Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Story nzuri nazani unataka kuifanya iwe ndefu sana maana kama kuchukua tu hela mpaka kufika mjini paragraph moja tu inatosha.

ila unaelezea kiti hicho hicho mpka inafikia hatua "itaendelea"!!!!!
 
Mimi ni wa tofauti sana ndugu yangu,jipe nafasi hata ya kuandika japo episode moja tu kati ya hizo episode 20 za mkasa husika,acha wivu alafu si vyema kuiga upumbavu au ukikaa kimya unajihisi hautaonekana? Jiheshimu damu yangu! Imeisha hiyo!
Ww hauna akili yaani mimi nikuone wivu kwa kitu gn hasa!! Una kitu gn hapa JF chakuonewa wivu[emoji706][emoji706]

Alafu me sijakutusi nimetoa maoni tu, ulikua na uwezo wa kupuuza pia.
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 8





Ahadi ambayo nilimuahidi huyu kaka ambaye nilikutana nae gerezani nakunifanyia yote haya sijaitimiza bado yaani kama kungekuwa na mtu angekuwa anaijua hii stori angeniuliza kwanini hadi muda huu sijaenda gerezani kwa mtu aliyenipa mwongozo kuhusu hizi pesa,yaani kwanini naanza kufanya kinyume na makubaliano tuliyoyafanya,kiukweli nilikuwa sina jibu,mipango ikaanza kuwa mingi sana yaani kila ninachofikiria kufanya naona sahihi,kila nikiwaza naona hiki ni bora zaidi ya kile kwa sababu sijawahi kuwaza katika maisha yangu kama naweza kukutana na pesa nyingi kiasi hiki,pengine ningewahi kuwaza ningelishakuwa na mipango thabiti lakini kwa sababu nilikuwa na fight for food yaani maisha ya kupambana kwa ajili ya tumbo tu yaani siku nenda siku rudi na sasa nimepata pesa,nikajiwazia hivi kula ni nini yaani kwa pesa niliyokuwa nazo hizi ni za kwenda kufanya vitu vikubwa sana na wala si za kuwaza tena kuhusu kula,nikajikuta nawauliza watu "hivi kwa mfano ukipata pesa nyingi unaweza kufanya kitu gani?" Kila mmoja ana mawazo yake wengine wanasema "nitajenga nyumba nyingi sana na nitapangisha huku mwenyewe nikiwa nimekaa tu nakula kodi" yaani mawazo ni mengi nawezaje kufanya kiukweli akili ilikuwa inawaka moto.

