Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salute kwako,ubarikiweDB Cooper hakuwa tajiri ila alikuwa ni mfungwa aliyefungwa kwa kesi ya kuiba hela nyingi, Scofield alikalkuleti mambo yake na akawa na jibu kuwa Wesmoland ndio DB Cooper. Lengo la kumuweka kwenye mchongo wa kutoroka ni ili awasaidie pesa Scofield na lincoln watumie mbele baada ya kusepa USA.
T Bag hakuambiwa hela zilipo, aliyeambiwa ni Michael na mzee DB cooper mwenyewe, ila T Bag alikuwa karibu kwa hiyo alisikia map nzima. DB Cooper sababu alikuwa na kidonda kikubwa akaona hawezi kutoroka kwa hiyo akamwambia Michael aende kuchukua hela na amzike mwanae (mtoto wa DB Cooper) fresh kama ambavyo angefanya yeye DB Cooper.
Abruzzi aliwekwa kwenye mchongo sababu alikuwa anamtafuta sana mtu aliyemfanya afungwe jela (Fibernach), na jamaa alikuwa amemsnitch na kupata ulinzi wa CIA (Witness Protection), lakini Scofield aliweza kujua mahali Fibanachi alipo, akasema hamtajii Abruzzi, ila atamwambia watakapotoka nje ya jela, hivyo Abruzzi. Pia jamaa zake Abruzzi walikuja kumpiga mkwara akiwa jela wakasema wataua watoto wake akiwachoma, Abruzzi akaona hamna namna, inabidi atoroke ili aende kuilinda familia yake na kulipiza kisasi.
Fedha ya DB Cooper ilichimbwa na wote, Scofield, Sucre, C Note na T Bag ila sasa kwenye kuweka kwenye mabeg, T Bag ali-switch bags, moja aliweka vitabu na lingine hela, akawapa jamaa lenye vitabu yeye akaondoka na lenye hela
UbarikiweStory tamu
InavutiaDaaa inatisha
We jamaa wa mapacha kumbe umeona,ubarikiweIla Rojas anajichanganya sana, umeona jamaa alivyoficha Siri kwamba fedha alitoa wapi, mpaka amekufa ajamwambia Rojas. lkn Rojas ni mrahis sana kutoboka Kwa brother kuhusu fedha zilipotoka, maisha ni Siri, hakuna tajiri atakupa Siri ya mafanikio na Wala usitegemee. Maisha n Siri, story inamafunzo mazuri.
Eti niko pale😂Mganga atatengeneza tukio na Rojas anaenda kulizwa mkwanja wote. Niko paleeeee
Shikamkono pls rudisha avatar ya mwanzo nimeangaika kutafuta hii story sisi wengine avatar ndio tunazishika mkuu nilikuwa najiuliza toka lini kukawa na arosto jamaniUkawa unapiga miuno ya paka chongo mwenyewe[emoji23][emoji23][emoji23]
Daah kipande cha rojas na yule rafiki yake wa gerezani mpaka machozi yamenitoka alivyokuwa anamwambia rojas kuhusu pesa zake ukweli siku zote mchungu na unauma sanaMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Sitasahau’ cha Radio Free Africa
Sehemu ya 16
Baada ya kuhasi kwa muda mrefu kwa kutokwenda gerezani kumuona yule ndugu yangu kwani ilishapita miaka miwili na siku kadhaa toka mara ya mwisho niende kumtembelea yule ndugu leo nikaamua kwenda uko kumtembelea,kiukweli moyo wangu ulijaa usaliti sana kwa haya yote ninayoyafanya juu ya huyu ndugu kwani Rojas huyu wa leo asingekuwa Rojas kama sio fadhila za huyu ndugu na nikajiuliza sana hivi amewaacha watu wangapi na hadi kuja kwangu na kunipa yote haya leo ninayotamba nayo,ni huzuni sana!
Nikiwa nimenunua vitu ambavyo niliamini kwa mazingira ya gerezani vinahitajika na nikafika pale na kufanya kama utaratibu wa mtu anayekwenda kumtembelea mfungwa ufanyika na nilipotaja la mfungwa ninayekwenda kumuona nikaelezwa kuwa yule ndugu ameamishwa gereza na nikatajiwa gereza ambalo yupo kwa wakati huu,nikaondoka pale gerezani nikiwa na sononeko kubwa moyoni kwa haya yote ninayomtendea huyu ndugu,hivi ni kweli nimekuwa busy kiasi cha kufikia kusahau chanzo cha huo ubusy wangu kimeletwa na nani? Nilijihisi hatia kuawa ndani yangu na nikajiapiza iwe itakavyokuwa lazima nifike katika hilo gereza alilohamishiwa huyu ndugu mara moja,siku ya pili nikafika uko na kweli nilifanikiwa kumuona,hali yake niliyomkuta nayo iliniumiza sana,sana,sana kwani alikuwa amekuwa dhohofu sana,amepungua mwili,hali ya kukata tamaa ilikuwa inajionesha katika uso wake na machozi yalinidondoka kwa yale yote niliyoyafanya na nikikumbuka maneno yake,matumaini yake kwangu je imekuwaje leo namtenda kinyume mwokozi wangu huyu? Naye alinishangaa kwakuwa nilikuwa nimebadilika sana nimekuwa mnene kwa sababu maisha ambayo nimekuwa nikiishi mimi kwa pesa nilizopata mifumo ilikuwa imebadilika,starehe ambazo nilikuwa nafanya na utumiaji wa vilevi,kupenda kula kula nyama nyama na vyakula tofauti tofauti vyakupendeza machoni pangu vikanifanya kuwa na mwili mkubwa,nikawa na kitambi yaani nimeshiba kweli kweli na nimependeza sana kwahiyo wote tukashangaana lakini nakumbuka sentensi alinambia "nilijua tu,nilijua tu hauwezi kuwa vile vile kama ambavyo nilikuona lakini siwezi kuilaumu nafsi yangu kwa sababu niliyafanya kwa mapenzi mema sana lakini hofu yangu ni hii pesa kukumaliza mapema wewe"
Hii ni sentensi aliyonambia mara tu tulipoanza mazungumzo" nikamwambia "unapenda sana lawama,unajua umekuwa mtu wa kunipa sana msongo wa mawazo kwa sababu ya pesa,sikuwa naishi na msongo wa mawazo nikaona sasa bora nitulie nipunguze kuja ili niishi maisha ya amani kwa sababu kila nikija kuna kitisho kipya unanipa sasa kwanini niishi maisha ya vitisho? Tazama nimekuja tu unaanza kuniattack moja kwa moja kwa maneno ya vitisho,akanambia "haya nakusikiliza maana najua umefunga safari ukaenda pale na ukaambiwa sipo nimehamishwa na ukaja mpaka huku naamini kuna jambo ambalo limekuleta huku" nikamwambia "nimekuja kukuona na pia kukujulisha kuhusu hali ya watoto wako" akasema "ni muda sana na nilishapoteza hata matumaini,mimi ni mtu ambaye nimeshasahaulika kama wewe ndio ulikuwa unakuja na nilibakiza tumaini pekee wewe na wewe tena ukaingia mitini basi nikapoteza tumaini,lakini nafurahi nimekuona na naona sasa umeingia katika muonekano mpya,naona umenenepa sana,pesa zangu zimekunenepesha sana,naona pesa zangu zimekupa kitambi lakini haukutakiwa kutumia hivyo pesa,pesa zina kanuni zake kwani haiwezekani kwa sababu una pesa ukawa una kulakula tu unakulakula tu,unatakiwa unakula na pia unatenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa imara kiafya kwa sababu mwisho wa siku wewe utapata magonjwa na ukipata magonjwa ni hatari kwa sababu unaweza kufa cha ghafla" alinambia maneno hayo sikuyapenda nikachukizwa nayo sana,nikamwambia "kwahiyo ni hayo tu baada ya kutokuonana kwa muda mrefu" akanambia "naweza nikakwambia kipi ambacho kinaweza kukurudisha katika uhalisia ule wa Rojas ninayemfahamu mimi ambaye ni kijana aliyekuja gerezani akiwa amesingiziwa kesi,amekuja akiwa amechoka,ni kijana ambaye hana chochote aliyeshindwa kujipigania ili atoke mapema kwa kesi ndogo iliyokuwa inamkabili lakini akajikuta anakaa mwaka unakaribia lakini leo ni mtu mwingine,leo ni mtu mwingine naona hata kuongea kwako kumebadilika kabisa,ni masikitiko yangu kwa sababu pesa niliyoitafuta kwa bidii yote inaenda kunaliza kijana ambaye familia ilikuwa inamtegemea sana" nikamwambia "tuzungumze mambo mengine,tuzungumze mambo mengine"
Akanambia "nimejua wapi tatizo lilipoanzia" nikamuliza "kwanini unasema hivyo" akasema "kwa sababu uliitoa siri yetu kwa watu na baada ya kuitoa siri yetu watu wamekuharibu kiakili ili wakutumie,ili uwanufaishe na wamefanikiwa kukutumia sana tazama nikikutazama machoni mwako hata sio wewe unayezungumza sasa ni mtu mpya kabisa ambaye amezaliwa ndani yako,utaisingizia pesa ni kweli pesa inabadilisha watu lakini niamini mimi kuwa watu wa karibu wameshaiharibu saikolojia yako wameshakutumbukiza katika mambo ya uovu ili waendelee kujinufaisha na mwisho wa siku watakumaliza,kwani wewe haujaanza kutumia madawa ya kulevya? Nikashtuka na nikamuuliza "kwanini unaniambia hivyo? Akanambia "moja kati ya uteja mbaya kabisa ni huo watu wengi ambao ni wajanja hapa mjini uwafata watu ambao wana uwezo kifedha au wao kama hawawezi kufanikiwa basi watoto wao uwaingiza katika magenge ya madawa ya kulevya maana wanajua pesa za kuchuma mahali zipo basi watu hawa utumika sana kwa sababu arosto uwa zinawasumbuawatajikuta wanamaliza pesa zao zote mpaka wanabaki masikini, lakini ni akina nani wanafanya hayo? Wala si watu wa mbali na wewe,ni walewale unaotoka nao,ni walewale unaowapenda,ni walewale unaokula nao bata,ni walewale ukipata tatizo unawapigia simu kuomba ushauri hawa ndio maadui zako"
Mpaka sasa hivi nikikwambia mengi nimefanya kama kufanya starehe ninao washkaji ambao wameniambia "Rojas unatakiwa upate kitu ambacho unatakiwa ufeel vizuri yaani unajisikia vizuri na gharama hata sio kubwa kwahiyo nimeshaingia katika huo ulimwengu yaani anazungumza hapa kuhusu hilo jambo mimi nimeshajiconnect umo ni katika mazingira hata nikikueleza niliingiaje mpaka kufikia kutumia hivyo vitu sijui hata lakini tu katika mambo ya starehe starehe nikajikuta na mimi nimeingia na wao wananiambia hii ndio the best zaidi kwahiyo nimejikuta pia naweka pesa uko kwa ajili ya kupata hizo feelings ambazo nimeanza kuzipata baada ya kutumia iko kitu kwahiyo mtu huyu anazungumza kana kwamba yuko nje,yaani anavyozungumza kana kwamba anajua hatua zangu,anajua mimi nimefikia wapi yaani anajua mpaka sasa hivi nipo katika mazingira gani kwamba hujaanza kutumia hiki kitu,akanambia "Rojas ukiwa na pesa alafu ukawa mpumbavu pesa zako zitatumika na wajanja wenye akili nyingi mjini,unataka kutajirisha watu,wakati unatajirisha watu huku unaathirisha afya yako,ungekuwa na watoto wakati wewe ni mtu mzima wangekuwa wanatumia mbinu kuwaattack watoto wako ili wajiingize katika hayo magenge,unajua huo mtandao ni mkubwa kiasi gani?
