It's just a matter of time, dada yako ATAJUA TU, hata wewe usipomwambia, siku moja mazingira yatamfanya dada yako ajue tu, ni suala la muda tu. Usisubiri dada yako aje ajue mwenyewe, inabidi umwambie dada yako haraka sana, yaani leo leo. Lazima atakasirika sana, anaweza kupata mshituko na taharuki fulani, lakini ni bora yote hayo yatokee sasa hivi na yaishe sasa hivi, kuliko shemeji yako aka 'bwana wako', aendelee kuwatafuna nyote atakavyo, kwa miezi na miaka kadhaa huko mbele.
Usirudie kufanya makosa. Kosa la kwanza umelala na shemeji yako, kosa la pili unafanya siri inayompa mwanya shemeji yako kuendelea kumla mdogo wako, yaani wewe ndiye unayetengeza mazingira ya mdogo wako kuliwa, kosa la tatu unavyoendelea kuuficha uchafu wako na wa shemeji yako, maana yake ni kwamba wewe na shemeji yako/yenu lenu ni moja, na mnamficha dada yako/yenu, unafikiri dada yako atakufirikiaje?!
Kuanzia sasa UKOME kumpa tunda shemeji yako na mwambie mdogo wako pia aache mara moja kumpa mchezo shemeji yenu aka 'bwana wenu' Hivi umewaza siku moja nyote , wewe, dada yako na mdogo wako mna mimba mlizopewa na mtu mmoja? Itakuwaje?
Ni ngumu lakini kwa kuwa wewe ndiye uliyelikoroga inabidi ulinywe