Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Salute kwako,ubarikiwe
 
We jamaa wa mapacha kumbe umeona,ubarikiwe
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa​


Sehemu ya 19


Mtaalamu alizidi kunidadisi na alinambia "pesa ziko kiasi gani zilizobaki toka wewe uzipate? Nikawa najiuliza je naulizwa maswali gani haya sasa,mbona kama mganga ananichimba sana? Na naomba ukumbuke hapa kwa huyu mganga nimeletwa na mtu na sijui dhamila yake ya ndani na mganga anataka nimletee pesa kadhaa kutoka katika pesa ninazozitunza uko ninapozitunza (yaani alinitaka kuchomoa kiasi flani cha pesa nilizonazo na nimletee)kuna kitu azifanyie kwa nia ya kuzifanyia ulinzi kwa sababu anaona kuna mambo yasiyo mema katika pesa ninazozitumia,nikamwambia "sawa" naye akazidi kusisitiza "nipe majibu ili niweze kukusaidia" majibu kwa maana nimueleze eneo nililohifadhi pesa.

Lakini mimi nikajiuliza "huyu kama ni mtaalam wa kuweza kuona vitu ambavyo mtu mwingine hawezi kuviona ameona kama pesa ninazozimiliki kuna shida,anaona kitu kilichoondoa uhai wa ndugu kule gerezani ndio kitu hicho kitakachokuja kunidhulu nami je kama ameweza kuona vyote hivyo iweje ashindwe kuona nilipoweka pesa mpaka nianze kumention ni sehemu flani nimeweka moja mbili tatu sasa kutokana na mimi kuingia katika ulimwengu wa biashara na kutapeliwa mara kadhaa hii ikanipa hofu kwa sababu nimeletwa hapa na mtu na huyu mtu ni mshkaji wangu,katika maisha huwezi kujua huyu mtu anakuwazia jambo gani pengine hata yeye anaumiza kichwa kujua vyanzo vya pesa zangu ni nini,huyu mganga itamuaminije na kumpa siri yangu hii,nikamwambia "mimi ntaleta pesa" akanambia "sio tu kuleta pesa" na akazidi kuning'ng'niza katika kupata jibu lake lakini sikumpa ushirikiano kabisa katika hilo,nilimwambia "pesa nitaleta na hayo majibu nitakujibu ntakapoleta pesa" mganga akanambia "kiburi chako kitakufanya uchelewe na kutatokea maafa makubwa,mimi nakuambia hivyo kwa sababu hizi mali si za kwako,yaani ukae ukijua hizi mali si za kwako na huyo aliyepata mali alikuwa na siri nazo na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana alizifukia mahali,wewe mahali ulipoziweka unaona ni shida kunitajia je unahisi ni nini"

Sikutaka kumpa sana nafasi na nikamwambia "ndio kwanza tumefahamiana na vile tunahitaji muda zaidi wa kuzidi kuzungumza zaidi pengine naweza kuzungumza mambo mengi zaidi" lakini nikazidi kujiuliza kama anaona visivyoonekana kwanini hajaona pesa? Nilifanya taratibu nilizoelezwa kwakuwa nilitakiwa kulipia pale,nikalipa kwani sikuona kama ni hela nyingi kwani makubaliano ilikuwa kulipia huduma ya kutizamia,kulinda pesa na mimi mwenye kunitibia ili kila kitu kirudi katika mstari wake,nikalipa na akanambia kadri siku zitakavyokuwa zinaenda nitajionea jinsi ulinzi wa pesa na mali zangu unavyoimarika,nilimpatia laki tano na uko mbeleni nitalipia kwa kadri ya matibabu husika.