Huo mtandao ni mkubwa kwani leo hii unaweza kuwa hapa Tanzania unafanya biashara zako,unainvest katika vitu vyako wewe hawajakunasa lakini una mtoto wako umempeleka mahali flani,umempeleka nchi flani wao kwa sababu wanajua pesa zinaweza kuchumwa wanaweza kutuma mtu wao,wanaweza wakacreate mtu wao uko watahakikisha anakuwa close na mtoto wako na mwisho wa siku mtoto wako anaingia katika 18 na akishaingia katika 18 basi pesa za wewe zitakuwa zinanyonywa kupitia mtoto wako maana watamuharibu kabisa na mtoto wako hataweza kustahimili bila ya kupata chochote cha kumpa starehe hiyo ambayo itakuwa imeshamuhathiri,wewe unaingia umo katika magenge hayo,mtu ambaye umeishi katika maisha ya umaskini ukiwa mtaani,umehustle hata kupata elfu kumi kwa siku,leo umepata pesa unaenda kuwatajirisha watu?"
Nilisikia maneno yamepenya kabisa yaani yameingia ndani katika moyo wangu na nikajisikia vibaya sana,akanambia "Rojas mimi nakupenda,mimi nakupenda upendo wangu kwako mimi ni mkubwa toka siku nimekupokea kama mdogo wangu gerezani Mungu ni shahidi katika hilo,sijawahi hata siku moja kukutoa katika maisha yangu hata pamoja na wewe kunitelekeza,sijawahi kumshirikisha mtu mwingine siri hii ili aje akufanyie ubaya ili ile pesa mimi niichukue nimpatie mtu mwingine kwa sababu nilikuamini toka siku ya kwanza na wewe Rojas ni mtu mzuri ila umeruhusu watu wabaya wameharibu moyo wako,wameharibu uhalisia wako,wamepanda mapando mabaya ndani yako,Rojas hivi pesa unataka ikuzike,yaani kwakuwa umekuwa tajiri pesa unataka ikuzike yaani unafikiri unaweza kumaliza wanawake wote yaani wanawake wote,kuna wanawake wazuri ajabu yaani unazungumza wanawake wa nchi moja ambayo umeishi labda na hizo umeenda lakini Rojas kuna wanawake wazuri wana muonekano wa kuvutia unaweza kumuangalia muda wote lakini wazuri hawaishi wanazaliwa kila siku,huwezi ukawamaliza wewe ndio utamalizwa" maneno yake yalinichoma sana nikajikuta nasema "sielewi,mimi sielewi nahisi kuchanganyikiwa mimi sielewi (nikitaja jina lake),akanambia "najua,najua Rojas pesa ambavyo zinaweza zikambadilisha mtu hasa watu wabaya wanavyoingia" nikawa mpole sana kwakuwa maneno yalikuwa yamenigusa sana,akanambia "Rojas hata siku moja mimi siwezi kukunyang'anya hizo pesa lakini sio furaha yangu pesa hizi zikuzike mapema hata kabla yangu mimi,natamani uishi,uoe mke sahihi upate familia,familia yako inufaike na mali ambazo umezipata,unataka uishie bila familia?
Nikamwambia "hata sielewi,sielewi,sielewi" akanambia "bado haujachelewa wameshatumia pesa yako sasa hivi inatosha bado haujachelewa waweza kubadilisha njia ambayo ulikuwa unapita na ukaenda katika njia nzuri" nami nikamwambia "kama unajua yote haya kwanini bado unaongea na mimi vizuri,kwanini haujachukia?" Akasema "wewe ni mdogo wangu Rojas,wewe ni mdogo wangu" maneno ambayo yalinigusa sana kweli,kiukweli nimemkosea mtu huyu,ahadi nilizompa sijafanya lakini hajaanza kunifokea na kunisema kwa mabaya ila ameniambia ukweli ili niweze kubadilika na akanambia "sasa hivi niko mbali na mahali uliko lakini unapopata nafasi usiache kuja kunitembelea afya yangu imekuwa dhaifu pengine siku utakuja na ukakuta mimi siko tena" nikamwambia "nini shida,nini shida" akanambia "maradhi tu" nikamwambia "niambie" akaniambia "naumwa sana,naumwa sana,afya yangu imekuwa dhaifu figo yangu moja imefeli kabisa na unajua tuliko huku tupo tu"
Niliguswa sana kwa sababu huyu mtu sikumtembelea muda sikujua hata mapito anayopitia nikajisikia kujihukumu sana katika haya,naikumbuka sana siku hiyo,naikumbuka sana siku hiyo kwa sababu ilizaa jambo jipya katika maisha yangu,inawezekana,inawezekana ni pesa imenibadilisha mimi,inawezekana ni watu wamenibadilisha,inawezekana nimebadilishwa na maneno ya watu ambayo yamekuwa yakipandwa kwangu yaani kile nimekuwa nikikipokea ndani ya moyo wangu kuhusiana na mtu mwenye pesa "mbona unakaakaa tu kama mtu ambaye hauna pesa bwana" labda hayo yamepandwa sana ndani yangu au inawezekana mimi nachezewa,labda nalogwa yaani mbona sijielewi yaani.
Aliendelea kuniambia "Rojas hizi pesa nikikuambia mimi nilipozitoa,nikikwambia pesa hizi nilikozitoa hukutakiwa kutumia hata senti moja kwakuiteketeza tu,Mungu anisamehe,lakini pesa hii ambayo wewe unaiteketeza leo hii ilitakiwa ilipe gharama ya mengi ambayo mimi nilifanya katika nyakati za utafutaji wangu na nilipanga nikiwa uraiani nitayafanya hayo lakini naona mwenzangu umeshindwa,umeshindwa lakini kama nilivyokwambia waweza kurudi katika maisha yako na ukafanya vizuri tu,mimi nakuamini unaweza" nikaachana na mtu huyu na hayo ndio maneno aliyoniambia.
Nilifunga safari na kurudi zangu nyumbani lakini nilikuwa ni mtu niliyeinama moyo wangu umekosa raha kabisa yaani sina raha,nilipigiwa simu na washkaji yaani ukiwa na pesa simu yako inapigiwa zaidi ya mtu asiye na pesa,ukiwa hauna pesa yaweza pita siku nzima haujapigiwa simu lakini mimi napigiwa simu mpaka naamua kuzima,nikifungua meseji nakuta meseji nyingi huyu anaomba hiki,huyu anataka hiki,huyu anataka urafiki,huyu anataka tutoke tena meseji za wanawake ndio nyingi lakini nilijikuta nimekuwa down kabisa,mimi ni mtumiaji wa kilevi sana lakini sikuwa hata na hamu yakusema nitoke nikapate hata kilevi najikuta niko ndani na moyo wangu unaugua sana.
Katika nyakati moyo wangu unaugua sana mke wa rafiji yangu ambaye huyu mama amekuwa akinishauri shauri mambo ambayo sijawahi kuyapokea,alikuwa akiniambia "pesa sio kila kitu katika maisha,waweza kuwa na pesa na ikakugeuza kuwa mtumwa,Mungu anapotawala pesa zako yeye atakupa amani ya moyo,unaweza kuwa na pesa lakini inaweza kukuondolea amani wewe mwenyewe ya moyo" sasa wakati niko katika mazingira kama hayo huyu mama alinipigia simu n huyu mama uwa akipiga simu unikumbusha majukumu ambayo napaswa kufanya katika kile kituo cha watoto yatima(wakati ule nilipoenda kwake alinishauri kutoa sadaka yangu ya shukrani kupitia kituo flani cha watoto yatima nami nikaafiki),nilipokea simu na huyu akanambia "shemeji unaendeleaje? Nikamwambia "naendelea vizuri""nimekukumbuka tu niko hapa nimekaa nikakukumbuka sana nikasema hata nisikie sauti ya shemeji yangu na siku mbili tatu hizi nilikuwa nasikia mzigo ndani yangu na najisikia kukuombea na sijui unaendeleaje" nikamwambia "naendelea vizuri" huyu mama akanambia "Rojas sadaka zako ambazo umekuwa ukitoa kwa yatima,sadaka zako ambazo umekuwa ukitoa kwa wahitaji tangu umeanza kutoa kwa moyo wako wa dhati kwa uaminifu naomba nikwambie umewaponya watu hawa kwenye mengi wanakuombea kila siku na wana ratiba za ibada na kwenye kila ibada zao wanataja jina lako Mungu akukumbuke katika kila jambo,naamini maombi ya wahitaji hawa,wasiojiweza yatima hawa Mungu atakugusa nawewe pia" sikuwa na mengi yakusema nikamwambia shemeji "niombee,niombee shemeji yangu" akanambia "ni nini mbona nasikia sauti yako iko down sana?" Nikamwambia "sina hata raha sijui kwanini sina hata amani,sina amani kabisa" akanambia "tunaweza tukaonana tukaongea" nikamwambia "labda twende tena kwa wale watoto,twende tukawatembelee labda tukaarrange tupate nao chakula pamoja" akasema "sawa basi mimi ntafanya hivyo" nikasema "sawa basi utatoa taarifa alafu utamcheki mhasibu na kila kitu aweke sawa.
