Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Huu mkasa umenikumbusha movie ya prison break, nimemkumbuka mfungwa mmoja John Abruuz(Mbabe gerezan na alikua na crew zake ndani gerezani za kibabe na nje ya gereza alikua na crew za kibabe ,,(business man)) na upande wa pili ni mfungwa wa muda mrefu dp cooper(Tajiri,humble down to earth,lakin pia mafia wa kichinichini, ukiingia kwenye anga zake kindez[emoji38]) ambaye alikuwa na hela ndefu sana, alizozichimbia mji fulan uraiani , kabla ya kuingia gerezani ,hivyo crew ya kina scolfied lilimuunga John Abruuz kwny mpango(msafara) wao wa kutoroka coz ndo aliepewa mchongo na db cooper,yaan aliujua mji zilipo hela na zilipochimbiwa,na alikua na raman,pia alikua na access ya kuagiza watu wake nje walete helikopta nje karibu na gereza usiku ,ili waitumie ku escape from the prison, ili iwe easy kuwachenga polisi japo walichemka, helikopta iliwaacha baada ya wao kuchelewa kufika eneo la tukio kwa sababu ya obstacles walizokua wakizipata wakati wa kutoroka zikala muda wao waliohadiana na watu wa helikopta,coz ile wanakimbilia helikopta na polisi hao nyuma yao,watu wa helikopta wakawa washasepa,wacha wakimbizwe na mijibwa ya polisi pori kwa pori,ndimi njee,daah, polisi nao nyuma yao full armed,, hivyo walivyotoroka gerezani scolfied na wenzie , moja kwa moja walikuwa wanazifata zile pesa,siunajua tena mtu akitoroka jela hana mishe wala nini, uhuru zero,kuishi kwa mashaka,pesa ndio kila kitu na ukizingatia kaka scolfied alikuwa na msala mkubwa,unaohitaji pesa kujificha na kuufanyia research kesi yake na kupata solutions,lakini bahat mbaya mfungwa mwenzao(walotoroka nae) mtukutu TBAG(alikua selfish Sana huyu jamaa) ,akaisoma Raman chap walipokua karibu na mji wenye ambao ndio tajiri dp cooper kafukia pesa zake ndani ya nyumba flan,baada ya kuisoma Raman chap kaimeza ili wenzie wasijue ni wap,akakimbia kwenda kufukua mwnyww ,alizifaid hela kidogo mtaan,kabla hajadabwa,ila kuna mahali alijikata mkono wake mwenyewe wenye pingu ,na kukimbia bila mkono kisa kuwakimbia polisi, very interesting story ,sema movie nimeona Zaman kidogo ,najaribu kuvuta kumbukumbu za kurelate na hii story. .wadau mnaoikumbuka hii movie mtanikosoa ni kitambo sana , naweza kuwa nimechanganya hapo kwenye mchongo wa hela ya dp cooper km alipewa scolfied basi John Abruuz alikua kwa ajili ya kufanikisha helikopta kufika eneo husika siku ya tukio. .anyways kumbe hayo mambo yanatokea kweli kwny jamii na si kwny movies tu.
 
Umejitahidi kuielezea ndugu hongera na yule dp cooper ni mtu aliyevalishwa uhusika wa mhalifu flani wa kweli ambaye hadi leo serikali ya Marekani haiwajahi kumpata baada ya kuiba mamilioni ya dola na kusepa nayo so ktk prison break alivaa uhusika wa mtu aliyekamatwa kwa uhalifu wa pesa nyingi ambazo hazikupatikana
 
