Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Umeeleweka vyema mkuu, piga kazi
 
Ombi kwako mkuu mleta mada, pindi utakapoimaliza kuisimulia yote, nitaomba audios za stori nzima, kama hautojali mkuu wangu, shemejiyako mvivu kusoma ila kusikiliza itakuwa rahisi, nami kuhadithia kila kitu siko vizuri.
 
Mashuka nayo taratibu,asnt sn kwa uji huu
 
Ombi kwako mkuu mleta mada, pindi utakapoimaliza kuisimulia yote, nitaomba audios za stori nzima, kama hautojali mkuu wangu, shemejiyako mvivu kusoma ila kusikiliza itakuwa rahisi, nami kuhadithia kila kitu siko vizuri.
Utani pm ndugu yangu zipo
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa​



Sehemu ya 18


Ukipata fursa ya kusikia mikasa iliyowakuta wanadamu kiukweli kuna watu wamekutana na vitu vingi,mikasa mingi katika maisha yao,watu wamebeba vitu vingi ndani ya mioyo yao nami kama Rojas naelezea yale ambayo yamenisibu ili msomaji wangu nawe uweze kujua ya upande mwingine wa dunia,kinachotesa sasa hivi ni huu msiba,naumia sana kwani katika vitu ambavyo nimezungumza sana na mtu huyu na nikataka sana kujua lakini hakuwahi kuniambia hata siku moja,nilitaka kujua pesa alizitoa wapi? Mimi nakueleza leo jinsi matumizi yangu yalivyo makubwa,jinsi ambavyo nimekuwa nakitumia pesa zangu kwa namna tofauti tofauti lakini hata ukiniuliza hizi pesa ulizitoa wapi nitakwambia wapi nilipotoa lakini yule mtu aliyenipa je yeye amezitoa wapg? Hicho kilikuwa ni kitu kama fumbo kwangu na mtu huyu nimetengana nae kwa muda mrefu na hata nilipokuja mtu huyu alishaanza kuwa mdhaifu na sasa amepatwa na umauti.

Lakini katika vitu alivyoniambia ni "nimekusamehe wewe pamoja na kizazi chako,niliyafanya haya kwa mapenzi yangu tu mema" lakini hakunieleza wapi pesa ametoa na zaidi alisema "nenda ukatumie pesa,yafuate yale niliyokueleza" nilitamani mimi niwe mmoja kati ya watu ambao nitapata nafasi ya kumzika mtu huyu kwa heshima,najua ni mtu ambaye ni mfungwa,amekuwa akitumikia kifungo chake na amepatwa na umauti akiwa bado anatumikia kifungo chake lakini mimi nilisema mtu huyu kiu yangu,shauku yangu nimpumzishe mahali pa heshima,chochote nitafanya,nimekuwa nazungumza hii sentensi chochote ntafanya kwani tangu nimekuwa na pesa nimejua jinsi pesa inavyoweza kufanya vitu visivyowezekana japo kuna vitu haviwezekani hata kwa pesa lakini hivi ninavyovizungumza mimi vinawezekana,unapokutana na watu ambao mnaweza mkabargain nao kitu hata kama kutakuwa na mifumo flani ambayo ni migumu,wakakuletea ugumu lakini wanaweza wakafanya tofauti kwa sababu kuna pesa inapita hapo na pesa ina nguvu sana sana sana,ukiwa na pesa na ukaishi pesa utaelewa maana ya hii sentensi mimi nasema,kwako wewe mambo yasiwezekana ni machache sana,mengi yanawezekana,popote unaweza ukaenda,yoyote unaweza ukamface ukazungumza nae,unakuwa unajiamini isivyo kawaida hata unavyokuwa unatembea barabarani pesa inakupa ujasiri mkubwa sana kwahiyo nilisema hili ntaliweka sawa ili kuhakikisha mimi nakamilisha hilo.

