pretta360
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 632
- 1,005
Wa gerezaniRojas mwenyewe au nani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wa gerezaniRojas mwenyewe au nani?
Changamoto hiyo nimeiona ndugu nami najitahidi kufanyia kazi maoni yenu
Umeeleweka vyema mkuu, piga kaziNdugu hoja yako ina tija ila changamoto ninayoipata kwanza ninakubali urudiaji wa maneno unapunguza ladha,pili mimi ni mpya katika fani ya uandishi naomba kuvumiliwa ktk hilo na naamini kupitia ukosoaji chanya nami ntakuwa bora siku moja,tatu kama nilivyosema awali masimulizi yako katika mfumo wa sauti nami nayaleta ktk maandishi na msimuliaji anaswaga hizo nami najikuta ktk uandishi wangu naingia ktk mtego wa kurudiarudia maneno,nne kutokana na wingi wa maneno na kubanwa na harakati nyingine nakuwa nakosa muda wa kuweza kuhariri ingawa hata hayo unayoyasoma nimejitahidi sana kupunguza urejeaji wa matamshi,tano natumai nitakapoleta kisa kingine nitajitahidi kuzingatia hilo na mengine kadri nitakavyojaaliwa kwani hata ukitazama paragraph unajua tu huyu mwandishi bado Lena katika fani.
NB: Mfano sehemu ya 12 wakati nataka kuipost saa 12 jioni episode siioni ikanilazimu kuanza kuiandika upya na muda wa saa 4 hv usiku ndio nikaihitimisha na kuweza kuipost,sasa hapo hata kama kumekosewa neno inakuwa ngumu kurekebisha,tuvumiliane ndugu zangu natumai siku moja tutapata hadithi nzuri yenye mpangilio mzuri kuanzia uandishi hadi mvuto wa maneno kwani nakuwa nasikiliza na kuandika kwa kutumia simu,mbarikiwe wasomaji!
Mashuka nayo taratibu,asnt sn kwa uji huuMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
sdhemu ya 5
Katika maisha yangu ya kila siku nimekuwa ni mtu wa kujali sana matatizo ya jamii inayonizunguka na wanajamii kwa kiasi kikubwa walinifahamu hivyo kwahiyo nilivyokutana na huyu mtu gerezani na jinsi alivyokuwa nami kama kaka nimebeba hiyo roho yakuwa sehemu ya kwenda kumtembelea yeye mwenyewe na pia kuwatembelea watoto wake,huyu mtu yupo ndani lakini muda wote akili yake ipo uraiani anawawaza sana watoto wake,anawawaza sana wapo katika mazingira gani kwa sababu anajua mwanamke ambaye amepata nae hawa watoto akili yake kidogo haina utulivu,nakumbuka awamu hii nilipoenda nilienda kumpasha kuhusiana na maendeleo ya watoto wake kuwa wanaendelea vizuri na kumpasha habari nyingine nyingi nilizokuwa nazo kuhusu uraiani na harakati ambazo nimekuwa nazo huku nikimtia moyo huyu ndugu yangu kuwa asikate tamaa mambo yatakaa sawa wala asiwaze sana ajue tu familia yake inaendelea vizuri,katika mengi ambayo nilimueleza ya huku uraiani alinambia "nakuamini,nakuamini sana" nikamwambia "asante" akanambia "unajua niko huku gerezani ni muda sasa na sijawahi kukutana na mtu amenipa matumaini kama wewe,unajua niko huku gerezani toka yule mtoto wangu mdogo akiwa bado ni kichanga" nikamwambia "nakuelewa,nakuelewa" akasema "unajua ndugu zangu wamejua nimepotea huku,nimeishia huku sijawa na mtu wa kumuamini naomba nikuamini" nikamwambia "karibu na uwe na amani" baada ya maneno haya alinishukuru sana.
Shukrani ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wake kila tulipokuwa tukiongea na hata siku hii aliponishukuru sikuona kama ni jambo jipya kwakuwa amekuwa akiniambia mara kwa mara,akaendelea kunambia "toka ndani ya moyo wangu nimetokea kukubeba na kukupenda zaidi ya ndugu,naomba nikushirikishe jambo ambalo sijawahi kumshirikisha mtu yoyote katika maisha yangu,naomba nikushirikishe jambo ambalo nilikuwa nilifanye nikiwa uraiani lakini sikubahatika kulifanya" nikamuuliza "ni jambo gani" akanambia "linahitaji uaminifu baina ya mimi na wewe" nikamwambia "haina shida,haina shida" akanambia "basi nenda kajifikirie" nikamwambia "niambie tu wewe niambie lakini naweza kukusaidia kama si jambo baya" akanambia "wala si jambo baya" nikamwambia "sawa nieleze tu" nilimlazimisha anieleze kwa sababu nitakuja tena huku lini,lini ntakuja kwa sababu nami sasa hivi nimekuwa ni mtu ambaye napambana na mishemishe zangu unajua,akanambia "sawa,nataka nikubadilishie maisha yako" nikatabasamu,nikamwambia "mimi? Unibadilishie maisha mimi?" Akasema "ndio,kwani mimi nikiwa gerezani nashindwa kubadilisha maisha ya mtu mmoja uraiani?
