UPDATE-2: MONDAY 11TH JANUARY 2021
(TUNARUDI KIDOGO KULE KWA SIKU ZOTE, “KANISA A”)
TUKIO LILILOTOKEA JANA KANISA A, (LA TATU) NA LINALOSHAHIBIANA NA MENGINE MAWILI AMBAYO YAMEWAHI KUTOKEA NYUMA ILA KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI
Kuna J2 moja mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya pili, kiongozi mmoja (mhusika wa manunuzi ya Sanitizer), alisimama madhabahuni kutoa tangazo muhimu lililohusiana na zone za waumini wote wa Kanisa A
- Zone hizi huwa ni vikundi vidogovidogo vya waumini kwa ajili ya maombi na kujifunza neno la Mungu, na wanaoishi eneo moja au sehemu moja kama vile labda tuseme Riverside au Ubungo Kisiwani
- Zone hizi huwa zinahusisha vikundi vya familia kuanzia takriban tano na kuendelea, na huwa zina ukubwa kulingana na idadi ya waumini ilivyo kwenye eneo husika wanaloishi
- Waumini wakizidi idadi ya juu inayotakiwa kwenye vikundi hivi, zone hiyo husika hupelekea kuzaliwa kwa zone nyingine mpya; yaani zone hiyo hutakiwa kugawanywa mara mbili
J2 ya tangazo husika, kiongozi huyo alisimama madhabahuni na kuanza kusoma majina ya zone zilizopo Kanisa A na hatimaye kuwaomba washiriki wa kila zone husika kukusanyika sehemu moja kwenye eneo ambalo kiongozi huyo alielekeza, ila ndani ya uzio wa nyumba hiyo ya Ibada
- Zone ya mhusika iliposomwa, wao walielekezwa wakutane upande wa kulia wa madhabahu, au kushoto kwake yeye aliyekuwa amesimama madhabahuni
- Ili mtu aliyekaa ndani ya nyumba hiyo ya Ibada aweze kufika sehemu hiyo aliyoelekeza kiongozi huyu Zone ya mhusika wakutane, inabidi apite na kukanyaga sakafu ya mbele ya madhahabu, ambapo watu huwa wanasimama pindi wanapokuwa wameitwa kupita mbele ya madhabahu
- Mhusika alinyanyuka kutokea pale alipokuwa amekaa na kuelekea kule ambako alikuwa ameelekezwa kukutana na wenzake, yaani kulia mwa madhabahu, akiipita na kuikanyaga sakafu iliyoko mbele ya madhabahu hiyo
Kabla ya tangazo hilo, awali siku hiyo mhusika alipokuwa amewasili Kanisani hapo akiwa anatokea nyumbani,
alipitia kwanza kwenye banda au Kanisa la watoto, kabla hajaingia Kanisani ndani
Hilo likawa tukio la kwanza
Tukio la pili la iana hiyo lilitokea tena siku ambayo wanaume walitakiwa kukutana kwa dharura J2 moja, ili watoe sadaka ya elfu kumi (au chochote kile walichokuwa nacho hata chini ya hiyo pesa). Tukio hili ameshawahi kulitolea ufafanuzi wake wa kina ndani ya uzi huu
- Sadaka hiyo walitakiwa kuitoa wanaume wote ndani ya mwaka 2020 kabla haujapita
- Ni kwa sababu sadaka hiyo ilikuwa inaonekana kuchelewa na hivyo ndiyo maana tangazo la dharura lilikuwa ni muhimu
- Ilikuwa ni mara baada ya Ibada ya kwanza
- Mhusika alikuwa amehudhuria Ibada ya pili lakini wakati tangazo linatolewa, alikuwa tayari ameshafika Kanisani
- Kikapu cha sadaka kiliwekwa mbele ya madhabahu siku hiyo na watu wakaanza kupita mbele wakitoa sadaka
- Mhusika naye pia aliipita mbele ya madhabahu akikanyaga sakafu iliyoko mbele ya madhabahu na kwenda kutoa sadaka hiyo
Siku hiyo vile vile, alipowasili akiwa anatokea nyumbani
, alipitia kwanza kwenye banda au Kanisa la watoto, kabla hajaingia ndani Kanisani, sawa sawa kabisa na kama alivyowahi kufanya kwenye tukio lile la kwanza ambalo amelielezea hapo juu
Hilo likawa sasa ni tukio la pili
Tukio la tatu na la mwisho limetokea jana JUMAPILI YA TAREHE 10/01/2021
MAELEZO YA TUKIO LENYEWE: ILIKUWAJE?
Mara baada ya Ibada ya pili kumalizika, kuna tangazo muhimu lilitolewa ambalo details zake mhusika asingependa kuziongelea humu. Na illi mtu aweze kutimiza matakwa ya tangazo hilo jana, ilikuwa inambdi apite mbele ya madhabahu halafu, apititlize hadi kulia kwa madhabahu, kule ambako Zone ya mhusika iliwahi kukutana kwenye lile tukio la kwanza ambalo ameshalielezea hapo juu. Wakati tangazo linatoka, lilielekeza pia kwa uwazi kabisa kuwa sehemu aliyokuwa yupo ndani ya nyumba hiyo ya Ibada mtu aliyehusiana na tangazo hilo, ni hiyo
Kwa hiyo jana pia mhusika alipita mbele ya madhabahu akikanyaga sakafu iliyoko mbele ya madhabahu hatimaye kwenda kuonana na mtu ambaye tangazo hilo lilikuwa na uhusiano naye
Jana pia vile vile
, mhusika alikuwa mepitia kwenye banda au Kanisa la watoto, kabla hajaingia ndani Kanisani
MAZINGIRA MENGINE YALIYOJITOKEZA JANA J2 YA TAREHE 10/01/2021 YANAYOZIDI KUTOA IUSHAHIDI WA KILICHOELEZWA HAPO JUU
- Mhubiri alikuwa ni kiongozi yule ambaye ameanza kubuni mtindo wa kuhubiri maandiko matakatifu, mafungu yaliyo mengi au yote anayotumia, yakiwa yanasomwa na mmojawapo au baadhi ya watu awanaokuwa wamekaa kwenye hadhira ya waumini
- Katika kipindi chote ambacho mhusika amekuwa akimfahamu na kumuona mtumishi huyu akiwa amesimama madhabahuni, jJana ilikuwa mara ya pili kwa mtumishi huyu kuonekana akifundisha maandiko matakatifu kwa mtindo huu mpya
Wakati akiwa anahitimisha Ibada, mtuishi huyu alifanya mambo yafuatayo:
- Aliitoa wito wa wageni waliohitaji kuokoka na walijitokeza (mmoja au waiwili) na kupita mbele ya madhabahu
- Baadaye tena alitoa wito wa muumini mwingine yeyote yule mwenye hitaji lolote lile, kupita mbele ya madhabahu
- Walijitokeza waumini wengi kiasi wakapita mbele
- Mhusika yeye hakupita, japo mahitaji alikuwa nayo
- Ni kutokana na ukweli kwamba ilikuwa ni surprise kubwa kwake, kiasi kwamba mwanzoni hakuwa ameamini kama masikio yake yalikuwa yamesikia sawasawa
- Ni kwa sababu alikuwa hata hakumbuki ni lini mara ya mwisho aliwahi kuusikia wito wa namna hii ukitoka kinywani mwa mhubiri aliyesimama madhabahuni, kanisani hapo
Ni nadra muno kwa wito wa namna hii kutolewa Kanisani A
siku hizi. Tangu mhusika alalamike kuhusiana na swala la wazinzi kuonekana walikuwa wame-dominate madhabahu kipindi kirefu nyuma, tangia pale staili ilibadilika na kuwa dominated na wito za wageni wanaotaka kuokoka, ambao ameshawaongelea huko nyuma kwamba takribani asilimia tisini (90%) huwa ni mamluki, na wahubiri ambao wamekuwa wakitoa wito hizo muda wote huo, nao pia wanajua hilo siku zote. Vinginevyo kwa muda huu, Kanisa A lingekuwa linajaa hadi kwenye barabara ya morogoro
Kwa hiyo kwa ufupi J2 ya jana walianza wakaitwa wageni waliotaka kuokoka, baadaye tena wakaitwa waumini wote kwa shida yoyote ile.
- Baada ya waumini wote kuwa wameitwa hatimaye waliitwa watoto waliokuwa wanatarajia kuanza shule kesho yake, yaani leo
- Hawa wao hawakujitokeza hata mmoja na ilionyesha wazi kabisa kuwa mpango wa kuwaita watoto hawa ulikuwa ni wa dharura. Yaani ni mpango uliobuniwa ndani ya siku hiyo
- Ungekuwa umebuniwa kabla, watu wa aina hii wasingekosekana kwa sababu wangekuwa tayari wana taarifa in advance, lazima wangepatikana japo wachache
Baada ya miito yote hiyo kupita, hatimaye wakati wa matangazo ndiyo lilitoka tangazo ambalo liliwahusu baadhi ya waumini kuonana na mtu ambaye,
kwa mtu yeyote yule mwenye akili timamu, ilikuwa ni muhimu kuonana naye, japo haikuwa lazima. Mtu huyo alikuwa amekaa upande wa kulia kwa madhahabu na katika sehemu ambayo ili mtu aweze kumfikia, lazima apitie madhabahu mbele
HITIMISHO
Wito wa pili uliotolewa kwa muumini mwenye
hitaji lolote lile kupita mbele ya madhabahu wakati wa Ibada J2 hiyo, ulikuwa unam-qualify pia mhusika kufanya hivyo, ila hakufanya hivyo. Bado pia hapa anasisitiza kuwa hakumbuki ni lini mara ya mwisho, wito wa aina hiyo uliwahi kutolewa na mhubiri aliyesimama madhabahuni
Baada ya mhusika kuahirisha kupita mbele ya madhabahu kwa wito huu wa hitaji lolote lile, baadaye Ibada hiyo iilifika mwisho na hatimaye tangazo jingine tena ambalo nalo pia lilikuwa linam-qualify mhusika kupitia mbele madhabahuni, likatolewa.
Kwa hiyo, baada ya watu kutawanyika, mhusika alitembea akipita mbele ya madhabahu na baada ya hapo alipitiliza hadi upande ule wa kulia wa madhabahu ili kuonana na mtu husika na tangazo hilo.
Iwapo kama mhusika asingefanya hivyo, picha ambayo wangeipata watu walio wengi Kanisani hapo ni kwamba aidha ni kuwa mhusika tayari alishaonana na kuongea na mtu huyo kabla ya tangazo hilo, wakati kumbe hapana. Na kwa wale ambao walikuwa wanajua kuwa mhusika hakuwa amewahi kuonana na mtu huyo hadi kipindi tangazo hilo linatoka; kama wangemuona mhusika akiondoka bila kwenda kuonana na mtu huyo wakati tangazo alilisikia, basi watu hao wangeweza hata kudhani kuwa pengine mhusika ana tatizo fulani kichwani siku hizi ambalo bado hajaweza kuulifahamu
MUBARIKIWE TENA NA BWANA