Nilitimiza ahadi yangu kama vile nilivyotamani iwe ndivyo mimi nilifanya tena sikufanya tu katika hali ya mimi binafsi bali nilimchukua huyu mtu nakumpeleka mpaka nyumbani kwao,yaani kuusafirisha mwili na kuupeleka mpaka nyumbani kwao kule ambako mimi nilichukua pesa,mahali ambapo toka nimechukua pesa sikurudi tena,ni mengi yalitokea lakini pengine si muhimu sana kuyazungumza hasa ya kule lakini kiukubwa zaidi mimi nilifanikiwa hilo zoezi,nililifanya kwa unyenyekevu mkubwa sana japo katika mazungumzo ambayo tumewahi kuyazungumza aliwahi kuniambia "kuna siku utageuza kisogo chako na utakaporudi hautanikuta" nilimkatalia na hata sikupay attention kuzungumza nae kwahiyo hakuwahi kusema nikifa itakuwaje kwa sababu watu wanapoteza maisha wanazikwa,wanahifadhiwa tu na maisha mengine yanaendelea,unaweza kuwa na ndugu yako gerezani na haujawahi kumtembea hujui siku unaenda ibuka unashangaa mtu alishapoteza maisha,hakuma mawasiliano wengine wanahamishwa kwenda maeneo flani lakini kama unakuwa ni mtu wa kutembelea ndugvhata taarifa inapotokea mawasiliano yakawa rahisi kuweza kukupa taarifa bwana huyu mtu moja mbili tatu kama mimi ambavyo nilivyokuja kufanya awamu nyingine japo uko mwanzoni sikuwahi kufanya na ndio maana hata alipohamishwa gereza,hata alivyokuwa na afya dhohofu mimi sikujua.

Nimerudi kwenye maisha yangu kama kawaida kwa sababu mambo yameshapita,nilikuwa na muda kwelikweli unajua taratibu hizo mpaka kupumzisha mwili na nini kwahiyo kuna siku kadhaa nilizitumia kwa ajili ya hilo zoezi,nimerudi na siku zinazidi kusogea mbele niko hapa bado moyo wangu ulikosa amani kabisa,nakumbuka nilipata msukumo mimi,kuna mshkaji mmoja ambaye alikuwa karibu na mshkaji kule gerezani na yeye alibali kule gereza la mwanzo ambapo mimi na mshkaji tulikutana,nilisukumwa kwenda hata nizungumze nae mawili matatu,nilifunga safari nikaenda mpaka gerezani lengo tu angalau nizungumze na mtu huyu kwa sababu huyu mtu amekuwa karibu nae na natafuta kitu ambacho angalau kinaweza kikanipa unafuu kwa hali ninayoipitia sasa hivi ,hali ya kukosa amani ninayoipitia haielezeki,kuna watu pengine wameshapita katika situation kama hizo unakosa amani unasikia roho inaangaika tu yaani hapa kifuani unasikia kitu kiko hapa unaangaika ndivyo ambavyo mimi nilivyokuwa nasikia,nilipofika kweli nilibahatika kukutana na mtu huyo na alisikitika sana rafiki yake ambaye walikuwa wote gerezani kwa muda mrefu hayuko tena lakini aliniambia sentensi moja sentensi ambayo sikuwahi kuisikia mimi hata siku moja yaani sijawahi kusikia hata mtu huyu ambaye yeye ni marehemu kuniambia,hakuwahi lakini nilisikia kwa mtu huyu,aliniambia sentensi hii akitaja jina la yule mshkaji "unajua mshkaji alikuwa na nafasi kubwa sana ya kutoka,unaona ukimwambia habari za kutoka kuwa huru yaani atoke aende uraiani awe huru,kwa sababu kuna siku aliniambia umempa chance ya kupigania atoke lakini hakutoa ushirikiano lakini alikuwa na sababu kubwa sana" nikataka kusikia kwa sababu ni kweli mtu alichimbia pesa,yaani pesa zilikuwepo,pesa zipo uko zimekaa,amenipa nafasi hiyo mimi nimeenda kuchimba pesa na nimezimiliki na zimekuwa za kwangu,kwanini pesa hizi tusingefight yeye atoke,awe huru,nani hataki kuwa huru,nani hataki kuishi maisha ya uraiani uwe unaamua uoge saa ngapi,ule saa ngapi,maisha ya kupangiwa saa flani utakula saa flani utaamka nani anayapenda? Mwanadamu furaha yake ni kuishi maisha ya uhuru na ya amani lakini yeye ilionekana kama yatafanyika lakini sio sasa ni baadae,kwanini baadae na nafasi tunayo sasa hivi,tupigane tunapoweza na kama itashindikana tunawe mikono kwamba tumeshindwa,tumeshindwa basi haiwezekani lakini kuna bidii tumefanya,watu wangapi ambao walishakatiwa tamaa lakini mwisho wa siku wamekuja kuwa huru? Haijalishi ni miaka mingapi lakini hakuwa na ile shauku ya kusema atoke uraiani na hiki ni kitu nilikuwa namwambia kwanini yaani,kwanini yaani?

