Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh hatari sanaSehemu ya tatu....
Hakuna adui mbaya kama rafiki yako mwenyewe ambaye hajui yuko nawe au yuko kinyume na wewe. Huo ni moja ya mstari wa Legend Farid Kubanda maarufu kama Fid q katika wimbo wake wa sihitaji marafiki. Hii ngoma hua nikiisikiliza basi nashindwa kuamini kama haya mashairi yaliandikwa na mwanadamu wa kawaida Fid q is extra genius. Basi katika kipindi hiki kigumu huu wimbo ulikua ukinikonga sana moyo na kunifungulia ulimwengu kuhusu marafiki. Sio kwamba marafiki wote ni wabaya lakini katu usije wahi kumuamini rafiki maana hujui yupi atakae kusaliti.
Basi baada ya Esta kuondoka nilibaki nikitafakari sana maneno yake niliyaamini kwa 100% lakini kuna jambo lilinitatiza sana, hivi Eddy aliniibia vipi PC maana si mlango wala kufuli iliyokuwa imevunjwa kabla ya tukio la wizi. Niliwaza sana bila kupata majibu ila nilijipa moyo kua kila kitu kitabainika tu kikubwa nipate kwanza PC yangu hayo mengine ntayajua mbeleni kwakua mwanzo nshaujua haiwezi nisumbua mwishoni.
Ilibidi nimpigie simu bro ili nimpe zile taarifa tuone itakuaje, akanambia kua ametoka kwenda mjini na atarudi usiku nikamwambia nina fununu kuhusu mwizi wa kompyuta yangu, akasema haina shida akija tutadeal nae. Siku hiyo sikutoka hata kwenda misele nilikua nimechoka kimwili na kiakili, nilikaa ghetto hadi usiku nikapika nikala kisha nikalala. Kesho yake asubuhi bro alikuja nikamwelezea tukio zima jinsi lilivokua alishangaa sana. Akanambia hapa haina haja ya kupoteza muda tunasepa hadi kituo cha polisi na kuja kumkamata mhalifu wetu. Basi na mimi sikuona haja ya kupinga tulichukua boda akatupeleka hadi kituo cha polisi. Kwakua kesi ilikuepo pale na bahati nzuri tulimkuta yule polisi ambaye siku tunakuja kuripoti alikuepo haikutupa tabu sana kujieleza. Nilimwambia kua nimepata taarifa za mtu aloyeniibia kompyuta yangu na inasemekana kaenda kuiuza huko mjini. Yule polisi alishauri tukamkamate, wote tukakubaliana lakini bahati mbaya maaskari wengine hawakuepo kituoni walikua wameenda kufatilia gari ya mkubwa wao iliyokua imeibiwa siku iliyopita so akasema tuje kesho yake lakini tuhakikishe kuwa tunatunza siri ili "mwizi" asije akakimbia. Nasi tukamhakikishia kua tutatunza siri. Hao tukaondoka.
Ilikua mida ya jioni ambapo Eddy alinipigia simu kua ana shida muhimu sana anaomba tuonane. Nami nikaona yes huu ndo muda wa kwenda kumpeleleza zaidi japo nilitakiwa kuwa makini asihisi kama najua kila kitu. Nilienda pale aliponambia tukasalimiana fresh kisha tukaanza stori za hapa na pale. Baadae akaanza sasa kueleza kile alichoniitia. Ujue Ema wewe najua si mtu wa 'mila' lakini nilitaka kukuambia kua kuna mtu ni mganga hatari sana yaani tungeenda pale lazima mwizi angepatikana tu. Nilisitajabu sana kusikia hiyo taarifa ila nikajikaza, enhee huyo mganga yuko wapi na unamuamini kwa kiasi gani. Yupo kigoma wala huna haja ya kwenda huko yeye anamaliza mambo hapohapo ulipo. Sasa nikaona kweli Eddy kaniona mi ni bwege sana yaani baada ya kuniibia tena bado anataka kunitapeli hasira kali zilinipanda nikaona sasa uvumilivu umenishinda ikabidi nipasue jipu. Kwanza nilianza na kucheka kisha nikamwambia, ujue Eddy wewe hujui tu haya mambo ya mila kama kwenye ukoo wetu ndo yamejaa tele na kwa taarifa yako jana bibi alikuja pale nyumbani kwetu na ameshatutajia mwizi ila si vizuri nikimtaja kwa sasa, na najua aliiba kompyuta yangu na kwenda kuiuza mjini na ameshalipwa malipo nusu, sasa mi nimeona nimpe muda lakini lazima ntamkamata tu maana shauri tayari lipo polisi ngoja niache wafanye kazi yao maana mimi ni mdai tu. Aisee Eddy alishtuka kama vile ameona zimwi ingawa alijikaza ila niligundua tayari huyu kwisha habari yake, na mimi sikumpa nafasi nikasema ujue Eddy wewe ni rafiki yangu najua utanipa ushirikiano mzuri na mimi nataka niwahi home natakiwa nimpelekee mama mzigo flani hivi niliongea huku nikimpa mkono wa kwakheri tayari kwa safari. Sawa tuko pamoja ngoja na mimi niwahi home tutawasiliana aliongea kinyonge tena haraka haraka huku akiona aibu flani hivi , mi sikujali nikalala mbele.