Jamaa muongo ww
 
Kwenye pb hakuna character anayeitwa db cooper..ila kuna story inamuhusu db
 
Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​

Sehemu ya 9

Siku mpya ikafika na mawazo yakiendelea kunitawala kichwani mwangu kwani mzigo wa pesa ulikuwa mkubwa sana pamoja na mawazo aliyonipa ndugu yangu kule jela yakufungua duka la nafaka lakini bado mawazo hayakuondoka kwani nikifikiria wingi wa pesa zile,maneno yale aliyonambia kule kiukweli mtanziko ulikuwa mkubwa tena sikuwa nimesema mwanzoni katika zile pesa kulikuwamo na pesa za kigeni aina ya dola,kiukweli mawazo juu ya chanzo cha pesa hizi hayakwisha kichwani,kiukweli napenda pesa ila nilitaka kujua kama kumefanyika dili hadi kupatikana kwake je ni dili la kiwango gani? Na mtu wa kunambia chanzo chake ni huyu ndugu naye kashanambia nisiulize chanzo nijue tu ni pesa halali,nikaanza kufanyia kazi yale mawazo yakufungua duka la nafaka kwani nikakubali kuwa sitaweza kujua ni kiasi gani cha pesa nilicho nacho na nikaachana na mawazo hayo na nikachukua milioni ishirini zakufanyia zoezi kama tulivyopanga na liwe duka la nafaka la jumla,nilitafuta nyumba nzuri ya kupanga, watu wanajua maisha yetu unajua na hata familia yangu wanajua mwenendo wangu,wanajua wapi napata pesa na kaka alipojua nimekwenda kupanga nyumba ya thamani kama ile aliniuliza "mdogo wangu unawezaje kuishi kwenye nyumba kama ile,naona sasa hivi unatukwepakwepa mishe zako sizielewi,unaweza kunishirikisha lolote?"

Nampenda sana kaka yangu tena ni kaka mwema kabisa hilo ndilo ninalolijua ni kaka mzuri sana lakini nawezaje kumshirikisha hili jambo japo kiukweli ndani yangu natamani kushea na mtu kuhusiana na hili jambo uenda akanishauri kitu kikanifaa kwa leo au kwa siku za baadae maana sasa hivi mawazo yote najiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe lililo sahihi na lisilo sahihi yote nayawaza mimi mwenyewe kwani zaidi ya yule mtu hakuna mwingine anayeijua hii siri wakusema naweza nikashea nae na amenambia hata siku moja nisitoe siri hii kwa mtu yoyote,nilimwambia kaka "ni mtu tu ndio amepanga sio mimi ila amenambia mimi naweza nikakaa lakini yeye atakuja kukaa siku sio nyingi" akanambia "ni mfanyabiashara gani huyo,yuko hapa hapa nchini? Nikamwambia "ana mishe mishe zake tu anafanya" zaidi kaka alinisisitiza kuwa mwangalifu sana "kuwa makini sana na watu" nikamwambia "ni kweli kaka ila ni mtu mwema" akasema "kuwa mwangalifu unajua kwa shughuli unayofanya unakutana na watu wengi wengine sio wazuri si unaona kwa mfano ishu iliyokukuta kipindi kile ikatuletea taharuki kubwa,usije kuingia kwenye matatizo napenda kushirikisha ndugu katika mambo ambayo unakutana nayo hata katika watu ambao unakutana nao" lakini sikuweza kumwambia chochote kaka zaidi ya haya niliyomwambia.

Kwa wingi wa pesa nilionao yaani nikisema nianze kufanya matanuzi lazima nitaleta taharuki hasa kwa familia yangu na hata jamii inayonizunguka zaidi zaidi nikajikuta ni mtu wa kujiongelesha,nakumbuka niliwaambia familia yangu nina mpango wa kukopa,kuna mtu amenipa connection ya kukopa,wakanambia "unakopa kwa kipi ambacho utakirejesha yaani kwa hazina ipi itatumika kama dhamana ya mkopo maana unapoenda kukopa kuna taratibu zao kwamba una nini" nikasema "kuna mtu uko yupo anafanya kazi anasema kuna namna" "kuna namna ipi?p" ndugu wanahoji kwakuwa wote wanajua kama mimi nafanya deiwaka tu kwahiyo nakosa vitu vya kutetea hoja yangu lakini sikuacha kujisemesha nikaendelea kujisemesha ili mambo yatakapoanza kutokea yasije kuwashangaza wakumbuke matetezi yangu ambayo niliyasema awali kwamba kuna mtu yuko benki anataka kunikopesha,anataka kunifanyia mpango na vitu kama hivyo.