Tumetoka pale na yule mshkaji aliyenipeleka na tukiwa njiani akawa ananiambia "huyu ni mganga sahihi sana,wako waganga lakini huyu ni mganga mahiri" nikamwambia "lakini mimi sijawahi kushiriki katika mambo ya waganga" akanambia "shida yako,tatizo lako fata tu maagizo anayokupa utafanikiwa sana" nakumbuka sana nilitakiwa kurudi kwa mganga kupeleka pesa (mfano wa pesa)ambazo ninazo lakini nikatingwa na mambo mengi kwani mambo yalikuwa yamepandiana sana na nikasema ngoja nikamilishe alafu ndio niende,nakumbuka siku hiyo niko katika vitu vyangu vinavyoniingizia uchumi nikiwa napiga mahesabu ya hapa na pale nakumbuka hatua yangu ya kwanza kabisa nikapokea taarifa ya gari yangu kubwa kabisa ambayo nilinunua kwa gharama kubwa na linaendelea kufanya kazi nikapewa taarifa limepata ajali mbaya sana lakini pia ambacho kiliniuma zaidi na watu ambao walikuwamo mule katika gari ambao ni madereva wangu wote walipoteza maisha,nilisikitika sana,nilipofatilia kuona ajali ya gari yangu kiukweli ilikuwa lite off lakini stori za ajali hiyo kutokea zilikuwa ni nyingi sana lakini wakati nikiendelea na mchakato wa kuhakikisha hawa wapendwa wetu wanapumzishwa katika nyumba yao ya milele taxi moja ikapata ajali,ajali ilitokea lakini dereva alitoka akiwa hai lakini gari lilikuwa nyang'anyang'a na nakumbuka sentensi ambayo dereva alizungumza "aah mimi nimeaga bwana mtu hawezi kunichukua kizembezembe" yaani ikiwa inaaminika haikuwa ajali ya kawaida kwa maelezo yake anasema jinsi alikuwa anaendesha gari kuna vitu aliviona mbele ambavyo havikuwa vya kawaida na anaamini kabisa ulikuwa mkono wa mtu,kama nikaanza kupata ishara flani kuwa kuna vitu haviko sawa.

Kuna matukio ya ghafla yaliibuka hata sijui yalitokea wapi na hii ikanifanya nikimbie sasa moja kwa moja kwenda kwa yule mtaalam na nikawa nimepeleka pesa,nikapeleka na kumueleza changamoto ambazo zimetokea na alisikitika na kuniambia "nilikwambia kuwa hizi pesa unazomiliki aliyekuwa anazimiliki zimemtaabisha zimemtesa na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana hakutaka kumtesa ndugu yake yoyote na ndio maana alikutafuta wewe ili hizi pesa zikumalize" nikasema "hapana,hapana mtu amenipa hizi pesa na siku zote nimekuwa nikizitumia kwa amani, kwanini na kwanini? Mtaalam akachukua zana zake pale na kuongea ongea maneno yake na kunipa dawa flani akawa amenipakaa maeneo tofauti tofauti ya mwili wangu na pia akazichukua zile pesa nilizokwenda nazo nakuzifanyia mambo mambo yake mwenyewe ndio anajua zaidi na akanambia "mambo yatasettle,mambo yatasettle" na alinipa utaratibu wa kufanya vitu katika ofisi ambazo nazimiliki na akanirejeshea zile pesa ambazo alishazifanyia mambo yake niende nikazichanganye na zile pesa zingine kwamba ni ulinzi na hata mie kuanzia muda ule niko salama.

Nilitoka pale na nikafanya kama nilivyoelekezwa lakini moyo wangu ukawa unasikitika sana,nakumbuka nikapigiwa simu kutoka katika duka langu la nafaka kuwa kuna moto mkubwa na duka limeteketea lote na watu ambao walikuwa karibu na mimi wakaanza maneno "unaona,unaona,huyu mtoto alikuwa anamiliki mali zisizo za halali angalia matukio jinsi yanavyofululiza pengine amekosea masharti" lakini mimi kwa upande wangu nikawa najiamini hakuna sharti ambalo nililikosea kwa sababu hizi pesa nimemiliki katika mfumo ambao nimeshauelezea,ikabidi nirudi tena kwa mtaalam ili nijue ni nini tena na mbona nimeshaanza kupoteza sehemu yangu ya kupata pesa na watu wamekuwa wakipata pesa kwa ajili ya kutunza familia "imekuwaje tena,ni nini kinaendelea mbona haunipi ufafanuzi" akanambia kuna kazi kubwa anatakiwa kuifanya na inabidi anipeleke makaburini,sasa kwakuwa niko katika hali ya kutatua tatizo na ukiniuliza nini chanzo yaani ni sijui,yaani sijui kwa sababu nilikuwa na hizi pesa siku zote na ni hofu tu ilinipata ndio kwenda kwa mganga,yaani pesa nilizotoa kwa mganga ni pesa nyingi sana na ikawa kila ninapoenda ananitajia mabei makubwa ya vifaa hitajika na kwa mfano hili zoezi la kwenda makaburini aliniambia hili zoezi ni kubwa sana kwa sababu tunahitaji nguvu zaidi za kuhakikisha tunaweka ulinzi kwa hizi pesa kwahiyo alinitaka nitoe milioni tano ili kumaliya tatizo kabisa,nikatoa na kweli tulikwenda makaburini na akanifanyia madawa na kuniambia "sasa wewe umepikwa na umepikika na hakuna ubaya wowote dhidi yako kuanzia sasa hivi".

