Mkasa gani umewahi kukutana nao kwenye nyumba za kulala wageni (gesti) mpaka ukajisemea nini hii?

Nilienda semina Mtwara..nikalala lodge moja hivi..huko mitaa ya stendi ya zamani..mida kama ya sa6 usiku..niliguswa na mguso wa ajabu ambao sijawahi upata tangu ni zaliwe..huku nikiwa nimekabwa...daaah...nilipiga yowe kama nakata roho sijawahi lia vile..kuja kushtuka na kuwasha taa sioni kitu..baada ya muda mhudumu akaja kugonga kuuliza nini kimetokea..nika mweleza ni ndoto mbaya..nilikuja kusinzia badae sana..kesho yake nikasepa sikurudi kulala tena kwenye ile gest..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…