Katika harakati hizi nakumbuka sana siku moja,naikumbuka sana hiyo siku,nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa nne usiku nilikuwa nimechoka sana nikasema ngoja nijiegeshe nipumzike tu,sikuwa nimejipumzisha kitandani bali ilikuwa kwenye kochi,wakati nimejipumzisha nikaota ndoto na uwaga sinaga kumbukumbu mimi ya mambo ya ndoto kwani kile ntakachokiota kinapotelea juu kwa juu lakini ndoto hii kwanini naizungumza pengine naiona kwangu haikuwa ya kawaida kwani nimeota ndoto niko kwenye kijiji kile nilichokuwa nimeenda kwenda kuchukua hizi pesa na nimejiona nipo ndani ya kile kijumba ambacho mshkaji amenielekeza na taratibu zote mpaka kufanikiwa kupata hizi pesa,nikiwa katika hiki kijumba nikawa najiona nimelala katika kile kitanda cha kamba,kitanda ambacho ndicho nilielekezwa kufata zile pesa,yaani nimelala hapo alafu nikawa najiuliza kwanini nimelala hapa ilihali mimi ni mtu mwenye pesa nyingi na nikiwa katika hiki chumba hakikuwa na mwangaza wakutosha yaani kama mshumaa umewashwa yaani mwangaza wake ni hafifu,nilisikia sauti ya mwanamke akinambia maneno haya "geuka huku unione" nami katika ndoto nikageuka,yaani sasa huu mwangaza ambao niliuelezea kuwa ni hafifu na sikujua unatokana na nini na fikara zangu zikawa zinahisi labda ni mshumaa kwa sababu ilikuwa ni ngumu kitu kukiona vyema na nilimuona mwanamke mmoja mnene sana,mnene mno katika kona ya hiki chumba,sauti ya huyo mwanamke naikumbuka siku zote katika maisha yangu kwa sababu alinambia "maisha yako wewe ni ya hapa,hizo pesa unazoziwaza uko nazo ziko wapi? Hizo pesa si za kwako,unajua yeye kazitoa wapi? Kwanini unaingiwa tamaa? Mbona ni mapema sana unaingiwa tamaa? Ni rahisi sana mtu kupata pesa? Mbona wewe katika maisha yako haujawahi kupata pesa kama ni rahisi,unajua huyu alifanya nini mpaka kupata hizi pesa?" Kiukweli katika ile ndoto huyu mwanamke mnene alinifokea sana na alinambia "usile jasho la mtu bila ya ruksa yake,rudisha jasho la mwenzako maana haujui vyanzo vya pesa hizi,fanya haraka rudisha pesa za mwenzako" nimekuja kustuka kwende ndoto niko kawaida nimelala pale kwenye kikochi kiukweli niliogopa sana yaani huyu mwanamke mnene ambaye sura yake sikuiona vyema ambaye kiumbile ni mwanamke sikuwahi kumuona wala kumsikia kabla,yaani ni vitu vipya kabisa kwangu,nikawa najiuliza "ndoto gani hizi au kwa sababu nawaza sana kuhusu pesa?" Yaani kama alarm ikalia kwenye kichwa changu,nikawaza lakini ni kweli mtu azifukie pesa kule mashambani na bila kumpa mtu yoyote ambaye ni ndugu yake,watoto wake wanateseka kule,amesema ana mwanamke wa maisha wake je ameshindwa kumueleza hata huyo mwanamke anayempenda sana pengine hasiteseke kwa maisha anayoishi uko uraiani aje anipe mimi? Au ni pesa za mambo ya nguvu za giza? Hofu iliingia ndani yangu,nilipatawa na hofu sana kwa sababu ni kweli kupata pesa si kitu rahisi mbona mie napambana sana,mbona mie napambana katika kazi nyingi ninazofanya na sijawahi kupata za kusema angalau nipate pesa nijenge,ninunue gari na nipate hivyo vitu angalau moyo wangu unatamani,mbona sijawahi kupata? Yeye hizi pesa alipata wapi? Kiukweli mpaka kumepambazuka sikupata usingizi kabisa yaani nikajiwa na hofu sana kwa sababu kama nilitishwa katika hii ndoto sikujua imekuja katika mazingira ya wema,sijui kwanini ndoto inijie lakini imekuja kunipa hofu.

