Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

ndiyo kipindi chake ilikuwa na mafinikio
Mpangwa,
Yepi hayo Maendeleo, wakati Mwenyewe Mkapa ananukuliwa Akisema "Anaogopa kuongea bila kuweka rekkodi" na punde tu kadai ana sifa za Uongozi?. Si abainishe tu kuwa WaTz: MBICHI ni hizi KIWIRA, RADA, NDEGE nk na Mbivu ni hizi: USHURU, BARABARA, UWANJA WA MPIRA nk halafu tutaona ukurasa ataufunga vipi. Asialete za kuleta haya ni ya KAISARI na yaishie hapahapa kwa KAISARI!!
 
Bado najiuliza kundi gani hilo "maalumu" bwana Nkapa analiongelea? This guy behaves as if he is elitist!!! Anatudharau watanzania wote kwa gharama ya kudumisha urafiki na maswahiba wake wa kundi maalumu. Tusubiri tuone. Ndio maana nilijiuliza sana mungu aliyemwachia yote ni mungu gani!!!!
 
Na pesa zote alizoacha hazina zilikwisha ndani ya miaka miwili tu ya uongozi wa Kikwete.
 
Anahaki ya kijigamba, hata mabondi wanajigamba kuwa na uwezo zaidi ya mwingine lakini mwisho wa mchezo ndo unaamua kama alikuwa sahihi katika maneno aliyo toa.
Kwa mkapa, angelitoa datas kuonyesha positive na negative za uongozi wake, na watu watajua kweli kama alifanikiwa au la.
 
Kamanda! Data zipo chungu nzima sema tu hutaki kuziona.

mkuu kibunango
ukiweka natumaini asieziona kipofu asie na macho...wewe kama mdau halisi embu zimwage hapa utuidhinishie yalioandikwa hapo juu
 
Date::11/21/2009Mkapa: Majigambo ya uongozi bora kama kuchokoza nyuki
Mkapanyuki.jpg


Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, kujitetea kwake kama kuchokoza nyuki.Na Sadick Mtulya
Mwananchi



UAMUZI wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuvunja ukimya na kuzungumzia mazuri aliyoyafanya katika utawala wake, sasa unaonekana kumwigiza katika matatizo zaidi baada ya kutafsiriwa na watu kuwa ni kujisafisha.


Hivi karibuni Mkapa alijisifia kwamba ana sifa za uongozi na kwamba tuhuma zake anamwachia Mungu, baadhi ya wasomi na wanasiasa nchini wameyatafsiri maneno hayo kwamba ni ya kutaka kujinasua katika kashfa zinazomkabili kutaka kuwaachia wananchi wapime nani kafanya mazuri kati yake na Rais Jakaya Kikwete.


Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana wadau hao walisema kauli hizo za Mkapa ama zinakwepesha hoja ya msingi ya watanzania kumtaka azungumzie tuhuma zake na zina lengo la kubadalisha ajenda ili waangalie mabaya ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Mwesiga Baregu amesema, Mkapa anatakiwa kujitokeza hadharani na kukiri kwa kujibu tuhuma zote zinazomkabili ikiwemo kutolea ufafanuzi maeneo aliyofanikiwa na aliyoshindwa katika utawala wake.


"Haitoshi kwa Mkapa kueleza maeneo uliyofanikiwa tu pia anatakiwa aeleza na maeneo ambayo hukufanikiwa na hili si jambo la ajabu, kwani katika maisha ya binadamu kukosea kupo.
"Kila binadamu anakosea na si kwamba Mkapa na utawala wake haukufanya mambo mazuri., Sasa ili ajisafishe na watanzania wamsamehe ajibu tuhuma zote zinazomkabili," alisema Profesa Baregu.

Alisema haitoshi Mkapa kusema yeye ni kiongozi bora kwani watanzania wana kiu na maswali mengi yanayohitaji majibu ya kina kutoka kwake kwa kuwa masuala yote ya kifisadi pamoja na matitizo mengine yanayoendelea kuikumba nchi yalianzia katika kipindi chake.

"Unapozungumzia kiongozi bora cha kwanza kuangaliwa ni uadilifu hivyo Mkapa aonyeshe uadilifu aliofanya katika utawala wake na sifa anazojipa si bora kuliko za wenzake," alisema Profesa Baregu.


Alisema kwa vile Mkapa ana uwezo wa kujibu tuhuma hizo na sababu ya kufanya hivyo ipo, anapaswa kujitokeza hadharani kueleza kama tuhuma hizo ni za kweli au la.

Alifafanua kwamba pamoja na mambo yote, uadilifu wa Mkapa una mashaka kwa kuwa mara alipoingia madarakani alitangaza mali zake, lakini alipomaliza awamu yake hakufanya hivyo.


''Mkapa ana tuhuma nyingi tu na kitu ambacho kinanishangaza wakati akiingia madarakani alitangaza mali zake kwa nini wakati alipomaliza utawala wake wa miaka 10, hakusema mali zake ili watanzania wajue kama kavuna au hakuvuna,'' alisema Profesa Baregu.


