UPDATE: 30 NOVEMBA 2020
BAADHI YA YANAYOJIRI MUDA HUU HAPO KANISA A:
MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZIMETENGENEZA FURSA NYINGINE KWENYE KANISA A, SAWA NA ILE ILIYOTENGENEZWA NA UJIO WA COVID-19 MWEZI APRIL 2020
Safari hii sehemu husika ni kwenye banda la watoto, ambalo huwa wanatumia kuabudu kama nyumba yao ya Ibada
- Utafiti kwa kutumia muda wa kutosha hatimaye umeonyesha kuwa kuna bonde lililoachwa kwa makusudi, kwenye banda la watoto ambalo linatuamisha maji mengi kiasi, na hivyo limetengenezwa na kuachwa hapo makusudi
- Bonde hilo limeachwa pembezoni mwa banda hilo na hivyo kupelekea maji kujitenga na kusababisha baadhi ya watoto kuingia bandani kwa kukanyaga juu ya makreti ya soda yaliyopangwa chini ili kuwakinga wasikanyage maji
- Watoto wanaoingia bandani kwa mtindo huo ni wale tu ambao wana uwezo wa kukanyaga juu ya makreti hayo, wengine wasiokuwa na uwezo huo inabidi wakanyage kwenye maji
- Bonde hilo linalotunza maji hayo pindi mvua inaponyesha, na limekuwa likitunza maji hayo tangu msimu wa mvua za mwaka huu uanze
- Hapo kabla bonde hilo halikuwahi kuwepo na hivyo hakuna maji yaliyokuwa yakijitenga hapo siku za nyuma
- Inaonyesha kama kuna ukarabati ulifanyika na hiyo sehemu hiyo ndiyo ikawa imejitengeneza hivyo kutokana na pilika pilka za kazi iliyokuwa ikiendelea mahali pale
- Kwa hiyo mafundi baada ya kumaliza kazi yao, hapakufanyika jitihada zozote za kulisawazisha na hivyo bonde hilo limeenfdelea kuwepo mpaka leo hii
Kwa utafiti mdogo sana wa kiroho ambao mpaka sasa mhusika ameshaufanya kuhusiana na maji yanayojitenga mahali hapo, ni kwamba
maji hayo yanafanya kazi sawa na kile kinyesi kilichokuwa kimeachwa kinatiririka kule kwenye chemba ya banda la wakubwa
Kwa hiyo kuna
kuna air base nyingine mpya ya mapepo imetengenezwa kwenye banda hilo la watoto, na carrier wa mapepo hayo safari hii ni watoto, wao ndiyo wanaoya-supply kwenye sehemu zingine ndani na nje ya nyumba hiyo ya Ibada, nadhani hadi hata majumbani kwao wanakoishi au majumbani kwa watu wengine
UTHIBITISHO JUU YA UWEPO WA KARAKANA MPYA YA MAPEPO KWENYE BANDA LA WATOTO
- Nyumba ya Ibada ya watoto hawa ni Banda, siyo nyumba
- Kwa watoto wa umri wao, na kutokana na tabia zao zilivyo, banda hilo linawafaa zaidi kuliko nyumba yenye kuta ambayo ingeweza kuwa-confine ndani
- Hii ni kutokana na ukweli kuwa watoto wa umri huo wanahitaji kukaa kwenye sehemu ambayo ina uwazi na yenye hewa ya kutosha ukizingatoa kuwa huwa wana pilika pilika nyingi sana muda wote
Kwa hiyo banda hilo linawafaa sana watoto hawa Kanisani hapo, kiasi kwamba pengine labda hapana hata haja ya kujenga nyumba kama Kanisa lao, kwa ajili ya ya Ibada zao.
Kwa hiyo kwa upande mwingine, maamuzi ya kuwatengenezea watoto banda hilo yalikuwa ni ya hekima sana.
Kwa hali hiyo basi ni wazi kabisa kuwa kuna gharama ya fedha, tena kubwa tu ambayo Kanisa A imewakwepa (na si kwamba wao wameikwepa)
ambayo walitakiwa waiingie kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Ibada kwa ajili ya watoto hao.
TATIZO AMBALO LIMEKUWEPO KWA MUDA MREFU KWENYE BANDA HILO LA WATOTO
Pamoja na sifa nzuri za banda hilo, bado kumekuwepo na tatizo kubwa kwenye banda hilo, na kwa muda mrefu, mithili ya lile lililokuwa likisumbua kwenye banda la watu wazima.