Ndio nasikia huyu mtu ananiambia,ananiambia "(akitaja jina lake)alikuwa anahofia sana kuuawa" nikashtuka "kuuawa? Kuuawa na nani? Akasema "amesema ni bora aendelee kuwa gerezani lakini aendelee kuwa hai ili aendelee kupata taarifa kuhusu watoto wake na akawa na furaha kwa sababu wewe ulizidi kumpa taarifa za kuhusu watoto kitu ambacho ndio alikuwa anakihitaji katika maisha yake kwahiyo kwa sababu ulikuwa unamfanyio hivyo ndio ilikuwa ni furaha kwake" nikamuuliza "kwanini alikuwa anahofia kifo,kwanini? Akanambia "hata mimi nimewahi kumuuliza sana lakini hajawahi kuniambia hata siku moja lakini ninachojua ni hofu ya umauti ndio uliokuwa unamsumbua" nilistuka na kuogopa kwelikweli kwa sababu tangu nimemfahamu mtu huyu hajawahi kuniambia,nikamwambia "natamani sana kujua" akanambia "mimi sijui chochote na mimi pengine naweza kuwa mtu ambaye najua mengi yake lakini sijui chochote"

Niliondoka nikiwa mnyonge zaidi "kwa sababu gani mtu huyu aliogopa,aliogopa umauti na akitoka uraiani anaweza akauawa bora akae kule aendelee kupata taarifa za watoto wake na mimi japo niliendelea kuwahudumia watoto kwa namna moja au nyingine lakini nilifunga ukurasa wa kumpelekea taarifa,kwahiyo kama mimi ndio alikuwa ananitegemea mpeleka taarifa,mpeleka habari kwamba watoto wameendea hivi na mimi sasa ndio nikakata mguu,sijui alipita katika mazingira ya kimaumivu ya kiasi gani,leo sasa ndio naona kama zaidi nilikosea,kumbe hiki ndicho mtu huyu kwake kilikuwa ni kikubwa kuliko vyote lakini ni nani hasa aliyekuwa anamuhofia,ni nani huyo aliyekuwa anamuhofia? Nikajikuta naanza kuwa na stress sana na zikawa zinanisumbua sana kwa sababu nikaanza kuogopa na mimi,kama yeye alikuwa anaogopa kutoka uraiani labda ni kwa sababu ya hizi pesa nami niko na hizi pesa lakini mbona siku zote niko na hizi pesa na nimetumia kwa mambo mengi sana mbona sijawahi kuona mtu ananifata au hata kunihoji kwamba hizi pesa ni za nani? Sijakutana na mtu kama huyo,yeye alikuwa anamuhofia nani?

