Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu.
Alitoa kauli hiyo jana jioni, kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa taasisi yake jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, kufungua mkutano wa siku mbili wa Mkapa Foundation, taasisi inayojihusisha na Ukimwi, Mkapa alisema kuwa anamfahamu vizuri Makamu wa Rais kwa siku nyingi na kwamba wamewahi kufanya kazi pamoja.
Alisema lakini yeye (Mkapa) katika siku za karibuni, hajawahi kusemwa kwa mazuri wala kusifiwa lakini yote anamwachia Mungu.
Baada ya kusema hayo, alimkaribisha Dk. Shein kufungua mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam bila kusoma hotuba yake, ambayo baadaye waligawiwa waandishi wa habari.
Mkapa amekuwa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya bila kufuata taratibu na kwa bei ya kutupa.
Inadaiwa kuwa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali yake, Daniel Yona, kujimilikisha mgodi huo kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani yake halisi ya Shilingi bilioni nne.
Hata hivyo, licha ya kujimilikisha kwa gharama ndogo, pia inadaiwa kuwa waliishia kulipa Sh. milioni 70 tu.
Chanzo: IPP Media Web