Yaani nimetoka gerezani amani furaha imekata,yaani nilipokutana na yule kaka ambaye amenipa utajiri kila kitu kimekata,kama ambavyo tulikubaliana na huyu mama kweli nilipata muda na nikaenda kwa watoto hawa ambao nilipoenda kwa mara ya kwanza niliguswa sana na maisha ambayo wanaishi,niliguswa kufanya kitu kwani nimekuwa natumia pesa zangu kwa makahaba,nikitumia pesa zangu kwa starehe mbalimbali nikaona basi nifanye hata kwa ajili ya watu hawa lakini ni huyo mama ndio alinipa mwongozo kama nitakapoweka kwa watu wahitaji kama hawa basi ulinzi utaambatana pamoja na mimi na mimi sifanyi uchawi wowote,yaani mimi ukiniuliya kwa Mungu sipo kwa shetani sipo yaani mimi hizi pesa nimepata yaani sio kwa namna ya nguvu za giza za kishirikina kwamba kuna masharti ya kumwaga damu na nini,hizi pesa nimepata katika mazingira ambayo nilishayaeleza,nilienda kuzichimba mahali nikazimiliki zikawa za kwangu lakini kwa Mungu sipo yaani kwamba na muda nimetenga sijui msikitini,sijui kanisani yaani mimi ijumaa,jumapili ni siku za mishe zangu kama kawaida kwahiyo pesa zangu hakuna kitu ambacho kinakipa ulinzi na huyu mama ni moja ya kitu ambacho aliniambia "hayo ni maisha mabaya na hatari sana lazima uchague kati ya sehemu mbili ukiwa vuguvugu utapigwa,utaangamizwa" mengi aliniambia huyu mama kwahiyo tumekuja huku nilipata faraja,watoto hawa wanaimba kwahiyo tuliimba,tukapata chakula nikajikuta kama napata relief napata unafuu ndani yangu baada ya kukaa na hawa watoto kwa muda na nilikaa nao sana kwa muda mrefu na shemeji ameona jinsi nikifurahia maana nilikuwa mnyonge lakini nikafurahia kupata chakula na mengi yaliyofanyika pale na nikatoa ofa nikasema "na kitu kingine ambacho kitahitajika mimi hii ni familia yangu mimi niko na nyinyi kuhakikisha hii safari tunafika pamoja" kwahiyo nikajisikia kufanya vitu vingi nikiwa hapa lakini nilipata unafuu mkubwa na hata nilipata nafasi ya kuongea na shemeji nikamwambia "shemeji nasikia angalau nasikia kama moyo umetulia kidogo" akanambia "nini shemeji yangu,nini kinausonga moyo wako,nini kinakukosesha raha mimi niko hapa na mimi ni mtu sahihi sana kwako unajua nishirikishe hata kidogo" nikamwambia "ni mambo mengi,ni mambo mengi sana shemeji yangu,nakosa hata wapi nianze,wapi nianze kuzungumza na hata kinywa changu ni kizito kuweza kuzungumza" akanambia "sawa shemeji yangu kwani unaweza kuona ni ngumu kuzungumza na mwanadamu mwenzako lakini Rojas shemeji yangu yuko Mungu waweza kuzungumza nae,Mungu ni wa sisi sote haijalishi una dhambi kiasi gani,haijalishi watu wanakuona haustahili kwa kiasi gani lakini Mungu wetu ni Mungu wa rehema unapokwenda mbele zake na kumwambia Mungu mimi wewe ni baba yangu sina mwingine naweza nikazungumza nae,nimekuja mbele zako sikia haya ambayo yamejaa kwenye moyo wangu tamka kwa kinywa chako Mungu anasikia na Mungu atakupa majibu,unaweza kufanya hilo zoezi kuanzia leo unapofika nyumbani kabla ya kwenda kulala zungumza hayo maneno mwambie Mungu unanisikia uko karibu na mimi zaidi kuliko akili yangu inawaza hata hapa uko na mimi,mwambie Mungu vile unasikia moyoni mwako atakupa majibu" alirudia kunambia maneno hayo mara mbili na nilimwambia "sawa" na hakunilazimisha niseme kilicho ndani yangu kwa sababu nilimwambia mdomo wangu ni mzito akanambia "nenda kamwambie Mungu,usijihesabie kuwa wewe ni mchafu usiyestahili mbele ya Mungu,Mungu pia anawahitaji walio wachafu,anawahitaji pia na anawasikia pia"
Sina utaratibu wowote katika maisha yangu wa kuwa na muda kusema nitenge japo dakika ngapi niseme na Mungu ambaye simuoni yaani mimi naamini Mungu yupo lakini ule muda wa kutenga kuanza kujieleza yaani kwa njia hiyo ya maombi sasa hapo kwangu imekuwa ni kazi kweli kweli lakini kukosa amani na mashauri ambayo nilipewa na shemeji yangu niliona angalau nitoe hata dakika mbili nitoe labda naweza hata kupata nafuu,kuna vitu huwezi kuongea na mtu kwa sababu huwezi amini katika starehe zote ambazo nimefanya sijatoa siri zaidi ya kumueleza kaka,hakuna mtu anajua vingi zaidi,kijiji nilichoenda na mengi zaidi sijayazungumza haya,ndipo nilipopata muda wa dakika chache kusema na Mungu.
ITAENDELEA!
Asante mkuu wa story nzuri nimejifunza kitu pia story ya Rojaz imeishia sehemu nzuri matarajio yangu nilifikiri jamaa atafirisika kabisa kitu ambacho nimeona mwisho still anapambana na biashara zake hongera Kwa kusimulia vizuri huo ni moyo wa pekee Mungu akubariki sana asante pia wa muda wako.SHUKRANI SANA:
Ndugu zangu nawashukuru nyote kwa kutumia muda wenu kusoma mkasa huu wa Rojas na hapa ndio hitimisho lake,tukutane tena katika mkasa mwingine siku nyingine kwani haikuwa jambo rahisi ukizingatia kutoa maneno katika mfumo wa sauti kuleta katika mfumo wa maandishi kulileta changamoto kidogo ili kuweza kuifanya hadithi ibaki na mvuto wake ule ule,kuna baadhi ya maeneo ilinilazimu kuongeza nyama ili kuweza kuleta muunganiko kwani upande wa audio kulikuwa ama kukatikakatika,kukosekana kipande kirefu au episode kutosikika kwa zaidi ya dakika 10 hapo ikanibidi nijiongeze.
Mkasa huu umenipa mzuka wa kufanya kazi nyingine na nyingine na kama kuna mtu kati yetu anakifahamu kisa chochote kilicho katika mfumo wa sauti na akapendezwa tukilete jukwaani asiwe mchoyo aniPM nami ntatimiza wajibu wangu kama mwana jukwaa,mbarikiwe sana!
Daaah pole rojas ni kiasi gani umeumia sana kumpoteza rafiki yako inaumiza sana sanaMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Sitasahau’ cha Radio Free Africa
Sehemu ya 17
Nilipata muda kweli kwa sababu moyo wangu ulijaa vitu na mtu ambaye labda naweza nikazungumza nae kwa uhuru pengine nikazungumza zaidi ni yule kaka wa kule gerezani kwani ndio anayejua mambo yanayoendelea kwenye maisha yangu lakini nimekuwa nikitunza siri nyingine kwa kuwa kaka nilishawahi kumshirikisha japo sikumshirikisha kaka wapi pesa zangu natunza,mifumo yangu ya pesa iko vipi ingawa kaka alijitahidi kwa hali zote lakini kwa hilo hakufanikiwa pengine amefanikiwa yale aliyoyaamini ni ya maana sana kwa sababu kaka yangu amefanikiwa mpaka kujenga,kiukweli nimegeuka kuwa baraka kwa familia yangu sio kama najisifia kiukweli sikula pekeyangu kwani hata sasa hivi nakosa amani mimi ila kuna watu wanafurahia pesa ambazo nimezipata,nakumbuka maneno ambayo nilimwambia Mungu. Unaambiwa Mungu ni wa sisi sote,Mungu ni wa wote wenye mwili haijalishi,ni maneno ambayo niliambiwa na yule mama na ni kweli mimi najua hivyo lakini kuyaishi katika hilo ndio shughuli,nalijua hilo na navyoambiwa tena na tena nakuwa napata msisitizo na ninakumbushwa kile ambacho najua.
Nilizungumza maneno haya "Mungu mimi ni mkosaji sana mbele zako na pia nimemkosea rafiki yangu ambaye nilishawahi kuapa mbele zako kwamba nitafata yale aliyoniambia lakini nimeenda kinyume na vile niliwahi kuahidi,nasikia huzuni ndani yangu,nasikia kukosa raha ndani yangu,naomba Mungu wangu unisaidie,naomba kwanza unisamehe lakini pia unisaidie,hali ya huzuni ninayoisikia,kukosa raha ninakokusikia kusiendelee kudumu katika maisha yangu" sikuwa na mengi yakusema kwa sababu na mengi yakusema na Mungu yapi? Yaani sina kwa sababu pia mimi sikuwa muombaji kwamba najua kuomba na nini kwahiyo nilizungumza hayo kwakuwa ndio yalikuwa yanajaza moyo wangu.nilichokuwa nataka ni amani ya moyo,hicho tu ndio nahitaji,ushawahi kukosa amani? Pengine katika maisha ushawahi pitia situation kama hiyo yaani unakosa amani kabisa,unakosa raha kabisa,yaani hiyo hali ndio mimi naipitia kwa sasa hivi.
Nakumbuka baada ya kuzungumza maneno hayo nikalala na kukapambazuka na yule shemeji yangu alinipigia akanambia "vipi Rojas unajisikiaje? Nikamwambia "najisikia vizuri" akanambia "muda wowote,wakati wowote ukitaka kwenda pale kituoni waweza kwenda pale ukakaa na watoto kwani ni faraja tosha sana "nikamwambia "sawa nikijisikia ntafanya hivyo"
Wakati hizi harakati zote kuanzia yule mshkaji wangu dereva taxi kunialika kwake,mke wake kuniambia juu ya kujiepusha na shetani na kumrejea Mungu hadi harakati za kwenda kule katika kituo cha watoto yatima na kufanya haya maombi kwa Mungu mtaani nilikuwa na mwanamke ambaye ndio alikuwa amenishika hatamu,huyu mwanamke kiukweli amekuwa kwenye maisha yangu kwani nimekutana na wanawake wengi lakini huyu alifanikiwa kuninasa kwa sehemu kubwa sana vitu vingi sana nimeshamfanyia kwani nimewekeza,nimewekeza na nimewekeza tena yaani nimekutana na mwanamke ambaye anajua kuchuna,kweli nimetumika na nikakubali kutumika kwa sababu nilimpenda mwanamke huyu,kwahiyo hata yeye ananiuliza "beby vipi mbona sikuelewi? kwa sababu anaona si kawaida yangu "au umesharudi kwenye mambo yako? Yaani nimesharudi kujichanganya tena na wanawake wengine kwa sababu yeye ndio mwanamke aliyefanikiwa sana kunikamata yaani kwa sababu anajua mimi nina kona kona kwahiyo muda mwingi akawa ananishika na mimi kwa sababu nampenda nikajikuta kuna muda hata naona ngoja nikae na huyu,ngoja nikae na huyu kwahiyo hata idadi ikapungua na hata kuna wanawake walizidi kunisumbua kwa sababu mimi ni mtu wakutoa sana pesa na sio hivyo tu kuna wanawake nilikuwa nimewapangia,kuna wanawake walikuwa wanaendelea kusoma vyuo uko mimi ndio nalipa ada kwahiyo sasa wanakucheki tena ili uweze kuwawezesha sasa huyu mwanamke akawa ananibana kwelikweli kwani hata simu akawa anapokea yeye "wewe ni nani nakuuliza wewe ni nani?" kwa sababu mimi nilikwama hapa sikuona shida hata nikiwapoteza hao,yaani sio muhimu kwangu,kwahiyo alipoona hali kama hiyo kwangu alinambia "ni nini ambacho unapitia? Nikamwambia "nina hali naipitia sio ya kawaida,sina amani,moyo wangu hauna amani" "kwanini sasa? Nikamwambia "hata sielewi" akanishawishi kuhusu pombe na nini lakini kuna hali flani unafikia ya kukosa amani hata pombe ukinywa haisikii,yaani mi nasikia roho inaangaika tu inaangaika kweli kweli na hata akanambia "au wenzako wanaanza kukuchezea? michezo ya kuchezeana hivi labda kulogwa,nikasema "hata sijui" "eeh kwa sababu gani usikie hivyo,kwanini usikie hivyo wakati una vitu vyako unavipenda ukivifanya uwa unaskia raha? Mengi ambayo aliniambia hata washkaji waliniambia kwa mfano niliwaeleza nilishaanza kutumia vilevi mbalimbali mpaka madawa ya kulevya nikawa nimeshaingia umo lakini sikusikia relief,sikusikia nafuu yoyote.