Naamini kati ya siku ambayo Eddy alipitia wakati mgumu basi ni siku hiyo na kwa vyovyote vile aliamini kua bibi yangu ni mganga hatari sana kumbe wapi [emoji16][emoji38][emoji1787]. Sasa ikawa ni kupimana ubavu nani ana taasisi bora ya ujasusi kati yangu mi na yeye hadi hapo niliamini nipo mbele hatua themanini. Nilirudi home na kuendelea na mishe zingine.
Kesho yake asubuhi bro alinipigia simu kua nijiandae twende kituo cha polisi. Wakati najiandaa Eddy alinipigia simu na kuniambia niende kule kwao ana fununu flani kuhusu mahali PC yangu ilipo. Nikatabasamu nikajua baasi tayari kashaingia kwenye formula yangu huyu hachomoki katu. Bro alikuja na boda hao tukapanda bahati nzuri kwao Eddy ilikua ni njiani tu na ndo hiyo njia ya kwenda kituo cha polisi.. So tulipofika kwao Eddy ilibidi bro anisubiri njiani mi nikaenda hadi kwao. Nilikuta kama kuna kikao flani hivi cha dharura maana nilimkuta Eddy, mama yake na baba yake wamekaa kama wanateta jambo niliwasilimia kisho Eddy akaja tukatoka pembeni. Eddy alianza kuongea kwa huzuni sana kwanza alianza kuniomba samahani kwa kile atakachoniambia. Akakili kua ni yeye ndie alieniibia PC lakini hakupenda iwe hivyo bali ni tamaa tu huku akilaumu umasikini alidai kua umasikini ni mbaya sana na katika maisha yangu niogope sana umasikini aisee nilichoka kabisa. Aliendelea kunipa michongo kua hata siku ile kwenye mahindi walikua akiniviazia yeye na baraka ili wanipige ikibidi nife ili ionekane kama nilivamiwa njiani na vibaka ndo walionipora PC sema baadae akanionea huruma. Aisee hii ilinitisha sema yaani rafiki yangu alipanga kuniua kisa kompyuta! Eddy !!!!? Nilimuita kwa mshangao. Kweli ulitaka kuniua kisa PC wewe Eddy wewe ni wakunifanyia hivo. Da nilichoka sana. Aliniomba sana msamaha nami sikutaka kugombana nae nilichokua nataka kwa wakati ule ni PC yangu tu hayo mengine nilimuachia Mungu yeye ndo angeweza kutoa hukumu.
Akanambia PC ipo mjini kwa yule fundi kompyuta aliyekushushiaga window, na alikua kweli kampa hela nusu na alitakiwa amalizie jumamosi inayofuata. Nikamuuliza kwani ulimuuzia shilingi ngapi akasema laki tatu kwahiyo alimpa laki moja na nusu so ilibaki tena kiasi kama hicho. Na mbaya zaidi akadai walikua wawili kwenye mchongo so wameshagawana hela na nyingine katumia hapo alibakiwa na elfu hamsini tu so kama vipi niongezee hiyo laki ili nipate kompyuta yangu. Nikaona huyu Eddy analeta utani sasa nilimuaga na kuondoka nikamwambia ngoja tutawasiliana. Nilirudi na kumweleza bro aisee kila mtu alishangaa. Basi ikabidi tuondoke kwenda kituo cha polisi. Kule kituoni polisi walishauri nikubaliane na Eddy nimuongezee hiyo laki halafu twende nae hadi kwa huyo fundi kompyuta na hapo ingekuwa rahisi kuwatia nguvuni wezi wote kwa pamoja. Kila mtu alikubaliana na hilo shauri tukapanga huo mchongo ufanyike kesho yake asubuhi tukarudi nyumbani.