Nikacheka na nikamwambia "hata sikuelewi unamaanisha" akasema "namaanisha ninachokisema,unakumbuka nilikwambia umekuja gerezani kwa ajili yangu?" Nikatabasamu na kumwambia "unajua sikuelewi unachosema" akasema "utanielewa" katika harakati zangu nilitamani maisha mazuri,nilitamani maisha mazuri,maisha bora lakini sikuweza kutimiza ndoto zangu najikuta niko katika maisha ambayo sikuwahi kuwaza kama nitaishia uko lakini pengine maisha yangu naweza nikamalizia uko,sijui ni neema gani yaweza ikaja kwangu na nikatoka,nikamwambia "kwanini unasema hivyo,kwanini unasema hivyo na wakati haya mambo tumeshakaa na tukayazungumza unatumikia kifungo chako na kina miaka tajwa" akasema "hauwezi kuelewa,elewa hili ninalosema nataka kukubadilishia maisha yako na ulikuja gerezani kwa ajili yangu" alinambia nirudi nyumbani na niendelee na harakati zangu na nije tena,nikamwambia "unaniweka njia panda sana mshkaji wangu sielewi hata unachomaanisha,hivi mtu aliyeko gerezani anawezaje kumbadilishia maisha mtu niliyeko uraiani? Ambapo mimi napiga mishemishe,napambana na maisha,ujue gerezani mtu unakaa tu,unakaa tu unawezaje kubadilisha maisha yangu mtu namna hiyo?" Alinambia tutangea na kunisisitiza nisiache kwenda kuwatizama watoto wake nami nikamwambia "usiwaze kuhusu hilo na uwe na amani tu ujue umepata mdogo wako ambaye yupo pamoja nawe hata kama uko gerezani uko pamoja na mimi,usiendelee kunung'unika kuhusu ndugu zako ambao wanaona wewe umeishia huku gerezani Mungu ana njia zake za kuinua ndugu basi ujue na mimi Mungu ameniinua niwe ndugu yako,nitafanya hayo kwa moyo wangu wa dhati" nilimwambia hayo na baada ya muda niliondoka zangu lakini niliyawaza maneno aliyonambia,mtu huyu ni mfungwa tu,mfungwa tu wa kawaida na katika nafasi nilipoingia hapa gerezani na nilipokuwa ninaishi hapa nilimuona ni mfungwa tu ambaye ni mtu mbabe mbabe kwa sababu sio mtu wa kuonewaonewa unajua maisha ya uko kuna watu wababe,watu ambao wana nguvu zao yaani yeye hakuwa mtu wa kuonewa na alikuwa mtu wa kutetea wengine kiufupi nilimuona ni mtu mwema kwa muda wote niliopata nafasi yakuwa nae gerezani lakini kwa habari yakunibadilishia maisha kiukweli ni kitu chakuchekesha unajua yaani nilikuwa nikicheka tu.
Nilirudi uraiani na maisha yalikuwa yanaendelea nilikuwa nikiendelea kupiga mishe zangu kwa sababu sasa hivi si haba japo sijapata gari rasmi napiga tu mishe za udeiwaka japo si haba napata chochote,toka nimetoka kule gerezani ulipita kama mwezi na nikapata nafasi ya kwenda kuwatembelea tena wale watoto,nilienda kuwacheki na kuwapelekea vizagazaga kidogo sawa na kipato changu ambacho napata,wakanambia "anko umekuja tena?" Hii sentensi huyu mtoto alikuwa anapenda kuniambia hivi nami nikamuuliza "ulidhani sitakuja tena? Akanambia "nilidhani hautokuja tena" nikamuuliza "kwanini?kwanini unawaza hivyo? Nilishawaeleza mimi ni anko wenu ambaye nitakuwa nakuja mara nyingi sana,mnaendeleaje?" Lakini pia niliwapelekea mahitaji ya hapa na pale kwa ajili ya shule na walifurahi sana na huyu mama sasa kishajua kama nakuja kwa ajili ya kuwatembelea watoto kwa ajili ya rafiki yangu ambaye alikuwa ni mtu wake ambaye hawako tena kwenye mahusiano kwa sababu wao wenyewe wanazijua,nilizungumza na watoto lakini pia nilizungumza na huyu mama na kikubwa nilimwambia "kwanini siku usitenge muda wa kwenda kumuangalia mwenzio gerezani" kwa mara ya kwanza nazungumza na huyu mama sentensi kama hiyo akasema "mimi nikapoteze muda wangu kudili na mtu aliyeniharibia maisha yangu? Nikamwambia "ujue watu ukosea lakini na watu hujirekebisha,unajua watu hujirekebisha sana wakiwa gerezani? Watu wanabadilisha nienendo yao na inawezekana alipokuwa uraiani hakuwa mtu mwema lakini kule ameshabadilika" akasema "hawezi kubadilika yule mtu,hawezi kubadilika yule mpaka mwisho wa dunia,hawezi kubadilika,mbaya yule kuliko unavyodhani na nashangaa unaangaika kumsaidia mtu yuko gerezani na ataozea uko,nakuangalia tu nione hatua zako zitaishia wapi" aliniambia hayo maneno yakunivunja moyo nami nakumbuka nilimwambia "mtu anaweza kuwa mbaya kiasi gani yaani hadi asiweze kuonewa huruma na kwenda kutembelewa" alinambia "mwanaume mbaya sana amenipotezea maisha yangu na kunipotezea muda,ebu tazama wakati mimi niko nae kumbe yuko na mwanamke tena amekwenda hadi kumtambulisha kwao naye ameshakwenda kutambulishwa hadi kwa huyo mwanamke na wako katika hatua flani za uchumba lakini mimi huku kashanipa tena ujauzito,amenifanya nimeishi maisha magumu sana ya ajabu,namchukia sana na siwezi kunyanyua mguu wangu kwenda kumtizama shetani kama yule hata siku moja" yaani mtu huyu anavyotafiriwa unaona si mtu mwema na kuna sentensi ambazo nimekutana nazo nikiwa gerezani "huyu mtu uko nae karibu kivipi? kama hatafsiriwi kwa wema lakini kiundani kwanini mtu huyu si mwema lakini yeye mwenyewe anasema yupo anatumikia kifungo kwa sababu yeye mwenyewe amestahili wala hajaonewa na yoyote,ni malipo ya madhambi yake,nilimsikiliza huyu mama maneno na hasira zake lakini mimi sio yaliyonileta,hata kama baba yao ni mbaya hawa watoto sio wabaya kwahiyo ntazidi kuja kuwaona pale ntakapopata nafasi hata kama navunjwa moyo na mama yao nitajipa moyo kwa sababu nimewapenda hawa watoto nitakuja tena na tena kuwatizama.