Katika ile nyumba niliyopanga nilifanya mchakato kama nilivyoelekezwa,katika chumba ambacho mimi ndio ninalala nilitindua mwenyewe kwa sababu ilikuwa hauwezi kusema niite mtu aje afanye hilo zoezi lazima atagundua kwamba kwanini huyu anachimba hapa chini anataka kuhifadhi nini na watu ni wepesi katika kushea vitu na watu kwahiyo ataenda kusema mbona yule alichimba hivi kwahiyo wakataka kujua kuna nini,hili zoezi nililifanya mwenyewe na halikuwa gumu kivile na ukizingatia makuzi yangu mimi ni kijana mpambanaji toka kitaa chochote ukinipa nafanya,niite kwenye ujenzi mi naendaa,niite kwenye jambo loloje mimi nafanya kwahiyo nilichimba kwa kadri nilivyoweza mwenyewe inatosha nikaweka sawa mazingira vizuri ili fedha zikikaa zikae vizuri na nikafanikiwa kufunika kwa namna sahihi kabisa ambayo mimi nikitaka naweza kwenda kuzichota sehemu salama na kuwa ngumu mtu kugundua kama mimi nina pesa ndani kwa nilivyohifadhi.

Nikaanza kufatilia mchakato wa suala zima la nafaka kwani nilimpata mtu akanipa mwongozo na nilimwambia mimi nina mtaji wa milioni ishirini na akanambia kwa mwanzo kwa biashara ya nafaka milioni ishirini ni mtaji mzuri kabisa,akasema "pesa hiyo hata ukitaka kuwekeza katika biashara nyingine inaweza kukupush ila wewe umesema nafaka yafaa sana,tutafungua duka na kuuza nafaka za jumla" nikamwambia "basi naomba mwongozo wako,naomba nisaidie katika hili kwa sababu nimekuwa nikitamani sana" ndipo alipofatilia na kupata eneo na kulipa eneo,yaani kulipia flemu na michakato mingine ikaendelea ili kuweza kuanza biashara na mimi ni mtanzania wa asili ya kutoka hapahapa Tanzania na nikalipa jina fremu yangu kwa jina la asili ya kutoka nyumbani kwetu,nilianza kuwa bize sana na kuna muda nilipata wakati nikaenda kuwatizama watoto wa mshkaji na safari hii sikuenda kinyonge kama nilivyokuwa naenda safari za nyuma,nilikwenda na vitu vingi sana kwa sababu nilienda kufanya shopping ya vyakula vya kutosha kabisa na hata yule mama yao alishangazwa sana na kitendo changu chaa mimi kupeleka vyakula vingi kama vile yaani karibu vyote vilivyokuwa vikihitajika nyumbani nilipeleka na akasema "eeh vyote unatuletea sisi? Nikasema "ndio" akasema "kwanini,kwanini? Kwani wewe hauna ndugu?" Na yeye ananiuliza nami nikacheka na kumwambia "hata nyinyi ni sehemu ya ndugu zangu kwa sababu nimeshakuwa marafiki na nyinyi" nikamwambia naomba nitoke na watoto,nikatoka na watoto na kuwapeleka shopping katika maduka na sikuwapeleka maduka madogo madogo ni maduka ya ukweli na kuwapa uhuru wachague wanachotamani kuvaa,yaani watoto walifurahi wakachagua viatu,majinzi,fulana,mashati nami nikalipa kwa ukweli watoto walifurahi sana,walifurahi mno na kikubwa mimi niliwaambia "baba yenu anawapenda sana" na kwakuwa baba yao yupo gerezani na watoto hawa wamekuwa hawapati nafasi kwa baba yao kwahiyo wanapokea tu sio ile usiliasi sana katika mapokeo ya kuhusu baba yao lakini mimi nikawa nimefanya kwa nafasi na niliyakamilisha hayo na nikarudi tena kule gerezani.

