Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Kama unadhani nimetumia program yoyote kuibadili hii story nakujuza si kweli,nimeandika kwa mkono wangu kipande kwa kipande,sitaki kujisifu ila ninajitahd ktk upande wa kuandika tena natumia simu tu wala si computer,kuna story km 3 nimeshazidownload ila changamoto ni muda tu

Tafadhali mkuu kama utaona inafaa naomba utuwekee kisa cha Zabron
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 8





Ahadi ambayo nilimuahidi huyu kaka ambaye nilikutana nae gerezani nakunifanyia yote haya sijaitimiza bado yaani kama kungekuwa na mtu angekuwa anaijua hii stori angeniuliza kwanini hadi muda huu sijaenda gerezani kwa mtu aliyenipa mwongozo kuhusu hizi pesa,yaani kwanini naanza kufanya kinyume na makubaliano tuliyoyafanya,kiukweli nilikuwa sina jibu,mipango ikaanza kuwa mingi sana yaani kila ninachofikiria kufanya naona sahihi,kila nikiwaza naona hiki ni bora zaidi ya kile kwa sababu sijawahi kuwaza katika maisha yangu kama naweza kukutana na pesa nyingi kiasi hiki,pengine ningewahi kuwaza ningelishakuwa na mipango thabiti lakini kwa sababu nilikuwa na fight for food yaani maisha ya kupambana kwa ajili ya tumbo tu yaani siku nenda siku rudi na sasa nimepata pesa,nikajiwazia hivi kula ni nini yaani kwa pesa niliyokuwa nazo hizi ni za kwenda kufanya vitu vikubwa sana na wala si za kuwaza tena kuhusu kula,nikajikuta nawauliza watu "hivi kwa mfano ukipata pesa nyingi unaweza kufanya kitu gani?" Kila mmoja ana mawazo yake wengine wanasema "nitajenga nyumba nyingi sana na nitapangisha huku mwenyewe nikiwa nimekaa tu nakula kodi" yaani mawazo ni mengi nawezaje kufanya kiukweli akili ilikuwa inawaka moto.

Katika harakati hizi nakumbuka sana siku moja,naikumbuka sana hiyo siku,nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa nne usiku nilikuwa nimechoka sana nikasema ngoja nijiegeshe nipumzike tu,sikuwa nimejipumzisha kitandani bali ilikuwa kwenye kochi,wakati nimejipumzisha nikaota ndoto na uwaga sinaga kumbukumbu mimi ya mambo ya ndoto kwani kile ntakachokiota kinapotelea juu kwa juu lakini ndoto hii kwanini naizungumza pengine naiona kwangu haikuwa ya kawaida kwani nimeota ndoto niko kwenye kijiji kile nilichokuwa nimeenda kwenda kuchukua hizi pesa na nimejiona nipo ndani ya kile kijumba ambacho mshkaji amenielekeza na taratibu zote mpaka kufanikiwa kupata hizi pesa,nikiwa katika hiki kijumba nikawa najiona nimelala katika kile kitanda cha kamba,kitanda ambacho ndicho nilielekezwa kufata zile pesa,yaani nimelala hapo alafu nikawa najiuliza kwanini nimelala hapa ilihali mimi ni mtu mwenye pesa nyingi na nikiwa katika hiki chumba hakikuwa na mwangaza wakutosha yaani kama mshumaa umewashwa yaani mwangaza wake ni hafifu,nilisikia sauti ya mwanamke akinambia maneno haya "geuka huku unione" nami katika ndoto nikageuka,yaani sasa huu mwangaza ambao niliuelezea kuwa ni hafifu na sikujua unatokana na nini na fikara zangu zikawa zinahisi labda ni mshumaa kwa sababu ilikuwa ni ngumu kitu kukiona vyema na nilimuona mwanamke mmoja mnene sana,mnene mno katika kona ya hiki chumba,sauti ya huyo mwanamke naikumbuka siku zote katika maisha yangu kwa sababu alinambia "maisha yako wewe ni ya hapa,hizo pesa unazoziwaza uko nazo ziko wapi? Hizo pesa si za kwako,unajua yeye kazitoa wapi? Kwanini unaingiwa tamaa? Mbona ni mapema sana unaingiwa tamaa? Ni rahisi sana mtu kupata pesa? Mbona wewe katika maisha yako haujawahi kupata pesa kama ni rahisi,unajua huyu alifanya nini mpaka kupata hizi pesa?" Kiukweli katika ile ndoto huyu mwanamke mnene alinifokea sana na alinambia "usile jasho la mtu bila ya ruksa yake,rudisha jasho la mwenzako maana haujui vyanzo vya pesa hizi,fanya haraka rudisha pesa za mwenzako" nimekuja kustuka kwende ndoto niko kawaida nimelala pale kwenye kikochi kiukweli niliogopa sana yaani huyu mwanamke mnene ambaye sura yake sikuiona vyema ambaye kiumbile ni mwanamke sikuwahi kumuona wala kumsikia kabla,yaani ni vitu vipya kabisa kwangu,nikawa najiuliza "ndoto gani hizi au kwa sababu nawaza sana kuhusu pesa?" Yaani kama alarm ikalia kwenye kichwa changu,nikawaza lakini ni kweli mtu azifukie pesa kule mashambani na bila kumpa mtu yoyote ambaye ni ndugu yake,watoto wake wanateseka kule,amesema ana mwanamke wa maisha wake je ameshindwa kumueleza hata huyo mwanamke anayempenda sana pengine hasiteseke kwa maisha anayoishi uko uraiani aje anipe mimi? Au ni pesa za mambo ya nguvu za giza? Hofu iliingia ndani yangu,nilipatawa na hofu sana kwa sababu ni kweli kupata pesa si kitu rahisi mbona mie napambana sana,mbona mie napambana katika kazi nyingi ninazofanya na sijawahi kupata za kusema angalau nipate pesa nijenge,ninunue gari na nipate hivyo vitu angalau moyo wangu unatamani,mbona sijawahi kupata? Yeye hizi pesa alipata wapi? Kiukweli mpaka kumepambazuka sikupata usingizi kabisa yaani nikajiwa na hofu sana kwa sababu kama nilitishwa katika hii ndoto sikujua imekuja katika mazingira ya wema,sijui kwanini ndoto inijie lakini imekuja kunipa hofu.

Nilikaa kama siku mbili nikaamua kwenda kule gerezani,mimi mwenyewe nikaenda kule gerezani na nilipofika nikapata nafasi ya kuzungumza na yule mshkaji wangu na kiukweli aliponiona alifurahi sana,alifurahi sana akanambia "nilijua tu Rojas utakuja lakini mbona umekuja kwa kuchelewa?" Nikamwambia "unaona nimechelewa? Mbona sijachelewa" akasema "hapana nilitegemea ungekuja mapema zaidi kuliko leo ambavyo umekuja" nikatabasamu nikamwambia "nimekuja huu ni wakati sahihi" akanambia "mbona nakuona huna furaha,kwanini hauna furaha kwani haujafanikiwa katika jambo letu? Nikamwambia "nimefanikiwa" akanambia "najua una shauku ya kutaka kujua nini kipo ndani ya ile mizigo,unadhani ulitegemea kukuta dhahabu kama dhahabu zikiwa wazi lakini umekuta vitu vimefungwa na kufuli" nikamwambia "kwani nilitakiwa nisijue kilichomo ndani mpaka ntakapokuja na mzigo mpaka huku? Akanambia "ndio" nikamwambia "ningewezaje kutembea na kitu ambacho sijui kuna nini ndani?" Akanambia "Rojas lakini nilikwambia utakapokuja na huo mzigo utakuja kwangu na mimi ndio ntakupa maelekezo" nikamwambia "ni kitu ambacho hakiwezekani wewe unajua,tazama mambo yalivyo barabarani kukaguliwa na isitoshe mimi nimeenda kule nikiwa siko vizuri kiuchumi kwahiyo sikuweza kuhatarisha maisha yangu ilibidi nijue nini nabeba isije nikabebeshwa maiti za watu au nikabebeshwa viungo vya watu bila kujua nikajikuta nimeingia tena katika matatizo pasipo kujua na si nitaonekana mimi ni kijana mpumbavu" akanambia "mbona Rojas unaongea maneno hayo" nikamwambia " hapana nimekuja,nimekuja kukusikiliza" akasema "sawa,nashukuru sana,nashukuru sana umekuja nilikuwa nasikia sauti ndani yangu ikinambia hautakuja Rojas,hautakuja,ulivyoziona pesa ulijisikiaje? Haukujisikia kuchanganyikiwa?" Nikacheka,.nikamwambia "kwanini" akanambia "ndivyo inavyokuwa kama haujawahi kama mtu haujawahi kukutana na pesa labda katika maisha yako umeshawahi kuona shilingi ngapi,umeshashika shilingi ngapi? Labda milioni tano,milioni kumi,milioni ishirini au thelasini au hata milioni hamsini,sabini au mia lakini pindi unapokutana na pesa nyingi sana unaweza jikuta unachanganyikiwa,haujawahi kuchanganyikiwa?" Nikamwambia "kwanini unambie hivyo,pesa ambazo sijazitafuta nawezaje kuchanganyikiwa nazo zaidi tu yakupewa mwongozo" akasena "vizuri,Rojas umefanya vizuri sana kuja,si nilikuambia? Umeniamini katika kila nililolisema? Basi na wewe timiza ahadi uliyonipa" nikamwambia "kwani nilikosea kufungua yale matranka na kuzitoa zile pesa na kuzihifadhi katika mazingira mazuri?" Akasema "nilitamani uyabebe matranka yote lakini nimekuelewa mambo yamebadilika na ningekuwa mimi ningefanikiwa kuyabeba matranka lakini mambo uko uraiani sijui yakoje wewe ndio unajua siwezi kukupinga unachosema,kuna kiasi cha pesa chochote ulichotumia?