Lakini haikuwa kama yule mganga alivyosema kwani vitu vyangu vilizidi kupukutika,naviita vitu vyangu kwakuwa nilivitafuta mimi,nilivitafuta kupitia zile pesa na kama ningeamua si ningekaa tu huku nachomoa pesa natumia lakini pesa zile nilifanya uzalishaji ambao ndio umeleta matunda ambayo ndio hivyo vitu na hata pesa zake nikaweza kupeleka hata benki,nakumbuka sana,nakumbuka nyakati naendelea kuliwa pesa na vitu vinazidi kupotea na huku huyo mtaalam akiendelea kunipa vitisho,nakumbuka siku moja yule mama ambaye ni shemeji yangu ambaye tumekuwa tukishea mambo mengi alikuwa ameona mapito ambayo napitia na nilikuwa lesi sana kwahyo sikuwa hata na muda wa kuzungumza mimi niko kwa ajili ya kuzitatua changamoto nilizokuwa nazipitia,alinitafuta na akanambia "shemeji tuongee kidogo,shemeji kuyumba kwenye biashara ni jambo la kawaida,nini hasa kimesonga moyo wako? Mbona umekuwa hauna raha,nakuona ni mtu ambaye hauko smart tena,ni nini tena kiko katika maisha yako? Nikamwambia "sielewi" alizungumza na mimi kwa ukaribu na upole sana "Rojas nilikwambia kuna mambo hauwezi kumwambia mtu lakini Mungu yupo,Mungu wetu ni kila kitu katika maisha yetu" alizungumza na mimi mambo makubwa sana,nikamwambia "unajua leo hii mnaniona niko na pesa lakini hizi pesa leo zimegeuka mateso kwangu" akanambia "kwanini,kwanini mbona mimi hizi pesa naona ni pesa halali kabisa" nikamwambia "hujui tu" akasema "hapana naziona ni pesa halali kabisa na wala sina mashaka na wewe kama watu wanavyosema kuwa umetoa sadaka watu,minong'ono ya watu kuwa eti umekosea masharti na wanatisha watu ambao wanakufanyia kazi wakiwaogopesha kuwa watapata matatizo na kupoteza maisha,mimi siamini katika hilo"
Huyu mama alionesha kuniamini kuliko kawaida kwamba anaamini iko kitu,kwa mara nyingine ya kwanza nikamueleza huyu shemeji yangu,nikamwambia "hizi pesa mimi alinipa" na nikamweleza mazingira yote ya mimi kumiliki hizi pesa na nikamweleza jinsi nilivyomtelekeza huyu mtu na nikamwelekeza hadi mahali nilipozihifadhi hizi pesa kitu ambacho sikumweleza mtu yoyote tofauti na yule marehemu na nikamwambia yule shemeji "nimekushirikisha kwa sababu umekuwa karibu na mimi na umekuwa unazungumza vitu ambavyo vinagusa sana maisha yangu" akanambia huyu mama " Rojas unapoamua kuamua kuwa kuna miungu mingine asiyekuwa Mungu inaweza ikakusaidia tambua unakosea na uko ndiko ulikoenda kuharibikiwa,kama siku zote ulikuwa unafanya biashara zako katika hali ya amani ina maana sasa wewe umeenda kujiconnect na miungu ambayo ni mibaya na ndio labda imeharibu pesa zako" nikamwambia "hapana yule mtu alikuwa anahofia kutoka" nikamweleza hofu niliyokuwa nayo,akasema "hiyo ni hofu yako imekupandikiza wewe kwenda kuamini mambo ya kishirikina" nikamwambia "sasa mimi nafanyaje maana nahisi kuchanganyikiwa" akanambia "cha kwanza stop kabisa kujihusisha na mambo ya kishirikina,siku zote umekuwa ukitumia hizi pesa bila ya shida yoyote,mambo ya kuambiwa pesa haukutakiwa kuzimiliki aliyemiliki ameshaondoka je alikwambia kitu chochote?