Nilipofika gerezani nikampa salamu zake kutoka kwa watoto na nikamuelezea kuwa nimewafanyia shopping na ni kwa kiasi gani watoto wamefurahia naye akafurahi sana kwa maelezo yangu na kusema "nakushukuru sana Rojas,nakushukuru na sina neno jingine zuri lakusema,nakushukuru sana lakini mbona wewe haujavaa mavazi yale ninayotamani kukuona nayo umevaa?" Nikamwambia "unatamani kunionaje?" "Nenda kanunue nguo nzuri sasa maisha yako Rojas yameshabadilika haiwezekani una pesa ndani uwe unavaa hivyo bwana" nikacheka nikamwambia "nimekuelewa" akasema "zile pesa ni za kwako Rojas,nikisema zile pesa ni za kwangu na zangu ujue ni za kwako kwakuwa wewe ndio upo uraiani hata ukisema uniletee haya mimi nafanya matumizi gani hapa? Sina matumizi ya kufanyia hapa ila wewe unayo,furahia maisha Rojas tena uwe na amani kabisa kwani mimi nafurahi unaponiletea habari za watoto wangu mimi moyo wangu unajawa na furaha,sina furaha nyingine zaidi ya watoto wangu mimi,nataka nione wanasoma vizuri sijui una mpango gani sasa?" Nikamwambia nimefanya moja,mbili,tatu nikamueleza mengi ambayo nimefanya akafurahi sana na nikamueleza kuwa kuna haja ya watoto sasa kuwapa elimu iliyo bora na akasema iliyobora sioni kama nimechelewa? Nikasema "kwa mfano huyo mdogo wala usiwaze nitatafuta shule nzuri kwa namna yoyote ile waingie uko" akaniuliza "unawaza nini kingine" nikamjibu "mengi nayawaza kuhusu watoto wake ikiwapo kuwapa elimu bora na maisha mazuri,nataka niwahamishe pale wanapokaa" basi ninapozungumza hivi anafurahi sana,anafurahi kweli kweli,alifurahi sana na katika mazungumzo akanigusia swala ambalo tulilizungumza mwanzoni "Rojas wewe ni bosi sasa,wewe ni tajiri mtoto" nikacheka na akanambia "biashara ya taxi kwakuwa unaifahamu na una uzoefu nayo kwanini usinunue taxi nyingi" nikamuuliza "nyingi ngapi bwana?" Akanijibu " kwa pesa ulizonazo unaweza unaweza kununua ngapi? Nunua gari tano,nunua gari tano alafu zitupe sokoni naamini hautajuta" nikamuuliza "kweli?" Unajua mimi nimekulia kitaa nimekuwa sina connection zozote sifahamu naanzia wapi?" Akanambia "najua,najua na sasa mimi nipo gerezani je nikusaidie kukukutanisha na mtu?"

Nikamwambia "mtu? Kuna mtu uko uraiani unafahamiane nae kwa ukaribu hivyo anaweza kunisaidia?" Akasema "yupo kuna mshkaji mmoja alikuwa anadili na mambo ya magari sasa umekuwa muda umeshaenda sana sijajua kama bado anaendelea kufanya hivyo " nikamwambia "wala usiwaze kwa sababu niko uraiani hakuna sab kitakachoshindikana nitatafuta namna yoyote kujua wapi naweza nikapata na sio mambo ya kutapeliwa" akasema "hilo la msingi sana,sawa,lini tena utaenda kuwaangalia watoto" nikamwambia "naangalia,naangalia namna bora lakini mimi nimewaza jambo moja zuri sana" akasema "jambo gani?" Nikamjibu "ikiwezekana,ikiwezekana kama yule mama atakataa habari ya kuwapeleka watoto boarding ikiwezekana niwachukue nikae nao" akasema "hatakubali yule mwanamke,hatakubali kabisa,hawezi kukuamini hivyo kukupa wale watoto hata kama umekuwa unaenda,hawezi kuruhusu kitu kama hicho,wala usiwaze kuhusu hilo pengine litakuja kufanyika baadae akishajenga imani na wewe na mimi nataka wale wakaa na mama yao pia wala sitaki kumnyang'anya yule mwanamke watoto maana yake na yeye ni faraja yake pia ila waweza watengenezea mazingira mazuri,wakaishi pazuri wakapata mahitaji yote,hilo ndio naona bora zaidi" nikamwambia "sawa,nimetamani kukuletea vitu vingi sana huku gerezani ila vichache hivyo nimeleta" akasema "si unajua hivyo vingi ntaviweka wapi tena lakini nashukuru sana,asante sana" alishukuru saana yaani kiwango cha kushukuru kilikuwa cha juu mno,ile hofu aliyonipa mwanzoni hakunipa safari hii,niliondoka nikiwa na furaha nasikia moyo wangu umeanza kuwa na amani kwa mazungumzo tuliyoyafanya.