Nikamwambia "ndio,si nilikwambia nimeenda katika mazingira gani nikawa nahitaji pesa kwa ajili ya kuhonga ili nipite,nilitoa zile pesa na kuweka katika visalfeti" akasema "pesa zote zile? Ulizipangaje? Nikamwambia "nilitumia akili ya ziada kama ulivyonielekeza" akanambia "jicho langu lilipokuona mara ya kwanza lilikuwa na imani na wewe,nashukuru sana" nikamuuliza "hizi pesa umezipata wapi,pesa nyingi kiasi hiki na kwanini pesa hizi haukuzihifadhi benki sehemu ambako ni salama,kwanini umezihifadhi pesa kwenye kijumba tena cha zamani" akanambia "nilijenga kile kijumba kwa kusudi sana,kwani ni mimi peke yangu ndio nimefanya hivyo? Ngoja nikusimulie jambo moja,hizi fedha ni fedha halali kabisa,hizi fedha wala si fedha bandia,hizi ni fedha ambazo nimezipata mimi kwa jasho langu,kwa nguvu zangu,kwa kutumia akili zangu na uwezo wangu wote,niliona sehemu sahihi yakuzihifadhi ni pale" nikamwambia "bado haujanipa majibu lakini kwakile nataka kujua,mbona benki zipo ambapo watu wanahifadhi pesa nyingi sana" akasema "unajua mimi nilikuwa nafanya kazi gani? Nikamwambia "sijui" akasema "mimi nilikuwa ni raia tu nilikuwa nafanya shughuli zangu mbalimbali japo nilikuwa na kipaji cha tofauti kidogo ambacho nilikuwa naweza kuwasaidia watu wengine ambao hawana kipaji nilichokuwa nacho mimi" nikamwambia "kipaji gani hicho" akajibu "ni kipaji ambacho naweza kuzungumza hata na watu wenye elimu kubwa sana,watu wenye uwezo mkubwa wanaweza wakanifata na hata wakazungumza na mimi na wakaniuliza nina shauri kipi katika haya,ndipo nilipo pata pesa hizi kwa jasho langu na kwa nguvu zangu,nikazihifadhi pale na wala usiniulize maswali mengi kwa sababu pesa umeshazipata na ni muda wa kutumia pesa,Rojas kuanzia sasa maisha yako yanaenda kubadilika" nikamwambia "naomba niambie chanzo cha wewe kupata pesa ili niwe na amani na hizi pesa" akanambia "pesa hizi zina amani tu kama utafata na kusikiliza yale nitakayosema lakini kama utaenda kinyume na yale unayoyazungumza hizi pesa haziwezi kuwa pesa nzuri sana kwako" nikamwambia "mbona unanitishia? Mbona sentensi hiyo haukuniambia toka mwanzo" akanijibu "nilikwambia,nilikwambia na ndio maana nikakwambia uape au nani aliapa? Wewe si ndio uliyeapa Rojas? Mbona naona sasa hivi sentensi zako na sauti yako vimekuwa kama vimebadilika,kwani Rojas pesa zimekuchanganya? Mbona mimi nakuona una utulivu sana na katika watu niliowaamini ni wewe,kuna kitu kimebadilika kwako? Kuna vitu ambavyo tulizungumza mwanzo unaona hauwezi kuendelea kuvishikilia? Rojas hizi pesa ni zetu sote na mimi nilizitafuta lakini siwezi kuzitumia kwa sababu niko gerezani lakini wewe waweza kuzitumia hizi pesa lakini kwa makubaliano ambayo tumekubaliana" nikamwambia "sawa,nimekuwa na hofu sana kuhusu hizi pesa" akanambia "kwanini" nikamwambia "sijawa na amani nazo" akaniuliza "kwanini hauna amani nazo? Kwanini ukose amani nazo au uliziwazia mabaya? Kama uliziwazia mabaya lakini kama uliziwazia mema hakuna jambo lolote baya Rojas" kiukweli sentensi zake zikaanza kama kunipa ukakasi hivi kwa sababu ni kweli nilianza kuwaza mabaya na mimi nimekuja huku kwa sababu ya ile ndoto tu niliyoota ndio kimenisukuma ndio nimekuja hapa,kwanini aniambie sentensi hizi niliziwazia mabaya na nini hivyo yaani,nikamwambia "nilishafanya ulichonielekeza sasa nipe maelekezo mengine kwa sababu hizi ni pesa nyingi ni hatari zaidi kukaa nazo pengine nitastahili kuzipeleka benki au unanielekeza vipi" akanambia "hata senti moja haitakiwi kwenda benki" nikamwambia "kwanini,kwanini zisiende benki na nawezaje kukaa na pesa nyingi ndani kiasi hicho,vipi kuhusiana na usalama wangu? Nawezaje kukaa na hizo pesa zote? Kama pesa ni halali hakuna shida yoyote kwanini tusipeleke benki? Akanambia "Rojas kumbe hujui? Si utaulizwa maswali mengi ukizingatia wewe ni dereva taxi tena ambaye hata usafiri hauna ni deiwaka unapata wapi pesa kama hizo,unaweza kuthibitisha kuwa pesa umepata wapi? Kama una mahali unaweza kuorodhesha maelekezo yakujitosheleza kuhusiana na hizo pesa basi unaweza ukazipeleka kwa sababu watu wanaweka pesa benki sama sawa na kile wanachokipata kwenye movement za maisha yao ya kila siku,ebu niambie mzunguko wa pesa yako,pesa nyingi kama zile umezipaja wapi,utasema umezipata mashambani,kwenye shamba la nani? Utasema ulioteshwa,ulioteshwa vipi? Unataka pesa zote nilizozipambania kwa maisha yangu yote zishikiliwe kwa ajili ya uchunguzi?"