Nikamwambia "hajawahi kuniambia kitu kibaya" akanambia "watu upata neema ya kupata pesa katika mazingira ambayo hayaelezeki,kuna mtu anawez akazitafuta pesa na asizitumie neema ikamuangukia mtu mwingine na akazitumia,haimaanishi yule mtu aliyepata ni kwa njia mbaya" huyu shemeji yangu tulizungumza kwa muda mrefu sana na akanambia kuna vitu nimeviweka kwenye biashara uenda hivyo pengine sasa ndio vinakula biashara yangu ili niendelee kutishiwa na niendelee kutoa pesa kwa yule mganga" nikipiga hesabu toka nimeanza kwenda kwa yule mganga pesa ngapi nimetoa kiukweli imefika hata milioni ishirini ambayo nimetumia kwa njia mbalimbali kwa maelekezo yake na vitu ambavyo alinipa nikaviweka katika maduka yangu ambapo naweka lakini nazidi kupata matatizo na huyu shemeji akiniambia "hivyo ambavyo umeweka ndio vinazidi kuharibu biashara yako,vinazidi kukupa hofu na hofu inakufanya wewe uendelee kutoa pesa na utaendelea kutoa pesa huku ukihofia kitu ambacho hakipo.
Hakipo Rojas na umewasaidia watoto yatima wale,umetoa sadaka zako,sadaka zako zimekuwa ni baraka,pesa hiyo ni pesa halali mtu huyo alikupa kwa upendo wa dhatina Mungu alitaka wewe uwe na pesa,unajua Rojas katika maisha tunaishi kuna watu wanapata pesa kwa neema ya Mungu tu,yeye mwenyewe ukimuuliza anasema nilihustle kweli lakini katika nyakati sielewi nilipata pesa,wewe ulibahatika kupata pesa katika mazingira ambayo Mungu aliamua kukupa pesa ila wewe ulipoikamata pesa ukajikuta unachanganyikiwa,unazifanyia anasa,unazifanyia katika mambo yasiyofaa lakini Mungu ni wa rehema,Mungu wetu ni wa upendo anakusamehe kabisa ndio kama hivi na maisha yanaendelea" huyu mama hakuishia tu bali alinambia "twende ofisi baada ya ofisi niambie hivyo vitu ambavyo umevificha uko unaogopa kuvitoa mimi nitavitoa" tukaambatana pamoja na yeye maana nilikuwa nimehifadhi vibuyu ambavyo vimefungwa na vitambaa,vibuyu na vidudedude vingi tu kwahiyo kila ofisi nikawa nimewekakwa siri mfanyakazi asione yaani kuhakikisha vinakuwa salama kwa ajili ya ulinzi na hivi vitu nimeanza kuvifanya baada ya kupata hofu na mimi kutaka majibu sana ya kile ambacho nimekuwa ninapitia,tulivitoa vyote katika maeneo yote,alivikusanya na yeye mwenyewe alivichoma moto na akasema "tunaye Mungu wetu asiyeshindwa na jambo lolote,hakuna pesa ambayo isiyokuma pesa halali,pesa zote ni za Mungu hakuna pesa ya shetani,hizo pesa za shetani ni za kwao lakini sisi hatutayasujudu hayo,hakuna uharibifu wowote utakaotokea tena kwa sababu vyote vyakuleta uharibifu visharudi kwao"