Wakati lile la watu wazima lilikuwa linasumbuliwa na kinyesi kilichokuwa kinavuja kutoka kwenye chemba, hili la watoto lenyewe lina tatizo tofauti na hilo, isipokuwa linatuamisha maji kwenye sehemu ya kuingilia
Ni kwamba sehemu ya kuingilia ndani ya banda hilo, inayotumiwa na watoto pamoja na walimu wao, kuna kama bonde ambalo linaweza kuwa lilitengenezeka wakati mafundi wanafanya kazi zao kwnye banda hilo
- Inaonyesha kama baada ya mafundi kumaliza kazi yao, hawakupewa maelekezo ya kuhakikisha kuwa wanalisawazisha ili maji yasiweze kutuama pale pindi mvua inapokuwa imenyesha
- Kwa hiyo mafundi hawakupatiwa resources za kuweza kulisawazisha bonde hilo
- Kwa hiyo bonde hilo lipo mpaka leo na linaonyesha kama “permeability” yake ni ndogo kutokana na ukweli kwamba kunaweza kukawa kuna chembe chembe za cement ambazo zilibaki zimesakafia pale chini, na ndizo ambazo zinasababisha maji yatuame pale kwa muda mrefu
Kutokana na hali hiyo basi,
bonde hilo limekuwa likituamisha maji pale tangu ukarabati wa mwisho wa banda hilo ulivyomalizika na katika kipindi chote cha mvua za msimu wa mwaka huu
MAISHA YA WATOTO NA WALIMU WAO KWENYE BANDA HILO
- Kwa mtu mzima, ili uweze kuingia kwenye banda hilo, inabidi utumie hatua kubwa, yaani hatua ndefu
- Hata hivyo, kuna baadhi ya sehemu ambazo hata hatua za mtu mkubwa haziwezi kutumika kwa sababu urefu wake unazidi hatua za mtu
- Kwa hiyo kwenye sehemu hizo, kuna makreti matupu ya soda, yamepangwa kwenye maji hayo na kuzama kiasi na kubakiza migongo juu
- Makreti hayo ndiyo yanayotumika sasa kukanyaga juu yake, halafu ndiyo mtu anapita na kuingia kwenye banda hilo
- Watoto pia, hasa wale wenye umri mkubwa kiasi, wanakanyaga kwenye makreti hayo
- Wale wadogo kabisa lakini ambao wana uwezo wa kutembea, inabidi walimu wao wawabebe na kuwaingiza kwenye banda hilo
- Wengine wale wenye umri wa kati, inabidi wakanyage kwenye maji hayo kwa sababu hata hayo makreti ya soda yaliyopangwa hapo, hayatoshi
- Still, hata wale watoto wenye uwezo wa kukanyaga juu ya makreti hayo, kuna wakati inabidi wayakanyage maji hayo inategemea na uelekeo ambao motto huyo anatokea kwa sababu kama ilivyoelezwa hapo juu, makreti hayo hayatoshi na yamewekwa kwenye kipande tu cha sehemu
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MAJI HAYO
- Maji hayo ni mengi kiasi na yanaweza kuwa hatari sana kwa baadhi ya watoto hasa wale ambao ni wa umri wa chini kabisa, isipokuwa tu uzuri ni kwamba watoto wa rika hili la chini kabisa, mara zote huwa wanakuwa karibu sana muda wote na walimu wao, na muda wote kunakuwa na walimu wapo pamoja na watoto
- Hata hivyo ukweli ni kuwa, kungekuwa na uwezekano wa kwamba walimu wote huwa wakati mwingine wanatoka kwenye banda hilo na kuwaacha watoto peke yao, maji hayo yana uwezo wa kuhatarisha maisha ya baadhi ya watoto na hata kusababisha upotevu wa maisha ya watoto, iwapo ikitokea mtoto akaanguka humo kwa bahati mbaya. Kwa uwingi wa maji unaotuama pale, uwezekano wa hatari hiyo unaweza kuwepo kwa kiasi kikubwa, sema tu walimu wa watoto ni waangalifu.Mashahidi wa maelezo haya ni walimu wote wa watoto hao
Hata hivyo Mungu azidi kuhimidiwa tu kwamba hali huwa haiko hivyo, muda wote walimu huwa wanakuwa na watoto, na wale wadogo kabisa muda mwingi wanakuwa wamewabeba
- Ni wazi kuwa maji yaliyotuama mara zote huwa ni chanzo kikubwa sana cha magonjwa ya kuambukiza. Kumbuka kuwa baadhi ya watoto wanayakanyaga maji haya wanapokuwa wanatoka na kuingia kwenye banda hilo, tena wengi tu
- Vile vile maji yaliyotuama, ni chanzo kikubwa sana cha mazalia ya mbu. Mpaka muda huu kuna baadhi ya waumini wa kike ambao huwa wanalazmika kuhudhuria Ibada za jioni wakiwa na khanga za ziada kwa ajili ya kujifunga miguuni wakati wa Ibada kama njia ya kuwawezesha kukwepa kung’atwa na mbu
- Mhusika hajawahi kuhudhuria mikesha inayofanyika Kanisani hapo, lakini nadhani hata wale ambao huwa wanafanya hivyo nao pia wanaweza wakawa wana ushuhuda wa ufasaha zaidi kuhusiana na swala hili la uwepo wa mbu.