Nayakumbuka haya maneno aliyonambia huyu kaka,tunazungumzia pesa nyingi ambazo mpaka sasa hivi nimezikusanya idadi yake ya pesa nimezihesabu mpaka nachanganyikiwa,nikatulia na kusubiria maelekezo yaidi kujua nini sasa nafanya na hizi pesa,akanambia "nini unawaza kichwani mwako,kuna kitu ambacho umekuwa ukitamani kufanya pale utakapopata pesa nyingi?" Nikamwambia "hapana,sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ntakuja kupata pesa kiwango kama hiki" akanambia "pale ulipofanikiwa kuzileta hizi pesa na kuwa nazo ndani nini ulifikiria kichwani kwako,nini,kufanya kitu gani?" Nikamwambia "vitu vingi sana nimefikiria ila kwa sababu pesa sio yangu nikarudi kwa mwenye pesa anipe maelekezo kwa sababu najua ulihifadhi hizi pesa kwa siku zote ina maana ulikusudia kufanya kitu labda nisikie ulikusudia kufanya kitu gani" akanambia "nyakati hizo wakati nimepata hizi pesa sikuwa na uwezo wakuzitumia kwa nyakati hizo japo kuna vitu niliviwaza ingawa najua kwa sasa hivi mambo uko nje yatakuwa yamebadilika,wewe unaendesha taxi vipi? Unauonaje ulimwengu wa taxi kwa ujumla je niku chenye faida? Unajua kwa pesa zile tunaweza kununua taxi ngapi? Nikamwambia "na ndio maana nikazungumzia habari yakupeleka pesa benki kwa sababu mojawapo ni tujue zile pesa ni shilingi ngapi" akasema "hauwezi kujua idadi ya zile pesa,wewe ni kuzitumia tu" nikamwambia "kwanini unasema hivyo,mbona unanipa wakati mgumu sana na ni pesa gani ambazo hazihesabiki wakati watu wanahesabu hadi mabilioni na mabilioni na mabilioni lakini inajulikana ni kiasi gani cha pesa kwanini zile ziwe shida kuzihesabu?" Nilimuuliza hivyo na mengineyo kadhaa ila kwa sababu muda ni mdogo haujitoshelezi kuzungumza hayo yote na alinambia "muda ni mdogo lakini nikupe muda ukajifikirie,rudi baada ya muda mfupi usikawie sana,utakachokiwaza njoo unishirikishe nakutegemea sana kwa sababu wewe ndio unajua hali ya uko nje,angalia ulimwengu wa udereva wa taxi kwa ujumla uone unaweza kuagiza magari mangapi" nikamwambia "siwezi kuagiza magari ngapi wakati sijui idadi ya kiwango cha pesa,ni dhambi kujua kiasi cha pesa nilichokuwa nacho mule ndani? Akasema "Rojas hauwezi kujua kiasi cha pesa kilichomo mule ni nyingi sana" nikamwambia "naomba hata nipambane nitafute hata mashine nihesabu zile pesa" akasema "uliahidi kunisikiliza kwa kila ntakachokisema mbona tena kama unataka kuzungumza vya kwako wakati pesa ni ya kwangu? Nikamwambia "pesa ni ya kwako lakini usinitumikishe" akanambia "kwanini unanambia hivyo" nikamjibu "hapana kwa sababu unavyozungumza vitu mimi sivielewi" akanambia "nenda nyumbani kidogo pumzika,tafuta nyumba nzuri Rojas,tafuta nyumba nzuri ya wewe kuishi,tafuta kitu uanze kukifanya mapema ili watu watakapoanza kuona macdiliko yako wasihisi vitu vibaya" nikamwambia "una maana gani? Akanijibu "tafuta hata biashara ndogo" nikamuuliza " kwa mfano kama nini" akanambia "fungua duka la nafaka" nikamwambia "sina hobie na hivyo vitu" akanisisitiza "fungua duka la nafaka muweke hata ndugu yako hapo na naamini mtaji unaweza kufika milioni ishirini,mtaji wa milioni ishirini kwenye nafaka unaweza kuuza nafaka za jumla,wewe unauza vitu vya jumla" nikamwambia "kumbe una mawazo" akanambia "nina mawazo,milioni ishirini inaweza kukuwezesha kwanza,tafuta nyumba nzuri,usijenge panga nyumba nzuri haraka sana,usipange kwenye nyumba ndogo kwani zile pesa zinahitajiwa kuchimbiwa chini unakuwa unaweka mazingira mazuri kabisa kwani wewe ndio utakuwa unaenda kuzichukua,ndio usalama na ni lazima uzihifadhi katika matranka"
Baada ya maagizo haya ya mwisho nikayabeba na kuondoka zangu kurejea nyumbani ingawa mara baada ya kutoka katika mazungumzo na huyu mtu hofu ikawa juu zaidi kutokana na majibu aliyokuwa akinipa,hofu ikanijia katika hali ya kibinadamu kwani kweli pesa anazo lakini kwanini hazihesabiki na wakati idadi ya pesa zinaweza kuhesabika yalinipa hofu!
Yajayo yanafurahisha!


ITAENDELEA
Kweli pata pesa tujue tabia yako
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 11



Moyo wangu unatunza siri na moja kati ya vitu nilimuahidi huyu kaka kule gerezani ni kuhusiana na kutunza siri,niliifanya siri hii kuwa ya sisi wawili peke yetu na yeye akiniambia "nimekupa siri ya maisha yangu sijawahi kumpa mtu yoyote hii siri mahali nimetunza pesa sikuwahi kumwambia mtu na ndio maana kile kijumba watu hupita na pengine wengine uenda kufanya shughuli zao uko na hawajawahi kujua chini ya ardhi ziko pesa nyingi,mimi nikamuahidi ya kwamba nitaitunza siri hii lakini kaka amezungumza nami katika lugha ya urafikiya undugu kabisa,nasikia moyoni mwangu angalau niweze kusema nae jambo,nikamwambia kaka "kuna vitu ni vigumu sana hata kusema,naogopa hata kusema" kaka akanambia "ni kitu gani mdogo wangu kama ni cha hatari niko tayari hata mimi kuingia kukusaidia sitamani kukuona unapata matatizo,unajua" nikamwambia "kaka najua" nikaketi na kaka na nikamwambia "hii ni siri,ni siri ambayo sijawahi kutaka kumwambia mtu yoyote yule" kaka akanambia "hata mimi ntaifanya kuwa siri kwa sababu wewe mdogo wangu umetaka iwe siri,niambie" ndipo nilipoanza kumwambia kaka ila nilimwambia kwa uchache sikumueleza kwa upana kama safari ya huyo mtu na mimi ilipoanzia,nilimwambia "kaka ni kweli nina pesa,unaona nafanya maendeleo haya unaona ninavyoagiza magari,unaona jinsi nimefungua biashara yaani kufungua duka la jumla na nimeweka pale kiasi cha milioni ishirini,ni kweli nina pesa lakini kaka hizo pesa si zangu,ni pesa za mtu na huyo mtu amekuwa anatamani kufanya makubwa sana lakini yeye amekosa hiyo bahati ya kuishi maisha ambayo mimi naishi ya uhuru" kaka anakanambia "una maanisha nini,ni nini ambacho unamaanisha? Ni mtu gani ambaye kakosa uhuru,ni vitu gani unazungumza,nikamwambia "kuna mtu amenipa majukumu ya kumfanyia vitu vyake kwakuwa yeye hawezi kufanya hivyo" akanambia "ni nani huyo na kiasi gani cha pesa akupe hata uweze kuagiza magari mengi kiasi hiki na hizo pesa unaweka wapi mwisho wa siku uweze utahatarisha maisha yako na hizo pesa unazijua amezitoa wapi? Kaka alinihoji kwa kuonesha kunijali sana na ni kweli kaka ananijali sana,nikamwambia "mtu huyu yuko gerezani kaka" kaka akashangaa sana "yupo gerezani? Sasa mtu yupo gerezani anawezaje kukupa wewe pesa? Nikamwambia "kaka ni stori ndefu sana ila elewa niko na pesa ila si za kwangu,mtu huyo yuko gerezani anatumikia kifungo na ameniomba nimsaidie kufanya hivi vitu nikiwa uraiani,kwahiyo nimechukua majukumu yake nafanya vitu ambavyo yeye alitamani kuvifanya ili siku moja akitoka gerezani aone hatua ameshaipiga kuliko pesa kuendelea kukaa sehemu bila kuzalishwa" nakumbuka kaka alinambia "kwahiyo umekaa chini na kunitungia kastori,umenitungia kasimulizi kakusadikika flani hivi,iko kitu kinawezekanaje? Hakuna kitu kama iko unanidanganya" nikamwambia "kaka nilihisi hata nikikwambia hautaweza kuniamini" akanambia "ni nani uko gerezani,ni nani ambaye awe na pesa hizi akupe wewe,hana ndugu? Hana watu wa karibu akupe wewe?

Nikamwambia "kaka huyu ni mtu ambaye yuko gerezani ana muda kidogo lakini ndugu zake walimtelekeza uko gerezani,hakuna watu wamekuwa wakienda kumwangalia hata kumtia moyo,hakumuona mv wa kumpa hilo jukumu,kipindi mimi naenda gerezani na nikaanza kuwa na urafiki naye ndio kipindi aliniamini nakuniona ni mtu mwema na akaniomba kama naweza kuwa mwaminifu kwake,ndicho kaka kilichotokea" kaka akaniuliza "ndio mwenye wale watoto uliokuwa ukijipa stress? Nikamwambia "ndio kaka" kaka akaanza kuamini katika nnachokisema baada ya kuendelea kumwambia lakini kaka aliyashangaa sana haya maelezo ambayo mimi namwambia nakumbuka sikutaka kumuweka kaka kiundani zaidi niliongea hayo tu kwa uchache,aliniuliza "pesa ziko wapi? Nikamwambia "kaka siwezi kukwambia" akasema "mimi ni kaka yako" nikamwambia "kaka naweza kukwambia vyote lakini nilimwambia mtu huyo sitasema kwa sababu ni maelekezo yake aliyonipa,kama nilivyokwambia kaka hizi pesa si za kwangu ila yeye aliniruhusu nifungue duka,lile duka la nafaka ni la kwangu lakini kuhusu magari sio ya kwangu,hivi vitu vingi sio vya kwangu"

Nilimueleza kaka yangu kwa upendo kabisa kwa sababu huyu ni kaka yangu na niko nae karibu sana katika mahangaiko yangu,katika mateso yangu kwa mfano kipindi kile nimekwenda gerezani ni kaka ndio alinipigania mpaka hatua ya mwisho akunyamaza,hakutulia mpaka alipoona mimi mdogo wake nimeachiwa huru kwahiyo yupo na mimi siku zote kwahiyo naamini nimemwambia kaka yangu naamini nimemwambia mtu sahihi,nilishea na kaka hayo na kaka alizidi kuniuliza maswali lakini sikujibu yote kwa sababu sikutaka kuzungumza kila kitu,aliniuliza "sasa ulipataje hizo pesa,alizihifadhi wapi?" Hayo yote aliniuliza lakini sikusema.
Baada ya kumwambia kaka hayo maneno nakumbuka niliporejea nyumbani nilisikia moyo wangu unauma sana,nilisikia moyo wangu unapatwa na uchungu kwanini nimesema,nilijilaumu kwanini kinywa changu kimezungumza siri ambayo nimeitunza kwa ahadi kuwa nitaitunza na sitaisema,mbona naumia hivi nami naona nimemwambia mtu sahihi,mbona nimemueleza kaka yangu kwanini nasikia hivi vibaya? Sikulala mpaka asubuhi,ushawahi kufanya jambo alafu ukawa unajilaumu kwanini unafanya? Mimi nilisikia hatia ndani yangu kwanini nimemwambia kaka,kama ningenyamaza kwani nini kingetokea,angenifanya nini? Niliona nimekosea,sikutakiwj kufanya hivyo.