Niliaga na kwenda kuendelea na mishe zangu na maisha yangu yakawa yanasonga mbele na siku zikasogea ikapita kama miezi mitatu niko na mishe zangu sikupata nafasi ya kwenda kuwatizama wale watoto wala sikwenda kule gerezani niko na mambo yangu naendelea,nakumbuka siku moja nikasikia kuwiwa sana kwenda kuwatembelea wale watoto,nilienda lakini nilimkosa huyu mama,nilipouliza kwa majirani nikaambiwa yule mtoto mdogo anaumwa,anaumwa sana na amelazwa,kwahiyo nikafatilia hadi kujua wamelazwa wapi,nikaenda kwenye hiyo hospitali na nikamkuta yule mama pamoja na baadhi ya ndugu zake wakiwa katika hali yakumuangaikia mtoto walisema amepata amoeba sijui nini mambo ya watoto basi nami nikawatia moyo nikasema "nilikuja kuwaona na isitoshe mambo yamekuwa ni kukimbizana muda umepita sana sijaja" huyu mama akasema"nilijua hautakuja tena unadhani utakuwa unakuja kutuangalia kila siku kwa maagizo ya huyo mtu ambaye yuko gerezani ambaye atafia uko gerezani" nikamwambia "siji kwa sababu ya rafiki yangu wa kule gerezani,nakuja kwasababu nimeshakuwa na urafiki na hawa watoto" aliniangalia tu huyu mama lakini hali ya mtoto haikuwa mbaya sana basi nami kwakuwa nilipata taarifa ya mtoto kuumwa nikawa nakuja hadi pale aliporuhusiwa na kurudi nyumbani nami nikaendelea na mishe zangu lakini nilitafuta muda siku hiyo nikajisikia tu nikaenda gerezani kwenda kumtizama mshkaji,kweli nilipata nafasi ya kuzungumza nae,nilimpelekea sabuni na vitu vichache vichache na akanambia "mbona umechelewa sana kuja mshkaji wangu?
Nikamwambia "kwanini? Akanambia "mbona nilikwambia uje tuzungumze" nikamjibu "unajua mambo uko uraiani ni kupambana sana,mambo yamekuwa mengi mshkaji wangu unisamehe bure ila nilipata nafasi nilikwenda kuwatizama watoto nikakuta mtoto wako anaumwa" akasema "nini tena? Ina maana taarifa hana,hana mtu wakumpelekea taarifa,yaani watu walishamkataa yaani yuko tu huku hana taarifa zozote lakini nikamwambia usiwaze kwani anaendelea vizuri kwa sababu alipatiwa matibabu nami nilikuwa naendaenda pale kwakweli anaendelea vizuri mpaka ameruhusiwa amerejea nyumbani,yaani mtoto anaendelea vizuri kabisa wala usiwaze" akanambia "aisee nashukuru sana,nashukuru sana ndugu yangu,nakushukuru mno na asante sana kwa vitu ambavyo umeniletea" nikamwambia "wala usijali,karibu" akasema "najua moyo wako iko siku utachoka kuja kunitembelea,najua utachoka na hautakuja tena" nikamwambia "sijui,lakini ndugu yangu nikuahidi pale nitakapopata nafasi nitakuwa ninakuja" akasema "lakini naomba tuendelee na mazungumzo yetu ya siku ile tulipoishia " nikamwambia "nakusikia" akanambia "tuliishia pale nilipokwambia nataka kubadirisha maisha yako" nikamwambia "nakumbuka" akanambia "hujaiwaza hiyo sentensi? Nikamwambia "sijaiwaza chochote,kwasababu unaweza wewe kunibadilishia maisha wakati wewe mwenyewe umekosa uhuru na upo tu unafanya kazi za humu ndani,unawezaje kunibadilishia maisha mimi ambaye niko uraiani na nina mwanya wakubadilisha maisha yangu mimi mwenyewe" akasema "ni kweli umesema vyema lakini mimi nimekaa hapa ni kwa sababu nimekosa uhuru wakufanya kitu lakini natamani nifanye kitu nikiwa uraiani" nikamwambia "utawezaje sasa? Akanambia "nataka wewe ukafanye" nikacheka,nikamwambia "kufanya nini? Akanambia "ninao utajiri" nikacheka yaani ni mambo yakuchekesha,nikamwambia "yaani wewe unao utajiri wewe? Akasema "hakuma mtu anajua kama mimi nina utajiri mwingi" nikamwambia "eeh niambie kuhusu utajiri wako" akanambia "hii ni siri nazungumza na wewe na sijawahi kuzungumza na mtu yoyote,natamani uwe rafiki yangu,ndugu wangu wa damu,sina mwingine wa kumuamini moyo wangu umesukumwa na wewe na hata nilipokuwa gerezani nilikuwa nikiomba Mungu usiku na mchana anipe mtu ambaye si ndugu moja na mimi lakini akamfanye awe ndugu yangu,akatimize ndoto zangu uraiani,hivi unajua ni kama vitu visivyoeleweka" nikamwambia "haya nambie,nambie kuhusu utajiri wako" akanambia "ninazo pesa nyingi zakuweza kubadilisha maisha yako,nyingi hata zakuweza kubadilisha maisha ya familia yako lakini niahidi hautawaacha watoto wangu,utawabeba nakuwatunza na kuwalea,utawasomesha,utamsaidia na mama yao,utamsaidia na msichana wangu lakini niahidi,niahidi kitu kimoja,hautamgusa yule mwanamke,utamuacha ataolewa na mtu mwingine,mimi sitaweza kumuoa lakini wewe usimuoe,aolewe na mtu mwingine na msaidie akiwa na matatizo"
