Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Maisha ni fumbo kubwa sana,imagine jamaa alitakiwa aende jela ili akakutane na jamaa wa kumpa utajiri..so far nimejifunza yafuatayo..

1.maisha ni fumbo,kufanikiwa au kufeli ni siri.
2.Uaminifu ni silaha kubwa sana maishani.
3 Mungu akitaka kukupa lazima upitie shida,kiasi unaweza kuhisi kakuacha,kumbe yupo hapo hapo ulipo.
4.Wema ni akiba.
5.Mungu yupo.
Wewe jamaa ni smart kama id yako,ubarikiwe
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 7





Macho yalipoizoea hali ya kile kijumba ndipo nilipoweza kukiona kile kitanda cha kamba na kukisogelea kwani yule ndugu aliniambia hazina ilikuwa imefukiwa chini ya kile kitanda,nikakiweka pembeni na kuanza kutindua pale usawa wa kile kitanda,ardhi haikuwa ngumu kiasi cha kunipa tabu kwani nilitoka nje na kwenda kuchukua kijembe kidogo kwa kunisaidia katika kuchimba,nikachimba kiasi kama cha mita moja nikasikia kitu kama mlio wa bati hivi,nikangea spidi ya kuchimba,nikachimba,nikachimba na nikakutana na kitu kama tranka,matranka yale kama wanayobebea wanafunzi wanaokwenda shule za bweni sasa nikawa nachimba kwa pembeni kuweza kulitoa mule shimoni,nikakumbuka maneno ya yule ndugu kuwa kuna "hazina" na ndipo nilipoamini ukweli wa maneno yake,alichoniambia ni kweli kwa sababu nimeona tranka na lilikuwa tranka kubwa sana.

Nikiwa naendelea kuchimbua ili kulitoa lile tranka kuweza kuipata hiyo hazina niliyoelekezwa na rafiki yangu,nikakumbuka kuwa alinambia kitu cha kweli,nilifanikiwa kulitoa huku jasho likinitoka kwa hofu na moyo ukinidunda ndipo nikagundua kuwa tranka alikuwa moja katika lile shimo,hili tranka lilikuwa na kufuli ambayo ilmeshakuwa na kutu kabisa tena kufuli gumu kabisa,kuna tranka jingine nalo pia ni kubwa na pia lina kufuli kama ya hili la mwanzo,kuna nini ndani? hilo likawa kitendawili kingine na utaratibu wake mwingine wakujua baada ya kuzing'oa hizi kufuli ili kuweza kujua kuna nini ndani na nawezaje kuondoka na mizigo kama hii hapa kijijini na nikatoka salama? Nakumbuka alinambia "tumia akili yako ya ziada,fanya unavyoweza hakikisha unakuja na mzigo hapa alafu njoo tutazungumza" haya ndio maneno aliyoniambia,sijui kuna nini ndani,lazima nijue kwani nitawezaje kubeba mzigo ambao sijui nimebeba nini ndani,vipi nikikamatwa wakati sijajua natoa maelezo yapi kuhusu haya matranka? Wakati naangaika kulitoa tranka la pili mule shimoni ndipo nikaja kugundua kuwepo tena kwa tranka la tatu kwenye lile shimo,kiukweli woga uliniongezeka na nikawa najisemea peke yangu ni nini hiki huyu ndugu alikifukia humu? Nikifikiria mazingira hayo yalivyo na ukubwa wa yale matranka na idadi yake kiukweli hofu ilinivaa sana,nayatoaje haya hadi kuweza kuyafikisha mjini? Inaonekana huu mzigo pengine umewekwa muda mrefu sana,muda ule ule niliona ni vyema kutafuta namna ya kuhakikisha kujua kuna nini ndani yake na kwa sababu nilikuwa nimeshayatoa katika lile shimo na sijapata kujua kuna nini ndani ikanibidi niyarudishe mule shimoni na kujipanga upya kwani nimejua kuna matranka matatu kilichobaki ni kujua kuna nini ndani ndio mtihani unaonikabili,nikayarudisha na kufikiria kama ni suala la usafiri au nini ili nitafute njia ya kutoka na huu mzigo hapa.