- Hoja ya mhusika hapa ni kuwa ni kawaida kwa mazingira yetu kuwepo mbu, lakini bado hatuna haki ya kutengeneza kwa makusudi mazingira kwa ajili ya mazalia ya mbu
KIPINDI AMBACHO MAJI HAYO YAMEKUWA YAKITUAMA MAHALI HAPO
Hali hii ya maji haya yaliyotuama, imekuwa hivyo kwenye msimu wa mvua za mwaka pindi zilipoanza kunyesha, na mhusika anadai kuwa mara ya mwisho kukuta hali iko hivyo ilikuwa ni
Jumapili iliyopita ya tarehe 29 Novemba 2020.
Inaonyesha pengine waumini wenye watoto hao, labda hawatoi zaka na sadaka za kutosha kuuwezesha uongozi wa Kanisa A, kupata fedha za kutosha kusawazisha bonde hilo na possibly labda wengi wao wanamalizia pesa zao kwenye uzinzi, (maana uongozi huwa unawatuhu hivi) wanashindwa kutoa zaka na sadaka kama inavyotakiwa. Kwa hiyo watoto hao na walimu wao watajijua wenyewe na banda lao.
Vinafanyika vitu Kanisani hadi mtu unashindwa kuelewa kama kuna watumishi wa Mungu kwenye nyumba hiyo ya Ibada!
Hata hivyo, ukweli ni kuwa bonde hilo limeachwa hapo makusudi, kwa kusudi maalumu.
NYONGEZA YA MUHIMU
KUHUSU JUMAPILI IJAYO YA TAREHE 06 DESEMBA 2020 ALMAARUFU KAMA
“SIKU YA KUMSHIKA MKONO MCHUNGAJI”
Mhusika anaomba aongee machache kuhusiana na siku hii, akiihusianisha na uzoefu aliowahi kuupata kutoka Kanisa B, kule alikohamia mwaka 2014 akiwa anatokea Kanisa A
Kipindi akiwa bado yupo Kanisa A (kabla hajahamia Kanisa B); kwenye siku hiyo tajwa, mhusika alikuwa anashuhudia mambo yafuatayo kila ilipokuwa siku hiyo inawadia
- Zawadi zilitolewa kwa Kiongozi Mkuu (KM) ikiwa ni pamoja na kadi moja kubwa sana
- Zawadi zilikuwa zinatolewa pia kwa viongozi wengine wasaidizi isipokuwa wao kadi zao zilikuwa ni zile ndogo za kawaida, hazikuwa kubwa kama ile ya KM
- Ibada zilikuwa zinafanyika kwenye mfumo kama wa sherehe hivi, na si kama Ibada ya kumwabudu Mungu
Baada ya kuhamiia Kanisa B mwaka 2017, kila ilipokuwa inawadia siku hiyo, mhusika akaenda akakutana na mambo kadhaa yafuatayo hapa chini. Ni kati ya mambo ambayo Kanisa hili B atalisifu hata mbele ya uwepo wa Mungu (physical presence of God
Mhusika aligundua kuwa kwenye Kanisa B, siku hiyo haikuwa siku ya viongozi kupewa zawadi za fedha na vitu isipokuwa ilikuwa:
- Ni siku ya kuwaanda viongozi hao (pamoja na wake zao/ waume zao) kwa ajili ya utumishi wa Mungu kwa mwaka mwingine unaofuata
- Ni siku ya kuwaombea watumishi wote hawa na Ibada ya siku hiyo huhudumiwa na muumini mwingine yeyote wa kawaida, hata asiyekuwa na cheo chochote Kanisani
- Wakati wa Ibada, watumishi wote hawa (na wake zao/ waume zao) hukaribishwa kupita mbele ya madhabahu na kupiga magoti
- Baada ya hapo kiongozi anayehusika na huduma ya Ibadaa huanza kuwaombea huku akipita na kuwawekea mikono kila mmoja, (mtu na mke wake, mtu na mume wake) wakiwa wamepiga magoti mbele ya madhabahu, huku kanisa zima nalo likiwa llianawaombea
Hiki ndicho huwa kinafanyika Kanisa B kwa ajili ya kuwaandaa watumishi hawa kwa utumishi wa mwaka mwingine unaofuata, na hatimaye zawadi nazo huwa zinatolewa, ila ni by the way. Zawadi huwa siyo dili sana kanisa B.
