Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, pamoja na kuibuliwa kwa uchafu wakati wa utawala wake ukweli unabaki pale pale mengi mazuri.
Wakati anaondoka madarakani bundle moja ya bati tulinunua 87,000/= lakini ilipofioka January 2008 ilishafika 280,000/=, nauli za daladala zilisimama kwa miaka yake yote ya utawala katika 100/=; haya ndiyo mambo sisi watu wa kawaida tunayoyaangalia;
Wakati wa Mkapa tulikuwa tuki budget, leo hii haiwezekani, tumebaki kuishi kwa matumaini tu.
Sio sahihi kabisa kumbeza mzee huyu kwamba hajafanya kitu, hapana amefanya makubwa kuliko hayo mabaya.
Kwanza mikataba ya madini ilianzia kwake, tuwe wakweli, IPTL nani alikuwa waziri wa madini na nishati na nani alikuwa rais!!!!
Mwacheni mzee wa watu apumzike.