Baregu alisema kutokana na Mkapa kukosa sifa ya uadilifu ndio maana hata Taasisi ya Mo Ibrahim imeshindwa kumchagua na kumpa tuzo ya kiongozi bora.

''Kama kweli Mkapa alikuwa msafi basi angeweza kuibuka na tuzo ya Mo Ibrahim kama ilivyokuwa kwa rais wa Msumbiji, kutokana na hilo sidhani kama ni kiongozi bora kama anavyodai, usafi wake sijui ni wa vigezo vya aina gani lakini kwangu hakuna kitu.''


Kauli ya Profesa Baregu iliungwa mkono na Profesa Abdallah Safari ambaye alisema kutokana na mfumo wa uendeshaji nchi, Mkapa anaweza kuzungumza lolote kwa kuwa anajua hawezi kubugudhiwa.

"Mkapa ataendelea kuzungumza vyovyote atakavyo kwa kuwa Rais Kikwete tayari alikwisha mkingia kifua na kumtetea katika masuala mbalimbali," alisema Profesa Safari.

Akizungumza wiki hii katika mkutano wa pili wa wadau wa taasisi yake ya mapambano ya Ukimwi, Benjamin Mkapa HIV/AIDS, Foundation, Mkapa alisema tuhuma zake anamwachia Mungu na kwamba anaamini anazo sifa za uongozi.


Kauli ya Mkapa inakuja huku utawala wa Kikwete ukiwa katika matatizo makubwa ya mgawanyiko ndani ya chama, ufisadi matatizo ambayo yanatishia kuisambaratisha serikali yake.


Dalili za kusambaratika kwa chama chake cha CCM kilijionyesha hivi kasribu mjini Dodoma baada ya kamati ya Rais Ali Hassan Mwinyi, kushudia wabunge na mawaziri wa chama hicho wakirushiana matusi ya nguoni.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema licha ya Mkapa kutuhumiwa inawezekana kauli zake zikawa ni wosia mwema kwa mustakabali wa taifa.
''Kwa sasa taifa lilipofikia linahitaji hekima, umoja na amani hivyo inawezekana Mkapa akawa ametoa wosia kulingana na hali halisi ya mambo yalivyo katika utawala wa hivi sasa na wa kwake,'' alisema Mbatia

Hata hivyo, Mbatia alisema nchi kwa sasa inakwenda mlama kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Mkapa ya kukimbilia Ubepari.
Mbatia alisema suala ambalo anampongeza rais huyo ni kuweza kudhibiti mfumuko wa bei nchini na kuongeza kuwa makosa aliyoyafanya ni pamoja na ubinafsishaji ambao haukujali maslahi ya watanzania.


Utakumbuka ile mikataba ya madini chini ya mrabaha wa asilimia tatu sidhani kama ulikuwa uzalendo kwa sababu watanzania hawakunufaika na madini haya ambayo baba wa taifa mwalimu Nyerere alitahadhalisha juu ya ubinafsishaji huo ambao kwangu sioni kama ulikuwa na tija.

Alisema licha ya kuwa kila kiongozi ana mchango wake katika jamii na nchi kwa ujumla lakini Mkapa hana sifa za kuweza kuibuka hadharani na kujitamba kuwa yeye ana sifa za kiongozi bora kwa kuwa ni miongoni mwa viongozi waliyevunja Katiba ya nchi.
'' Mkapa alivunja ibara ya 3 ya Katiba ambayo ilikuwa ikielekeza nchi kuendeshwa kwa itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea,lakini yeye akalazimisha twende katika ubepari'' alisema na kuongeza; '' Haya yote yanayojitokeza kwa viongozi kunyooshewa vidole ni uwepo wa mfumo mbaya wa Katiba.''


Naye Mbunge wa Kishapu Fred Mpendazoe amesema Rais Mstaafa Benjamin Mkapa ameiweka katika mazingira magumu serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutokana na kumlinda kwake.


Mpendazoe alisema pamoja na Mkapa kufanya mambo makubwa katika utawala wake lakini hayawezi kulinganishwa na madhara wanayoendelea kuyapata watanzania kutokana na maamuzi mbalimbali aliyofanya ikiwemo ubinafsishaji wa mali za umma .

"Kujisafisha kwa Mkapa ni kuwaomba radhi watanzania kwa yote mabaya aliyowafanyia ya kubinafsisha mali za Umma, uuzaji wa nyumba za serikali, ununuzi wa ndege ya Rais, Rada pamoja na mengine mengi," alisema Mpendazoe.


Mbunge huyo alisema rais Mkapa anapata jeuri na ujasiri wa kuzungumza hayo kutokana na kulindwa na utawala wa awamu ya nne.


"Lawama zote za Mkapa zimemuangukia Rais Kikwete kutokana na kumlinda kwake, nimwekwisha waambia waache kumlinda ili awajibike kwa mabaya aliyawafanyia watanzania," alisema Mpendazoe


Alisema kamwe Mkapa hawezi kukumbia kivuli chake cha mabaya hadi hapo atakapokubali madhambi yake na kuomba msamaha kwa watanzania.

Mpendazoe allitaka serikali ya Kikwete kuacha kuendekeza na kuendeleza tabia ya kuwalinda viongozi wanaofanya maovu.



Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo la Taasisi ya Mkapa alimwuliza rais huyo mstaafu, " ..Umezungumzia sifa tisa za uongozi, je katika miaka kumi ya uongozi wako sifa hizi unazo?."

Katika jibu lake Mkapa alisema, "..Naogopa kuongea bila kuweka rekodi, lakini juu ya suala hilo sina shaka kwamba ninazo na ndiyo maana uongozi wangu ulikuwa wa mafanikio."

Aliongeza: " Huwezi kufanya usichokujua, lazima ujue wapi pa kuanzia, nini ufanye leo, nini usifanye, kipi kipaumbele na nini kisubiri. Ukiwa na hayo unaweza kuonyesha unazo sifa za uongozi." Moja ya kshfa ambazo Rais Mkapa anatuhumiwa kuzifanya akiwa Ikulu ni familia yake kununua mgodi wa Mawe wa kiwira, kubinafshaji mashirtika ya umma bila ya utaratibu na mikataba kwenye sekta ya madini.
 
Hata kabaila, kupe, bwenyenye au fisadi kwa sasa anadiriki kusema anamwachai mungu....????

Hii inji imetoka mbali wajameni.....enzi za Mwalimu toka chekeche unaimba ahadi za TANU ya kwanza mpaka kumi:


Leo waliotufundisha kuimba ndo mafisi kuliko....
 
Ladi mkuu, sisi sote ni wana CCM, lakini hii yako imepitwa na wakati.
Inaitwa parroting, kasuku.
Hii mwachie Komba, he is paid for that.Kama na wewe unalipwa kwa hilo ,fine.
Ukumbi huu weka argument na mantiki ya argument hiyo, full stop.

Kama kweli wewe ni mwana CCM, naomba utuandikie namba ya kadi yako na ilitolewa mwaka gani?
 
Nimeshasema na ninasema tena Mkapa ni fisadi tu kama mafisadi wengine wanaotuhumiwa kwa kuchota mabilioni ya fweza za Watanzania.

Kama kina Yona, Mramba,Liumba wameshafikishwa mbele ya Sheria na hawa wote walifanyakazi wakti wa uongozi wake yeye anasubiri nini kupelekwa kwa Plato???

Sheria siku zote huwa haiangalii wewe huko nyuma ulifanya mema au mazuri mangapi!Kosa hata ni la mara moja tu lazima upate hukuma unayostahili. Sheria haitasema kuwa huyu jamaa Bwana alikuwa mwaminifu miaka yote kakosea leo tu kwa hiyo asamehewa. Watu ndicho wanachojaribu kutushawishi ili tumwonee huruma Mkapa kwasababu sijui alijenga uchumi imara na kuzuia mfumko wa bei!!!!!

Acheni sheria ichukue mkondo wake na yeye akajitetee mbele ya Pilato na amwambie hayo maneno ya kuwa ANAMWACHIA MUNGU sijui mungu yupi ambaye anakubaliana na UFISADI NA UNYAMA wake aliotufanyia Watanzania.

Kumbukeni Mkapa ndiye Rais wa kwanza kumwaga damu ya Watanzania baada ya Nchi yetu kupata Uhuru. Ndugu zetu pale Unguja wapatao 21 walipoteza maisha kwa sababu ya ubabe,ujeuri,kiburi na dharau za Mkapa. Aliamrisha askari polisi kuwafyatulia risasi Wananchi kwasababu tu walikuwa wana andamana kupinga ushindi wa CCM baada ya kuwadhulumu ushindi wana-CUF!!!!Na kwa mara ya kwanza Tanzanai ikatengeneza wakimbizi wa kisiasa kutokea Tanzania!!!!!

Madudu yote haya NKapa na mashabiki wake hawayasemi.Halafu leo bila ya aibu anathubutu kusimama mbele ya Watanzania na kudai ati alikuwa Rais bora. Yeye hakuwa Rais bora hata kidogo baali alikuwa Bora rahisi.
 
na kweli bora amwachie Mungu maana hata kama asingemwachia lazima moto wa kiberiti atachomwa tu na Mungu huyu..maisha ya watu maskini wanaolia kwa sababu ya ufisadi wake..Mungu hawezi mwacha huyu..
 
Kama kweli wewe ni mwana CCM, naomba utuandikie namba ya kadi yako na ilitolewa mwaka gani?
Bwana mdogo kuona ni kuamini, hebu niPM ili tupange wasaa na mahali nikuonyeshe!!
Sisi tulikunywa maji ya bendera bwana.
Lakini binafsi nasikitishwa sana na hali chama changu.
 
Kazi ya CCM siyo kulinda makosa ya wanachama wake hata kama wanafikiri ni wakubwa kiasi gani.
 
jamani jamani jamani. hebu wakati mwingine tuwe na nyoyo za shukrani. kipindi mr Clean amechukua nchi hadi anaikabidhi kwa Kj ni kigumu sana. hebu muacheni apumzike mopambane na hawa wanotukoroga leo. kwani kosa la jana tena la mtu ambaye hana nafasi ya kulirekebisha halitusaidii.
 
Back
Top Bottom