Nakumbuka nina mshkaji wangu wa karibu aliona niko down sana na aliniambiaa "Rojas hauko sawa" nikamwambia "kuna kitu kinaniumiza sana kichwa najikuta nakosa raha kabisa" akanambia "ni nini? Nikamwambia "hata sijui naanzia wapi kukueleza lakini ni ngumu sana kukueleza ila nataka kupata majibu ya kitu ila sijui nani anaweza akanipa majibu,akaniambia "ni kuhusu mambo yako ya biashara? Rojas hujui kuna watu wanaweza kuviona vitu ambavyo kwa kawaida hauwezi kuviona? Nikamwambia "unamaanisha nini? Akajibu "eeh wako wataalam kuna kitu kinakusumbua na haukielewi unataka kupata majibu wako wataalam wanaweza kujua kwamba majibu ya hiki kitu ambacho unakiwaza ni haya hapa" kwa yale maneno yake akawa kama akanipa akili mpya hivi, "ndio ni wapi naweza kupata wa namna hiyo" akanambia "wapo,sasa hawa watu wanazidiana uwezo,sasa ngoja labda tuangalie nani anayeweza akakufanyia,ni nini hasa kwanza unataka kujua,vipi kwenye biashara unachezewa? Nikamwambia "sio kuchezewa ila sielewi mambo yangu jinsi yanavyoenda kwahiyo nataka ufafanuzi" akasema "ooh mambo ya biashara biashara wako wengi sana,sasa mimi ntakuconnect na mtu atakupa majibu ya maswali yako yote" kutokana na hali ya msongo wa mawazo alafu nimejikuta tu najiuliza maswali mengi alafu sina majibu.

Kweli mshkaji aliniambia "nakupigania kuhakikisha unapata mtaalamu kwelikweli" tukizungumza mtaalam huyu ni mtu anayefanya uganga,yeye alitumia lugha ya mtaalam mwenye uwezo,mtaalam ambaye anaweza akanipa majibu ya maswali yangu na mimi kwakuwa sikuwa mwepesi sana kumshirikisha kwakuwa najua waganga wakati mwingine uwa hawana siri pengine anaweza akamueleza lakini potelea mbali lakini mimi ninachotaka ni anisaidie,kwa sababu sikutaka kumshirikisha sana alinisindikiza lakini nikamwambia "wewe kaa tu hapa mimi ngoja niingie nizungumze nae" kwahiyo niliingia mimi peke yangu kwa mtaalam,huyu mtaalam akanambia "hapa ndipo jambo lako linapofanikiwa karibu sana" nikamwambia "nina shida ninapitia sana,sijajua chanzo cha haya mambo" lakini nilimwambia "mimi kuna mtu amenipa pesa,amenipa pesa kwa kunielekeza mahali pesa zilipo,nikaenda kuchukua hizo pesa,nikazitumia lakini akanipa masharti ambayo sikuwa nayaelewa na ikafika kipindi nikaona kama yule mtu aliyenipa pesa ananisumbua na kunipa msongo wa mawazo na nikbmua kuachana nae na kufocus katika maisha yangu mengine lakini huyo mtu amepoteza maisha sasa nimekuja kujua kwamba huyo mtu kuna vitu labda alikuwa anaviishi ambavyo alikuwa anavifanya siri na hakuweza kumueleza mtu" kwahiyo nikawa nasubiria mtaalam anipe majibu sasa kwakuwa nilikosa kupata majibu katika hali ya kawaida basi njia zipo nipate ufafunuzi ni nini kinaendelea,wao si wana nguvu wanaweza wakajua basi nami nijue na je wakijua wataweza kunisaidia ili moyo wangu ubaki na amani na vitu kama hivyo.