Mimi ninayasikia haya,unajua ni kama mambo yasiyoeleweka narudia tena kwa sababu mtu anawezaje kunambia maneno hayo,ananipima? Tunazungumzia habari za pesa ambazo niko huku napambania kweli na udeiwaka mtu ananambia nina utajiri,niliyasikia haya maneno kutoka kwa kaka huyu ambaye tulikutana gerezani na kuishi kama familia na leo ninapoelezwa haya mambo ya pesa na utajiri na mfungwa aliyepo gerezani ananiambia nimuahidi kwanza sikuamini,niamini vipi,niamini vipi kirahisi? Kwanza nikabaki nikitabasamu kwa sababu nimekuwa nikitabasamu hivyo na akanambia "mimi sikutanii na siko kwa ajili ya matani na mimi nilisogea na kuzungumza na wewe toka ulipofika na nikakutana na wewe,nilikuja kwa sababu ya kusudi maalum ili unikamilishie ndoto zangu,wafanye watoto wangu kuwa bora,waishi katika nyumba nzuri,wafanye watoto wangu kuwa watu wa thamani,mama yao pia,sikwambii sana kuhusu ndugu zangu endapo ukiguswa waweza fanya hivyo lakini huu utajiri nakupa wewe,nakutunuku wewe" sasa mfungwa aliyeko
gerezani anawezaje kuwa na pesa,"pesa ziko wapi? Nakumbuka nikamwambia "unanambia mambo mazito yaani sijawahi hata kusikia mtu aliyeko gerezani anaweza kumpa utajiri mtu aliyeko uraiani,basi mimi naweza nikawa nimebahatika ila ndugu yangu nashukuru sana ila huo utajiri sidhani kama mimi nafaa kuupata,naogopa sana vitu hatarishi katika maisha yangu,natamani kufanya vitu vya halali tena vya haki,sitaki matatizo katika maisha yangu,umeniona nimetumikia kwa muda gani hapa gerezani ilihali sijatenda lolote,maisha yangu yalirudi nyuma sana,harakati zangu nilizokuwa nazo zikarudishwa nyuma,unataka na mimi niishie gerezani kama wewe?
Inaonekana maisha yako uraiani hayakuwa mema wewe mwenyewe umesoa unatumikia kile ambacho wewe umestahili kutumikia je unataka na mimi niyaishi maisha ambayo wewe umeyaishi yakakufanya hadi uje gerezani? Akasema "hapana,sio kweli,sio kweli na haijalishi kwa sababu mimi nilikuwa mbaya basi na pesa yangu itakuwa mbaya,unajua nini mimi natamani kufanya,natamani pesa yangu ikafanye mambo mazuri mema" nikamwambia "pesa yenyewe iko wapi? Tunazungumza,tunazungumza nini kwani? Yaani pesa iko wapi unayozungumza wewe? Akanambia "pesa ipo na nataka uniahidi katika mambo niliyokwambia kwa sababu ukitoka hapa unaenda kuchukua pesa kwahiyo ahadi yangu inabidi unipe leo na ahadi yangu nataka uape mbele ya Mungu ya kwamba unaniahidi hata kama mimi kesho nitaondoka ahadi yako kwa Mungu isimame na ikuhukumu kama utaenda kinyume na hayo,mimi nataka kukupa utajiri leo,leo nakupa utajiri,niahidi,najua hauwezi niahidi kwa maandishi lakini kwa kinywa chako niahidi ,niahidi utatunza ahadi hiyo mpaka pale mwisho wa safari ya maisha yako" nikamwambia "kaka we usiongee sana we nambie" akasema "siwezi kuzungumza zaidi ya nilichosema niahidi utawatunza watoto wangu" nikamwambia "ndio nakuahidi nitafanya hivyo" niahidi utamtunza mama wa watoto wangu yaani wale watoto mama yao" nikamwambia ndio nakuahidi, "niahidi utamsaidia mwanamke niliyempenda na kutamani kuishi nae nikiwa uraiani,mwanamke wa ndoto zangu" nikamwambia "ndio" "lakini niahidi huyo mwanamke hautamfanya kuwa mwanamke wako,utamuhudumia na kumsaidia na atakwenda kuolewa na mwanaume anayemtaka yeye lakini sio wewe" nikamwambia "ndio" akasema niapie mbele za Mungu,mimi niko gerezani sasa namjua Mungu,najua mtu ukiapa mbele za Mungu hiyo inasimama kweli" nikamwambia "mbona unanipa vifungu vigumu hivyo kwanini tuape Mungu hapa?
Akasema "niapie mbele za Mungu" haya yalikuwa ni mazungumzo na huyu mtu ambaye amenambia atanipa pesa na hizo pesa ziko wapi? Ananipa katika mazingira gani? Anasema anataka kunipa utajiri abadilishe maisha yangu!
Itaendelea!
Utani pm ndugu yangu zipoOmbi kwako mkuu mleta mada, pindi utakapoimaliza kuisimulia yote, nitaomba audios za stori nzima, kama hautojali mkuu wangu, shemejiyako mvivu kusoma ila kusikiliza itakuwa rahisi, nami kuhadithia kila kitu siko vizuri.
UbarikiweMashuka nayo taratibu,asnt sn kwa uji huu
Acha na madogo hao mkuu makuzi mengiUnaujua umri wangu? Alafu unadhani naishi kwa kuogopa maneno ya mtu? I'm 40+ bro! Behave!
