Co-Chair Benjamin Mkapa, former President of Tanzania
'This new and exciting facility will act on key obstacles to doing business in Africa. Through it, we hope to generate and shape policies nationally and regionally to make Africa more attractive to domestic and foreign investment, while fighting negative images of the continent. I have great hopes for the ICF and I urge all development partners and big companies with long term interest in Africa to rally around it and support it in practical terms. Africa is poor, but potentially rich: rich in terms of its natural resources, and rich in terms of the latent entrepreneurship and remarkable resilience of its people. Obstacles facing Africa include an inappropriate business environment, infrastructure, barriers to competition, customs procedures and taxation, bureaucratic red tape and image issues. Together we can remove the obstacles that stand in the path to Africa's prosperity.'


I don't think that Mkapa is really supporting Africa prosperity.. Nafikiri matendo yake yanaendana kinyume kabisa na anachokidai mara zote akiwa kwenye international arena. Kama angekuwa anatilia maanani issue ya prosperity kwa citizens wa Tanzania, asinge-loot economy ya Tanzania kwa kujilimbikizia isivyo halali mali (Kiwira plus others), majumba, n.k.

What he's doing here is preaching a certain belief or way of life, but not, in fact, holding these same virtues oneself. This is HYPOCRISY!!!. Ni kitendo cha aibu kwa mtu kama Mkapa kujiweka katika situation kama hii.

Ukiendelea kusoma kwenye site yao, kwenye section ya "Governance" utakutana na maneno haya:
"An independent board accountable to the ICF's investors as well as African and other high-level stakeholders governs the ICF. The ICF's Board of Trustees is made up of African business and political leaders, and individuals strongly committed to Africa. NEPAD has observer status on the Board. "...

I don't think hawa watu wako serious. Kama wangekuwa serious basi wangemwondoa Mkapa kwa kuwa Mkapa si mmojawapo wa individuals strongly committed to Africa in a good way.. Kulingana na kashfa alizonazo Mkapa na ambazo hajazitolea maelezo ya kueleweka, mimi nafikiri yeye bado yuko strongly committed ku-loot African economy, na kama hii taasisi inazidi kumlea, basi na wao wanatu-force tuwaelewe kwamba na wao wako katika direction hiyo. They should get rid of him now!!!
 
Tufahamishe tafadhali ni "facts" gani hizo zinazokufanya uamini kwamba tuhuma zote za ufisadi dhidi ya Mkapa (kuanzia kuanzisha kampuni ya biashara ANBEN Ikulu, hisa kwenye Bank M hadi kutaifisha mgodi wa Kiwira) zote ni uwongo (na zinatokana na chuki binafsi ya baadhi ya watu aliowanyima vyeo wakati wa urais wake?)

Mkuu unajua ndio maana mimi huwa sukugusi ninakuheshimu sana maana you are too much, naona kuna mtu haelewi hilo, kwi!kwi!kwi!kwi!kwi!

I Love JF!
 
Mnaodai Kumfungulia mashtaka Mkapa... Je kuna sheria ndani ya katiba inayoondoa kinga ya rais mstaafu kushtakiwa na Mwa/Wa-nanchi ktk mahakama zetu?
Je, ikiwa rais aliyepo madarakani kasema tumwache, bado korti inaweza kuendesha mashtaka hayo kulingana na sheria zetu..

Mkitupa jibu nadhani itakuwa mmeturahisishia zaidi wananchi na bila shaka JF tutaanza kupiga la mgambo!
 
Mnaodai Kumfungulia mashtaka Mkapa... Je kuna sheria ndani ya katiba inayoondoa kinga ya rais mstaafu kushtakiwa na Mwa/Wa-nanchi ktk mahakama zetu?
Je, ikiwa rais aliyepo madarakani kasema tumwache, bado korti inaweza kuendesha mashtaka hayo kulingana na sheria zetu..

Mkitupa jibu nadhani itakuwa mmeturahisishia zaidi wananchi na bila shaka JF tutaanza kupiga la mgambo!