Nilimueleza haya yule mtaalam na nakumbuka huyu mtaalam alikuwa ni mtu mzima tu na nilielezwa yuko vizuri na niko hapa kutatuliwa kile ambayo nataka ufafanuzi nacho,mtu huyu kila nilivyokuwa namueleza alikuwa na karatasi na kalamu nyekundu na akawa anaandika maandishi ya kiarabu na michoro na akawa anazungumza maneno flani ambayo nadhani ni ya kiarabu na alipomaliza alinambia sentensi moja "hizi pesa sio zako" nikamwambia "ni kweli lakini aliyenipa alinipa hizi pesa kwa moyo mweupe" akasema "ndio hata mimi naona alikupa kwa moyo mweupe na hata yeye hizo pesa zilimtaabisha sana" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "eeh naona hizo pesa zimemtaabisha sana,ni kweli amezipata lakini ameishia mateso mpaka kifo chake ameishia kuteseka" nilishtuka sana kwa maneno hayo,katika vitu mimi nilikuwa na amani navyo na natumia hizi pesa kwa uhuru na nilifanya biashara na biashara zinaenda na kama kwa namna moja au nyingine mimi nakuwa sijafanya vizuri ni mambo yangu mimi,matumizi yangu mimi,matumizi yakawa makubwa zaidi kama nilivyokwambia ni starehe kwa kwenda mbele,wanawake zaidi ya saba na hapo kuna waliopangiwa vyumba,kuna wakulipiwa ada za chuo,wa driving school na mengineyo.

Nashtuka sana kwa yale huyu mtaalam anayoyaeleza na nikamuuliza "ina maana hizi pesa mimi nilizichukua kimakosa? Sikuwa na makosa yoyote kwakuwa huyu mtu alitaka msaada na mimi nikamsaidia na ndio maana nasema alinipa kwa mapenzi yake ya dhati,sijui zilimtaabisha kwa kiasi gani lakini ninachojua ni pesa halali ambazo sio za magumashi kabisa" akaniuliza swali "ni wapi umehifadhi hizi pesa? Hii ni siri ambayo simwambiagi mtu na mganga anauliza wapi nilikohifadhi pesa[emoji23] na nilishamwambia vitu vinavyonipa mashaka ni huyo mtu kutotaka mimi nipeleke pesa benki kwahiyo nikajikuta zile pesa ambazo nimeanza kuendeshea biashara ndio nilikuwa napeleka benki lakini zile pesa ambazo nilichukua kule nilikuwa natumbukiza kwenye vitu ambavyo vinatembea km kuagiza bidhaa moja kwa moja na si kupeleka benki,akaniuliza kwa mara nyingine tena "hizi fedha ni wapi umezihifadhi kwa sababu hapa naona natakiwa kufanya kitu kuna mambo mabaya yanaenda kukutokea" nikaogopa,nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "ndio,mambo mabaya naona yanaenda kukutokea na afadhali umekuja mapema ili nikupe msaada" nikamwambia "naomba unisaidie sana"akasema "nakusaidia na ndio maana nataka unipe majibu ya maswali ninayokuuliza kwani mimi sio mganga wakupindisha maneno yangu.