Salute mkuu na najiepusha kudeal na mtu anayemuogopa mtu na anataka akuambukize uoga wake na wewe
Nimeanza kuogopa mganga sio anataka kuzichukua hela zilizohifadhiwa kweli?[emoji134]Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa
Sehemu ya 18
Ukipata fursa ya kusikia mikasa iliyowakuta wanadamu kiukweli kuna watu wamekutana na vitu vingi,mikasa mingi katika maisha yao,watu wamebeba vitu vingi ndani ya mioyo yao nami kama Rojas naelezea yale ambayo yamenisibu ili msomaji wangu nawe uweze kujua ya upande mwingine wa dunia,kinachotesa sasa hivi ni huu msiba,naumia sana kwani katika vitu ambavyo nimezungumza sana na mtu huyu na nikataka sana kujua lakini hakuwahi kuniambia hata siku moja,nilitaka kujua pesa alizitoa wapi? Mimi nakueleza leo jinsi matumizi yangu yalivyo makubwa,jinsi ambavyo nimekuwa nakitumia pesa zangu kwa namna tofauti tofauti lakini hata ukiniuliza hizi pesa ulizitoa wapi nitakwambia wapi nilipotoa lakini yule mtu aliyenipa je yeye amezitoa wapg? Hicho kilikuwa ni kitu kama fumbo kwangu na mtu huyu nimetengana nae kwa muda mrefu na hata nilipokuja mtu huyu alishaanza kuwa mdhaifu na sasa amepatwa na umauti.
Lakini katika vitu alivyoniambia ni "nimekusamehe wewe pamoja na kizazi chako,niliyafanya haya kwa mapenzi yangu tu mema" lakini hakunieleza wapi pesa ametoa na zaidi alisema "nenda ukatumie pesa,yafuate yale niliyokueleza" nilitamani mimi niwe mmoja kati ya watu ambao nitapata nafasi ya kumzika mtu huyu kwa heshima,najua ni mtu ambaye ni mfungwa,amekuwa akitumikia kifungo chake na amepatwa na umauti akiwa bado anatumikia kifungo chake lakini mimi nilisema mtu huyu kiu yangu,shauku yangu nimpumzishe mahali pa heshima,chochote nitafanya,nimekuwa nazungumza hii sentensi chochote ntafanya kwani tangu nimekuwa na pesa nimejua jinsi pesa inavyoweza kufanya vitu visivyowezekana japo kuna vitu haviwezekani hata kwa pesa lakini hivi ninavyovizungumza mimi vinawezekana,unapokutana na watu ambao mnaweza mkabargain nao kitu hata kama kutakuwa na mifumo flani ambayo ni migumu,wakakuletea ugumu lakini wanaweza wakafanya tofauti kwa sababu kuna pesa inapita hapo na pesa ina nguvu sana sana sana,ukiwa na pesa na ukaishi pesa utaelewa maana ya hii sentensi mimi nasema,kwako wewe mambo yasiwezekana ni machache sana,mengi yanawezekana,popote unaweza ukaenda,yoyote unaweza ukamface ukazungumza nae,unakuwa unajiamini isivyo kawaida hata unavyokuwa unatembea barabarani pesa inakupa ujasiri mkubwa sana kwahiyo nilisema hili ntaliweka sawa ili kuhakikisha mimi nakamilisha hilo.
Nilitimiza ahadi yangu kama vile nilivyotamani iwe ndivyo mimi nilifanya tena sikufanya tu katika hali ya mimi binafsi bali nilimchukua huyu mtu nakumpeleka mpaka nyumbani kwao,yaani kuusafirisha mwili na kuupeleka mpaka nyumbani kwao kule ambako mimi nilichukua pesa,mahali ambapo toka nimechukua pesa sikurudi tena,ni mengi yalitokea lakini pengine si muhimu sana kuyazungumza hasa ya kule lakini kiukubwa zaidi mimi nilifanikiwa hilo zoezi,nililifanya kwa unyenyekevu mkubwa sana japo katika mazungumzo ambayo tumewahi kuyazungumza aliwahi kuniambia "kuna siku utageuza kisogo chako na utakaporudi hautanikuta" nilimkatalia na hata sikupay attention kuzungumza nae kwahiyo hakuwahi kusema nikifa itakuwaje kwa sababu watu wanapoteza maisha wanazikwa,wanahifadhiwa tu na maisha mengine yanaendelea,unaweza kuwa na ndugu yako gerezani na haujawahi kumtembea hujui siku unaenda ibuka unashangaa mtu alishapoteza maisha,hakuma mawasiliano wengine wanahamishwa kwenda maeneo flani lakini kama unakuwa ni mtu wa kutembelea ndugvhata taarifa inapotokea mawasiliano yakawa rahisi kuweza kukupa taarifa bwana huyu mtu moja mbili tatu kama mimi ambavyo nilivyokuja kufanya awamu nyingine japo uko mwanzoni sikuwahi kufanya na ndio maana hata alipohamishwa gereza,hata alivyokuwa na afya dhohofu mimi sikujua.