Nilikaa kama siku mbili nikaamua kwenda kule gerezani,mimi mwenyewe nikaenda kule gerezani na nilipofika nikapata nafasi ya kuzungumza na yule mshkaji wangu na kiukweli aliponiona alifurahi sana,alifurahi sana akanambia "nilijua tu Rojas utakuja lakini mbona umekuja kwa kuchelewa?" Nikamwambia "unaona nimechelewa? Mbona sijachelewa" akasema "hapana nilitegemea ungekuja mapema zaidi kuliko leo ambavyo umekuja" nikatabasamu nikamwambia "nimekuja huu ni wakati sahihi" akanambia "mbona nakuona huna furaha,kwanini hauna furaha kwani haujafanikiwa katika jambo letu? Nikamwambia "nimefanikiwa" akanambia "najua una shauku ya kutaka kujua nini kipo ndani ya ile mizigo,unadhani ulitegemea kukuta dhahabu kama dhahabu zikiwa wazi lakini umekuta vitu vimefungwa na kufuli" nikamwambia "kwani nilitakiwa nisijue kilichomo ndani mpaka ntakapokuja na mzigo mpaka huku? Akanambia "ndio" nikamwambia "ningewezaje kutembea na kitu ambacho sijui kuna nini ndani?" Akanambia "Rojas lakini nilikwambia utakapokuja na huo mzigo utakuja kwangu na mimi ndio ntakupa maelekezo" nikamwambia "ni kitu ambacho hakiwezekani wewe unajua,tazama mambo yalivyo barabarani kukaguliwa na isitoshe mimi nimeenda kule nikiwa siko vizuri kiuchumi kwahiyo sikuweza kuhatarisha maisha yangu ilibidi nijue nini nabeba isije nikabebeshwa maiti za watu au nikabebeshwa viungo vya watu bila kujua nikajikuta nimeingia tena katika matatizo pasipo kujua na si nitaonekana mimi ni kijana mpumbavu" akanambia "mbona Rojas unaongea maneno hayo" nikamwambia " hapana nimekuja,nimekuja kukusikiliza" akasema "sawa,nashukuru sana,nashukuru sana umekuja nilikuwa nasikia sauti ndani yangu ikinambia hautakuja Rojas,hautakuja,ulivyoziona pesa ulijisikiaje? Haukujisikia kuchanganyikiwa?" Nikacheka,.nikamwambia "kwanini" akanambia "ndivyo inavyokuwa kama haujawahi kama mtu haujawahi kukutana na pesa labda katika maisha yako umeshawahi kuona shilingi ngapi,umeshashika shilingi ngapi? Labda milioni tano,milioni kumi,milioni ishirini au thelasini au hata milioni hamsini,sabini au mia lakini pindi unapokutana na pesa nyingi sana unaweza jikuta unachanganyikiwa,haujawahi kuchanganyikiwa?" Nikamwambia "kwanini unambie hivyo,pesa ambazo sijazitafuta nawezaje kuchanganyikiwa nazo zaidi tu yakupewa mwongozo" akasena "vizuri,Rojas umefanya vizuri sana kuja,si nilikuambia? Umeniamini katika kila nililolisema? Basi na wewe timiza ahadi uliyonipa" nikamwambia "kwani nilikosea kufungua yale matranka na kuzitoa zile pesa na kuzihifadhi katika mazingira mazuri?" Akasema "nilitamani uyabebe matranka yote lakini nimekuelewa mambo yamebadilika na ningekuwa mimi ningefanikiwa kuyabeba matranka lakini mambo uko uraiani sijui yakoje wewe ndio unajua siwezi kukupinga unachosema,kuna kiasi cha pesa chochote ulichotumia?