Baadae nikampigia simu Eddy na kumwambia kua kesho itabidi twende huko mjini kwa huyo fundi kompyuta, mi sitaki maneno yawe mengi ntatoa hiyo laki moja kikubwa nipate tu PC yangu jamaa akafurahi sana na kunishukuru kwa kua muelewa. Kesho yake asubuhi ilipowadiwa ikabidi bro atangulie kituo cha polisi akachukua maaskari wawili wakawa stand by na mimi nikachukua boda nikapita kwao Eddy akapanda pikipiki tayari kwenda mjini. Tulipofika pale kituoni nikawapa ishara safari ikaiva kwenda mjini. Sisi mbele wao nyuma bamba to bampa... Eddy hakujua kama nina "kampani" ya kikachero.
Tulipofika pale town, Eddy akasema nimpe hiyo laki akaifate ile kompyuta ili kuepusha jamu ofisini kwa fundi kompyuta lakini mimi nilikataa kua hilo haliwezekani lazima twende wote vipi kama huenda ukaniletea kompyuta ambayo sio ile yangu? basi akashindwa kujitetea ikabidi tuongozane twende wote. Wakati huo bro na wale maaskari wawili wanatuchora tu. Basi tulienda na Eddy hadi kwa yule fundi kompyuta bro yeye akajificha ila wale polisi wakaja pale ofisini kama wateja wa kawaida na kukaa. Usingeweza kuwatambua maana walivaa kiraia tu. Basi yule jamaa akaileta ile kompyuta aisee nilipigwa na butwaa. Ilikua ni ileile nikaikagua na kuthibitisha kua ni yenyewe pale pale wale askari wakaweaka Eddy na fundi kompyuta chini ya ulinzi ni kama movie hakuna aliyetegemea tukio lile. Yule fundi kompyuta akataka kukimbia lakini hakujua anacheza na makamanda ngangari wa kamanda Siro alichotwa mtama akadondoka kama gunia la korosho linapotupwa kwenye rori kule masasi akatulia tuli. Watu pale mtaani wakabaki wanashangaa tu lile tukio wale polisi wakawapigia polisi wa pale mjini. Dakika nne nyingi kitu defender ikatua pale wakapandishwa moja kwa moja hadi kituoni.....
Hapo kati kuna mambo mengi yalitokea ilibidi twende hadi mahakamani but to cut off the story nilikabidhiwa PC yangu nami sikuona haja ya kuendelea na kesi ukizingatia Eddy alikua rafiki yangu japo ndo hivo aligeuka Yuda Iskariote akanisaliti ila nilimsamehe tu mambo yakaisha.
Jambo moja ambalo nilipenda kujua naamini hata wewe ungependa kujua ni jinsi gani Eddy aliweza kuniibia PC bila kuvunja mlango wala kufuli. Kumbe ilikua hivi kumbe jamaa alikuaga amenunua kufuli kama lile nalotumia so akuwaga amenibadilishia bila mi kujua so alikua na access ya kuingia ghetto kwangu na kufanya chochote kile, thus why alikuja kuiba PC na kusepa kilaini kabisa siku ile nimeenda kucheki mechi ya usiku. Dah nilimkubali kua alitumia akili mingi sana kama majasusi ya KGB ila tatizo alichokosea ni kushindana na ngome ya CIA bora angejaribu kwingine. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mwisho.
Kwa sababu ni story tu not true..50/50 situation, umemla demu wa baraka yeye kala pc yako.
Sema story yako ina ngono nyingi mpaka inapoteza lengo sasa.
Acha uvivu!Ndefu sana naombeni Samaritan puliiizz!
Usiumize kichwa mkuu hii ni story ya kutunga tu japo kajitahidi..Mkuu samahani hapo sijaelewa vizuri, kwamba alinunua kufuli akakubadilishia, je funguo ziliingiliana? Kama ziliingiliana kwanini asingefungua tu hadi akabadili kufuli?
Jamaa alinunua kufuli kama ile niliyokua natumia so alinibadilishia hadi funguo kumbuka alikua rafiki yangu. Na hilo alilifanya siku nyingi kabla ya tukioMkuu samahani hapo sijaelewa vizuri, kwamba alinunua kufuli akakubadilishia, je funguo ziliingiliana? Kama ziliingiliana kwanini asingefungua tu hadi akabadili kufuli?
Simulizi ndefu kidogo ndio nzuri,unasoma mpaka unatosheka.Ndefu sana km RELI
oWe.kajamaa umewah pima ukimwi kweli manaa Kwa stori Yako ulikua una mtandao wa ngono mkubwa sana