Nimerudi kwenye maisha yangu kama kawaida kwa sababu mambo yameshapita,nilikuwa na muda kwelikweli unajua taratibu hizo mpaka kupumzisha mwili na nini kwahiyo kuna siku kadhaa nilizitumia kwa ajili ya hilo zoezi,nimerudi na siku zinazidi kusogea mbele niko hapa bado moyo wangu ulikosa amani kabisa,nakumbuka nilipata msukumo mimi,kuna mshkaji mmoja ambaye alikuwa karibu na mshkaji kule gerezani na yeye alibali kule gereza la mwanzo ambapo mimi na mshkaji tulikutana,nilisukumwa kwenda hata nizungumze nae mawili matatu,nilifunga safari nikaenda mpaka gerezani lengo tu angalau nizungumze na mtu huyu kwa sababu huyu mtu amekuwa karibu nae na natafuta kitu ambacho angalau kinaweza kikanipa unafuu kwa hali ninayoipitia sasa hivi ,hali ya kukosa amani ninayoipitia haielezeki,kuna watu pengine wameshapita katika situation kama hizo unakosa amani unasikia roho inaangaika tu yaani hapa kifuani unasikia kitu kiko hapa unaangaika ndivyo ambavyo mimi nilivyokuwa nasikia,nilipofika kweli nilibahatika kukutana na mtu huyo na alisikitika sana rafiki yake ambaye walikuwa wote gerezani kwa muda mrefu hayuko tena lakini aliniambia sentensi moja sentensi ambayo sikuwahi kuisikia mimi hata siku moja yaani sijawahi kusikia hata mtu huyu ambaye yeye ni marehemu kuniambia,hakuwahi lakini nilisikia kwa mtu huyu,aliniambia sentensi hii akitaja jina la yule mshkaji "unajua mshkaji alikuwa na nafasi kubwa sana ya kutoka,unaona ukimwambia habari za kutoka kuwa huru yaani atoke aende uraiani awe huru,kwa sababu kuna siku aliniambia umempa chance ya kupigania atoke lakini hakutoa ushirikiano lakini alikuwa na sababu kubwa sana" nikataka kusikia kwa sababu ni kweli mtu alichimbia pesa,yaani pesa zilikuwepo,pesa zipo uko zimekaa,amenipa nafasi hiyo mimi nimeenda kuchimba pesa na nimezimiliki na zimekuwa za kwangu,kwanini pesa hizi tusingefight yeye atoke,awe huru,nani hataki kuwa huru,nani hataki kuishi maisha ya uraiani uwe unaamua uoge saa ngapi,ule saa ngapi,maisha ya kupangiwa saa flani utakula saa flani utaamka nani anayapenda? Mwanadamu furaha yake ni kuishi maisha ya uhuru na ya amani lakini yeye ilionekana kama yatafanyika lakini sio sasa ni baadae,kwanini baadae na nafasi tunayo sasa hivi,tupigane tunapoweza na kama itashindikana tunawe mikono kwamba tumeshindwa,tumeshindwa basi haiwezekani lakini kuna bidii tumefanya,watu wangapi ambao walishakatiwa tamaa lakini mwisho wa siku wamekuja kuwa huru? Haijalishi ni miaka mingapi lakini hakuwa na ile shauku ya kusema atoke uraiani na hiki ni kitu nilikuwa namwambia kwanini yaani,kwanini yaani?
Ndio nasikia huyu mtu ananiambia,ananiambia "(akitaja jina lake)alikuwa anahofia sana kuuawa" nikashtuka "kuuawa? Kuuawa na nani? Akasema "amesema ni bora aendelee kuwa gerezani lakini aendelee kuwa hai ili aendelee kupata taarifa kuhusu watoto wake na akawa na furaha kwa sababu wewe ulizidi kumpa taarifa za kuhusu watoto kitu ambacho ndio alikuwa anakihitaji katika maisha yake kwahiyo kwa sababu ulikuwa unamfanyio hivyo ndio ilikuwa ni furaha kwake" nikamuuliza "kwanini alikuwa anahofia kifo,kwanini? Akanambia "hata mimi nimewahi kumuuliza sana lakini hajawahi kuniambia hata siku moja lakini ninachojua ni hofu ya umauti ndio uliokuwa unamsumbua" nilistuka na kuogopa kwelikweli kwa sababu tangu nimemfahamu mtu huyu hajawahi kuniambia,nikamwambia "natamani sana kujua" akanambia "mimi sijui chochote na mimi pengine naweza kuwa mtu ambaye najua mengi yake lakini sijui chochote"
Niliondoka nikiwa mnyonge zaidi "kwa sababu gani mtu huyu aliogopa,aliogopa umauti na akitoka uraiani anaweza akauawa bora akae kule aendelee kupata taarifa za watoto wake na mimi japo niliendelea kuwahudumia watoto kwa namna moja au nyingine lakini nilifunga ukurasa wa kumpelekea taarifa,kwahiyo kama mimi ndio alikuwa ananitegemea mpeleka taarifa,mpeleka habari kwamba watoto wameendea hivi na mimi sasa ndio nikakata mguu,sijui alipita katika mazingira ya kimaumivu ya kiasi gani,leo sasa ndio naona kama zaidi nilikosea,kumbe hiki ndicho mtu huyu kwake kilikuwa ni kikubwa kuliko vyote lakini ni nani hasa aliyekuwa anamuhofia,ni nani huyo aliyekuwa anamuhofia? Nikajikuta naanza kuwa na stress sana na zikawa zinanisumbua sana kwa sababu nikaanza kuogopa na mimi,kama yeye alikuwa anaogopa kutoka uraiani labda ni kwa sababu ya hizi pesa nami niko na hizi pesa lakini mbona siku zote niko na hizi pesa na nimetumia kwa mambo mengi sana mbona sijawahi kuona mtu ananifata au hata kunihoji kwamba hizi pesa ni za nani? Sijakutana na mtu kama huyo,yeye alikuwa anamuhofia nani?
Nakumbuka nina mshkaji wangu wa karibu aliona niko down sana na aliniambiaa "Rojas hauko sawa" nikamwambia "kuna kitu kinaniumiza sana kichwa najikuta nakosa raha kabisa" akanambia "ni nini? Nikamwambia "hata sijui naanzia wapi kukueleza lakini ni ngumu sana kukueleza ila nataka kupata majibu ya kitu ila sijui nani anaweza akanipa majibu,akaniambia "ni kuhusu mambo yako ya biashara? Rojas hujui kuna watu wanaweza kuviona vitu ambavyo kwa kawaida hauwezi kuviona? Nikamwambia "unamaanisha nini? Akajibu "eeh wako wataalam kuna kitu kinakusumbua na haukielewi unataka kupata majibu wako wataalam wanaweza kujua kwamba majibu ya hiki kitu ambacho unakiwaza ni haya hapa" kwa yale maneno yake akawa kama akanipa akili mpya hivi, "ndio ni wapi naweza kupata wa namna hiyo" akanambia "wapo,sasa hawa watu wanazidiana uwezo,sasa ngoja labda tuangalie nani anayeweza akakufanyia,ni nini hasa kwanza unataka kujua,vipi kwenye biashara unachezewa? Nikamwambia "sio kuchezewa ila sielewi mambo yangu jinsi yanavyoenda kwahiyo nataka ufafanuzi" akasema "ooh mambo ya biashara biashara wako wengi sana,sasa mimi ntakuconnect na mtu atakupa majibu ya maswali yako yote" kutokana na hali ya msongo wa mawazo alafu nimejikuta tu najiuliza maswali mengi alafu sina majibu.