Nikatoka pale katika kile kijumba na kurudi katika mazingira yale na ilipofika muda wa jioni nikaamua kwenda pale senta na Kaombwe hakuwa amerejea,niliamua kwenda senta kwakuwa niliamini vitu vingi naweza kuvipata katika mazingira yale,nilipofika pale nikaenda kwenye kijiwe ambacho kuna magari wanafanya kama taxi na nikamkuta kijana mmoja nikaongea nae na kiu yangu ilikuwa aniazime gari lakini sasa nani ananijua? Ataniamini vipi kuweza kunipa gari lakini nikamuomba nikamwambia "kuna mzigo nataka kuuchukua lakini naomba hii gari nataka kuiendesha mimi kana kwamba mimi nina ndugu yangu na rafiki yangu na vitu kama hivyo" akaniuliza "una vitu gani?" Nikamwambia "nina mazao yangu nahitaji kuyafikisha mjini nitakulipa,nitakulipa pesa nzuri iwapo utanikubalia" kwakuwa nilikuwa na vijiakiba vyangu vya pesa na ujue thamani ya pesa inabebwa na mazingira kwani 5,000 kwa matumizi ya mjini ni tofauti na mazingira yale ya kijijini kwani kijijini inakuwa na nguvu sana,kuna kiasi cha pesa nikamtajia na yule ndugu alistua na kuona mbona nimemtajia pesa kubwa hivi lakini kwa mimi nilikuwa naona ni pesa ya kawaida.

Baada ya maongezi na kukubaliana nikatoka nae hadi pale kwa shangazi ambaye alikuwa amesharudi kutoka shambani, nikamtambulisha shangazi kuwa huyu ni ndugu yangu na niliona vyema kwenda kumsalimia na shangazi akaniuliza "ana gari?" Nikamjibu "ndio ana gari na anaitumia kwa mambo yake na atakuwepo around hapa" lakini lengo langu lilikuwa niichukue hii mizigo niipandishe katika hii taxi lakini bado hadi wakati huo sijajua ndani ya yale matranka kuna nini lakini inabidi nichonge mchongo na huyu mtu na nikamwambia "mimi nina mazao yangu,mazao yangu nataka niyasafirishe lakini mfumo nitakaotumia nimeyahifadhi katika matranka" akasema "mazao gani unayahifadhi katika mtranka?" Yaani kama akashtuka hivi na kule kushtuka nami kama akawa amenishtua akili yaani kweli naweza kusema kwenye matranka makubwa kama vile nimebeba nini,nimebeba nini,yaweza kuhatarisha hata usalama kwa sababu hata mimi mwenyewe sijajua umo ndani kuna nini,basi nikamseti na kumuahidi nitamlipa kwa sababu mimi nimebobea kwenye mazao nataka tufanye kazi nachukua kupeleka mjini,naye akasema "yaani mimi wakati wowote niko tayari" kwahiyo siku hii niliyokuja naye na kuona mazingira na kupiga stori na kuyajenga nikamwambia "naomba uje kesho" yaani siku inayofuata aje,aje kesho nafikiri aje tuchukue mzigo na tundoke nao kwa sababu alistuka namna ya njia ya ubebaji wa hayo mazao katika matranka,kiukweli sikutaka kulichangia kwani niliona kabisa linaweza kuniletea matatizo uko mbele ya safari.