Lakini unajua neno linapotamkwa linakuwa lishatamkwa unakuwa hauna namna yoyote yakuweza kulifuta tayari linakuwa lishatamkwa,nakumbuka kulipopambazuka na siku mpya kuingia kaka alinitumia meseji ikisema Rojas nataka tuongee,naomba nije nyumbani kwako tuzungumze,nilikuwa na ratiba za mishe zangu za hapa na pale lakini kaka yangu namheshimu sana na kama anasema ana jambo anataka kuja nyumbani litakuwa ni muhimu sana,nikamwambia kaka sawa na kaka alikuja nyumbani akanambia "mdogo wangu sijalala usiku kwa maneno uliyoniambia nimekosa usingizi,sijajua uko katika hatari kwa kiasi gani sijui lakini tu kwa experience yangu ya maisha,kwa maisha mimi nimeishi,mimi ni kaka yako najua vitu vingi,napata mashaka sana,nasikia kukosa amani sana kuhusiana na kile umenieleza jana lakini kuna kitu nimesikia amani nacho ndani ya moyo kwa sababu umesema huyo mtu yuko gerezani na hajawahi kumwambia mtu yoyote kuhusiana na hizo pesa,sasa mdogo wangu mimi najambo nataka kukwambia,mtu yupo gerezani na pesa unazo wewe uraiani unajua anatoka lini? Sikujua kaka kwanini ananiuliza maswali kama haya tena akiwa siriasi kweli amefunga safari tuje tuzungumze kuhusiana na hili na nikamwambia "kaka, sijui labda kuna neema itakuja ya yeye kutoka au pengine hiyo neema isipotokea uenda maisha yake yote akamaliza gerezani" "kwani amefungwa kifungo cha maisha? Nikamwambia "kaka kesi ya huyo mtu ilikuwa ngumu sana kwa maelezo ambayo nimepata,alinambia ni miaka 30 lakini nikaja nikagundua yule mtu amefungwa maisha" akasema "amewezaje kukudanganya wakati ni rahisi tu kujua miaka ya mtu" nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "mimi naweza kuifanya hiyo kazi nikajua miaka yake ambayo anatumikia uko gerezani,yaani tujue miaka yake ni mingapi,ni wa kutoka au siwakutoka kwa sababu hapo tupate uhakika" sasa nikawa najiuliza kwanini kaka azungumze hivyo,nikamwambia "yanini kuyajua hayo kwa sababu mimi nimemshauri kitu kwa sababu anazo pesa nyingi alizitafuta katika nafasi yake akiwa uraiani na pesa inanguvu nami nilimshauri ikiwezekana sehemu ya pesa yake ebu atumie uenda akaupata uhuru kwa nguvu akarudi huku uraiani kama ni rushwa au namna yoyote ile itakavyowezekana" nakumbuka kaka akanambia "wewe umshauri maneno kama hayo kwanini? Nikamwambia "kaka ni mtu mwema tu" akanambia "unajua hizi pesa amezitoa wapi? Nikamwambia "hajawahi kunieleza wapi alipozitoa" akanambia "hawa ndio watakuwa watu ambao ni wahujumu uchumi" nikamwambia "unamaanisha nini? Akanambia "kuna watu ambao walijilimbikizia pesa lakini kuna nyakati kuna msako uwa unapita na watu uhofia kuhusiana na hizo pesa kwa sababu hawaziweki benki wanaogopa,watu wengi kumekuwa na historia walikuwa wakichimbia pesa ardhini,vipi hizi pesa hakukwambia ukazichukue ardhini?

Nikashtuka,nikamwambia "kaka kwanini tunazungumza haya na wakati tulishazungumza jana na tumeshamaliza kwa sababu niliona nikushirikishe kaka yangu" akasema "ah umenishirikisha ila wewe bado mdogo hujui vitu vingi mimi ni kaka yako,sasa mimi ni kaka yako mimi najua maisha na najua vitu vingi,unajua ni kwanini huyu mtu kakutafuta wewe? Kwanini uwe wewe ushawahi kujiuliza? Hana watu ambao ameshawahi kufanya nao dili? Hawapo? Kwanini iwe wewe? Unajua kwanini? Nikamwambia "ndio najua" akaniuliza "unajua nini? Nikamwambia "najua kwakuwa tulikuwa marafiki,tuliishi kwa furaha na akaona mimi ni mtu ambaye sina shida yoyote" akasema "sio kweli,iko sababu nyuma ya huyo mtu kukutafuta wewe" sasa mimi kweli uenda kaka yangu ana upeo mpana na akili nyingi kuliko mimi siwezi kataa,sasa mimi namuuliza kaka "kwa sababu zipi? Anasema "si unaona hujajua kwanini akutafute wewe,ngoja nikwambie mdogo wangu mitego ya pesa ni mikubwa sana,waweza pesa itumia leo pesa isiyo halali inaweza ikakuletea shida hata baada ya miaka 10 baadae inaweza ikakuhukumu,ikawa kitanzi kwako,ikatesa moyo wako na maisha yako na ndugu zako" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "pesa hiyo siyo halali,hiyo pesa ni pesa haramu na amefanya hivyo ili siku hukumu ikija ikukute wewe na yeye akiwa pembeni ametulia" nikamwambia "sasa litampata vipi mtu aliye gerezani" nakumbuka kaka akanambia "ndio maana nakwambia wewe bado mdogo,uelewa wako bado mdogo haujajua kuchanganua mambo,usalama wako Rojas ni kukata kila connection ya wewe na huyo mtu wa gerezani na kukata connection na majukumu yote aliyokupatia na hizi pesa zisiwe chini yake,ziwe ni pesa zako sijui kama unanielewa? Kaka alinambia maneno hayo tena ni siku ya pili tu yaani nimemwambia jana na leo ananiamkia asubuhi kumepambazuka kaka anakuja na ujumbe kama huu,nikamwambia "kaka mimi Rojas siwezi kufanya kitu kama hicho,siwezi kufanya kama hivyo,siwezi kutumia pesa isiyo ya kwangu kuifanya ya kwangu siwezi,siwezi kaka kufanya hivyo,ahadi niliyompa mtu huyu nitaitimiza siku zote siwezi kuikengeuka hata kiku kimoja maana nimetafuta pesa katika nyakati zote sikuwahi kupata kwanini nimsaliti mtu ambaye amekuwa mwaminifu kwangu ambaye ameamua kunitunuku na kunitoa katika umaskini nakunipa maisha mengine,kwanini kaka unazungumza maisha ya ushetani hivyo" nakumbuka kaka akacheka na akasema "ushetani? Mdogo wangu kweli hauyajui maisha? Nazungumza mambo ya maana wewe unasema ushetani mimi nazungumza ushetani?" Kiukweli sikupenda kabisa kauli za kaka kabisa na nikamwambia "ndio maana moyo wangu umekosa amani kabisa kukushirikisha,hukustahili kunambia maneno haya tena ikiwa mapema kama hivi" akanambia "nakwambia mapema kwakuwa wewe hujui,wewe bado mdogo hujui kadri unavyozidi kwenda gerezani,wewe si kila siku uwa unaenda gerezani mwisho wa siku utastukiwa,huyu mtu bado anafatiliwa kule gerezani usihisi watu wametulia kumfatilia nisikilize mimi ninachosema" kaka akanambia "huyu ni mhujumu uchumi hawezi kukwambia na mimi ndio nakwambia sasa kwa sababu najua haya mambo ziko nyakati hata wewe ulikuwa bado mdogo kuna watu walifanya hujuma,walihujumu uchumi hawa watu walifanya namna nyingi hawajaacha kufatilia siku mpaka anapokufa ndio huyo mtu ndio wanaacha hivi ninakwambia we si uwa unaenda si una route za kwenda? Unavyoenda watu wameshachora ramani,kuna mtu ana dot dot alikuwa gerezani ametoka lakini anaendeleza ukaribu na huyu mtu,mdogo wangu sasa hivi unakamatwa,unakamatwa na unaniingiza kwenye matatizo kata hiyo connection haraka sana usiende gerezani unakamatwa na ninavyozungumza hivi na pengine si siku nyingi kutoka leo na umezungumza kwangu kwa sababu Mungu hataki upate matatizo"