Mimi ni mganga ambaye nimefanya hii kazi kwa miaka mingi na nimewasaidia watu sio wa Tanzania tu hata wa nje ya Tanzania kusolve matatizo yao ambayo ni magumu yaliyoshindikana kwahiyo utamshukuru mtu aliyekuleta kwa sababu wewe hautakufa hata kama yeye aliyetafuta hizo pesa amekufa,wewe hautakufa na utashuhudia wajukuu na vitukuu vyako lakini inabidi uwe muwazi kwangu kwani tabia ya kuficha vitu ambavyo vinanifanya naanza kuhisi pengine unanidanganya utafanya kazi iwe ngumu" nikamwambia "kuna vitu nilishamuahidi mtu huyu sitamwambia mtu lakini nimejikuta katika harakati za maisha nazungumza,nilielekezwa na mtu huyo wapi nihifadhi hizo pesa ili ziwe salama na pamoja na mafanikio ambayo mimi niliyapata sikuwahi kuhamisha hizo pesa toka mahali ambako niliweka toka siku ile nilipozihifadhi" akaniambia "ni sawa vyote unavyosema,kuwa muwazi kwangu nikusaidie,ni wapi hizo pesa umehifadhi? Kiukweli sijui kwanini kwani nilikuwa mzito sana kusema pesa ziko nyumbani kwangu,nilipozihifadhi ni kwenye chumba ninacholala,nimechimba na kufukia pesa ila ukweli nilimwambia kuna pesa ambazo zinazunguka katika biashara,hizo sikuwa nazihifadhi ndani,akanambia "mbona unasitasita,unapokuja kwa mganga kwa mganga amini unatatuliwa mambo yako lakini na wewe unatakiwa kuwa muwazi lakini wewe unaonekana moyo wako ni mzito kusema ukweli na ndivyo ambavyo naona umauti unafata kwako baada ya huyo mtu mwenye pesa kupoteza maisha"



ITAENDELEA!
 
Nimeanza kuogopa mganga sio anataka kuzichukua hela zilizohifadhiwa kweli?[emoji134]

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
T Bag alijikata mara ya pili baada ya mkono kushonwa.

Alikamatwa na kina Belick na Roy waliomnywesha dawa ili anye ufunguo alioumeza wa lock za jiji alipoficha begi lenye hela na baada ya kunya wakapiga simu polisi waje kumchukua T Bag kwenye nyumba waliyomfunga, ndio T Bag akaona hawezi kukamatwa kindezi bora ajikate kiganja chenye pingu asepe.
 
DB Cooper hakuwa tajiri ila alikuwa ni mfungwa aliyefungwa kwa kesi ya kuiba hela nyingi, Scofield alikalkuleti mambo yake na akawa na jibu kuwa Wesmoland ndio DB Cooper. Lengo la kumuweka kwenye mchongo wa kutoroka ni ili awasaidie pesa Scofield na lincoln watumie mbele baada ya kusepa USA.

T Bag hakuambiwa hela zilipo, aliyeambiwa ni Michael na mzee DB cooper mwenyewe, ila T Bag alikuwa karibu kwa hiyo alisikia map nzima. DB Cooper sababu alikuwa na kidonda kikubwa akaona hawezi kutoroka kwa hiyo akamwambia Michael aende kuchukua hela na amzike mwanae (mtoto wa DB Cooper) fresh kama ambavyo angefanya yeye DB Cooper.

Abruzzi aliwekwa kwenye mchongo sababu alikuwa anamtafuta sana mtu aliyemfanya afungwe jela (Fibernach), na jamaa alikuwa amemsnitch na kupata ulinzi wa CIA (Witness Protection), lakini Scofield aliweza kujua mahali Fibanachi alipo, akasema hamtajii Abruzzi, ila atamwambia watakapotoka nje ya jela, hivyo Abruzzi. Pia jamaa zake Abruzzi walikuja kumpiga mkwara akiwa jela wakasema wataua watoto wake akiwachoma, Abruzzi akaona hamna namna, inabidi atoroke ili aende kuilinda familia yake na kulipiza kisasi.

Fedha ya DB Cooper ilichimbwa na wote, Scofield, Sucre, C Note na T Bag ila sasa kwenye kuweka kwenye mabeg, T Bag ali-switch bags, moja aliweka vitabu na lingine hela, akawapa jamaa lenye vitabu yeye akaondoka na lenye hela
 
Ila Rojas anajichanganya sana, umeona jamaa alivyoficha Siri kwamba fedha alitoa wapi, mpaka amekufa ajamwambia Rojas. lkn Rojas ni mrahis sana kutoboka Kwa brother kuhusu fedha zilipotoka, maisha ni Siri, hakuna tajiri atakupa Siri ya mafanikio na Wala usitegemee. Maisha n Siri, story inamafunzo mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…