Siku iliyofata nikajiwahi kabla yule mwenye gari hajafika nikajipa kazi mimi binafsi ya kuyafungua nijue je kuna nini ndani ya yale matranka,nilitumia akili ya ziada nikapata muda ndipo nilipofanikiwa kufungua tranka moja,nilipofungua lile tranka nilisisimkwa mwili mzima na kuanza kutetemeka,nilipatwa na hali ambayo sikuwahi kuipata toka kuzaliwa kwangu na nikawa najiuliza ni nini hiki,ni nini hiki? Mikono inanicheza,moyo inanienda mbio,miguu inapoteza uimara wake wa asili! Nilikuta pesa,nlikuta pesa,nilikuta pesa! Hili tranka ni kubwa na ninaposema ni kubwa elewa ni kubwa sio yale matranka madogo na lilijaa pesa alafu pesa zimepangwa,pesa zimepangwa umo alafu hilo ni tranka moja kati ya yale matranka matatu na hili tranka ni kubwa sasa nikawa najiuliza "hivi hizi pesa ziko mpaka chini? Mpaka chini kuna pesa?" Nilipatwa na mshangao pesa zimehifadhiwa mashambani huku,unajua watu wanahifadhi pesa benki maana uko ndio kuna usalama zaidi kwanini pesa zihifadhiwe chini ya ardhi,zichimbiwe uko na ziweke kwenye matranka,nilifunika,nilifunika haraka na nikasema kweli hii ni hazina,kweli na imekuwaje mtu huyu aniamini mimi na sio ndugu zake na ndugu zake wana shida kama nilivyokwambia maisha ya huku kijijini,yaani wana shida sana na kwanini aniamini mimi kwa kiwango hiki,sikuweza hata kupumzika,sikuweza hata kutulia nilijisikia roho yangu inaangaika,moyo unapaparika,pesa ni kitu cha ajabu sana na ukiwa haujawahi kukutana na pesa nyingi kama mimi hizi nilizokutana nazo,ukikutana nazo unastuka alafu kama unajua hizi pesa zinakuwa mikononi mwako,unaweza kupata wehu! Pesa sijajua zina nini ndani yake hadi kuweza kumuwehua mtu,yaani nilikuwa najiona naelekea kupata wehu kwa hilo tranka moja tu,nilitumia akili zangu zote na kuchanganua kujua nitafanyaje kuweza kutoka na hizi pesa mahala hapa salama ndipo nilipoamua kuchukua hivi visalfeti vikubwa na hizi pesa jinsi zilivyopangwa pembeni kulikuwa na nailoni imezungushiwa na mpaka chini kwanza lilitandikwa nailoni.

Nilichukua kisalfeti na kuanza kudumbukiza hizi pesa,kiukweli zilikuwa pesa nyingi sana,peke yangu yaani peke yangu nikawa naifanya hiyo kazi ya kudumbukiza hizo pesa na sikutaka kumshirikisha mtu yoyote yule hata kwenye yale matranka mengine,nikaingiza,nikaingiza huku nikijiwazia kuwa pengine watu uwa wanakuja humu kufanya mambo yao (wazinzi) na hawajui kama kuna utajiri umefukiwa chini yake,watu wanakiona tu kama kijumba,kiasi cha pesa nilichoweka katika kile kisalfeti ukiniuliza hata kukadilia kiukweli sijui,yaani hizi pesa niliwaza naenda kuziweka wapi? Naenda kufanyia nini? Maana zilikuwa ni nyingi mno,nikayakumbuka maneno ambayo niliambiwa "nina hazina ya utajiri,utajiri mkubwa,niahidi katika haya uliyoniambia"

Muda si muda alikuja yule bwana wa gari ambaye nilimpanga kuwa nina nafaka na nataka kuzisafirisha nikawa najiuliza tunaubebaje huu mfurushi? Lakini hauwezi kuamini nguvu ya pesa ni nguvu ya ajabu sana kwanza nilipata nguvu ya kuongea yaani nguvu ya mamlaka nikawa naongea kwa kujiamini nikajiona nina nguvu ya kujiamini kusiko kwa kawaida,nikanyanyua lile loba na kulitia kwenye boneti la gari yule kijana akiniuliza "ni nini hiki umebeba?" Unajua kama ni nafaka muonekano wake unajionesha tu na loba langu likawa linaonekana kama limebeba makaratasi,nikamwambia "naomba nifikishe mahali nataka kwenda ndugu yangu na nafaka zangu hii ni biashara ninayofanya na nitakulipa pesa yako nyuzi na nasema ntakulipa dabo!" Kwenye hela kuna mtu anashindwa kufanya kitu? Na kama anaona hakina shida yoyote? Nikatoka bila ya kuaga wenyeji wangu na tukaianza safari na hata njiani nikawa naona kama dereva anapata mashaka na akanambia "mimi nabebaga mizigo ya mazao lakini sijawahi kuona mazao kama hivi,ni nini umebeba?" nikaona huyu ataniletea shida nikamwambia "uwe na amani,tulichokibeba ni kile kile nilichokwambia ni nafaka,sasa wewe unajua nafaka za iana ngapi?akaanza kunitajia nami nikamwambia "kweli unaweza kujua nafaka lakini sio zote unazozijua,tukifika ntakuonesha wala usiwe na wasiwasi,amani tu imetawala hapa,uwe na amani" na kule tulipotoka yale matranka niliyarudishia mule katika lile shimo na kufukia kama awali,safari awali haikuwa na mikwamo na tulienda mwendo mrefu hadi nikawa najijutia kwanini nisingeacha zile pesa katika yale matranka na pesa ndio kila kitu kwani kama kutatokea kikwazo chochote nguvu ya pesa ingechukua mkondo wake mpaka nifike nyumbani,kuna baadhi ya maeneo maaskari walijaribu kuweka vikwazo ingawa havikuwa vya kivile sikutaka kuweka ugumu maana hata kama ni kosa la gari nilipatana nao mimi na kumaliza mchezo hadi nikafanikiwa kufika na mzigo mjini,nilifika mjini na pesa,yaani ninazo pesa😂

Nilipofika nyumbani nikiwa natweta nikawa naisikia sauti mawazoni ikinambia "Rojaz kwa purukushani za kupambana mpaka pesa hii umeishika mkononi mwako je unataka kurudi kwa yule mtu aliyekwambia kama kuna pesa? Nani anajua kama kuna pesa kule? Kwasababu hakuna anayejua" na sauti inanambia mtu huyu yuko gerezani na atafia gerezani sasa kuna haja gani ya kwenda kumwambia eti nimefanikiwa kuja na mzigo,nasikia sauti inanambia na pesa tayari niko nazo hapana sijui nafanyaje kwani toka nimeziona hizi pesa nimekutwa na hali isiyo ya kawaida yaani nimekuwa na ujasiri na kujiona hizi ni za kwangu nimezipambania mwenyewe,nimezipambania mpaka zimefika mjini yaani nahisi kupambana kwangu mpaka kupata hizi pesa kuzitoa kijijini na kuzifikisha mjini yaani ndio kama nimezipambania mimi lakini hizi pesa ni za mtu,hizi pesa mwenyewe yuko gerezani na hajamuamini mtu yoyote ameniamini mimi.

Kuna kitu nilikiona kimeingia moyoni mwangu na nilikaa na hizi pesa kwa siri kubwa sikumwambia mtu yoyote yule na sikufanya chochote niko na hizi pesa,unajua katika maisha ambayo tunaishi kila siku,maisha ya kupambana kwa ajili ya msosi ni maisha ambayo watanzania wengi tunaishi kwa mfano kama mimi ninafanya deiwaka kuna siku unakosa gari yaani,unakosa gari unakuwa uko idol idol,ukikosa ina maana mambo hayaendi ina maana unatumia kile ambacho ulikihifadhi kwa ajili ya kula na mahitaji ya hapa na pale sasa hivi nimepata pesa nyingi kwa ghafla na yaani kuna watu wananidaidai hela zile nilikopa kutatua changamoto ndogo ndogo nimepanga siku nawalipa wote😂,nilitulia kwanza na ukiniuliza kwanini nilitulia makubaliano na yule ndugu kule jela ilikuwa mimi nikifika na mzigo na hizo hazina niende kule gerezani niende nikamwambie mshkaji nimeenda nini kinachofata,kwanini mimi nasitasita kwenda na ahadi nilishamuahidi na hata kwa watoto siendi tena nimekaa tu na hizi pesa na mipango mingi inanijia kichwani mwangu,nina mipango mingi najisemea hizi pesa zinanitoa kwenye umaskini mazima,hizi pesa zinaenda kunitajirisha mimi,mimi niliyekuwa naitwa Rojaz mtu wa kuomba deiwaka naenda kuwa na magari yangu,kichwa changu hivi sasa kimekuwa na mambo mengi nayafikiria ninunue magari yangu,nitafute vijana wawe wanaendesha taxi za kwangu,niziite kwa majina yangu,nina mawazo nina mawazo kwa sababu hizi pesa zimekuja kwa ghafla unajua kuna zile pesa zinakuwa unazikusanya unazikusanya unajipangia nikifikisha kiasi flani nitafanya moja mbili tatu kwahiyo unakuwa na malengo yako tayari unayo hivyo zikija tu ni moja kwa moja ni kutupia katika vile vitu ambavyo umevipanga sasa mimi hizi zimekuja kama upepo yaani paap! Hizi hapa,mzigo huu hapa,mzigo umenona huu hapa nahisi kuchanganyikiwa nifanye nini,nikapata muda nikaanza kuzihesabu kwa sababu hizi pesa hauwezi kwenda nazo nyumbani kwa sababu ya mazingira ya pale nyumbani,nlitafuta sehemu,sehemu yaani nitulie hapo,nilihesabu,nilihesabu,nilihesabu hadi nikahisi kuchanganyikiwa,ushawahi kuhesabu pesa hadi ukahisi kuchanganyikiwa? Kwa mfano mtu haujazoea kushika pesa ukapata milioni kumi hapa usilale usingizi,haupati usingizi, mimi leo nina pesa na pesa unahesabu hadi unahisi kuchanganyikiwa,hizi pesa zinahitaji mashine kabisa yaani iwepo hapa kwa ajili ya kufanya kazi ya kuhesabia maana ni kwenye masalfeti pesa zimejazwa umo,sijui kama unaona hiyo hali,uelewi unafanya nini kwahiyo nikakaa nimetulia,nikapitisha wiki mbili nimekaa na hizi pesa na ajabu ya hela niliposhika hela na sijaanza kutumia matumizi lakini kila mtu anayeniona ananambia "Rojaz mbona unatakata,mbona hivyo unashine mwenzetu,tunaona mambo mazuri" ulishawahi kusikia wanasema pesa tunda la roho?

Pesa tunda la roho unatakata bila ya kutumia mafuta,moyo wako unatawaliwa na amani tu yaani wewe una raha tu "Rojaz mwenzetu mbona wiki hii tunaona si haba?" Nina hela nyumbani,nina hela lakini huwezi kumwambia mtu hata kuna kauli zangu zimebadilika kuna namna ya kuongea mimi nimebadilika ukiniuliza imekuwaje automatic nimejikuta nazungumza kimabadiliko,pesa ni kitu cha ajabu sana.



ITAENDELEA!
 
Bro Kama wewe ndo ulikua ukiihadithia hii simulizi radio free na mzee mzima sky Walker hongera Sana, na wewe kwangu umekua kiigizo chema kabisa katika kuwatendea wema watu wasio na hatia, naikumbuka ile beat iliokua inaplay background wakati wa simulizi, nlikua najitahidi Sana Kila jumapili niwe pembeni ya redio. Ni miongoni mwa vipindi Bora kabisa vya redio kuwahi kutokea hapa Tanzania, nasubiri simulizi ya kuitafuta kwa madiba na Mambo ya "makina"
Nikapiga tanchi kunako makina

Nikachange mind ya panya na kuweka mind ya njiwa😃😃

Mozambique kuna madereva wanaendesha magari aisee, mpira ulienda mpira uliendaa😀😀

Aisee kipindi niko advance ndio story inaunguruma, RFA mtambo mkubwa, vijana tumejikusanya vitandani kuisikiliza.
 
Nikapiga tanchi kunako makina

Nikachange mind ya panya na kuweka mind ya njiwa😃😃

Mozambique kuna madereva wanaendesha magari aisee, mpira ulienda mpira uliendaa😀😀

Aisee kipindi niko advance ndio story inaunguruma, RFA mtambo mkubwa, vijana tumejikusanya vitandani kuisikiliza.
Barikiwa ndugu!
 
Back
Top Bottom