Baadae nakumbuka nilipokaa nikiendelea kupitia katika hali kama hii niliamua kutoka tena na kwenda tena kumuona mshkaji kule gerezani,nimefika hapo nikaambiwa hali yake ilikuwa sio nzuri yupo anapata matibabu nikafosi sana mimi nipate nafasi ya kumuona tuzungumze nae,nikapewa tarehe niweze kuja ili naweza nikamuona,mambo yakawa ni mengi,utaratibu ukawa umenivuruga kwelikweli lakini nikawa siko sawa lakini nilipigania hilo,nilipigania kumuona hadi nikapata nafasi ya kumuona rafiki yangu ambaye nilimuhesabu kama kaka yangu,mengi tulipanga pamoja nyakati ambazo nilikwenda gerezani lakini baadae nikabadilika,nikambadilikia nikaishi katika njia yangu na nikaiacha njia yake ambayo yeye aliitamani aiishi akiwa uraiani,nilipata nafasi ya kumuona kiukweli alikuwa mgonjwa sana,nasikia hatia ndani ya moyo wangu,mshkaji ana hali mbaya,ana hali mbaya sana na mimi ni kama ndio ndugu niliyebaki,yaani kuna watu wamefungwa gerezani,yaani watu wanasahaulika,unasahaulika na vizazi vyako wote wanakusahau wewe,hakuna watu wanakuja kukutembelea,hakuwa watu wanakuja kukuona yaani wewe uko uko pambana na mazingira yako ndio hali ya mshkaji na mshkaji aliniamini sana mimi na akiamini sitamuacha kama ambavyo nilivyomuacha kwahiyo sasa hivi mimi kinachonipitisha katika wakati mgumu ni kusikia hatia ndani ya moyo wangu lakini Mungu ni mwema.
Mungu alimsaidia akarecovery akarejea katika maisha yake ya kawaida hicho ndicho kitu nimemshukuru sana Mungu,nikamwambia "natamani niwe sehemu ya mtu ambaye tutaipigania afya yako iweze kuamka tena,uweze kupata matibabu ya uhakika na mimi kwa sababu niko hapa sitakuacha uondoke kwa huo ugonjwa,tutapigana kadri tunavyowezakwa sababu madaktari wanasema kuna njia tu nzuri ya kupata matibabu" nakumbuka aliniambia "kama itakupendeza hivyo basi nitashukuru" alikuwa amepunguwa sana mtu huyu,nikamwambia "basi sawa" akaniuliza hali za watoto nikawaambia wanaendelea vizuri na akanambia "Rojas waweza leo kugeuza kichwa chako na kunigeuzia kisogo chako na kuanza safari kwenda kwenye majukumu yako lakini kuna siku Rojas utakuja na hautanikuta na pengine utaambiwa tayari nimeshazikwa" nikamwambia "hapana kwanini unasema hivyo,usiseme maneno kama hayo" akanambia "Rojas mimi nimeshakusamehe na hata kama utakuja hapa na ukanikosa mimi nimeshakusamehe Rojas.
Nimekusamehe wewe na kizazi chako wote nimewasamehe,nilifanya kwa mapenzi yangu lakini nimeona vile moyo wako umerudi,umenipigania sana kwa mazingira magumu ambayo si rahisi lakini umepenya,umehakikisha napata matibabu,umenipigania na hata watu wanauliza ni nani huyu anayempigania mtu huyu amesahaulika humu gerezani na hata watu wanataka kujua ni nani huyu anayempigania lakini kumbe umerudi katika ule urafiki wetu wa mwanzo,umerudi kwenye undugu ule ambao tuliuanzisha mwanzoni na mimi hata leo Mungu ananichukua napumzika nitakuwa na amani kwa sababu najua kama umerudisha mapenzi kwangu ndivyo utakavyoendelea kuwakumbatia watoto wangu ,ndivyo utakavyowashika mpaka wakuwe wakubwa na naamini wewe utashiriki katika baraka na mafanikio yao,hautawaacha,utawafanya sehemu ya familia yako" maneno yaliniumiza sana na kunifanya kujisikia kuumia sana,mtu huyu anawapenda watoto wake sana lakini maisha yanavyokwenda tofauti na jinsi ambavyo mtu unaweza ukawaza,mtu ambaye amesahaulika gerezani na anaonekana atadumu maisha yote uko matumaini kwenye mioyo ya watu haipo na huyu mama ni kitu ambacho alikataa yaani mama wa watoto ambao alipaja na huyu baba alisema "
Hata siku moja usije ukawatonesha watoto wangu vidonda ukaenda kuwaonesha baba yao ambaye alifanya uovu na yuko gerezani na atafia uko uko gerezani,sitaki watoto wangu wawe na kumbukumbu za kuwaumiza mimi mama yao nipo na nitapambana,ndugu zake akina nani wote walishamtelekeza" kwahiyo nilisikia pain sikutakiwa kumtenda haya mtu huyu pengine mimi naye tungeshikamana kwa mazingira yoyote labda apate haki,apate uhuru kwa sababu kwa maelezo huyu mtu alifungwa kwa kile ambacho anastahiki,nilimwambia "rafiki yangu,ndugu yangu najua ninaondoka nitarudi nitakukuta na tutazungumza pamoja na naondoka mimi nikiwa na mawazo ya kwamba matibabu sahihi yanahitajika,kukupigania nilikokukupigania sasa hivh naenda hatua ya mbele zaidi kwa pesa hizi ambazo zipo nataka kupenya mahali ambapo sio rahisi kupenya ili wewe upate matibabu sahihi iwe kwa kuhonga,iwe kwa kufanyaje mimi ntafanya kwa ajili yako" aliniambia "sawa basi utaenda kuwasalimia pia nyumbani,Rojas pata mke sahihi,oa,oa mke sahihi mwenye upendo wa kweli jenga nae maisha upate nae watoto.watoto ni baraka usiendelee tu kuwa na wanawake wa kila namna,wakati ufike uoe na ujenge maisha yako yenye furaha" yaani nikawa nakinzana na maneno anayoyazungumza kwa sababu naona kwanini aniambie hivi na wakati mimi ntarudi na harakati za matibabu zitaendelea.
Niliondoka japo sikutaka kuondoka,nilikaa hapa toka nimekuja kujua mgonjwa kwa awamu hii sikutulia ina maana niliendelea kuhakikisha mtu huyu anapata matibabu,nikakaa wiki mbili nikiwa mbali kabisa na mazingira yangu,nimerudi mtu ukiwa na pesa na una kundi kubwa sana la watu unapokuwa hupatikani huonekani kuna watu wanateseka ,kuna watu wanataabika kweli kweli wote wanataabika uko wapi wakati umeshawajuza kuwa niko mbali kidogo nina majukumu yangu binafsi,watu ambao wamezoea kufanya starehe na wewe wanapata shida kweli kweli.
Kwahiyo niliporudi kampani yangu inataka tujoin tena inataka kula raha na maisha mengine yaendelee,nakumbuka nilikataa,nilikataa nikasema "siko sawa leo,nahitaji muda wa kupumzika lakini nitalipa bili,chochote mtakatumia ntaniambia mtaclea bili ntalipa" walistahajabu yaani mimi Rojas nina nguvu hizo za kutoa wapi kwa sababu chakula changu ni pombe na ni sehemu ya starehe na mimi mara zote uwa nasema hakuna starehe nyingine zaidi ya pombe,pombe ndio starehe,mwanaume unatakiwa unywe pombe,mwanaume unatakiwa uwe na watoto wazuri yaani wanawake warembo ndio furaha ya mwanaume,nini unaweza kufurahia mwanaume unafanya kazi kwa bidii pata muda uenjoy katika hivyo vitu,kwahiyo mimi ndio nimekuwa naviona vilevi na wanawake ndio starehe yangu lakini sasa najiona nimekata mood kabisa,siko sawa,mimi ni mlevi sana lakini ukiniuliza nasemaje sina mood nikashindwa kunywa pombe kwa wale watumiaji wa vilevi wanaelewa yaani ukiwa na msongo wa mawazo ukataka kushushia kidogo angalau uwe sawa lakini mimi siko sawa nasema sijisikii kunywa ,hayo ni mabadiliko mapya ndani yangu kwa sababu hata washkaji waliniambia hauko sawa,kwa tunaokujua wewe hauko sawa,wako marafiki wao furaha yao wewe ulewe,wewe uchangamke kwa sababu kuchangamka kwako kunakufanya wewe ufanye ya zaidi ambavyo ungekuwa kawaida usingevifanya sasa kwa mfano kama mshkaji amekwambia "mshkaji hapa ana shida ya hela" "shilingi ngapi? "Milioni" ukiwa na akili timamu utasema "ah mshkaji wewe si nilikupa siku flani tena" lakini ukishalewa mtu akikupa sifa "aah Rojas wewe ndio mwenyewe bwana,wewe ndio baba lao,hakuna mtu kama wewe Rojas" unaona pombe pamoja na sifa zinaenda kwelikweli unajikuta unasema "kitu gani,baadae njoo uchukue ile hela" hata kama mwanzo ulikuwa haujaplan lakini kwa sababu ya sifa unajikuta unafanya,kwahiyo wale washkaji wanasikitika nini nimepatwa na nini lakini ni mabadiliko automatically nilianza kuyaona kwangu lakini ni nyakati ambazo niliendelea kushikilia msimamo wangu mpya.
Nilipata wasaa wa kwenda kuwasabahi watoto na katika wale watoto kuna mmoja kati ya hawa watoto anafanana sana na yule mshkaji kule gerezani,anafanana nae sana basi stori mbili tatu nikafurahi kupiga nao stori nikamkumbuka sana na nikasema "nikipata muda ntapigana sana ili niweze kwenda" kwahiyo katika ratiba ya jumapili ile baada ya kuachana na wale watoto nikasema "jumanne sasa yaani uko naweza nikatumia muda mrefu zaidi kwa ajili ya kukamilisha hilo zoezi.
Nakumbuka jumanne niliyotaka kusafiri mambo yangu yalikuwa hayakukaa vizuri,sijasettle mambo kwahiyo nikapanga siku za mbeleni ikishindikana basi ijumaa niondoke au jumamosi niondoke niende kule,nakumbuka nilipigiwa simu,mimi kutokana na hali ya mshkaji nilihakikisha napata taarifa vile anavyoendelea na ukiniuliza ni kwa namna gani yaani ni kwa namna yoyote inayowezekanaga taarifa ya kile kinachoendelea,siku za mwanzo sikufanya hivyo na ndio maana hata taarifa za mtu huyu kuhamishwa kwenda gereza jingine mimi taarifa sikuwanazo lakini mimi safari hii niliona anastahili mtu wa kumuangalia,kwahiyo nilipokea simu na nilipopokea akanambia "bwana Rojas unaendeleaje? Nikamwambia "naendelea vizuri,simu yako ina jambo jema? Akanambia "sina jambo jema,wewe ni mwanaume siwezi kusema nitapoteza muda maana sina habari nzuri,nina habari mbaya sana" nikastuka sana na nikamuuliza "ni nini kinaendelea" akasema "ulisema utakuja lakini ndugu yako hali yake imebadilika sana,amefunga kauli,amefunga kauli tunajitahidi kama utaweza kumuwahi pengine unaweza hata ukawahi kumuona maana hawezi kuongea chochote,unaweza kumuwahi hata dakika za mwisho hata ukamuaga bwana"
Kiukweli nilistuka sana,kwa wema alionitendea na pesa aliyoielekeza kwangu na kufikia leo mimi kuwa nilivyo je ana ndugu wangapi lakini ameniamini mimi tena kwa kauli yake kuwa "sina ndugu aliye karibu na mimi wote wamenitelekeza gerezani basi nitampa mtu ambaye moyo wangu utanisukuma kumpa" na akaniona mimi kijana deiwaka wa mtaa tu ambaye nimebambikiwa kesi nikaenda gerezani akanitunuku hizo pesa "nenda bwana katika harakati zangu mimi kuna pesa nilishawahi kuzipata,nenda utaziona na ukizipata njoo bwana tuzungumze" lakini mimi ndani yangu mambo ya uovu yakapata nafasi,nilijisikia shauku na hata sikuweza kulala siku hiyo,nikawasha gari na moja kwa moja kuanza safari,nilianza safari ili nifike niweze kukutana na mtu huyu angalau niweze kumuona,naambiwa amefunga kinywa sijui Mungu anaweza kufanya muujiza wake wowote jambo likatokea lolote hata akazungumza na mimi kwa machache.
Nilipata nafasi ya kufika mahali hapa lakini moyo wangu ulikuwa unaugua sana katika maisha yangu ninapoyazungumza haya,nimefika shauku niliyonayo nimkute mtu huyu lakini nikawa nimechelewa,nimemkuta mtu huyu amepoteza maisha ,kwenye maisha yangu nimekutana na misiba mingi mpaka nimefika hapa,naweza nikalia waweza kuniona mnafikikwa sababu kama nilikuwa rafiki mwema mtu ambaye aliyenibadilishia maisha je nilistahili kumtelekeza nilivyomtelekeza?
Mbona sikwenda kumpelekea hata mahitaji? Tena ndugu zetu waliopo gerezani wanahitaji sana faraja wakati natumia mali ambazo amekuwa sababu ni yeye,nakula vyakula vizuri vyakunona sikuwa namuwazia yeye kumpelekea hata kipande cha sabuni? Sikuweza kumuwazia chochote mbona nilimtelekeza,unaweza kuniona mnafiki,moyo wangu uliugua na kujisikia vibaya sana,nikasema mimi naweza kuwa katika kundi la wanadamu wanaowavunja moyo watu wema kuwatendea binadamu wengine wema kwa sababu mimi nilitendewa wema lakini mimi sikutenda wema kwa mtu huyu,kwanza nimekuwa na mahusiano na mwanamke ambaye alinizuia nisiwe na mahusiano nae,mengi ambayo tumepanga pamoja mengi nimeenda kinyume nae lakini leo hayupo tena akiniambia "Rojas mimi nimekusamehe wewe na kizazi chako,niliyafanya kwa mapenzi mema kabisa"
Hakuna kuugua moyo kukubwa na kuzito kama unajiona ndani yako una usaliti,nilijisikia kusaliti pakubwa sana,nililia sana,nakumbuka niliomba "naombeni nipate nafasi mtu huyu nikampumzishe katika nyumba yake ya milele,mtu huyu nimjengee jeneza kubwa la thamani nikampumzishe mtu huyu,mtu huyu ambaye amepoteza ndugu zake wote baada ya yeye kupatwa na kesi gerezani,amesahaulika hana hata ndugu aliyekuwa anakuja kumuangalia,angalau basi nimpe heshima ya mwisho,angalau nimfanyie katika hili na kaburi lake nilijenge katika ustadi mkubwa" lakini haya yote nikiyazungumza utaniona mnafiki kwa sababu nilikuwa wapi angalau kwenda kumtembelea mtu huyu angalau hata kujua maendeleo ya kiafya angalau kuweza kupata matibabu mapema labda kutokana na pesa ambazo yeye mwenyewe alizitafuta na akanipa mimi,wema mtu huyu alionitendea umekuwa ni bure,mimi ni mmoja kati ya watu ambao nimetendewa wema na nimesikia hatia,najihukumu kwa kuchelewa kwangu kuja kumtembelea mtu huyu gerezani,nalia kama mtoto kwa sababu niliamini katika awamu hii ntakaporudi nitapenya zaidi kwa sababu utaratibu nilishaanza kuufanya ili mtu huyu apate matibabu anayostahili ili arudi arejee katika hali ya kawaida lakini mara zote amekuwa akiniambia "Rojas mimi maisha yangu pengine yanaweza yakaishia huku huku" ni mtu ambaye hakuwa na stress zozote za kutaka kurudi uraiani kwa sababu nilikuwa namsisitiza akawa ananambia "wewe nenda kayafanye hayo kwanza" lakini mimi ndio nilikuwa wakwanza kutokomea na kutaka uhuru wa pesa ambazo aliyezitafuta ni mtu mwingine.
ITAENDELEA!
Pole cuzo pole sana,i feel ur pain! UbarikiweDaah kipande cha rojas na yule rafiki yake wa gerezani mpaka machozi yamenitoka alivyokuwa anamwambia rojas kuhusu pesa zake ukweli siku zote mchungu na unauma sana
Nashukuru kwa maoni yako,kiukweli ukisona hisia zinakuja kama Rojas atarudi ktk umaskini kumbe lilikuwa ni funzo kwake na kwetu pia,ubarikiweAsante mkuu wa story nzuri nimejifunza kitu pia story ya Rojaz imeishia sehemu nzuri matarajio yangu nilifikiri jamaa atafirisika kabisa kitu ambacho nimeona mwisho still anapambana na biashara zake hongera Kwa kusimulia vizuri huo ni moyo wa pekee Mungu akubariki sana asante pia wa muda wako.
Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
Ameachiwa wajibu mkubwa sana wakuwasimamia watotoDaaah pole rojas ni kiasi gani umeumia sana kumpoteza rafiki yako inaumiza sana sana
Huyu mganga kweli au rojas mbona mambo yanazidi kuogopeshaMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa
Sehemu ya 18
Ukipata fursa ya kusikia mikasa iliyowakuta wanadamu kiukweli kuna watu wamekutana na vitu vingi,mikasa mingi katika maisha yao,watu wamebeba vitu vingi ndani ya mioyo yao nami kama Rojas naelezea yale ambayo yamenisibu ili msomaji wangu nawe uweze kujua ya upande mwingine wa dunia,kinachotesa sasa hivi ni huu msiba,naumia sana kwani katika vitu ambavyo nimezungumza sana na mtu huyu na nikataka sana kujua lakini hakuwahi kuniambia hata siku moja,nilitaka kujua pesa alizitoa wapi? Mimi nakueleza leo jinsi matumizi yangu yalivyo makubwa,jinsi ambavyo nimekuwa nakitumia pesa zangu kwa namna tofauti tofauti lakini hata ukiniuliza hizi pesa ulizitoa wapi nitakwambia wapi nilipotoa lakini yule mtu aliyenipa je yeye amezitoa wapg? Hicho kilikuwa ni kitu kama fumbo kwangu na mtu huyu nimetengana nae kwa muda mrefu na hata nilipokuja mtu huyu alishaanza kuwa mdhaifu na sasa amepatwa na umauti.
Lakini katika vitu alivyoniambia ni "nimekusamehe wewe pamoja na kizazi chako,niliyafanya haya kwa mapenzi yangu tu mema" lakini hakunieleza wapi pesa ametoa na zaidi alisema "nenda ukatumie pesa,yafuate yale niliyokueleza" nilitamani mimi niwe mmoja kati ya watu ambao nitapata nafasi ya kumzika mtu huyu kwa heshima,najua ni mtu ambaye ni mfungwa,amekuwa akitumikia kifungo chake na amepatwa na umauti akiwa bado anatumikia kifungo chake lakini mimi nilisema mtu huyu kiu yangu,shauku yangu nimpumzishe mahali pa heshima,chochote nitafanya,nimekuwa nazungumza hii sentensi chochote ntafanya kwani tangu nimekuwa na pesa nimejua jinsi pesa inavyoweza kufanya vitu visivyowezekana japo kuna vitu haviwezekani hata kwa pesa lakini hivi ninavyovizungumza mimi vinawezekana,unapokutana na watu ambao mnaweza mkabargain nao kitu hata kama kutakuwa na mifumo flani ambayo ni migumu,wakakuletea ugumu lakini wanaweza wakafanya tofauti kwa sababu kuna pesa inapita hapo na pesa ina nguvu sana sana sana,ukiwa na pesa na ukaishi pesa utaelewa maana ya hii sentensi mimi nasema,kwako wewe mambo yasiwezekana ni machache sana,mengi yanawezekana,popote unaweza ukaenda,yoyote unaweza ukamface ukazungumza nae,unakuwa unajiamini isivyo kawaida hata unavyokuwa unatembea barabarani pesa inakupa ujasiri mkubwa sana kwahiyo nilisema hili ntaliweka sawa ili kuhakikisha mimi nakamilisha hilo.
Nilitimiza ahadi yangu kama vile nilivyotamani iwe ndivyo mimi nilifanya tena sikufanya tu katika hali ya mimi binafsi bali nilimchukua huyu mtu nakumpeleka mpaka nyumbani kwao,yaani kuusafirisha mwili na kuupeleka mpaka nyumbani kwao kule ambako mimi nilichukua pesa,mahali ambapo toka nimechukua pesa sikurudi tena,ni mengi yalitokea lakini pengine si muhimu sana kuyazungumza hasa ya kule lakini kiukubwa zaidi mimi nilifanikiwa hilo zoezi,nililifanya kwa unyenyekevu mkubwa sana japo katika mazungumzo ambayo tumewahi kuyazungumza aliwahi kuniambia "kuna siku utageuza kisogo chako na utakaporudi hautanikuta" nilimkatalia na hata sikupay attention kuzungumza nae kwahiyo hakuwahi kusema nikifa itakuwaje kwa sababu watu wanapoteza maisha wanazikwa,wanahifadhiwa tu na maisha mengine yanaendelea,unaweza kuwa na ndugu yako gerezani na haujawahi kumtembea hujui siku unaenda ibuka unashangaa mtu alishapoteza maisha,hakuma mawasiliano wengine wanahamishwa kwenda maeneo flani lakini kama unakuwa ni mtu wa kutembelea ndugvhata taarifa inapotokea mawasiliano yakawa rahisi kuweza kukupa taarifa bwana huyu mtu moja mbili tatu kama mimi ambavyo nilivyokuja kufanya awamu nyingine japo uko mwanzoni sikuwahi kufanya na ndio maana hata alipohamishwa gereza,hata alivyokuwa na afya dhohofu mimi sikujua.
Nimerudi kwenye maisha yangu kama kawaida kwa sababu mambo yameshapita,nilikuwa na muda kwelikweli unajua taratibu hizo mpaka kupumzisha mwili na nini kwahiyo kuna siku kadhaa nilizitumia kwa ajili ya hilo zoezi,nimerudi na siku zinazidi kusogea mbele niko hapa bado moyo wangu ulikosa amani kabisa,nakumbuka nilipata msukumo mimi,kuna mshkaji mmoja ambaye alikuwa karibu na mshkaji kule gerezani na yeye alibali kule gereza la mwanzo ambapo mimi na mshkaji tulikutana,nilisukumwa kwenda hata nizungumze nae mawili matatu,nilifunga safari nikaenda mpaka gerezani lengo tu angalau nizungumze na mtu huyu kwa sababu huyu mtu amekuwa karibu nae na natafuta kitu ambacho angalau kinaweza kikanipa unafuu kwa hali ninayoipitia sasa hivi ,hali ya kukosa amani ninayoipitia haielezeki,kuna watu pengine wameshapita katika situation kama hizo unakosa amani unasikia roho inaangaika tu yaani hapa kifuani unasikia kitu kiko hapa unaangaika ndivyo ambavyo mimi nilivyokuwa nasikia,nilipofika kweli nilibahatika kukutana na mtu huyo na alisikitika sana rafiki yake ambaye walikuwa wote gerezani kwa muda mrefu hayuko tena lakini aliniambia sentensi moja sentensi ambayo sikuwahi kuisikia mimi hata siku moja yaani sijawahi kusikia hata mtu huyu ambaye yeye ni marehemu kuniambia,hakuwahi lakini nilisikia kwa mtu huyu,aliniambia sentensi hii akitaja jina la yule mshkaji "unajua mshkaji alikuwa na nafasi kubwa sana ya kutoka,unaona ukimwambia habari za kutoka kuwa huru yaani atoke aende uraiani awe huru,kwa sababu kuna siku aliniambia umempa chance ya kupigania atoke lakini hakutoa ushirikiano lakini alikuwa na sababu kubwa sana" nikataka kusikia kwa sababu ni kweli mtu alichimbia pesa,yaani pesa zilikuwepo,pesa zipo uko zimekaa,amenipa nafasi hiyo mimi nimeenda kuchimba pesa na nimezimiliki na zimekuwa za kwangu,kwanini pesa hizi tusingefight yeye atoke,awe huru,nani hataki kuwa huru,nani hataki kuishi maisha ya uraiani uwe unaamua uoge saa ngapi,ule saa ngapi,maisha ya kupangiwa saa flani utakula saa flani utaamka nani anayapenda? Mwanadamu furaha yake ni kuishi maisha ya uhuru na ya amani lakini yeye ilionekana kama yatafanyika lakini sio sasa ni baadae,kwanini baadae na nafasi tunayo sasa hivi,tupigane tunapoweza na kama itashindikana tunawe mikono kwamba tumeshindwa,tumeshindwa basi haiwezekani lakini kuna bidii tumefanya,watu wangapi ambao walishakatiwa tamaa lakini mwisho wa siku wamekuja kuwa huru? Haijalishi ni miaka mingapi lakini hakuwa na ile shauku ya kusema atoke uraiani na hiki ni kitu nilikuwa namwambia kwanini yaani,kwanini yaani?
Ndio nasikia huyu mtu ananiambia,ananiambia "(akitaja jina lake)alikuwa anahofia sana kuuawa" nikashtuka "kuuawa? Kuuawa na nani? Akasema "amesema ni bora aendelee kuwa gerezani lakini aendelee kuwa hai ili aendelee kupata taarifa kuhusu watoto wake na akawa na furaha kwa sababu wewe ulizidi kumpa taarifa za kuhusu watoto kitu ambacho ndio alikuwa anakihitaji katika maisha yake kwahiyo kwa sababu ulikuwa unamfanyio hivyo ndio ilikuwa ni furaha kwake" nikamuuliza "kwanini alikuwa anahofia kifo,kwanini? Akanambia "hata mimi nimewahi kumuuliza sana lakini hajawahi kuniambia hata siku moja lakini ninachojua ni hofu ya umauti ndio uliokuwa unamsumbua" nilistuka na kuogopa kwelikweli kwa sababu tangu nimemfahamu mtu huyu hajawahi kuniambia,nikamwambia "natamani sana kujua" akanambia "mimi sijui chochote na mimi pengine naweza kuwa mtu ambaye najua mengi yake lakini sijui chochote"
Niliondoka nikiwa mnyonge zaidi "kwa sababu gani mtu huyu aliogopa,aliogopa umauti na akitoka uraiani anaweza akauawa bora akae kule aendelee kupata taarifa za watoto wake na mimi japo niliendelea kuwahudumia watoto kwa namna moja au nyingine lakini nilifunga ukurasa wa kumpelekea taarifa,kwahiyo kama mimi ndio alikuwa ananitegemea mpeleka taarifa,mpeleka habari kwamba watoto wameendea hivi na mimi sasa ndio nikakata mguu,sijui alipita katika mazingira ya kimaumivu ya kiasi gani,leo sasa ndio naona kama zaidi nilikosea,kumbe hiki ndicho mtu huyu kwake kilikuwa ni kikubwa kuliko vyote lakini ni nani hasa aliyekuwa anamuhofia,ni nani huyo aliyekuwa anamuhofia? Nikajikuta naanza kuwa na stress sana na zikawa zinanisumbua sana kwa sababu nikaanza kuogopa na mimi,kama yeye alikuwa anaogopa kutoka uraiani labda ni kwa sababu ya hizi pesa nami niko na hizi pesa lakini mbona siku zote niko na hizi pesa na nimetumia kwa mambo mengi sana mbona sijawahi kuona mtu ananifata au hata kunihoji kwamba hizi pesa ni za nani? Sijakutana na mtu kama huyo,yeye alikuwa anamuhofia nani?
Nakumbuka nina mshkaji wangu wa karibu aliona niko down sana na aliniambiaa "Rojas hauko sawa" nikamwambia "kuna kitu kinaniumiza sana kichwa najikuta nakosa raha kabisa" akanambia "ni nini? Nikamwambia "hata sijui naanzia wapi kukueleza lakini ni ngumu sana kukueleza ila nataka kupata majibu ya kitu ila sijui nani anaweza akanipa majibu,akaniambia "ni kuhusu mambo yako ya biashara? Rojas hujui kuna watu wanaweza kuviona vitu ambavyo kwa kawaida hauwezi kuviona? Nikamwambia "unamaanisha nini? Akajibu "eeh wako wataalam kuna kitu kinakusumbua na haukielewi unataka kupata majibu wako wataalam wanaweza kujua kwamba majibu ya hiki kitu ambacho unakiwaza ni haya hapa" kwa yale maneno yake akawa kama akanipa akili mpya hivi, "ndio ni wapi naweza kupata wa namna hiyo" akanambia "wapo,sasa hawa watu wanazidiana uwezo,sasa ngoja labda tuangalie nani anayeweza akakufanyia,ni nini hasa kwanza unataka kujua,vipi kwenye biashara unachezewa? Nikamwambia "sio kuchezewa ila sielewi mambo yangu jinsi yanavyoenda kwahiyo nataka ufafanuzi" akasema "ooh mambo ya biashara biashara wako wengi sana,sasa mimi ntakuconnect na mtu atakupa majibu ya maswali yako yote" kutokana na hali ya msongo wa mawazo alafu nimejikuta tu najiuliza maswali mengi alafu sina majibu.
Kweli mshkaji aliniambia "nakupigania kuhakikisha unapata mtaalamu kwelikweli" tukizungumza mtaalam huyu ni mtu anayefanya uganga,yeye alitumia lugha ya mtaalam mwenye uwezo,mtaalam ambaye anaweza akanipa majibu ya maswali yangu na mimi kwakuwa sikuwa mwepesi sana kumshirikisha kwakuwa najua waganga wakati mwingine uwa hawana siri pengine anaweza akamueleza lakini potelea mbali lakini mimi ninachotaka ni anisaidie,kwa sababu sikutaka kumshirikisha sana alinisindikiza lakini nikamwambia "wewe kaa tu hapa mimi ngoja niingie nizungumze nae" kwahiyo niliingia mimi peke yangu kwa mtaalam,huyu mtaalam akanambia "hapa ndipo jambo lako linapofanikiwa karibu sana" nikamwambia "nina shida ninapitia sana,sijajua chanzo cha haya mambo" lakini nilimwambia "mimi kuna mtu amenipa pesa,amenipa pesa kwa kunielekeza mahali pesa zilipo,nikaenda kuchukua hizo pesa,nikazitumia lakini akanipa masharti ambayo sikuwa nayaelewa na ikafika kipindi nikaona kama yule mtu aliyenipa pesa ananisumbua na kunipa msongo wa mawazo na nikbmua kuachana nae na kufocus katika maisha yangu mengine lakini huyo mtu amepoteza maisha sasa nimekuja kujua kwamba huyo mtu kuna vitu labda alikuwa anaviishi ambavyo alikuwa anavifanya siri na hakuweza kumueleza mtu" kwahiyo nikawa nasubiria mtaalam anipe majibu sasa kwakuwa nilikosa kupata majibu katika hali ya kawaida basi njia zipo nipate ufafunuzi ni nini kinaendelea,wao si wana nguvu wanaweza wakajua basi nami nijue na je wakijua wataweza kunisaidia ili moyo wangu ubaki na amani na vitu kama hivyo.
Nilimueleza haya yule mtaalam na nakumbuka huyu mtaalam alikuwa ni mtu mzima tu na nilielezwa yuko vizuri na niko hapa kutatuliwa kile ambayo nataka ufafanuzi nacho,mtu huyu kila nilivyokuwa namueleza alikuwa na karatasi na kalamu nyekundu na akawa anaandika maandishi ya kiarabu na michoro na akawa anazungumza maneno flani ambayo nadhani ni ya kiarabu na alipomaliza alinambia sentensi moja "hizi pesa sio zako" nikamwambia "ni kweli lakini aliyenipa alinipa hizi pesa kwa moyo mweupe" akasema "ndio hata mimi naona alikupa kwa moyo mweupe na hata yeye hizo pesa zilimtaabisha sana" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "eeh naona hizo pesa zimemtaabisha sana,ni kweli amezipata lakini ameishia mateso mpaka kifo chake ameishia kuteseka" nilishtuka sana kwa maneno hayo,katika vitu mimi nilikuwa na amani navyo na natumia hizi pesa kwa uhuru na nilifanya biashara na biashara zinaenda na kama kwa namna moja au nyingine mimi nakuwa sijafanya vizuri ni mambo yangu mimi,matumizi yangu mimi,matumizi yakawa makubwa zaidi kama nilivyokwambia ni starehe kwa kwenda mbele,wanawake zaidi ya saba na hapo kuna waliopangiwa vyumba,kuna wakulipiwa ada za chuo,wa driving school na mengineyo.