Biashara iliposimama sasa na kaka alipojua kuhusiana na hili kiundani kwamba ni mimi ndio nimefungua hili duka alinambia "mdogo wangu njoo tuzungumze,njoo tuzungumze hauwezi kuendelea kunikwepa njoo tuongee" nikapata muda nikakaa na kaka,kaka alinambia "mimi ni nani kwako?" Nikamjibu "wewe ni kaka yangu" akaendelea "unaweza kunificha jambo lolete mimi na ukafanya mambo kwa siri? Pesa ya kufungua duka la nafaka umezipata wapi? Sisi tunajua maisha ya familia yetu,umekuwa unatoa pesa hata mimi nikasema labda ni huyo mfadhili lakini na hili duka ni nani tena? Ni yule mtu aliyekwambia upange ile nyumba kule? Nikamwambia "kaka kwani shida ni nini,inamaana kila kitu katika maisha yangu natakiwa kukiongea kwako? Nilipomwambia kaka alishangaa akanambia "Rojas unanijibu mimi hivyo?" Kwa sababu naweza kumueleza nini kaka kuhusiana na hizi pesa zaidi zaidi nitamdanganya nami sitaki kumdanganya na ndio maana sitaki kuzungumza habari kuhusiana na hizi pesa.

Nampenda sana kaka yangu lakini siwezi kumueleza huu ukweli lakini aliniambia sentensi moja "waweza kuona umewin kwa kutokusema au kunidanganya lakini Rojas wewe ni mdogo wangu na ninakupenda sana na sisi kama familia tunakupenda,hatutaki kukupoteza wala upatwe na matatizo yoyote,usiwaze kunishirikisha mimi naweza kukuharibia dili lako zaidi zaidi ntakushauri yaliyo mema,sijajua unafanya dili gani,sijajua la halali au sio la halali lakini mimi nipo kwa ajili ya kukushauri yaliyo mazuri,mimi ni kaka yako" hatukuelewana na kaka nikaondoka zangu niliendelea na mishe zangu kama kawaida.

Nilipata muda na nikamtafuta yule mwanamke ambaye yule mshkaji wangu wa jela alikuwa anampenda sana (yule mchumba wake),iwapo yule kaka angekuwa uraiani huyu ndio angekuwa mke wake wa ndoa kabisa,anasema "mwanamke wa ndoto yangu,mwanamke ambaye nilimpenda sana" nilipoenda kumtembelea nilimpelekea pia vitu mbalimbali hasa vyakula vya nyumbani,hii ni mara ya pili namtembelea huyu mwanamke na kikubwa nilienda kumwambia "nina salamu zako kutoka kwa mwanaume ambaye anakupenda sana" alicheka na akafurahi nilipompatia zile zawadi na akanambia "kwanini unaniletea hizi zawadi mimi,mimi nilishbmua kuanza maisha yangu mapya,hajakwambia chochote kwani? Nikamwambia pengine anajua umeshaamua kuanza maisha mapya lakini upendo alionao kwako ni mkubwa sana na kwa sababu anaishi anasema upendo wake kwako hauwezi kupotea na amenitumia kuja kukwambia nami ni mjumbe mwema,rafiki mwema nimekuja,nimekuja kukujulia hali,kukupa salamu na kukuletea hivi vitu,akasema "usijisumbue kuingia gharama na kuniletea mimi hivi vitu" nikamwambia "usijali nimekuja kukusalimia kwa upendo" akapokea na nikampatia kiasi cha pesa,nilimuachi laki nne akashangaa na kunambia "kwanini unanipa pesa? Yaani Kwanini?" Angejua kama hizi pesa zinatoka kwa mwanaume ambaye yuko gerezani ila ndio hivyo hauwezi kusema na kwakuwa mimi ni mjumbe tu nimekuwa nikiwatendea wema watu hawa ambao huyu mtu alitamani kama angekuwa uraiani wafurahie maisha,sikuishia hapo kwani nilirudi tena kwa yule mama na kuketi na kuzungumza nae anataka kufanya nini,alicheka sana siku niliyomuuliza hilo swali,alisema "eeh unataka kujua mimi nataka kufanya nini ili wewe ufanye nini?"