Kweli mshkaji aliniambia "nakupigania kuhakikisha unapata mtaalamu kwelikweli" tukizungumza mtaalam huyu ni mtu anayefanya uganga,yeye alitumia lugha ya mtaalam mwenye uwezo,mtaalam ambaye anaweza akanipa majibu ya maswali yangu na mimi kwakuwa sikuwa mwepesi sana kumshirikisha kwakuwa najua waganga wakati mwingine uwa hawana siri pengine anaweza akamueleza lakini potelea mbali lakini mimi ninachotaka ni anisaidie,kwa sababu sikutaka kumshirikisha sana alinisindikiza lakini nikamwambia "wewe kaa tu hapa mimi ngoja niingie nizungumze nae" kwahiyo niliingia mimi peke yangu kwa mtaalam,huyu mtaalam akanambia "hapa ndipo jambo lako linapofanikiwa karibu sana" nikamwambia "nina shida ninapitia sana,sijajua chanzo cha haya mambo" lakini nilimwambia "mimi kuna mtu amenipa pesa,amenipa pesa kwa kunielekeza mahali pesa zilipo,nikaenda kuchukua hizo pesa,nikazitumia lakini akanipa masharti ambayo sikuwa nayaelewa na ikafika kipindi nikaona kama yule mtu aliyenipa pesa ananisumbua na kunipa msongo wa mawazo na nikbmua kuachana nae na kufocus katika maisha yangu mengine lakini huyo mtu amepoteza maisha sasa nimekuja kujua kwamba huyo mtu kuna vitu labda alikuwa anaviishi ambavyo alikuwa anavifanya siri na hakuweza kumueleza mtu" kwahiyo nikawa nasubiria mtaalam anipe majibu sasa kwakuwa nilikosa kupata majibu katika hali ya kawaida basi njia zipo nipate ufafunuzi ni nini kinaendelea,wao si wana nguvu wanaweza wakajua basi nami nijue na je wakijua wataweza kunisaidia ili moyo wangu ubaki na amani na vitu kama hivyo.
Nilimueleza haya yule mtaalam na nakumbuka huyu mtaalam alikuwa ni mtu mzima tu na nilielezwa yuko vizuri na niko hapa kutatuliwa kile ambayo nataka ufafanuzi nacho,mtu huyu kila nilivyokuwa namueleza alikuwa na karatasi na kalamu nyekundu na akawa anaandika maandishi ya kiarabu na michoro na akawa anazungumza maneno flani ambayo nadhani ni ya kiarabu na alipomaliza alinambia sentensi moja "hizi pesa sio zako" nikamwambia "ni kweli lakini aliyenipa alinipa hizi pesa kwa moyo mweupe" akasema "ndio hata mimi naona alikupa kwa moyo mweupe na hata yeye hizo pesa zilimtaabisha sana" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "eeh naona hizo pesa zimemtaabisha sana,ni kweli amezipata lakini ameishia mateso mpaka kifo chake ameishia kuteseka" nilishtuka sana kwa maneno hayo,katika vitu mimi nilikuwa na amani navyo na natumia hizi pesa kwa uhuru na nilifanya biashara na biashara zinaenda na kama kwa namna moja au nyingine mimi nakuwa sijafanya vizuri ni mambo yangu mimi,matumizi yangu mimi,matumizi yakawa makubwa zaidi kama nilivyokwambia ni starehe kwa kwenda mbele,wanawake zaidi ya saba na hapo kuna waliopangiwa vyumba,kuna wakulipiwa ada za chuo,wa driving school na mengineyo.
Nashtuka sana kwa yale huyu mtaalam anayoyaeleza na nikamuuliza "ina maana hizi pesa mimi nilizichukua kimakosa? Sikuwa na makosa yoyote kwakuwa huyu mtu alitaka msaada na mimi nikamsaidia na ndio maana nasema alinipa kwa mapenzi yake ya dhati,sijui zilimtaabisha kwa kiasi gani lakini ninachojua ni pesa halali ambazo sio za magumashi kabisa" akaniuliza swali "ni wapi umehifadhi hizi pesa? Hii ni siri ambayo simwambiagi mtu na mganga anauliza wapi nilikohifadhi pesa[emoji23] na nilishamwambia vitu vinavyonipa mashaka ni huyo mtu kutotaka mimi nipeleke pesa benki kwahiyo nikajikuta zile pesa ambazo nimeanza kuendeshea biashara ndio nilikuwa napeleka benki lakini zile pesa ambazo nilichukua kule nilikuwa natumbukiza kwenye vitu ambavyo vinatembea km kuagiza bidhaa moja kwa moja na si kupeleka benki,akaniuliza kwa mara nyingine tena "hizi fedha ni wapi umezihifadhi kwa sababu hapa naona natakiwa kufanya kitu kuna mambo mabaya yanaenda kukutokea" nikaogopa,nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "ndio,mambo mabaya naona yanaenda kukutokea na afadhali umekuja mapema ili nikupe msaada" nikamwambia "naomba unisaidie sana"akasema "nakusaidia na ndio maana nataka unipe majibu ya maswali ninayokuuliza kwani mimi sio mganga wakupindisha maneno yangu.