Nikamwambia "ndio,si nilikwambia nimeenda katika mazingira gani nikawa nahitaji pesa kwa ajili ya kuhonga ili nipite,nilitoa zile pesa na kuweka katika visalfeti" akasema "pesa zote zile? Ulizipangaje? Nikamwambia "nilitumia akili ya ziada kama ulivyonielekeza" akanambia "jicho langu lilipokuona mara ya kwanza lilikuwa na imani na wewe,nashukuru sana" nikamuuliza "hizi pesa umezipata wapi,pesa nyingi kiasi hiki na kwanini pesa hizi haukuzihifadhi benki sehemu ambako ni salama,kwanini umezihifadhi pesa kwenye kijumba tena cha zamani" akanambia "nilijenga kile kijumba kwa kusudi sana,kwani ni mimi peke yangu ndio nimefanya hivyo? Ngoja nikusimulie jambo moja,hizi fedha ni fedha halali kabisa,hizi fedha wala si fedha bandia,hizi ni fedha ambazo nimezipata mimi kwa jasho langu,kwa nguvu zangu,kwa kutumia akili zangu na uwezo wangu wote,niliona sehemu sahihi yakuzihifadhi ni pale" nikamwambia "bado haujanipa majibu lakini kwakile nataka kujua,mbona benki zipo ambapo watu wanahifadhi pesa nyingi sana" akasema "unajua mimi nilikuwa nafanya kazi gani? Nikamwambia "sijui" akasema "mimi nilikuwa ni raia tu nilikuwa nafanya shughuli zangu mbalimbali japo nilikuwa na kipaji cha tofauti kidogo ambacho nilikuwa naweza kuwasaidia watu wengine ambao hawana kipaji nilichokuwa nacho mimi" nikamwambia "kipaji gani hicho" akajibu "ni kipaji ambacho naweza kuzungumza hata na watu wenye elimu kubwa sana,watu wenye uwezo mkubwa wanaweza wakanifata na hata wakazungumza na mimi na wakaniuliza nina shauri kipi katika haya,ndipo nilipo pata pesa hizi kwa jasho langu na kwa nguvu zangu,nikazihifadhi pale na wala usiniulize maswali mengi kwa sababu pesa umeshazipata na ni muda wa kutumia pesa,Rojas kuanzia sasa maisha yako yanaenda kubadilika" nikamwambia "naomba niambie chanzo cha wewe kupata pesa ili niwe na amani na hizi pesa" akanambia "pesa hizi zina amani tu kama utafata na kusikiliza yale nitakayosema lakini kama utaenda kinyume na yale unayoyazungumza hizi pesa haziwezi kuwa pesa nzuri sana kwako" nikamwambia "mbona unanitishia? Mbona sentensi hiyo haukuniambia toka mwanzo" akanijibu "nilikwambia,nilikwambia na ndio maana nikakwambia uape au nani aliapa? Wewe si ndio uliyeapa Rojas? Mbona naona sasa hivi sentensi zako na sauti yako vimekuwa kama vimebadilika,kwani Rojas pesa zimekuchanganya? Mbona mimi nakuona una utulivu sana na katika watu niliowaamini ni wewe,kuna kitu kimebadilika kwako? Kuna vitu ambavyo tulizungumza mwanzo unaona hauwezi kuendelea kuvishikilia? Rojas hizi pesa ni zetu sote na mimi nilizitafuta lakini siwezi kuzitumia kwa sababu niko gerezani lakini wewe waweza kuzitumia hizi pesa lakini kwa makubaliano ambayo tumekubaliana" nikamwambia "sawa,nimekuwa na hofu sana kuhusu hizi pesa" akanambia "kwanini" nikamwambia "sijawa na amani nazo" akaniuliza "kwanini hauna amani nazo? Kwanini ukose amani nazo au uliziwazia mabaya? Kama uliziwazia mabaya lakini kama uliziwazia mema hakuna jambo lolote baya Rojas" kiukweli sentensi zake zikaanza kama kunipa ukakasi hivi kwa sababu ni kweli nilianza kuwaza mabaya na mimi nimekuja huku kwa sababu ya ile ndoto tu niliyoota ndio kimenisukuma ndio nimekuja hapa,kwanini aniambie sentensi hizi niliziwazia mabaya na nini hivyo yaani,nikamwambia "nilishafanya ulichonielekeza sasa nipe maelekezo mengine kwa sababu hizi ni pesa nyingi ni hatari zaidi kukaa nazo pengine nitastahili kuzipeleka benki au unanielekeza vipi" akanambia "hata senti moja haitakiwi kwenda benki" nikamwambia "kwanini,kwanini zisiende benki na nawezaje kukaa na pesa nyingi ndani kiasi hicho,vipi kuhusiana na usalama wangu? Nawezaje kukaa na hizo pesa zote? Kama pesa ni halali hakuna shida yoyote kwanini tusipeleke benki? Akanambia "Rojas kumbe hujui? Si utaulizwa maswali mengi ukizingatia wewe ni dereva taxi tena ambaye hata usafiri hauna ni deiwaka unapata wapi pesa kama hizo,unaweza kuthibitisha kuwa pesa umepata wapi? Kama una mahali unaweza kuorodhesha maelekezo yakujitosheleza kuhusiana na hizo pesa basi unaweza ukazipeleka kwa sababu watu wanaweka pesa benki sama sawa na kile wanachokipata kwenye movement za maisha yao ya kila siku,ebu niambie mzunguko wa pesa yako,pesa nyingi kama zile umezipaja wapi,utasema umezipata mashambani,kwenye shamba la nani? Utasema ulioteshwa,ulioteshwa vipi? Unataka pesa zote nilizozipambania kwa maisha yangu yote zishikiliwe kwa ajili ya uchunguzi?"