Nashtuka sana kwa yale huyu mtaalam anayoyaeleza na nikamuuliza "ina maana hizi pesa mimi nilizichukua kimakosa? Sikuwa na makosa yoyote kwakuwa huyu mtu alitaka msaada na mimi nikamsaidia na ndio maana nasema alinipa kwa mapenzi yake ya dhati,sijui zilimtaabisha kwa kiasi gani lakini ninachojua ni pesa halali ambazo sio za magumashi kabisa" akaniuliza swali "ni wapi umehifadhi hizi pesa? Hii ni siri ambayo simwambiagi mtu na mganga anauliza wapi nilikohifadhi pesa[emoji23] na nilishamwambia vitu vinavyonipa mashaka ni huyo mtu kutotaka mimi nipeleke pesa benki kwahiyo nikajikuta zile pesa ambazo nimeanza kuendeshea biashara ndio nilikuwa napeleka benki lakini zile pesa ambazo nilichukua kule nilikuwa natumbukiza kwenye vitu ambavyo vinatembea km kuagiza bidhaa moja kwa moja na si kupeleka benki,akaniuliza kwa mara nyingine tena "hizi fedha ni wapi umezihifadhi kwa sababu hapa naona natakiwa kufanya kitu kuna mambo mabaya yanaenda kukutokea" nikaogopa,nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "ndio,mambo mabaya naona yanaenda kukutokea na afadhali umekuja mapema ili nikupe msaada" nikamwambia "naomba unisaidie sana"akasema "nakusaidia na ndio maana nataka unipe majibu ya maswali ninayokuuliza kwani mimi sio mganga wakupindisha maneno yangu.
Mimi ni mganga ambaye nimefanya hii kazi kwa miaka mingi na nimewasaidia watu sio wa Tanzania tu hata wa nje ya Tanzania kusolve matatizo yao ambayo ni magumu yaliyoshindikana kwahiyo utamshukuru mtu aliyekuleta kwa sababu wewe hautakufa hata kama yeye aliyetafuta hizo pesa amekufa,wewe hautakufa na utashuhudia wajukuu na vitukuu vyako lakini inabidi uwe muwazi kwangu kwani tabia ya kuficha vitu ambavyo vinanifanya naanza kuhisi pengine unanidanganya utafanya kazi iwe ngumu" nikamwambia "kuna vitu nilishamuahidi mtu huyu sitamwambia mtu lakini nimejikuta katika harakati za maisha nazungumza,nilielekezwa na mtu huyo wapi nihifadhi hizo pesa ili ziwe salama na pamoja na mafanikio ambayo mimi niliyapata sikuwahi kuhamisha hizo pesa toka mahali ambako niliweka toka siku ile nilipozihifadhi" akaniambia "ni sawa vyote unavyosema,kuwa muwazi kwangu nikusaidie,ni wapi hizo pesa umehifadhi? Kiukweli sijui kwanini kwani nilikuwa mzito sana kusema pesa ziko nyumbani kwangu,nilipozihifadhi ni kwenye chumba ninacholala,nimechimba na kufukia pesa ila ukweli nilimwambia kuna pesa ambazo zinazunguka katika biashara,hizo sikuwa nazihifadhi ndani,akanambia "mbona unasitasita,unapokuja kwa mganga kwa mganga amini unatatuliwa mambo yako lakini na wewe unatakiwa kuwa muwazi lakini wewe unaonekana moyo wako ni mzito kusema ukweli na ndivyo ambavyo naona umauti unafata kwako baada ya huyo mtu mwenye pesa kupoteza maisha"
ITAENDELEA!
Kwenda kwa mganga fake kuliharibu kila kitu kikubwa kumrudia MunguMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa
Sehemu ya 19
Mtaalamu alizidi kunidadisi na alinambia "pesa ziko kiasi gani zilizobaki toka wewe uzipate? Nikawa najiuliza je naulizwa maswali gani haya sasa,mbona kama mganga ananichimba sana? Na naomba ukumbuke hapa kwa huyu mganga nimeletwa na mtu na sijui dhamila yake ya ndani na mganga anataka nimletee pesa kadhaa kutoka katika pesa ninazozitunza uko ninapozitunza (yaani alinitaka kuchomoa kiasi flani cha pesa nilizonazo na nimletee)kuna kitu azifanyie kwa nia ya kuzifanyia ulinzi kwa sababu anaona kuna mambo yasiyo mema katika pesa ninazozitumia,nikamwambia "sawa" naye akazidi kusisitiza "nipe majibu ili niweze kukusaidia" majibu kwa maana nimueleze eneo nililohifadhi pesa.
Lakini mimi nikajiuliza "huyu kama ni mtaalam wa kuweza kuona vitu ambavyo mtu mwingine hawezi kuviona ameona kama pesa ninazozimiliki kuna shida,anaona kitu kilichoondoa uhai wa ndugu kule gerezani ndio kitu hicho kitakachokuja kunidhulu nami je kama ameweza kuona vyote hivyo iweje ashindwe kuona nilipoweka pesa mpaka nianze kumention ni sehemu flani nimeweka moja mbili tatu sasa kutokana na mimi kuingia katika ulimwengu wa biashara na kutapeliwa mara kadhaa hii ikanipa hofu kwa sababu nimeletwa hapa na mtu na huyu mtu ni mshkaji wangu,katika maisha huwezi kujua huyu mtu anakuwazia jambo gani pengine hata yeye anaumiza kichwa kujua vyanzo vya pesa zangu ni nini,huyu mganga itamuaminije na kumpa siri yangu hii,nikamwambia "mimi ntaleta pesa" akanambia "sio tu kuleta pesa" na akazidi kuning'ng'niza katika kupata jibu lake lakini sikumpa ushirikiano kabisa katika hilo,nilimwambia "pesa nitaleta na hayo majibu nitakujibu ntakapoleta pesa" mganga akanambia "kiburi chako kitakufanya uchelewe na kutatokea maafa makubwa,mimi nakuambia hivyo kwa sababu hizi mali si za kwako,yaani ukae ukijua hizi mali si za kwako na huyo aliyepata mali alikuwa na siri nazo na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana alizifukia mahali,wewe mahali ulipoziweka unaona ni shida kunitajia je unahisi ni nini"
Sikutaka kumpa sana nafasi na nikamwambia "ndio kwanza tumefahamiana na vile tunahitaji muda zaidi wa kuzidi kuzungumza zaidi pengine naweza kuzungumza mambo mengi zaidi" lakini nikazidi kujiuliza kama anaona visivyoonekana kwanini hajaona pesa? Nilifanya taratibu nilizoelezwa kwakuwa nilitakiwa kulipia pale,nikalipa kwani sikuona kama ni hela nyingi kwani makubaliano ilikuwa kulipia huduma ya kutizamia,kulinda pesa na mimi mwenye kunitibia ili kila kitu kirudi katika mstari wake,nikalipa na akanambia kadri siku zitakavyokuwa zinaenda nitajionea jinsi ulinzi wa pesa na mali zangu unavyoimarika,nilimpatia laki tano na uko mbeleni nitalipia kwa kadri ya matibabu husika.
Tumetoka pale na yule mshkaji aliyenipeleka na tukiwa njiani akawa ananiambia "huyu ni mganga sahihi sana,wako waganga lakini huyu ni mganga mahiri" nikamwambia "lakini mimi sijawahi kushiriki katika mambo ya waganga" akanambia "shida yako,tatizo lako fata tu maagizo anayokupa utafanikiwa sana" nakumbuka sana nilitakiwa kurudi kwa mganga kupeleka pesa (mfano wa pesa)ambazo ninazo lakini nikatingwa na mambo mengi kwani mambo yalikuwa yamepandiana sana na nikasema ngoja nikamilishe alafu ndio niende,nakumbuka siku hiyo niko katika vitu vyangu vinavyoniingizia uchumi nikiwa napiga mahesabu ya hapa na pale nakumbuka hatua yangu ya kwanza kabisa nikapokea taarifa ya gari yangu kubwa kabisa ambayo nilinunua kwa gharama kubwa na linaendelea kufanya kazi nikapewa taarifa limepata ajali mbaya sana lakini pia ambacho kiliniuma zaidi na watu ambao walikuwamo mule katika gari ambao ni madereva wangu wote walipoteza maisha,nilisikitika sana,nilipofatilia kuona ajali ya gari yangu kiukweli ilikuwa lite off lakini stori za ajali hiyo kutokea zilikuwa ni nyingi sana lakini wakati nikiendelea na mchakato wa kuhakikisha hawa wapendwa wetu wanapumzishwa katika nyumba yao ya milele taxi moja ikapata ajali,ajali ilitokea lakini dereva alitoka akiwa hai lakini gari lilikuwa nyang'anyang'a na nakumbuka sentensi ambayo dereva alizungumza "aah mimi nimeaga bwana mtu hawezi kunichukua kizembezembe" yaani ikiwa inaaminika haikuwa ajali ya kawaida kwa maelezo yake anasema jinsi alikuwa anaendesha gari kuna vitu aliviona mbele ambavyo havikuwa vya kawaida na anaamini kabisa ulikuwa mkono wa mtu,kama nikaanza kupata ishara flani kuwa kuna vitu haviko sawa.
Kuna matukio ya ghafla yaliibuka hata sijui yalitokea wapi na hii ikanifanya nikimbie sasa moja kwa moja kwenda kwa yule mtaalam na nikawa nimepeleka pesa,nikapeleka na kumueleza changamoto ambazo zimetokea na alisikitika na kuniambia "nilikwambia kuwa hizi pesa unazomiliki aliyekuwa anazimiliki zimemtaabisha zimemtesa na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana hakutaka kumtesa ndugu yake yoyote na ndio maana alikutafuta wewe ili hizi pesa zikumalize" nikasema "hapana,hapana mtu amenipa hizi pesa na siku zote nimekuwa nikizitumia kwa amani, kwanini na kwanini? Mtaalam akachukua zana zake pale na kuongea ongea maneno yake na kunipa dawa flani akawa amenipakaa maeneo tofauti tofauti ya mwili wangu na pia akazichukua zile pesa nilizokwenda nazo nakuzifanyia mambo mambo yake mwenyewe ndio anajua zaidi na akanambia "mambo yatasettle,mambo yatasettle" na alinipa utaratibu wa kufanya vitu katika ofisi ambazo nazimiliki na akanirejeshea zile pesa ambazo alishazifanyia mambo yake niende nikazichanganye na zile pesa zingine kwamba ni ulinzi na hata mie kuanzia muda ule niko salama.