Mimi ni mganga ambaye nimefanya hii kazi kwa miaka mingi na nimewasaidia watu sio wa Tanzania tu hata wa nje ya Tanzania kusolve matatizo yao ambayo ni magumu yaliyoshindikana kwahiyo utamshukuru mtu aliyekuleta kwa sababu wewe hautakufa hata kama yeye aliyetafuta hizo pesa amekufa,wewe hautakufa na utashuhudia wajukuu na vitukuu vyako lakini inabidi uwe muwazi kwangu kwani tabia ya kuficha vitu ambavyo vinanifanya naanza kuhisi pengine unanidanganya utafanya kazi iwe ngumu" nikamwambia "kuna vitu nilishamuahidi mtu huyu sitamwambia mtu lakini nimejikuta katika harakati za maisha nazungumza,nilielekezwa na mtu huyo wapi nihifadhi hizo pesa ili ziwe salama na pamoja na mafanikio ambayo mimi niliyapata sikuwahi kuhamisha hizo pesa toka mahali ambako niliweka toka siku ile nilipozihifadhi" akaniambia "ni sawa vyote unavyosema,kuwa muwazi kwangu nikusaidie,ni wapi hizo pesa umehifadhi? Kiukweli sijui kwanini kwani nilikuwa mzito sana kusema pesa ziko nyumbani kwangu,nilipozihifadhi ni kwenye chumba ninacholala,nimechimba na kufukia pesa ila ukweli nilimwambia kuna pesa ambazo zinazunguka katika biashara,hizo sikuwa nazihifadhi ndani,akanambia "mbona unasitasita,unapokuja kwa mganga kwa mganga amini unatatuliwa mambo yako lakini na wewe unatakiwa kuwa muwazi lakini wewe unaonekana moyo wako ni mzito kusema ukweli na ndivyo ambavyo naona umauti unafata kwako baada ya huyo mtu mwenye pesa kupoteza maisha"
ITAENDELEA!
Fine shukraniUtani pm ndugu yangu zipo
T Bag alijikata mara ya pili baada ya mkono kushonwa.Mzee mwenye hela ndani anaitwa dB cooper, na t_bag hakujikata,ila alijua jamaa watamuacha so ikabidi ajifunge pingu na michael, wakati wa kutoroka walimtumia John kupata ndege sio helicopter.
Ila kwenye season ya kwanza michael mwenyewe alimvuliaga kofia Alex mahone,nae alikuwa kichwa sana.
DB Cooper hakuwa tajiri ila alikuwa ni mfungwa aliyefungwa kwa kesi ya kuiba hela nyingi, Scofield alikalkuleti mambo yake na akawa na jibu kuwa Wesmoland ndio DB Cooper. Lengo la kumuweka kwenye mchongo wa kutoroka ni ili awasaidie pesa Scofield na lincoln watumie mbele baada ya kusepa USA.Huu mkasa umenikumbusha movie ya prison break, nimemkumbuka mfungwa mmoja John Abruuz(Mbabe gerezan na alikua na crew zake ndani gerezani za kibabe na nje ya gereza alikua na crew za kibabe ,,(business man)) na upande wa pili ni mfungwa wa muda mrefu dp cooper(Tajiri,humble down to earth,lakin pia mafia wa kichinichini, ukiingia kwenye anga zake kindez[emoji38]) ambaye alikuwa na hela ndefu sana, alizozichimbia mji fulan uraiani , kabla ya kuingia gerezani ,hivyo crew ya kina scolfied lilimuunga John Abruuz kwny mpango(msafara) wao wa kutoroka coz ndo aliepewa mchongo na db cooper,yaan aliujua mji zilipo hela na zilipochimbiwa,na alikua na raman,pia alikua na access ya kuagiza watu wake nje walete helikopta nje karibu na gereza usiku ,ili waitumie ku escape from the prison, ili iwe easy kuwachenga polisi japo walichemka, helikopta iliwaacha baada ya wao kuchelewa kufika eneo la tukio kwa sababu ya obstacles walizokua wakizipata wakati wa kutoroka zikala muda wao waliohadiana na watu wa helikopta,coz ile wanakimbilia helikopta na polisi hao nyuma yao,watu wa helikopta wakawa washasepa,wacha wakimbizwe na mijibwa ya polisi pori kwa pori,ndimi njee,daah, polisi nao nyuma yao full armed,, hivyo walivyotoroka gerezani scolfied na wenzie , moja kwa moja walikuwa wanazifata zile pesa,siunajua tena mtu akitoroka jela hana mishe wala nini, uhuru zero,kuishi kwa mashaka,pesa ndio kila kitu na ukizingatia kaka scolfied alikuwa na msala mkubwa,unaohitaji pesa kujificha na kuufanyia research kesi yake na kupata solutions,lakini bahat mbaya mfungwa mwenzao(walotoroka nae) mtukutu TBAG(alikua selfish Sana huyu jamaa) ,akaisoma Raman chap walipokua karibu na mji wenye ambao ndio tajiri dp cooper kafukia pesa zake ndani ya nyumba flan,baada ya kuisoma Raman chap kaimeza ili wenzie wasijue ni wap,akakimbia kwenda kufukua mwnyww ,alizifaid hela kidogo mtaan,kabla hajadabwa,ila kuna mahali alijikata mkono wake mwenyewe wenye pingu ,na kukimbia bila mkono kisa kuwakimbia polisi, very interesting story ,sema movie nimeona Zaman kidogo ,najaribu kuvuta kumbukumbu za kurelate na hii story. .wadau mnaoikumbuka hii movie mtanikosoa ni kitambo sana , naweza kuwa nimechanganya hapo kwenye mchongo wa hela ya dp cooper km alipewa scolfied basi John Abruuz alikua kwa ajili ya kufanikisha helikopta kufika eneo husika siku ya tukio. .anyways kumbe hayo mambo yanatokea kweli kwny jamii na si kwny movies tu.