Mpaka hapa sasa, waumini wanaweza kulinganisha namna ambavyo siku hizi mbili huwa zinasherehekewa kwenye nyumba hizi za mbili za ibada, kama ifuatavyo:
HUKO KANISA B, siku hii ni siku ya:
- Viongozi wote (na wake au waume zao) kupiga magoti mbele ya madhabahu wakiwa wameelekea kwenye madhabahu na kuombewa huku wakiwekewa mikono kwa ajili ya utumishi wa mwaka mwingine unaofuata
- Muumini yeyote yule aliyeteuliwa kuhudumu kwenye ibada ya siku hiyo, huwawekea mikono viongozi hao kwa ajili ya utumishi mwingine ulio mbele yao
- Kanisa zima kuwaombea watumishi hawa wakiwa wamepiga magoti mbele ya madhabahu
HAPA KWETU KANISA A siku hii ni siku ya:
- Kumshika mkono KM, kumpa zawadi na pesa
- KM kupita mbele ya madhabahu, si kwa ajili ya kupiga magoti ili awekwe wakfu tena kwa ajili ya utumishi wa mwaka mwingine unaofuta, hapana, bali apokee zawadi. Huwa anakaribishwa na ubavu wake pia kwa ajili hiyo tu ya kupokea zawadi
- Viongozi wengine nao pia huwa wanakaribishwa kwa minajili ile ile na kwa staili ile ile
Hapo kabla, kipindi mhusika hajahamia Kanisa A alikuwa anaona zawadi zinatolewa kwa KM zikiwa zimeambatana na
kadi moja kubwa sana, halafu wasaidizi wake walikuwa wanapewa hizi
kadi ndogo za kawaida.
Hata hivyo, tangu arudi kutoka Kanisa B mwaka 2017
amekuwa akiona zawadi zinatolewa kwa KM zikiwa zimeambata na kadi yenye ukubwa sawa na kadi za viongozi wale wenzake.
Hiki ndicho kinachoendelea kufanyika Kanisa A mpaka leo.
Tofauti moja kubwa sana iliyopo kati ya Kanisa A na Kanisa B ni kwamba ni kawaida kabisa kwa Kanisa B kumuona kiongozi amepiga magoti mbele ya madhabahu kwenye siku hii husika akiwa anaombewa na waumini, wakati kwa Kanisa A hiki kitu hakiwezekani na hakijawahi kufanyika hata siku moja. Yaani umuone kiongozi wa Kanisa A amepiga magoti mbele ya madhabahu? Hicho kitu hakipo
Hawa viongozi wa Kanisa A, inaonyesha kama:
- Wana upako wa hali ya juu muno, kiasi kwamba hawahitaji kabisa kupiga magoti mbele ya madhanbahu kwa ajili ya kuombewa na waumini ambao hawana cheo kama kile cha wao
- Wana uwezo wa kunena kwa lugha
- Hawajawahi hata siku moja na wao kuonekana wakiwa wamepiga magoti mbele ya madhabahu
Possibly, hao wengine wa kule Kanisa B, wao huwa wanapiga magoti mbele ya madhabahu kwa sababu pengine labda wao hawana upako kama ule wa wale wa Kanisa A. Kwanza hao wa kule Kanisa B huwa hata hawaneni kwa lugha na hivyo inawezekana wakawa hata hawana Roho Mtakatifu na ndiyo maana wao huwa wanapiga magoti mbele ya madhabahu
siku ya kumshika mkono mchungaji
HITIMISHO
Mhusika akiwa bado yuko Kanisa B alikokuwa amehamia, ilikuwa ni LAZIMA kumuona kiongozi mkuu kila alipokuwa akifika ASUBUHI kabla ya Ibada kuanza, akipiga magoti madhabahuni na kuanza kuomba, halafu baada ya hapo ndiyo Ibada inaanza. Vile vile viongozi wengine nao pia walikuwa wanafanya hivyo hivyo, walipokuwa wanaingia kwenye Ibada asubuhi
Huku kwetu Kanisa A, huwezi ukaona kitu kama hicho, watu ni viongozi Kanisani lakini utawaona wanajisondeka tu Kanisani utafikiri wanaingia chooni.