Nakumbuka mimi nilikuwa mtu wa kwanza humu kusema Mkapa ana kinga na Hosea baada ya siku chache akalisema hilo. Baada ya hapo ukaanza majadali wa kisheria lakini pamoja na hayo yote jukumu la kutafsiri sheria ni la mahakama. Ukifungua kesi na mahakama kama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo watakuambia ama baada ya malumbano ya kisheria ama kabla kesi haijaanza kusikilizwa na mara nyingi wanakuambia uende wapi. Kama kabla ya kufungua kesi tumeona kuna mapungufu ni jukumu ya chombo ambacho kinatakiwa kutunga au kurekebisha sheria kufanya kazi zao siyo kujipatia umarufu kwa mgongo wa mtu.
Kama rais aliyepo madarakani kasema asishtakiwe basi huyo ndiye wa kumhoji ana power gani ya kusema hivyo au ni kwa nini. Haya mambo yalianza toka kwa Mzee Mwinyi hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kubadilisha leo hii Mzee Mwinyi ni safi na shutuma nyingi zimejulikana kuwa zilikuwa ni uzushi sidhani kama ni jambo la busara tuendelee kuropoka bila kuchukua hatua ku-fix.
 
Nina ombi moja kwenu
badala ya kumuita mkapa, naomba aitwe Ras-FISADI In caps kwani kama Rais ataidhalilisha taasisi ya Urais huku akijua katiba itamlinda basi tumzomee mpaka atie akili.....

Kama Jk tumemuita muungwana basi na huyu aitwe Ras-FISADI
 
Jaji Sinde Warioba si Mropokaji. Hii ni kutoka katika gazeti la Raia Mwema

Mafisadi wa EPA ni wezi – Warioba

Mwandishi Wetu Mei 7, 2008

Vigogo wazito waanikwe, sheria isivunjwe


Asema viongozi wetu ni dhaifu


Amtaka Mkapa akajitetee mahakamani

KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.

"Niliyosoma hasa kutokana na taarifa ile ya Serikali, ukiisoma kwa makini unaona kuwa haukuwa ununuzi wa madeni, huo ulikuwa ni wizi wa fedha za umma," anasema Jaji Warioba.

Anasema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, baadhi ya madeni si madeni bali kuna watu wametumia ulaghai kuchukua madeni ambayo yamekwisha kulipwa na wao kufanya udanganyifu kuyadai.

"Wapo ambao wamefanya hivyo kwa kughushi. Sasa kuna makosa mawili hapo. Wizi na kughushi, ni makosa mazito, na kama nilivyosema wakati ule ilipotoka mara ya kwanza, ukiona makampuni ambayo yametajwa si makampuni makubwa na mengi yake yaliundwa kwa kazi hii tu," alisema katika mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.

Akionyesha kuwapo kwa watu wakubwa nyuma ya wizi wa fedha za EPA, Warioba anasema biashara ya kununua madeni inataka mtu mwenye fedha na mwenye ujuzi wa biashara hiyo lakini makampuni yaliyoorodheshwa na serikali mengi yanamilikiwa na watu wa kawaida kabisa wasio na uwezo huo.

"Kampuni hizi ni ndogo, watu wenye kampuni hizi wameandikwa watu wenye majina ya kawaida. Kwa mtu yeyote mwenye busara atajua hii ni hadaa tu. Wanaoshughulika hawakujiandika kwenye kampuni hizi, wamechukua watu wengine tu. Kwa hiyo, kuna kazi, kuna kazi ya kuwatafuta hawa wazito waliokuwa wanahusika. Na kama ni wazito na wameingia katika wizi wa mali ya Taifa na kughushi, suala hili ni zito kuliko tunavyoliona," anasema na kuongeza;

"Mimi naamini kama kweli tunaishughulikia kwa nguvu zote, EPA ni kubwa kuliko Richmond, kuliko haya yaliyotokea. Kwa hiyo tutangojea matokeo. Na hapa kwa kuwa walau ushahidi wa kawaida upo, taarifa zinasema zile nyaraka zilizowezesha madeni hayo kununuliwa ni za kughushi, basi unaanzia hapo. Ukihakikisha kwamba ni za kughushi, kwamba haya madeni hayakuwapo, ukithibitisha kwamba hili deni halikuwapo sasa huyo aliyechukua fedha hizo alitumia wapi?"

Alisema akiwa kama raia mwema wa Tanzania anasubiri kwa makini kuona matokeo ya EPA, na kuongeza kwamba kama kweli nia ya kusafisha ipo, ni lazima waliofanya makosa wapatikane na kushughulikiwa na si wale waliotangulizwa.

"Mimi sijui utaratibu wanaotumia. Lakini kwa utaratibu wa kawaida, mimi nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi, kwa suala hili la jinai unalishughulikia linakwenda mahakamani. Adhabu inatolewa pamoja na kurudisha hizo fedha, hilo ndilo nalitarajia," anasema.

Anasema kwa kawaida hatua za kisheria ni lazima zichukuliwe na kwamba unapokwenda mahakamani unaweza kutumia sheria kurudisha fedha zilizoibwa hata ikibidi kufilisi wahusika.

Hivi karibuni timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia waliochukua fedha za EPA ilieleza wazi kwamba imekua ikipokea fedha kutoka kwa watuhumiwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuepuka kupoteza fedha hizo huku wanaozirejesha wakiendelea kuwa siri.

Timu hiyo ya Rais inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, wote wakisaidiwa na maofisa kutoka ofisi zao na kutoka asasi nyingine za umma.

Akizungumzia kitendo cha viongozi hao wa juu wa dola kufanya mazungumzo na watuhumiwa, Jaji Warioba anasema; "Kwamba hawa ndio kweli viongozi wa ngazi ya juu wa vyombo vya dola vinavyoshughulika na uhalifu wanafanya kazi hiyo. Imani yangu ni kwamba hawatapinda sheria. Wakipinda sheria tutakuwa tumeleta madhara makubwa sana kwa nchi hii. Kwa sababu wananchi lazima kwa upande wa sheria waamini ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni lazima waamini ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, lazima waamini ofisi ya TAKUKURU."

Warioba anasema watendaji hao wa dola wakipinda sheria, imani ya wananchi itapungua na hivyo ni jukumu lao ni kubwa, na kwamba yeye ana imani kwamba hawatapinda sheria.

Akizungumzia hali ya kisiasa ya nchi kutokana na kukwama kwa mambo mengi ikiwamo muafaka wa kisiasa Zanzibar na kuibuka kwa wimbi kubwa la tuhuma za ufisadi, Jaji Warioba anaonekana kutokua na imani na hali hiyo na anakiri kuwapo kwa udhaifu katika uongozi wa juu wa kitaifa.

"Kama nilivyosema, kila mtu ni kuzungumzia ufisadi, hata mafisadi wenyewe, maana ukiona wote hawa wanaozungumzia, huwezi kusema ni watu safi, pamoja na vyombo vya habari, navyo haviwezi kujisifu. Wengine wanaoandika juu ya ufisadi ndio hao hao waliokuwa wakichukua fedha za hawa, wanawaandika kuwa ni wazuri wakati wa uchaguzi. Walikuwa wakiwapamba. Kwa hiyo kuna wengine ni unafiki tu, ama ni ufisadi na wenyewe," anasema.

Warioba anapongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari na wabunge katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini anaonya vita hiyo isitumike kufunika madhambi yaw engine ama kuwaumiza baadhi yao.

"Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?

"Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?" anahoji Jaji Warioba.

Anasema wamo wengi ambao ni sehemu ya uongozi, na hivyo isije tokea mapambano ndani ya uongozi yakageuzwa kuwa ni vita ya kweli kumaliza ufisadi.

"Mimi nataka niwe na uhakika tukifika mwaka 2010 tuweze kuchagua viongozi safi, tusipate viongozi ambao katika mchakato wa uchaguzi watakwenda na takrima kwa sababu kama wanakwenda na takrima wamezipata fedha hizo kwa ufisadi," anasema.

Akizungumzia muafaka kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Wariona anasema tatizo kubwa ni mgawanyiko katika uongozi. Anasema wapo ambao hawataki muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa.

Kuhusu wanaotishia kurejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF, Warioba anasema hivyo ni vitisho visivyo na maana katika mazingira ya sasa kwani hata wakiachwa hawana uwezo huo na kwamba tatizo kubwa ni udhaifu wa viongozi.

"Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu," anasema na kuongeza;

"Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi."

Pamoja na kuonekana kukwepa kumshutumu Rais Mstaafu Mkapa, Jaji Warioba anasema kinga waliyonayo viongozi akiwamo rais ni ya kisiasa tu, na hivyo kwake yeye suala la kinga ya kisheria si tatizo bali ukweli na uhakika wa tuhuma zinazomgusa kiongozi husika na kwamba ni mahakama inayoweza kutoa uamuzi wa haki.

"Nimeona wanaandika na nimeona mjadala mkubwa tu unaolenga kwenye immunity. Mimi nafikiri suala hilo si la msingi kwa sasa hivi. Na mjadala unalenga kwamba aseme, naona si la msingi. Kwa sababu hatutaki kwamba huyu awe tried na vyombo vya habari. Maana hapa naona kama ni trial kwenye vyombo vya habari.

"Waseme ni kosa gani, amefanya kwa msingi wa sheria gani, sasa waendelee. Sasa mengi wanayosema ni ya kisiasa. Yakisemwa ya kisiasa unataka mtu awajibike kisiasa. Kama ni kosa la jinai, waseme amevunja wapi sheria, lakini kusema kweli mimi sioni kwa vyombo vya habari kusema yote haya na wanachotaka ni kwamba ajitetee, ajitetee wao ndio wamekuwa Mahakama?" anahoji Jaji Warioba ambaye amewahi kufanya kazi kwa karibu na Mkapa.

Warioba anasema vyombo vya habari vinataka kuwa Mahakama na akashauri kwamba kama kuna kosa alilofanya Mkapa ni vyema wakasubiri afikishwe mahakamani ambako atakuwa na nafasi ya kujitetea na kueleza upande wake.

"Immunity nasema sasa hivi siyo issue. Sema kosa lililotendeka. Anashitakiwa lakini wanasema hatuwezi kuendelea kwa sababu kuna immunity. Bila kusema kosa huwezi kufika kwenye immunity. Huwezi kuanza na immunity bila kuwa na kosa, kwa hiyo mimi sitaki kujiingiza katika mjadala wa immunity. Hii ni ya kisiasa tu," anasema.
 
Kiini cha shutuma dhidi ya Mkapa ni kwamba alitumia visivyo cheo na wadhifa wake akiwa Rais kuendesha biashara na kujitajirisha yeye binafsi, familia yake na maswahiba wake. Hii ni kinyume na maadili, kanuni na taratibu za Uongozi serikalini na ni kosa kubwa sana. Ile kwamba amediriki kufanya yote hivi kwa kutumia nguvu kubwa (na isiyo na kipingamizi cha aina yoyote ile Jamhuri nzima ya Tanzania) ya cheo chake kama Rais wa nchi ni ukiukaji wa taratibu tayari na haisaidii kama procedure nyinginezo (maombi ya mkopo, usajili wa kampuni, nk) zilifuatwa. Jee, unabisha hata hili?


I hate to bust your buble Nyama Hatari on this. There is no effective leadership code in Tanzania!

Hawa jamaa wote Chenge, Mkapa, Karamagi, Msabaha na hata ya kudai Mkono na Rostam ambao ni wafanyabiashara wasiwe wabunge au waache kimoja ni kuwa wafuate maadili ni maadili yapi? kanuni zipi? taratibu zipi? Leadership code is something as mystic as Ballali saga!

Wote watahukumiwa kwa Uzembe na vijikosa vidogo vidogo kwa kuwa Sheria kali hakuna!
 
Nakumbuka mimi nilikuwa mtu wa kwanza humu kusema Mkapa ana kinga na Hosea baada ya siku chache akalisema hilo. Baada ya hapo ukaanza majadali wa kisheria lakini pamoja na hayo yote jukumu la kutafsiri sheria ni la mahakama. Ukifungua kesi na mahakama kama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo watakuambia ama baada ya malumbano ya kisheria ama kabla kesi haijaanza kusikilizwa na mara nyingi wanakuambia uende wapi. Kama kabla ya kufungua kesi tumeona kuna mapungufu ni jukumu ya chombo ambacho kinatakiwa kutunga au kurekebisha sheria kufanya kazi zao siyo kujipatia umarufu kwa mgongo wa mtu.
Kama rais aliyepo madarakani kasema asishtakiwe basi huyo ndiye wa kumhoji ana power gani ya kusema hivyo au ni kwa nini. Haya mambo yalianza toka kwa Mzee Mwinyi hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kubadilisha leo hii Mzee Mwinyi ni safi na shutuma nyingi zimejulikana kuwa zilikuwa ni uzushi sidhani kama ni jambo la busara tuendelee kuropoka bila kuchukua hatua ku-fix.


hao wanaomshutumu mkapa ni sawa sawa na kelele za mlango ambazo kwa mkapa ni kama mwenye nyumba hivyo hizo kelele hazimsumbui !
 
Back
Top Bottom