Mkasa wa Joseph Kasella Bantu na Picha ya Waasisi wa TANU

Mkasa wa Joseph Kasella Bantu na Picha ya Waasisi wa TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
Miongo minne iliyopita...
Hiyo makala "Now You See Him Now You Don't," yenye jina True Muslim huyo ni Mohamed Said.

Baada ya makala hii sikuficha tena jina langu.
Hii makala Ally Sykes aliisoma na ilimgusa sana moyo wake.

Nilikuwa nimemueleza mwanae mmoja kuwa nimeandika makala hiyo na yeye akamueleza baba yake.
Ally Sykes akamtuma mwanae aniite nikamuone.

Hii ndiyo siku aliyoniahidi kunionyesha Nyaraka za Sykes.
Katika makala hiyo kuna picha mbili za waasisi wa TANU

Picha moja yumo Kasella Bantu na nyingine hayumo.

Katika ile picha ambayo hayumo ile ndiyo picha yenyewe halisi na katika picha hiyo Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu walikaa pembeni kuhofia wasifukuzwe kazi na serikali kwa kuasisi chama cha siasa.

Kasella Bantu baada ya uhuru akapachika picha yake kati ya Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz ili aonekane.

Hapa ndipo lilipoanza tatizo la picha hii ya waasisi.

Katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere kuna maelezo ya picha hii lakini inasikitisha kwani yamekosewa.

Tatizo limezidi kuongezeka.
Huu ndiyo msukosuko wa historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

1784144123778.png
1784144154104.png
 
Makala iliandikwa na true muslim. Kwanini ulificha utambulisho wako!
 
If I may quote you, in your article you wrote that "...Abdul Waheed Sykes and Dossa Aziz then invited their friend Julius Nyerere to join the TAA. They together with many prominent muslims went out of their way to make him accepted in the largely muslim country".

My question is, do you have evidence to support your assertion that Tanganyika, then, was a largely muslim country?
 
Msingi wa TANU ulijengwa na watu waliokuwa na lack of full commitment kwa sababu ya maslahi yao binafsi.
 
Gagnija,
Hili suala huwa sipendi kulizungumza na sababu ni kuwa linazua hamaki kubwa na mtafaruku usiio na sababu.

Lakini nitakuwekea hapo chini In Shaa Allah yale niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

About two-thirds of East African Muslims reside in Tanzania[1] which is the most populous of the East African countries, i.e. Kenya, Uganda and Tanzania. This includes Zanzibar-a predominantly Muslim country with a 99% Muslim population and once the centre of Islamic ​
learning in East and Central Africa. According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara. But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.​
This was the last population census showing religious distribution. It is widely believed that the figures for the 1967 census were doctored for political reasons to show that Muslims were trailing behind Christians in numerical strength. There is evidence that the government in 1970, having realised that Muslims were a majority in Tanzania, directed the Statistical Department to destroy all the 1967 census results. [2] ​
Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these facts. Different sources provide different Muslim-Christian religious distribution figures. These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue. Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[3] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy. Tanzania is of no exception. D.B. Barret[4] gives figures which show Muslims as a minority in Tanzania. The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [5] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982. Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view. [6] ​

[1] August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Miannapolis, 1980, p.11.
[2] See Family Mirror, Second Issue, November, 1994, p. 6.
[3] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competititive Religion: Between Revivalism and Expansion’, in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.
[4] D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa ,Nairobi, 1976.
[5] Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.
[6]The only conclusive Muslim research is by Dar es Salaam University Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and Islam in Tanzania', in Al Haq International (Karachi) September/October 1992.
 
If I may quote you, in your article you wrote that "...Abdul Waheed Sykes and Dossa Aziz then invited their friend Julius Nyerere to join the TAA. They together with many prominent muslims went out of their way to make him accepted in the largely muslim country".

My question is, do you have evidence to support your assertion that Tanganyika, then, was a largely muslim country?

Msingi wa TANU ulijengwa na watu waliokuwa na lack of full commitment kwa sababu ya maslahi yao binafsi.
Marco...
Watu gani hawa na maslahi yapi waliyokuwanayo.

Hili jambo jipya kwangu ningependa kujifunza.
 
Gagnija,

​
​
​
Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [5] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. ​

Hizi takwimu zinahitaji uhakiki huru kuweza kuaminiwa. Miaka hiyo ya 1970 watanzania zaidi ya 70% waliishi vijijini. Huko vijijini zaidi ya 80% walikuwa wakristu % inayobaki ndio wapagani na waislamu.

Kijiji nilichokulia mimi miaka hiyo, yalikuwepo makanisa mawili ya Anglikana, moja la katoliki na moja jingine la wasabato. Haukuwepo msikiti japo walikuwepo waislamu wachache sana ambao hawakupata hata fursa ya kupata elimu ya dini yao.

Ingefanyika sensa kijijini hapo, zaidi ya 90% wangekuwa wakristu. Hali haikuwa tofauti sana kwenye vijiji vingi nchini. Wakristu walizingatia umisionari wakati waislamu walijikita mijini.
 
Ndipo nilipokutahadharisha tokea mwanzo.
Ngoja nikupe moto uliowaka katika mhadhara niliofanya University of Iowa, Marekani mwaka wa 2011.

Nilikuwa naeleza Uislam Tanganyika jinsi Waislamu walivyopambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha kisha na Waingereza kupitia siasa.

Sihitaji kueleza haya sana hapa kwani yanafahamika.

Nikaeleza elimu ilivyoingia mwanzo Pwani ya Afrika Mashariki kupitia madrasa na Waislamu kuwa watu wa kwanza kuelimika na kuwa na zile 3RS (Reading, Writing and Arithmetic) nikisisitiza kuwa elimu haikuletwa kwa Waislamu na Kanisa.

Nikaeleza njama za kuupiga vita Uislam mfano wa kupiga marufuku hati za Kiarabu zilizokuwa zikitumika na kuleta Roman Alphabet, nikaeleza kubadili historia ya Waislamu kwa kufuta majina ya Kiislamu na kuweka mengine mfano Nduna Songea Mbano jina lake la Abdulrauf likafutwa, Mkomanile mwanamke pekee jemadari wa Vita Vya Maji Maji jina lake la Khadija likafutwa, Mtwa Mkwawa jina lake la Abdallah likafutwa nk. nk.

Hapa nazungumza na wataalamu wa African History kutoka vyuo mbalimbali Marekani.
Hawakujisikia vyema kwa kuwa haya hawakuwa wanayajua.

Wanasomesha kitabu cha Abdul Sykes lakini haya humo hayamo.

Wakati wa maswali na majibu.
Mashambulizi dhidi yangu yakawa makali sana.

Bado dakika kama tano hivi kumaliza muhadhara wakawa wamenitegea swali ambalo wao waliamini litawarudishia heshima yao.

''Tanzania Waislam ni wachache na ushahidi ni takwimu za CIA.''
Jibu langu lilikuwa Takwimu za CIA ni propaganda.

Nikawaeleza kuwa hata mimi nina takwimu lakini mtazikataa kwa hiyo sitazitoa hapa ingawa zimo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Takwimu za CIA ni propaganda kwa kuwa ingekuwa Waislamu ni wachache harakati za kupambana na ukoloni zisingeongozwa na Waislamu.

Nipeni mfano wa nchi moja duniani ambayo uhuru wake ulipiganiwa na wachache (minority) na hao wengi wakawa pembeni.

Mnakijua kitabu cha Abdul Sykes.

Ukweli wote umo mle.

Naomba jina la nchi moja tu ambayo harakati za kupigania uhuru ziliongozwa na minorty.
Ukumbi ulikuwa kimya.

Nimeshuka nimekaa kwenye kiti changu ukumbi umejiinamia.
Hapakuwa tena na swali.

Jonathon Glassman Mkuu wa Idara ya African History, Northwestern University akanifata nilipokuwa nimekaa akaniambia, ''Mohamed nakuomba twende chuoni kwangu ukatoe muhadhara kama huu.''

Nilikwenda na nikazungumza Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

1784214133313.png

Prof. Michael Lofchie University of Iowa anaijua Tanzania na historia yake.
 
Marco...
Watu gani hawa na maslahi yapi waliyokuwanayo.

Hili jambo jipya kwangu ningependa kujifunza.
Ally Sykes, Tewa Said Tewa, na Kasella Bantu, hawa walikuwa miongoni mwa vijana walioanzisha TANU, maslahi yao ya awali yalikuwa usalama wa kazi ,walikuwa watumishi wa serikali ya kikoloni na waoga wa kufukuzwa kazi au kufungwa.

Hii ndiyo sababu walijitenga kwenye picha ya awali ili wasionekane hadharani kama waasi.
 
Haya nimeyaeleza.
 
Naelewa Mkuu, nimerudia kuyajibu ili kukuelewesha kuwa hoja yangu pia ilikuwa ndiyo hiyo.
Marco...
Hukupata kuwajua watu hawa ndiyo maana umekuwa mwepesi wa kuhukumu.

Abdul Sykes akimjua Jomo Kenyatta na kuzungumza katika vikao vya siri Nairobi 1950 akiwa kijana mdogo wa miaka 26.

Ally Sykes akihudhuria mikutano ya siri ya Mau Mau Nairobi 1947 kijana wa miaka 21.

Ally Sykes akiandikiana barua na Kenneth Kaunda 1953 huku Tanganyika hakuna amjuae.

Yote haya yamo katika Tanganyika Intelligence Summary taarifa za Special Branch.

Yapo mengi.

Wakati mwingine huamua kukaa kimya kuanua ngoma juani.
 
Marco...
Prof. Haroub Othman alipata mshtuko aliposoma kitabu cha Abdul Sykes.

Aliomba kuonana na Mwalimu Nyerere kutaka kujua kama niliyoandika ni kweli:
Alifanikiwa kuonana na Nyerere? Kama alifanikiwa, maoni ya Nyerere kwa kitabu chako yalikuwa yapi?
 
Alifanikiwa kuonana na Nyerere? Kama alifanikiwa, maoni ya Nyerere kwa kitabu chako yalikuwa yapi?
Gagnija,
Haya ninayokueleza akanieleza Prof. Haroub mwenyewe.

Prof. Haroub alimwambia Mwalimu kuwa kitabu changu kimebadilisha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na pia historia yake Mwalimu Nyerere.

Watu wanasoma historia ambayo haikuwapo na kubwa ni mchango wa Waislamu katika kumuunga mkono yeye na wao kuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru.

Prof. Haroub Othman akasema hii historia haikupatapo kuwepo.

Prof. Haroub akasema hii historia ndiyo iliyopo hivi sasa na imefuta historia ya zamani ambayo iliaminisha watu kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika inazunguka kwake Nyerere peke yake.

Kwa kuhitimisha Prof. Haroub akamwambia Mwalimu itakuwa vizuri endapo na yeye ataandika kitabu cha maisha yake ili ukweli ufahamike.

Prof. Haroub hakunieleza maoni ya Mwalimu kuhusu kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kitu kimoja kilichokuwa wazi na kumstaajabisha Prof. Haroub ni ule urafiki na udugu uliokuwapo baina ya Nyerere na Abdul Sykes na nduguze.

Bahati mbaya Mwalimu hakuandika historia ya maisha yake.
 
Back
Top Bottom