Kaka anaendelea kunambia vitu yaani mimi naenda gerezani kila siku sikuwahi kuwaza hata siku moja kuwa hizi route za kwenda gerezani ninazofanya labda zinaweza zikawa na ishara yoyote lakini kaka anasema huyu mtu bado yuko kwenye uangalizi kwani amehukumiwa lakini haimaanishi kwamba ameachiwa,huyu bado anafatiliwa yuko kwenye uangalizi.
Toka kaka amezungumza siku ile alinipa hofu,nilianza kuwa nahofu moyoni mwangu kwa maneno kaka aliyoniambia,nakumbuka kama baada ya siku mbili toka siku zile tumezungumza na nikamkatalia kaka akaja na akanambia kitu cha ajabu sana,mimi nilizungumza na kaka na sikuwa nimemtaja mtu kwa majina yake ambaye ndiye yuko gerezani,ambaye ndiye amenipa hili dili na mimi nafanya hivi katika mazingira na sikumuweka kaka kiuwazi sana,kaka alinijia na jina kamili,jina kamili la yule ndugu kule gerezani😂 na akanambia alikuwa gereza flani na akapelekwa gereza flani,yaani amemjua sasa kuliko hata mimi,kuliko mimi ambaye nafanya nae kazi katika mfumo ambao nimekuambia na akanambia uwa naenda gerezani mara ngapi (akanipa idadi),niliogopa sana na nikamuuliza "kaka umeyajuaje yote haya" akasema "nimejua kwakuwa mimi ni mkubwa kwako,mimi ni kaka yako,najua mambo kuliko wewe,hivi unajua kuna watu pale gerezani kila unapoenda kumtembelea uwa wanarekodi? Unajua wewe mpaka sasa hivi inawezekana umeshaanza kufatiliwa mpaka unavyoondoka asubuhi mpaka jioni shughuli zako unavyofanya na watu unaoongea nao,unajua iko kitu?" Niliogopa sana na kaka akasema "uko unatazamwa mdogo wangu,watu wanakufatilia" nikamuuliza "kaka umejuaje,umeyajuaje haya?" Kwa sababu kaka yangu ni mtu wa kawaida tu,ni mtu wa kawaida kusema amjue hadi mfungwa hivyo mimi nilivyomueleza hadi apate connection na kujua mimi nilienda siku flani na siku flani huyo ni mtu wa namna gani,si unaona unaogopa,unajua hii sentensi ninayokwambia maana yake nini,maana yake yule mtu ni kweli siku zimepita ila bado anaendelea kufatiliwa na amemtafuta mtu mdhaifu mdogo ili isiwe rahisi mtu yoyote kujua lakini mambo yashajulikana,unajua uko katika hatari kwa kiasi gani? Unajua?

Niko hapa kaka yako nataka nikusaidie,nataka nikusaidie,utapata matatizo upigwe kifungo cha maisha,kwanini hajatumia ndugu zake,kwanini akutumie wewe? Maneno ya kaka yalizidi kuniogopesha na labda kutokana na umri wangu sielewi lakini niliogopa,naogopa kwenda gerezani,sitaki kwenda tena uko.



ITAENDELEA!
Aisee
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 14


Maisha ni safari ndefu sana! Wale rafiki zangu wakanitengenezea ushawishi wao na kwakuwa nilikuwa na msongo wangu kichwani na kuanza kujaribu vileo tofauti tofauti lengo likiwa ni kujaribu kuupoza au kuondoa mzigo uliopo kichwani,na nikawa nakunywa pombe lakini zile pombe nikawa nakunywa kwa tahadhari nikihofia nisije nikapitiliza ulevi hadi nikafikiri kuja kuropoka kuhusu siri zangu na yule kaka.

Nakumbuka kuna siku kaka alinijulisha kuwa ana sherehe ya kijana wake na aliniomba nimpush katika suala la sherehe hiyo nami nikamwambia "sawa mimi niko na wewe na nitajitoa kadri nitakavyoweza yeye aniambie tu nini anataka na tutafanya" alinambia mahitaji yanayohitajika nami niliyafanya hayo kwahiyo tulikutana tena wakati mwingine wakati shughuli ikiwa inafanyika nami nikawa ni mmoja kati ya washiriki pale,tunafurahi kwa pamoja,siku njema tunafurahi na nini na kulikuwa na vilevi vya aina mbalimbali vilikuwa vimenunuliwa basi na mimi nikatumia kile ambacho kwa wakati huu nikikitumia nakuwa najiona napata stimu zaidi yaani najisikia furaha,kwahiyo ni siku ambayo nimejikuta nimekunywa,nimekunywa,nimekunywa zaidi tofautitna siku za nyuma hapa kidogo nilikuwa nakunywa kiasi flani,tulikuwa na kaka na rafiki zake na washkaji zangu pia ambao mimi nilikuwa nimewakaribisha na vitu kama hivyo,yaani ni pati ya furaha,nakumbukaka kaka alinambia "naona umechangamka mdogo wangu,haya sasa ndio maisha mdogo wangu unayotakiwa kuishi,unatakiwa kuishi kwa furaha,acha kujitenga,mambo ya kujitenga sio mazuri mimi najua hupendi vitu gani nimeshakuelewa,tuishi kwa amani sasa usianze kunikwepakwepa" ujue ukiwa katika hali umelewa unaweza ukazungumza vitu ambavyo katika hali ya kawaida unakuwa huwezi ukavizungumza,nikawa namwambia "kaka mimi unaniboa bwana,unaniboa sana" akanambia "mdogo wangu basi yaishe toa iko kinyongo moyoni tuishi kama zamani,mimi ni kaka yako na yote hayo ni kwa upendo wangu tu wa dhati lakini kama nilikuwa nakukosea nisamehe,angalia shughuli hii yote umeibeba wewe leo mimi hapa nasifiwa,napata heshima,watoto wangu wanaendelea vizuri,mahitaji mbalimbali naweza kuyafanya,nayafanya lakini sio mimi bali ni wewe ndio unawezesha hayo,sasa hivi familia yetu imekuwa bora,maisha yamekuwa mazuri na yote ni wewe ndio unayeyafanya hayo kwahiyo siko tayari kuona nagombana nawe mdogo wangu" hayo maneno kaka aliniambia nami nikawa nafuraha kwa sababu sisi ni ndugu unajua pamoja na yote yanayoweza kutokea na kukosa kuelewana,kiukweli nilifurahi sana.

Nikiwa hapa kwenye pati nilipigiwa simu,aliyenipigia simu alikuwa ni yule msicpgana wa yule kaka kule gerezani na sio mtu ambaye uwa ananipigia pigiaa simu kwani sijaweka mazoea hayo ya yeye kunipigia simu,nilipokea nakatika hali niliyonayo kichwani (kilevi) niliipokea ile simu kwa uchangamfu sana,akanambia "uko wapi? Nikamwambia mahali niliko,akanambia "natamani hata nije sijisikii hata vizuri" hii sentensi naikumbuka alinambia,sasa namimi tena nina kilevi,nikamwambia "njoo,uko wapi? Uko wapi nimwambie dereva akufate hapa kuna pati hapa tunafurahi yaani tunaweza tukakesha mpaka asubuhi"akanambia "sawa basi nifanyie mpango niweze kuja" nikamkodi mshkaji palepale ambaye ni dereva amfate alipo.

Sherehe ilikuwa kubwa kwani ilianza toka asubuhi kwa kuchoma nyama na watu kunywa supu yaani ni furaha na vinywaji vipo vya kutosha,nikiwa nimekaa hapa kweli yule msichana akaja na akanambia "yaani hata umejuaje hadi umeniita hapa,yaani hata sijui ingekuwa ni siku ngumu kiasi gani kwangu ,natamani hata nitumie wine yoyote sweet nami palepale nikatoa maagizo aletewe chaguo lake naye aweze kuenjoy,nikawa nimekaa nae kwa karibu nikawa nazungumza nae na akanambia "yaani nina msongo wa mawazo usio wa kawaida" nami nikamwambia "basi leo msongo wa mawazo unaisha hapa kwa sababu leo utafurahi na mastress yote utayaacha hapa"akanambia "kweli? Unanambia kweli,ntafurahi sana" namimi nikawa ni mwenye furaha,huyu msichana ni mkubwa,huyu msichana kwangu mimi ni mkubwa lakini kutokana na mazingira tuliyokuta kabla ni tunaheshimiana tu hatujawahi kuvunjiana heshima tukawa tunapiga stori za hapa na pale,muda ukasogea na kadri muda unavyosogea nami nikawa najikuta nalewa zaidi,pombe kadri muda unavyoenda ndio nami najisikia kutaka kuchangamka zaidi,nakumbuka huyu dada aliomba aende maliwato,aliposimama kuelekea maliwato yaani nilipomuangalia niliona ni msichana mwenye shepu nzuri ajabu wakati sijawahi katika hali ya kawaida kufeel kitu kama iko,yaani sijawahi kumtizama kabla huyu msichana na kupata matamanio yoyote,ni mwanamke ambaye mshkaji wangu wa gerezani alimpenda,alinipa maelekezo na moja kati ya ahadi niliapia ni nisimguse mwanamke anayempenda bali nimsaidie,nilikuwa sijawahi kuwaza lakini leo nilisikia hiyo kitu ndani yangu hata nikasema imekuwaje leo tena?