Nikamwambia naweza kukushauri kitu au kama unahitaji mtaji au kukukopea mtaji mahali ukafanya biashara" akasema "nina mawazo mengi ila sina tu msingi maisha yangu yamevurugwa,si unaona yule mwanaume yuko kule gerezani anafanya cha maana nini,maisha yake yameishia uko,ndugu zake hawajali lolote kuhusu mimi na siwataki hata kuwaona,watoto hawa naangaika nao mimi ndio kila kitu" nakumbuka nikamwambia "basi angalia biashara gani unaweza ukafanya alafu nishirikishe,kitu kingine pia naona hapa unapoishi naona mazingira sio mazuri kwa watoto,nina jambo nilifikiria na jambo nililofikiria kwanini nisitafute nyumba ambayo itakufaa zaidi wewe pamoja na watoto" akanambia "unitafutie nyumba mimi? Unitafutie nyumba kwa sababu gani? Nikamuuliza "kwanini umestuka nami nimeshakuwa sehemt ya familia" akaniuliza "unamaanisha nini,unataka nini kwangu? Nakumbuka huyu mama aliniuliza hili swali,unajua mimi ni kijana mdogo na huyu kwangu age ilikuwa imeenda kidogo,sio age zangu kidogo sio age zangu lakini kwa jinsi nilivyomwambia akaona labda ni wale vijana wahuni nini (wapenda majimama😂)au kijana anakuja kuja amenitamani nini? Yaani akili kama hizo na nikajua ndio mawazo anayoyawazia hayo,nikamwambia "mimi ninawapenda sana hawa watoto kwa sababu ya rafiki yangu na kama mimi Mungu amenibariki napata chochote kwanini nishindwe kufanya vitu vilivyo bora kwa watoto ambao ni wa rafiki yangu,fikiria kuhusu hilo alafu ntakapokuja utaniambia" huyu mama mara zote nyuma nilizokuwa nakuja uwaga ananikaziaga macho,tukiwa tunazungumza uwaga na maneno flani mfano ni nini? Umekuja kufanya nini na maneno kadha wa kadha ya shombo lakini leo huyu mama hata angalia yake ilikuwa ya uoga na nidhamu,unajua mtu anakuangalia anaona haya flani kwa matendo yake ya nyuma kwako,akanambia "kwahiyo utakuja lini?" 😂
Nikawa naulizwa mimi tena hapo wakati uwaga hana hata swaga hizo wakati ukija atakupa maneno ya shombo kama yote lakini leo nikaliona tabasamu lake,akaniuliza "utakuja lini?" Nami nikamjibu "nitakuja,kwani wewe ulitaka nije lini?" Akanijibu "wakati wowote hata kesho jioni ntakuwa nshapata majibu" nikawa najisemea moyoni mwangu "pesa,pesa ni kitu kingine kabisa katika maisha ya mwanadamu hapa duniani,pesa ina nguvu,pesa inasema,pesa inaongea,pesa ina siri nzito sana mimi katika maisha niliyopitia nikagundua siri ya nguvu ya pesa ni ya ajabu sana" nikaondoka kwa huyu mama nikiwa natabasamu lakini kaka yangu alizidi kunisumbua sana akitaka kujua vyanzo vyangu vya mapato vinatoka wapi,akiwauliza washkaji zangu,watu zangu wa karibu lakini hakuna hata mtu mmoja anayejua chochote kwa sababu sijawahi na mtu yoyote yule,wakati huo nikiendelea na michakato ya kujikita kwenye biashara ya taxi yaani naagiza magari mazuri na natafuta vijana na kwa sababu mimi nina uzoefu si haba hii inaweza kuwa mwanzo wa biashara hii kuweza kufanikiwa.

Itaendelea!

ITAENDELEA!
 
Back
Top Bottom