Nilitoka pale na nikafanya kama nilivyoelekezwa lakini moyo wangu ukawa unasikitika sana,nakumbuka nikapigiwa simu kutoka katika duka langu la nafaka kuwa kuna moto mkubwa na duka limeteketea lote na watu ambao walikuwa karibu na mimi wakaanza maneno "unaona,unaona,huyu mtoto alikuwa anamiliki mali zisizo za halali angalia matukio jinsi yanavyofululiza pengine amekosea masharti" lakini mimi kwa upande wangu nikawa najiamini hakuna sharti ambalo nililikosea kwa sababu hizi pesa nimemiliki katika mfumo ambao nimeshauelezea,ikabidi nirudi tena kwa mtaalam ili nijue ni nini tena na mbona nimeshaanza kupoteza sehemu yangu ya kupata pesa na watu wamekuwa wakipata pesa kwa ajili ya kutunza familia "imekuwaje tena,ni nini kinaendelea mbona haunipi ufafanuzi" akanambia kuna kazi kubwa anatakiwa kuifanya na inabidi anipeleke makaburini,sasa kwakuwa niko katika hali ya kutatua tatizo na ukiniuliza nini chanzo yaani ni sijui,yaani sijui kwa sababu nilikuwa na hizi pesa siku zote na ni hofu tu ilinipata ndio kwenda kwa mganga,yaani pesa nilizotoa kwa mganga ni pesa nyingi sana na ikawa kila ninapoenda ananitajia mabei makubwa ya vifaa hitajika na kwa mfano hili zoezi la kwenda makaburini aliniambia hili zoezi ni kubwa sana kwa sababu tunahitaji nguvu zaidi za kuhakikisha tunaweka ulinzi kwa hizi pesa kwahiyo alinitaka nitoe milioni tano ili kumaliya tatizo kabisa,nikatoa na kweli tulikwenda makaburini na akanifanyia madawa na kuniambia "sasa wewe umepikwa na umepikika na hakuna ubaya wowote dhidi yako kuanzia sasa hivi".
Lakini haikuwa kama yule mganga alivyosema kwani vitu vyangu vilizidi kupukutika,naviita vitu vyangu kwakuwa nilivitafuta mimi,nilivitafuta kupitia zile pesa na kama ningeamua si ningekaa tu huku nachomoa pesa natumia lakini pesa zile nilifanya uzalishaji ambao ndio umeleta matunda ambayo ndio hivyo vitu na hata pesa zake nikaweza kupeleka hata benki,nakumbuka sana,nakumbuka nyakati naendelea kuliwa pesa na vitu vinazidi kupotea na huku huyo mtaalam akiendelea kunipa vitisho,nakumbuka siku moja yule mama ambaye ni shemeji yangu ambaye tumekuwa tukishea mambo mengi alikuwa ameona mapito ambayo napitia na nilikuwa lesi sana kwahyo sikuwa hata na muda wa kuzungumza mimi niko kwa ajili ya kuzitatua changamoto nilizokuwa nazipitia,alinitafuta na akanambia "shemeji tuongee kidogo,shemeji kuyumba kwenye biashara ni jambo la kawaida,nini hasa kimesonga moyo wako? Mbona umekuwa hauna raha,nakuona ni mtu ambaye hauko smart tena,ni nini tena kiko katika maisha yako? Nikamwambia "sielewi" alizungumza na mimi kwa ukaribu na upole sana "Rojas nilikwambia kuna mambo hauwezi kumwambia mtu lakini Mungu yupo,Mungu wetu ni kila kitu katika maisha yetu" alizungumza na mimi mambo makubwa sana,nikamwambia "unajua leo hii mnaniona niko na pesa lakini hizi pesa leo zimegeuka mateso kwangu" akanambia "kwanini,kwanini mbona mimi hizi pesa naona ni pesa halali kabisa" nikamwambia "hujui tu" akasema "hapana naziona ni pesa halali kabisa na wala sina mashaka na wewe kama watu wanavyosema kuwa umetoa sadaka watu,minong'ono ya watu kuwa eti umekosea masharti na wanatisha watu ambao wanakufanyia kazi wakiwaogopesha kuwa watapata matatizo na kupoteza maisha,mimi siamini katika hilo"
Huyu mama alionesha kuniamini kuliko kawaida kwamba anaamini iko kitu,kwa mara nyingine ya kwanza nikamueleza huyu shemeji yangu,nikamwambia "hizi pesa mimi alinipa" na nikamweleza mazingira yote ya mimi kumiliki hizi pesa na nikamweleza jinsi nilivyomtelekeza huyu mtu na nikamwelekeza hadi mahali nilipozihifadhi hizi pesa kitu ambacho sikumweleza mtu yoyote tofauti na yule marehemu na nikamwambia yule shemeji "nimekushirikisha kwa sababu umekuwa karibu na mimi na umekuwa unazungumza vitu ambavyo vinagusa sana maisha yangu" akanambia huyu mama " Rojas unapoamua kuamua kuwa kuna miungu mingine asiyekuwa Mungu inaweza ikakusaidia tambua unakosea na uko ndiko ulikoenda kuharibikiwa,kama siku zote ulikuwa unafanya biashara zako katika hali ya amani ina maana sasa wewe umeenda kujiconnect na miungu ambayo ni mibaya na ndio labda imeharibu pesa zako" nikamwambia "hapana yule mtu alikuwa anahofia kutoka" nikamweleza hofu niliyokuwa nayo,akasema "hiyo ni hofu yako imekupandikiza wewe kwenda kuamini mambo ya kishirikina" nikamwambia "sasa mimi nafanyaje maana nahisi kuchanganyikiwa" akanambia "cha kwanza stop kabisa kujihusisha na mambo ya kishirikina,siku zote umekuwa ukitumia hizi pesa bila ya shida yoyote,mambo ya kuambiwa pesa haukutakiwa kuzimiliki aliyemiliki ameshaondoka je alikwambia kitu chochote?
Nikamwambia "hajawahi kuniambia kitu kibaya" akanambia "watu upata neema ya kupata pesa katika mazingira ambayo hayaelezeki,kuna mtu anawez akazitafuta pesa na asizitumie neema ikamuangukia mtu mwingine na akazitumia,haimaanishi yule mtu aliyepata ni kwa njia mbaya" huyu shemeji yangu tulizungumza kwa muda mrefu sana na akanambia kuna vitu nimeviweka kwenye biashara uenda hivyo pengine sasa ndio vinakula biashara yangu ili niendelee kutishiwa na niendelee kutoa pesa kwa yule mganga" nikipiga hesabu toka nimeanza kwenda kwa yule mganga pesa ngapi nimetoa kiukweli imefika hata milioni ishirini ambayo nimetumia kwa njia mbalimbali kwa maelekezo yake na vitu ambavyo alinipa nikaviweka katika maduka yangu ambapo naweka lakini nazidi kupata matatizo na huyu shemeji akiniambia "hivyo ambavyo umeweka ndio vinazidi kuharibu biashara yako,vinazidi kukupa hofu na hofu inakufanya wewe uendelee kutoa pesa na utaendelea kutoa pesa huku ukihofia kitu ambacho hakipo.
Hakipo Rojas na umewasaidia watoto yatima wale,umetoa sadaka zako,sadaka zako zimekuwa ni baraka,pesa hiyo ni pesa halali mtu huyo alikupa kwa upendo wa dhatina Mungu alitaka wewe uwe na pesa,unajua Rojas katika maisha tunaishi kuna watu wanapata pesa kwa neema ya Mungu tu,yeye mwenyewe ukimuuliza anasema nilihustle kweli lakini katika nyakati sielewi nilipata pesa,wewe ulibahatika kupata pesa katika mazingira ambayo Mungu aliamua kukupa pesa ila wewe ulipoikamata pesa ukajikuta unachanganyikiwa,unazifanyia anasa,unazifanyia katika mambo yasiyofaa lakini Mungu ni wa rehema,Mungu wetu ni wa upendo anakusamehe kabisa ndio kama hivi na maisha yanaendelea" huyu mama hakuishia tu bali alinambia "twende ofisi baada ya ofisi niambie hivyo vitu ambavyo umevificha uko unaogopa kuvitoa mimi nitavitoa" tukaambatana pamoja na yeye maana nilikuwa nimehifadhi vibuyu ambavyo vimefungwa na vitambaa,vibuyu na vidudedude vingi tu kwahiyo kila ofisi nikawa nimewekakwa siri mfanyakazi asione yaani kuhakikisha vinakuwa salama kwa ajili ya ulinzi na hivi vitu nimeanza kuvifanya baada ya kupata hofu na mimi kutaka majibu sana ya kile ambacho nimekuwa ninapitia,tulivitoa vyote katika maeneo yote,alivikusanya na yeye mwenyewe alivichoma moto na akasema "tunaye Mungu wetu asiyeshindwa na jambo lolote,hakuna pesa ambayo isiyokuma pesa halali,pesa zote ni za Mungu hakuna pesa ya shetani,hizo pesa za shetani ni za kwao lakini sisi hatutayasujudu hayo,hakuna uharibifu wowote utakaotokea tena kwa sababu vyote vyakuleta uharibifu visharudi kwao"
Huyu mwanamke ni shemeji yangu lakini alinitia moyo sana,akuishia hapo kwani alizidi kuongea na mimi,kukaa na mimi kwa upendo na akazidi kunishauri kuhusiana na yule mwanamke ambaye ameshakuwa sehemu ya maisha yangu akasema "lazima umtoe yule mwanamke katika maisha yako" yule mwanamke anafanya mambo ya kikahaba lakini ameshika akili yangu sana na nimejikuta natoa pesa nyingi kwake,akasema "huyu sio mke,huyu sio mke kabisa na Mungu atakusaidia kukuvusha hapo".
Tangu mimi nilipotoa vitu vyote vya kiganga sikuona shida yoyote yaani gari kudondoka wala matatizo yoyote kutokea,nikarudi nikaanza kuona amani inarudi na zaidi kumkumbuka rafiki yangu ambaye alinipa pesa,nikawekeza zaidi kwa hawa watoto mara nyingi zaidi ya ilivyokuwa kawaida na siku zilivyoendelea kusogea na nikazidi kuzipambania zile pesa ziendelee kudumu,ziendelee kudumu utajiri huu ambao ninaumiliki uendelee kudumu japo vipindi vya uchumi vinakuwa tofauti kuna kipindi mambo hayakuwa mazuri lakini sikudondoka kabisa,bado niliamka tena na kuendelea kupambana kila inayoitwa leo,kila inayoitwa leo kuhakikisha maisha yanasonga mbele.
Katika mengi ambayo yamekuwa ni faraja kwangu ni kuona watoto wa mshkaji wamekua na mmoja kati ya watoto wa mshkaji ameolewa na mimi nilisimama kama baba,nilisimama kama mtu muhimu katika tukio husika.
Muda umesogea sasa mimi ni baba wa familia niko na mke pamoja na watoto lakini sina kiwango kile ambacho nilipata cha nyakati zile pesa nyingi sana lakini sasa hivi nina pesa za kuweza kuendesha maisha yangu,kusaidia ndugu zangu,za kuendesha gari nzuri,za kuishi kwenye nyumba nzuri na maisha mengine yanaendelea.
MWISHO!
Tubarikiwe sote cuzo asante sana sana kwa story inayofundishaPole cuzo pole sana,i feel ur pain! Ubarikiwe
Nimekusoma cuzo ngoja niirejeshe kwa hisani,ile ni picha ya kijana na hii ni nembo ya timu yangu pendwaShikamkono pls rudisha avatar ya mwanzo nimeangaika kutafuta hii story sisi wengine avatar ndio tunazishika mkuu nilikuwa najiuliza toka lini kukawa na arosto jamani