Nayakumbuka haya maneno aliyonambia huyu kaka,tunazungumzia pesa nyingi ambazo mpaka sasa hivi nimezikusanya idadi yake ya pesa nimezihesabu mpaka nachanganyikiwa,nikatulia na kusubiria maelekezo yaidi kujua nini sasa nafanya na hizi pesa,akanambia "nini unawaza kichwani mwako,kuna kitu ambacho umekuwa ukitamani kufanya pale utakapopata pesa nyingi?" Nikamwambia "hapana,sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ntakuja kupata pesa kiwango kama hiki" akanambia "pale ulipofanikiwa kuzileta hizi pesa na kuwa nazo ndani nini ulifikiria kichwani kwako,nini,kufanya kitu gani?" Nikamwambia "vitu vingi sana nimefikiria ila kwa sababu pesa sio yangu nikarudi kwa mwenye pesa anipe maelekezo kwa sababu najua ulihifadhi hizi pesa kwa siku zote ina maana ulikusudia kufanya kitu labda nisikie ulikusudia kufanya kitu gani" akanambia "nyakati hizo wakati nimepata hizi pesa sikuwa na uwezo wakuzitumia kwa nyakati hizo japo kuna vitu niliviwaza ingawa najua kwa sasa hivi mambo uko nje yatakuwa yamebadilika,wewe unaendesha taxi vipi? Unauonaje ulimwengu wa taxi kwa ujumla je niku chenye faida? Unajua kwa pesa zile tunaweza kununua taxi ngapi? Nikamwambia "na ndio maana nikazungumzia habari yakupeleka pesa benki kwa sababu mojawapo ni tujue zile pesa ni shilingi ngapi" akasema "hauwezi kujua idadi ya zile pesa,wewe ni kuzitumia tu" nikamwambia "kwanini unasema hivyo,mbona unanipa wakati mgumu sana na ni pesa gani ambazo hazihesabiki wakati watu wanahesabu hadi mabilioni na mabilioni na mabilioni lakini inajulikana ni kiasi gani cha pesa kwanini zile ziwe shida kuzihesabu?" Nilimuuliza hivyo na mengineyo kadhaa ila kwa sababu muda ni mdogo haujitoshelezi kuzungumza hayo yote na alinambia "muda ni mdogo lakini nikupe muda ukajifikirie,rudi baada ya muda mfupi usikawie sana,utakachokiwaza njoo unishirikishe nakutegemea sana kwa sababu wewe ndio unajua hali ya uko nje,angalia ulimwengu wa udereva wa taxi kwa ujumla uone unaweza kuagiza magari mangapi" nikamwambia "siwezi kuagiza magari ngapi wakati sijui idadi ya kiwango cha pesa,ni dhambi kujua kiasi cha pesa nilichokuwa nacho mule ndani? Akasema "Rojas hauwezi kujua kiasi cha pesa kilichomo mule ni nyingi sana" nikamwambia "naomba hata nipambane nitafute hata mashine nihesabu zile pesa" akasema "uliahidi kunisikiliza kwa kila ntakachokisema mbona tena kama unataka kuzungumza vya kwako wakati pesa ni ya kwangu? Nikamwambia "pesa ni ya kwako lakini usinitumikishe" akanambia "kwanini unanambia hivyo" nikamjibu "hapana kwa sababu unavyozungumza vitu mimi sivielewi" akanambia "nenda nyumbani kidogo pumzika,tafuta nyumba nzuri Rojas,tafuta nyumba nzuri ya wewe kuishi,tafuta kitu uanze kukifanya mapema ili watu watakapoanza kuona macdiliko yako wasihisi vitu vibaya" nikamwambia "una maana gani? Akanijibu "tafuta hata biashara ndogo" nikamuuliza " kwa mfano kama nini" akanambia "fungua duka la nafaka" nikamwambia "sina hobie na hivyo vitu" akanisisitiza "fungua duka la nafaka muweke hata ndugu yako hapo na naamini mtaji unaweza kufika milioni ishirini,mtaji wa milioni ishirini kwenye nafaka unaweza kuuza nafaka za jumla,wewe unauza vitu vya jumla" nikamwambia "kumbe una mawazo" akanambia "nina mawazo,milioni ishirini inaweza kukuwezesha kwanza,tafuta nyumba nzuri,usijenge panga nyumba nzuri haraka sana,usipange kwenye nyumba ndogo kwani zile pesa zinahitajiwa kuchimbiwa chini unakuwa unaweka mazingira mazuri kabisa kwani wewe ndio utakuwa unaenda kuzichukua,ndio usalama na ni lazima uzihifadhi katika matranka"
Baada ya maagizo haya ya mwisho nikayabeba na kuondoka zangu kurejea nyumbani ingawa mara baada ya kutoka katika mazungumzo na huyu mtu hofu ikawa juu zaidi kutokana na majibu aliyokuwa akinipa,hofu ikanijia katika hali ya kibinadamu kwani kweli pesa anazo lakini kwanini hazihesabiki na wakati idadi ya pesa zinaweza kuhesabika yalinipa hofu!
Yajayo yanafurahisha!


ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom