Kama isingekuwa tamaa (bila shaka kutokana na kuwa na washauri wabovu), huyu jamaa alifanya mambo mazuri mengi kwa maendeleo ya nchi. Mpaka sasa sielewi kwa nini alikubali kununuliwa na makaburu walioitwaa NBC yetu. Sijui ilikuwaje pia akapata kichaa cha kutumia vibaya madaraka yake na kununua Kiwira. Ukiondoa dosari hizo na kiburi chake cha Kimachinga, alifanya vizuri.
Ni tamaa yake na siyo kushauriwa vibaya- alipouza NBC alijenga/alijengewa hotel kubwa south africa (Huko si kushauriwa bali ni tamaa), kumbuka wakati huo Nyerere alikuwa hai lakini hakumsikiliza!
Kujiuzia Kiwira ni ukichaa, nakubaliana nawe, ila kukomesha ukichaa huu kwake, kwa waliopo na kwa wajao, dawa si kumuachia Mungu - ni kuwafikisha mahakamani.
Hata kupanda kwa uchumi lazima tukuangalie kwa makini. Uchumi ulipanda kwa kuuza raslimali tulizokuwa nazo? Tuliuza lakini uzalishaji haukuendelea kufanyika ndani, na hata huo kidogo ulioendelea kwenye madini ni wizi mtupu - je uchumi ulipandaje? Hata Mkapa mwenyewe anakiri hivyo
"Ex-president of Tanzania Benjamin Mkapa nicely summed up his experience and that of many other countries: We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us.
Written by Roberto Savio / Inter Press Service
Wednesday, 19 August 2009 21:16
Chukulia mfano mdogo - wewe una shamba lakini unakosa hela ya matumizi, unaamua kumuuzia mtu hilo shamba anakupa hela halafu unajidai sasa hali yako ni nzuri kwa kuwa unazo hela za kutumia? Mpumbavu wewe hela hizo zitakapoisha unakuwa maskini zaidi ya hapo mwanzo kwa kuwa hata shamba sasa huna. Utabaki kumuomba huyo uliyemuuzia akuajiri katika shamba hilo hilo - akikataa akaamua kuleta ndugu zake wewe si utakuwa umekwisha kabisa?
Haya ndiyo yaliyotokea TZ na yanaendelea kutokea - hata wafagiaji wanaletwa na wawekezaji!
Mkapa kuna mazuri alifanya; ni wazi huwezi kuongoza miaka kumi na usifanye hata moja zuri, ila wadanganyika tunapaswa kujua kuwa rais anapaswa kufanya mazuri tu na kwa mazuri hayo tunamlipa mshahara mzuri na maslahi mazuri anapostaafu hadi kufa kwake; hapaswi kuwa na tamaa kwani maisha yake yako-guaranteed hadi kifo na kuzikwa!
Kama kwa mazuri tunamlipa je kwa mabaya tena ya maksudi, tumfanyeje? Tumwachie Mungu tu? HAPANA, Hata wana dini wanasema "Mungu nisaidie huku nawe ukiweka nguvu zako"; nguvu zetu ni kumpeleka mahakamani, huko ndiko atatueleza vizuri 'wivu tuliokuwa nao wa kijinga'