Huyu mwanamke ni shemeji yangu lakini alinitia moyo sana,akuishia hapo kwani alizidi kuongea na mimi,kukaa na mimi kwa upendo na akazidi kunishauri kuhusiana na yule mwanamke ambaye ameshakuwa sehemu ya maisha yangu akasema "lazima umtoe yule mwanamke katika maisha yako" yule mwanamke anafanya mambo ya kikahaba lakini ameshika akili yangu sana na nimejikuta natoa pesa nyingi kwake,akasema "huyu sio mke,huyu sio mke kabisa na Mungu atakusaidia kukuvusha hapo".

Tangu mimi nilipotoa vitu vyote vya kiganga sikuona shida yoyote yaani gari kudondoka wala matatizo yoyote kutokea,nikarudi nikaanza kuona amani inarudi na zaidi kumkumbuka rafiki yangu ambaye alinipa pesa,nikawekeza zaidi kwa hawa watoto mara nyingi zaidi ya ilivyokuwa kawaida na siku zilivyoendelea kusogea na nikazidi kuzipambania zile pesa ziendelee kudumu,ziendelee kudumu utajiri huu ambao ninaumiliki uendelee kudumu japo vipindi vya uchumi vinakuwa tofauti kuna kipindi mambo hayakuwa mazuri lakini sikudondoka kabisa,bado niliamka tena na kuendelea kupambana kila inayoitwa leo,kila inayoitwa leo kuhakikisha maisha yanasonga mbele.

Katika mengi ambayo yamekuwa ni faraja kwangu ni kuona watoto wa mshkaji wamekua na mmoja kati ya watoto wa mshkaji ameolewa na mimi nilisimama kama baba,nilisimama kama mtu muhimu katika tukio husika.
Muda umesogea sasa mimi ni baba wa familia niko na mke pamoja na watoto lakini sina kiwango kile ambacho nilipata cha nyakati zile pesa nyingi sana lakini sasa hivi nina pesa za kuweza kuendesha maisha yangu,kusaidia ndugu zangu,za kuendesha gari nzuri,za kuishi kwenye nyumba nzuri na maisha mengine yanaendelea.



MWISHO!
 
SHUKRANI SANA:

Ndugu zangu nawashukuru nyote kwa kutumia muda wenu kusoma mkasa huu wa Rojas na hapa ndio hitimisho lake,tukutane tena katika mkasa mwingine siku nyingine kwani haikuwa jambo rahisi ukizingatia kutoa maneno katika mfumo wa sauti kuleta katika mfumo wa maandishi kulileta changamoto kidogo ili kuweza kuifanya hadithi ibaki na mvuto wake ule ule,kuna baadhi ya maeneo ilinilazimu kuongeza nyama ili kuweza kuleta muunganiko kwani upande wa audio kulikuwa ama kukatikakatika,kukosekana kipande kirefu au episode kutosikika kwa zaidi ya dakika 10 hapo ikanibidi nijiongeze.
Mkasa huu umenipa mzuka wa kufanya kazi nyingine na nyingine na kama kuna mtu kati yetu anakifahamu kisa chochote kilicho katika mfumo wa sauti na akapendezwa tukilete jukwaani asiwe mchoyo aniPM nami ntatimiza wajibu wangu kama mwana jukwaa,mbarikiwe sana!
 
Daah kipande cha rojas na yule rafiki yake wa gerezani mpaka machozi yamenitoka alivyokuwa anamwambia rojas kuhusu pesa zake ukweli siku zote mchungu na unauma sana
 
Asante mkuu wa story nzuri nimejifunza kitu pia story ya Rojaz imeishia sehemu nzuri matarajio yangu nilifikiri jamaa atafirisika kabisa kitu ambacho nimeona mwisho still anapambana na biashara zake hongera Kwa kusimulia vizuri huo ni moyo wa pekee Mungu akubariki sana asante pia wa muda wako.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Daaah pole rojas ni kiasi gani umeumia sana kumpoteza rafiki yako inaumiza sana sana
 
Nashukuru kwa maoni yako,kiukweli ukisona hisia zinakuja kama Rojas atarudi ktk umaskini kumbe lilikuwa ni funzo kwake na kwetu pia,ubarikiwe
 
Huyu mganga kweli au rojas mbona mambo yanazidi kuogopesha
 
Kwenda kwa mganga fake kuliharibu kila kitu kikubwa kumrudia Mungu

Asante sana shikamkono ukipata story nyingine tuletee barikiwa sanaa
 
Shikamkono pls rudisha avatar ya mwanzo nimeangaika kutafuta hii story sisi wengine avatar ndio tunazishika mkuu nilikuwa najiuliza toka lini kukawa na arosto jamani
Nimekusoma cuzo ngoja niirejeshe kwa hisani,ile ni picha ya kijana na hii ni nembo ya timu yangu pendwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…