Aliporejea tukawa tunaendelea na vinywaji na maongezi na pombe zikawa zinanituma tuondoke eneo lile na kwenda eneo jingine tofauta na nikamwambia yule msichana "unaonaje tukahamia eneo jingine? Akanambia "mbona hapa pametulia tu,tukae hapahapa" nikamwambia "nimesikia sana makelele eneo hili,tukae kidogo alafu tutaenda uko" akasema "sawa" dada amechangamka nami nimechangamka yaani ilikuwa balaa,nakumbuka alinambia "leo imekuwa ni siku ya furaha sana kwangu" nikamwambia "kweli? Akanambia "kabisa,najisikia amani,najisikia amani kama nimetua mizigo" nikamwambia "kwanini? Akasema "hata sijui,nasikia tu hivyo" nikamwambia "vizuri,vipi changamoto zako" akanambia "yaani sitaki hata tuzungumzie kuhusu yule mtu,sitaki hata kumuona,mimi na yeye tumeshamalizana,sitaki tena" nikamwambia "kwanini mtu anakuumiza mwanamke mrembo kama wewe,ni mwanaume gani mwenye moyo mgumu kiasi hicho anakuumiza msichana kama wewe" akatabasamu,nikamwambia "unatabasamu vizuri sana" akatabasamu tena,nikamwambia "wewe ni msichana mzuri sana na hautakiwi kuumizwa" akanambia "unajua wewe umekuja kwenye maisha yangu na ukanipa tumaini jipya kabisa,sapoti ambayo umenipa nilikuwa sijawahi kuipata katika maisha yangu,yaani umenifanya sasa hivi nione kama naweza kusimama mwenyewe na kutokuhangaika kuhusu mambo ya mahusiano kwa sababu sasa hivi naweza kujipambania katika mwanzo mzuri ambao umenipa" msichana alinambia maneno mazuri sana,pombe ilinifanya nimuone huyu msichana ni mrembo isivyo kawaida lakini mimi mpaka kesho uamini ile haikuwa akili yangu.

Unajua waweza kumuona mtu tofauti kwa sababu ya pombe lakini pale akili yako inaporudi clear kabisa unashtuka sana,mimi nilishtuka kwanza nakutana na mwanga kukiwa kumeshapambazuka,akili yangu inajiuliza kwani uko wapi? Kwani niko wapi? Nafumbua macho naangalia najikuta niko kwenye room,hiki si chumba ambacho mimi uwa nalala,naangalia naangalia najikuta nimelala na msicpgana pembeni! Ndipo kumbukumbu zinanijia kwa haraka sana,wakati kumbukumbu zinanijia na huyu msichana alikuwa amegeuka upande mwingine akajigeuzia kwangu namuona sasa ana kwa ana! Dah nimevunja makubaliano na mtu ambaye niliapa mimi sitafanya iko kitendo,sijui kwanini alinambia ile sentensi nimuahidi kwamba nitamsaidia na sitakuwa nae katika ulimwengu wa mahusiano,sijui niyaite mahusiano au niyaiteje na sijazungumza na huyu msichana mimi mambo kuhusu kumpenda,sijazungumza,sijazungumza kabisa,ushawahi kusikia mtu anasema nimefanya jambo kwa bahati mbaya? Mimi kwangu niliona nimefanya kwa bahati mbaya,imeshatokea!

Sikutaka hata kupoteza muda nakumbuka nilivaa nguo zangu kwa sababu mimi nashtuka nikiwa niko mtupu yaani sina nguo yoyote ile na kumbukumbu inaniambia yapo yameendelea mambo! Huyu dada aliamka kwa tabasamu,akijinyoosha akinambia ""Rojas mbona unaonekana kama unaondoka? Nilimwambia "tulipanga tuwe hapa? Tulipanga tuwe hapa?" Akanambia "unasema nini Rojas,mbona tuliongea na kwanini unaniuliza swali kama hilo,mbona ni mapema sana ebu njoo tupumzike zaidi" nikamwambia "hapana" akasema "kwanini? Nikamwambia "nina mambo mengi sana ya kufanya naona nimechelewa" akasema "sasa unaniacha hivi,unaniacha hivi kweli? Nikasikia kichwa kinaniwaka moto,najua hii hali haijawahi nikuta mimi peke yangu kwangu naamini hata wewe msomaji unaweza kujikuta katika hali kama hii yaani umejikuta na mtu pasipo katika mazingira yasiyoelezeka alafu unajikuta kumepambazuka umeshafanya vitu ambavyo haukuvitarajia,haukupanga hata kabla ya kuanza kutumia iko kilevi,unajikuta ushafanya na mshtuko wake uwa mkubwa.

Narudia tena,maisha ni safari ndefu sana,mwanamke huyu ananiambia "naondokaje sasa,yaani namuachaje hivyo?" Nina kikao muhimu sana na nimeshachelewa sana,akanambia "sawa sasa kwahiyo? Nikamwambia "wewe endelea kupumzika alafu tutaendelea kuwasiliana" akasema "sawa basi njoo hata uniage" nikamwambia "tutawasiliana" akasema "no bwana usifanye hivyo" nakumbuka yule msichana alikuwa kitandani ma akashuka,alishuka akiwa mtu kabisa akaja akanikumbatia,akanikiss na kunambia "umenipa tumaini jipya kabisa,naomba ahadi uliyonipa toka jana ya kuanza mahusiano na mimi naomba iwe kweli" yaani sikumbuki hata kama nilimwambia huyu msichana kama nampenda,sikumbuki kabisa na maneno haya anayoniambia nachanganyikiwa kabisa,akanambia "nakupenda na nimegundua wewe ni mtu wa tofauti sana,yaani umeufanya usiku wangu ni kama nazaliwa upya,naona mwanga mpya,naomba basi ukimaliza kikao unitafute" sina jingine ambalo nilimwambia zaidi ya kumwambia "basi baadae" niliwaza,niliwaza,nilijuta,nilikaa kwenye gari kwa muda mrefu nawaza nikijiuliza nimefanya nini mimi leo? Ilikuwaje? Ilikuwaje? Sikuwa na kikao wala nini ile ilikuwa ni njia yakuondokea tu pale,nilienda nyumbani na nikajimwagia maji yaani akili yangu hainipi,akili haitulii na nikaamua kukaa ili kutuliza akili na nikawa niko chumbani nimekaa,nimekaa tu mpaka ikafika majira ya saa saba hivi "bado haujamaliza kikao? Nikamwambia "bado,bado sijamaliza kikao" akanambia "basi nilikuwa nawaza nikutengenezee kitu uje ule maana jana umetumia vilevi sasa angalau upate chakula chenye nguvu" inamaana hapa anataka niende kule kwake sasa ndio kwenda kula hicho chakula kwani alishatoka kule hotelini tulipolala usiku uliopita,akanambia "nilipiga simu ukawa haupatikani" nikamwambia "nimewasha muda sio mrefu,nitakupigia,nitakupigia" akasema "kwahiyo nakusubiri,si utakuja jioni? Nikamwambia "nitakupigia" Yaani hata sijui nilimwambia nini huyu msichana lakini niliona ni vitu ambavyo nikaona vinanichanganya kichwani.Mchana nikasema ngoja nitoke nijinyooshe miguu kidogo na nilipokuwa njiani nikakutana na kaka naye baada ya salamu akaniambia "vipi mbona ukatokomea kimoja,lazima utakuwa ulikuwa na furaha sana na yule mtoto mrembo" nikamwambia "kaka acha tu,acha tu niko na maumivu sana ya moyoni" akanambia nini tena? Nikamwambia "hata hayaelezeki,achana nayo.



ITAENDELEA!
Pombe siyo chai
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Stasahau’ cha Radio Free Africa​


Sehemu ya 19


Mtaalamu alizidi kunidadisi na alinambia "pesa ziko kiasi gani zilizobaki toka wewe uzipate? Nikawa najiuliza je naulizwa maswali gani haya sasa,mbona kama mganga ananichimba sana? Na naomba ukumbuke hapa kwa huyu mganga nimeletwa na mtu na sijui dhamila yake ya ndani na mganga anataka nimletee pesa kadhaa kutoka katika pesa ninazozitunza uko ninapozitunza (yaani alinitaka kuchomoa kiasi flani cha pesa nilizonazo na nimletee)kuna kitu azifanyie kwa nia ya kuzifanyia ulinzi kwa sababu anaona kuna mambo yasiyo mema katika pesa ninazozitumia,nikamwambia "sawa" naye akazidi kusisitiza "nipe majibu ili niweze kukusaidia" majibu kwa maana nimueleze eneo nililohifadhi pesa.

Lakini mimi nikajiuliza "huyu kama ni mtaalam wa kuweza kuona vitu ambavyo mtu mwingine hawezi kuviona ameona kama pesa ninazozimiliki kuna shida,anaona kitu kilichoondoa uhai wa ndugu kule gerezani ndio kitu hicho kitakachokuja kunidhulu nami je kama ameweza kuona vyote hivyo iweje ashindwe kuona nilipoweka pesa mpaka nianze kumention ni sehemu flani nimeweka moja mbili tatu sasa kutokana na mimi kuingia katika ulimwengu wa biashara na kutapeliwa mara kadhaa hii ikanipa hofu kwa sababu nimeletwa hapa na mtu na huyu mtu ni mshkaji wangu,katika maisha huwezi kujua huyu mtu anakuwazia jambo gani pengine hata yeye anaumiza kichwa kujua vyanzo vya pesa zangu ni nini,huyu mganga itamuaminije na kumpa siri yangu hii,nikamwambia "mimi ntaleta pesa" akanambia "sio tu kuleta pesa" na akazidi kuning'ng'niza katika kupata jibu lake lakini sikumpa ushirikiano kabisa katika hilo,nilimwambia "pesa nitaleta na hayo majibu nitakujibu ntakapoleta pesa" mganga akanambia "kiburi chako kitakufanya uchelewe na kutatokea maafa makubwa,mimi nakuambia hivyo kwa sababu hizi mali si za kwako,yaani ukae ukijua hizi mali si za kwako na huyo aliyepata mali alikuwa na siri nazo na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana alizifukia mahali,wewe mahali ulipoziweka unaona ni shida kunitajia je unahisi ni nini"

Sikutaka kumpa sana nafasi na nikamwambia "ndio kwanza tumefahamiana na vile tunahitaji muda zaidi wa kuzidi kuzungumza zaidi pengine naweza kuzungumza mambo mengi zaidi" lakini nikazidi kujiuliza kama anaona visivyoonekana kwanini hajaona pesa? Nilifanya taratibu nilizoelezwa kwakuwa nilitakiwa kulipia pale,nikalipa kwani sikuona kama ni hela nyingi kwani makubaliano ilikuwa kulipia huduma ya kutizamia,kulinda pesa na mimi mwenye kunitibia ili kila kitu kirudi katika mstari wake,nikalipa na akanambia kadri siku zitakavyokuwa zinaenda nitajionea jinsi ulinzi wa pesa na mali zangu unavyoimarika,nilimpatia laki tano na uko mbeleni nitalipia kwa kadri ya matibabu husika.

Tumetoka pale na yule mshkaji aliyenipeleka na tukiwa njiani akawa ananiambia "huyu ni mganga sahihi sana,wako waganga lakini huyu ni mganga mahiri" nikamwambia "lakini mimi sijawahi kushiriki katika mambo ya waganga" akanambia "shida yako,tatizo lako fata tu maagizo anayokupa utafanikiwa sana" nakumbuka sana nilitakiwa kurudi kwa mganga kupeleka pesa (mfano wa pesa)ambazo ninazo lakini nikatingwa na mambo mengi kwani mambo yalikuwa yamepandiana sana na nikasema ngoja nikamilishe alafu ndio niende,nakumbuka siku hiyo niko katika vitu vyangu vinavyoniingizia uchumi nikiwa napiga mahesabu ya hapa na pale nakumbuka hatua yangu ya kwanza kabisa nikapokea taarifa ya gari yangu kubwa kabisa ambayo nilinunua kwa gharama kubwa na linaendelea kufanya kazi nikapewa taarifa limepata ajali mbaya sana lakini pia ambacho kiliniuma zaidi na watu ambao walikuwamo mule katika gari ambao ni madereva wangu wote walipoteza maisha,nilisikitika sana,nilipofatilia kuona ajali ya gari yangu kiukweli ilikuwa lite off lakini stori za ajali hiyo kutokea zilikuwa ni nyingi sana lakini wakati nikiendelea na mchakato wa kuhakikisha hawa wapendwa wetu wanapumzishwa katika nyumba yao ya milele taxi moja ikapata ajali,ajali ilitokea lakini dereva alitoka akiwa hai lakini gari lilikuwa nyang'anyang'a na nakumbuka sentensi ambayo dereva alizungumza "aah mimi nimeaga bwana mtu hawezi kunichukua kizembezembe" yaani ikiwa inaaminika haikuwa ajali ya kawaida kwa maelezo yake anasema jinsi alikuwa anaendesha gari kuna vitu aliviona mbele ambavyo havikuwa vya kawaida na anaamini kabisa ulikuwa mkono wa mtu,kama nikaanza kupata ishara flani kuwa kuna vitu haviko sawa.

Kuna matukio ya ghafla yaliibuka hata sijui yalitokea wapi na hii ikanifanya nikimbie sasa moja kwa moja kwenda kwa yule mtaalam na nikawa nimepeleka pesa,nikapeleka na kumueleza changamoto ambazo zimetokea na alisikitika na kuniambia "nilikwambia kuwa hizi pesa unazomiliki aliyekuwa anazimiliki zimemtaabisha zimemtesa na ndio maana hakutaka kuzitumia na ndio maana hakutaka kumtesa ndugu yake yoyote na ndio maana alikutafuta wewe ili hizi pesa zikumalize" nikasema "hapana,hapana mtu amenipa hizi pesa na siku zote nimekuwa nikizitumia kwa amani, kwanini na kwanini? Mtaalam akachukua zana zake pale na kuongea ongea maneno yake na kunipa dawa flani akawa amenipakaa maeneo tofauti tofauti ya mwili wangu na pia akazichukua zile pesa nilizokwenda nazo nakuzifanyia mambo mambo yake mwenyewe ndio anajua zaidi na akanambia "mambo yatasettle,mambo yatasettle" na alinipa utaratibu wa kufanya vitu katika ofisi ambazo nazimiliki na akanirejeshea zile pesa ambazo alishazifanyia mambo yake niende nikazichanganye na zile pesa zingine kwamba ni ulinzi na hata mie kuanzia muda ule niko salama.

Nilitoka pale na nikafanya kama nilivyoelekezwa lakini moyo wangu ukawa unasikitika sana,nakumbuka nikapigiwa simu kutoka katika duka langu la nafaka kuwa kuna moto mkubwa na duka limeteketea lote na watu ambao walikuwa karibu na mimi wakaanza maneno "unaona,unaona,huyu mtoto alikuwa anamiliki mali zisizo za halali angalia matukio jinsi yanavyofululiza pengine amekosea masharti" lakini mimi kwa upande wangu nikawa najiamini hakuna sharti ambalo nililikosea kwa sababu hizi pesa nimemiliki katika mfumo ambao nimeshauelezea,ikabidi nirudi tena kwa mtaalam ili nijue ni nini tena na mbona nimeshaanza kupoteza sehemu yangu ya kupata pesa na watu wamekuwa wakipata pesa kwa ajili ya kutunza familia "imekuwaje tena,ni nini kinaendelea mbona haunipi ufafanuzi" akanambia kuna kazi kubwa anatakiwa kuifanya na inabidi anipeleke makaburini,sasa kwakuwa niko katika hali ya kutatua tatizo na ukiniuliza nini chanzo yaani ni sijui,yaani sijui kwa sababu nilikuwa na hizi pesa siku zote na ni hofu tu ilinipata ndio kwenda kwa mganga,yaani pesa nilizotoa kwa mganga ni pesa nyingi sana na ikawa kila ninapoenda ananitajia mabei makubwa ya vifaa hitajika na kwa mfano hili zoezi la kwenda makaburini aliniambia hili zoezi ni kubwa sana kwa sababu tunahitaji nguvu zaidi za kuhakikisha tunaweka ulinzi kwa hizi pesa kwahiyo alinitaka nitoe milioni tano ili kumaliya tatizo kabisa,nikatoa na kweli tulikwenda makaburini na akanifanyia madawa na kuniambia "sasa wewe umepikwa na umepikika na hakuna ubaya wowote dhidi yako kuanzia sasa hivi".