Zaidi ni kuwa kila siku asubuhi, huwezi hata siku moja, kumuona KM akiwa ameshaingia Kanisani na kuketi kabla ya Ibada kuanza. Yeye siku zote kawaida huwa ni lazima aingie kanisani wakati Ibada ya Kusifu na Kuabdu imeshaanza. Kabla ya hapo huwezi kumuona. Unajiuliza labda kwa sababu madhabahu iko kwenye banda haiko kwenye kanisa lenye kuta? Huwa anaingia tu tena kienyeji sana utafikiri ni mtu anaingia chooni
Mwisho kabisa ila si kwa umuhimu, kipindi mhusika aliporudi tena Kanisa A (safari hii akiwa ametokea Kanisa B) , alijaribu kuwasiliana na kiongozi mmojawapo wa Kanisa A (siyo KM) wakati kama huu ilipowadia wa siku kwa ajili ya wachungaji, kwamba waifanye kama ambavyo huwa inafanyika huko Kanisa B alikokuwa ametokea, kwamba viongozi na wake zao au waume zao, (wa Kanisa A) nao wawe wanapita mbele ya madhabahu, wanapiga magoti na kuombewa.
Baada ya hapo, kilichotokea ni kwamba huyu kiongozi mhusika aliongea naye wala hakuonekana kabisa siku hiyo, wakati kawaida alitakiwa awepo, na utaratibu huu alioushauri mhusika wala haukufanyika.
Kwa wale ambao wamekuwa wakimfuatilia mwandishi tangu kipindi kirefu nyuma, kiongozi huyu anayemwongelea hapa ni yule ambaye aliwahi kusema
“ukiona watu wanaanza kulalamika Kanisani ujue wamekosa kazi ya kufanya” Kiongozi huyu hakuhudhuria siku hii tajwa mwaka 2017, hakuwepo
Ukweli usiopingika ni kuwa viongozi wa Kanisa A wapo kwa ajili ya kupita mbele ya madhabahu (na wake zao) ili wapokee zawadi, hawapo kwa ajili ya kupita mbele ya madhabahu ili waombewe na kuwekewa mikono kwa ajili ya huduma iliyoko mbele yao na kwa ajili ya utumishi wa Mungu.
Hawa wa Kanisa A wao utumishi kwao wao ni by the way.
“kikubwa kwao ni mbesa”.
Still, inaonekana kama labda pia hayupo muumini mwingine wa kawaida aliye na upako wa kuwaombea viongozi hawa, isipokuwa wao pekee tu ndiyo wenye upako wa kuwaombea wengine na si wao kuombewa na waumini wengine
Na kwa staili hii ya viongozi hawa wa Kanisa A, LAZIMA TU BANDA LA WATOTO LIFURIKE MAJI na lazima tu watoto wawekewe makreti ya soda kwa ajili ya kukanyaga ili waingie bandani
Kama banda lenyewe tu linageuzwa kichaka cha mapepo kiasi cha hadi kufikia hatua ya kuyaweka maisha ya watoto wadogo hatarini, utumishi wa watu hawa uko wapi?
Kama mhusika yuko sahihi, Mungu lazima ataendelea kujibu maombi yake, na kama hayuko sahihi, basi Mungu atawabariki sana watumishi hawa
MUBARIKIWE TENA NA BWANA