Lakini haikuwa kama yule mganga alivyosema kwani vitu vyangu vilizidi kupukutika,naviita vitu vyangu kwakuwa nilivitafuta mimi,nilivitafuta kupitia zile pesa na kama ningeamua si ningekaa tu huku nachomoa pesa natumia lakini pesa zile nilifanya uzalishaji ambao ndio umeleta matunda ambayo ndio hivyo vitu na hata pesa zake nikaweza kupeleka hata benki,nakumbuka sana,nakumbuka nyakati naendelea kuliwa pesa na vitu vinazidi kupotea na huku huyo mtaalam akiendelea kunipa vitisho,nakumbuka siku moja yule mama ambaye ni shemeji yangu ambaye tumekuwa tukishea mambo mengi alikuwa ameona mapito ambayo napitia na nilikuwa lesi sana kwahyo sikuwa hata na muda wa kuzungumza mimi niko kwa ajili ya kuzitatua changamoto nilizokuwa nazipitia,alinitafuta na akanambia "shemeji tuongee kidogo,shemeji kuyumba kwenye biashara ni jambo la kawaida,nini hasa kimesonga moyo wako? Mbona umekuwa hauna raha,nakuona ni mtu ambaye hauko smart tena,ni nini tena kiko katika maisha yako? Nikamwambia "sielewi" alizungumza na mimi kwa ukaribu na upole sana "Rojas nilikwambia kuna mambo hauwezi kumwambia mtu lakini Mungu yupo,Mungu wetu ni kila kitu katika maisha yetu" alizungumza na mimi mambo makubwa sana,nikamwambia "unajua leo hii mnaniona niko na pesa lakini hizi pesa leo zimegeuka mateso kwangu" akanambia "kwanini,kwanini mbona mimi hizi pesa naona ni pesa halali kabisa" nikamwambia "hujui tu" akasema "hapana naziona ni pesa halali kabisa na wala sina mashaka na wewe kama watu wanavyosema kuwa umetoa sadaka watu,minong'ono ya watu kuwa eti umekosea masharti na wanatisha watu ambao wanakufanyia kazi wakiwaogopesha kuwa watapata matatizo na kupoteza maisha,mimi siamini katika hilo"
Huyu mama alionesha kuniamini kuliko kawaida kwamba anaamini iko kitu,kwa mara nyingine ya kwanza nikamueleza huyu shemeji yangu,nikamwambia "hizi pesa mimi alinipa" na nikamweleza mazingira yote ya mimi kumiliki hizi pesa na nikamweleza jinsi nilivyomtelekeza huyu mtu na nikamwelekeza hadi mahali nilipozihifadhi hizi pesa kitu ambacho sikumweleza mtu yoyote tofauti na yule marehemu na nikamwambia yule shemeji "nimekushirikisha kwa sababu umekuwa karibu na mimi na umekuwa unazungumza vitu ambavyo vinagusa sana maisha yangu" akanambia huyu mama " Rojas unapoamua kuamua kuwa kuna miungu mingine asiyekuwa Mungu inaweza ikakusaidia tambua unakosea na uko ndiko ulikoenda kuharibikiwa,kama siku zote ulikuwa unafanya biashara zako katika hali ya amani ina maana sasa wewe umeenda kujiconnect na miungu ambayo ni mibaya na ndio labda imeharibu pesa zako" nikamwambia "hapana yule mtu alikuwa anahofia kutoka" nikamweleza hofu niliyokuwa nayo,akasema "hiyo ni hofu yako imekupandikiza wewe kwenda kuamini mambo ya kishirikina" nikamwambia "sasa mimi nafanyaje maana nahisi kuchanganyikiwa" akanambia "cha kwanza stop kabisa kujihusisha na mambo ya kishirikina,siku zote umekuwa ukitumia hizi pesa bila ya shida yoyote,mambo ya kuambiwa pesa haukutakiwa kuzimiliki aliyemiliki ameshaondoka je alikwambia kitu chochote?
Nikamwambia "hajawahi kuniambia kitu kibaya" akanambia "watu upata neema ya kupata pesa katika mazingira ambayo hayaelezeki,kuna mtu anawez akazitafuta pesa na asizitumie neema ikamuangukia mtu mwingine na akazitumia,haimaanishi yule mtu aliyepata ni kwa njia mbaya" huyu shemeji yangu tulizungumza kwa muda mrefu sana na akanambia kuna vitu nimeviweka kwenye biashara uenda hivyo pengine sasa ndio vinakula biashara yangu ili niendelee kutishiwa na niendelee kutoa pesa kwa yule mganga" nikipiga hesabu toka nimeanza kwenda kwa yule mganga pesa ngapi nimetoa kiukweli imefika hata milioni ishirini ambayo nimetumia kwa njia mbalimbali kwa maelekezo yake na vitu ambavyo alinipa nikaviweka katika maduka yangu ambapo naweka lakini nazidi kupata matatizo na huyu shemeji akiniambia "hivyo ambavyo umeweka ndio vinazidi kuharibu biashara yako,vinazidi kukupa hofu na hofu inakufanya wewe uendelee kutoa pesa na utaendelea kutoa pesa huku ukihofia kitu ambacho hakipo.
Hakipo Rojas na umewasaidia watoto yatima wale,umetoa sadaka zako,sadaka zako zimekuwa ni baraka,pesa hiyo ni pesa halali mtu huyo alikupa kwa upendo wa dhatina Mungu alitaka wewe uwe na pesa,unajua Rojas katika maisha tunaishi kuna watu wanapata pesa kwa neema ya Mungu tu,yeye mwenyewe ukimuuliza anasema nilihustle kweli lakini katika nyakati sielewi nilipata pesa,wewe ulibahatika kupata pesa katika mazingira ambayo Mungu aliamua kukupa pesa ila wewe ulipoikamata pesa ukajikuta unachanganyikiwa,unazifanyia anasa,unazifanyia katika mambo yasiyofaa lakini Mungu ni wa rehema,Mungu wetu ni wa upendo anakusamehe kabisa ndio kama hivi na maisha yanaendelea" huyu mama hakuishia tu bali alinambia "twende ofisi baada ya ofisi niambie hivyo vitu ambavyo umevificha uko unaogopa kuvitoa mimi nitavitoa" tukaambatana pamoja na yeye maana nilikuwa nimehifadhi vibuyu ambavyo vimefungwa na vitambaa,vibuyu na vidudedude vingi tu kwahiyo kila ofisi nikawa nimewekakwa siri mfanyakazi asione yaani kuhakikisha vinakuwa salama kwa ajili ya ulinzi na hivi vitu nimeanza kuvifanya baada ya kupata hofu na mimi kutaka majibu sana ya kile ambacho nimekuwa ninapitia,tulivitoa vyote katika maeneo yote,alivikusanya na yeye mwenyewe alivichoma moto na akasema "tunaye Mungu wetu asiyeshindwa na jambo lolote,hakuna pesa ambayo isiyokuma pesa halali,pesa zote ni za Mungu hakuna pesa ya shetani,hizo pesa za shetani ni za kwao lakini sisi hatutayasujudu hayo,hakuna uharibifu wowote utakaotokea tena kwa sababu vyote vyakuleta uharibifu visharudi kwao"

Huyu mwanamke ni shemeji yangu lakini alinitia moyo sana,akuishia hapo kwani alizidi kuongea na mimi,kukaa na mimi kwa upendo na akazidi kunishauri kuhusiana na yule mwanamke ambaye ameshakuwa sehemu ya maisha yangu akasema "lazima umtoe yule mwanamke katika maisha yako" yule mwanamke anafanya mambo ya kikahaba lakini ameshika akili yangu sana na nimejikuta natoa pesa nyingi kwake,akasema "huyu sio mke,huyu sio mke kabisa na Mungu atakusaidia kukuvusha hapo".

Tangu mimi nilipotoa vitu vyote vya kiganga sikuona shida yoyote yaani gari kudondoka wala matatizo yoyote kutokea,nikarudi nikaanza kuona amani inarudi na zaidi kumkumbuka rafiki yangu ambaye alinipa pesa,nikawekeza zaidi kwa hawa watoto mara nyingi zaidi ya ilivyokuwa kawaida na siku zilivyoendelea kusogea na nikazidi kuzipambania zile pesa ziendelee kudumu,ziendelee kudumu utajiri huu ambao ninaumiliki uendelee kudumu japo vipindi vya uchumi vinakuwa tofauti kuna kipindi mambo hayakuwa mazuri lakini sikudondoka kabisa,bado niliamka tena na kuendelea kupambana kila inayoitwa leo,kila inayoitwa leo kuhakikisha maisha yanasonga mbele.

Katika mengi ambayo yamekuwa ni faraja kwangu ni kuona watoto wa mshkaji wamekua na mmoja kati ya watoto wa mshkaji ameolewa na mimi nilisimama kama baba,nilisimama kama mtu muhimu katika tukio husika.
Muda umesogea sasa mimi ni baba wa familia niko na mke pamoja na watoto lakini sina kiwango kile ambacho nilipata cha nyakati zile pesa nyingi sana lakini sasa hivi nina pesa za kuweza kuendesha maisha yangu,kusaidia ndugu zangu,za kuendesha gari nzuri,za kuishi kwenye nyumba nzuri na maisha mengine yanaendelea.



MWISHO!
Waganga wa kienyeji ni matapeli na waongo
Msaada pekee unatoka kwa Mungu,
Rojaz amshukuru Mungu sana kwa sababu ya huyo shemeji yake..ni mwanamke ambaye Mungu amemtumia ipasavyo kwa kweli.
 
Back
Top Bottom