shikamkono01
JF-Expert Member
- Mar 26, 2016
- 685
- 2,055
- Thread starter
- #341
Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
Sehemu ya 14
Maisha ni safari ndefu sana! Wale rafiki zangu wakanitengenezea ushawishi wao na kwakuwa nilikuwa na msongo wangu kichwani na kuanza kujaribu vileo tofauti tofauti lengo likiwa ni kujaribu kuupoza au kuondoa mzigo uliopo kichwani,na nikawa nakunywa pombe lakini zile pombe nikawa nakunywa kwa tahadhari nikihofia nisije nikapitiliza ulevi hadi nikafikiri kuja kuropoka kuhusu siri zangu na yule kaka.
Nakumbuka kuna siku kaka alinijulisha kuwa ana sherehe ya kijana wake na aliniomba nimpush katika suala la sherehe hiyo nami nikamwambia "sawa mimi niko na wewe na nitajitoa kadri nitakavyoweza yeye aniambie tu nini anataka na tutafanya" alinambia mahitaji yanayohitajika nami niliyafanya hayo kwahiyo tulikutana tena wakati mwingine wakati shughuli ikiwa inafanyika nami nikawa ni mmoja kati ya washiriki pale,tunafurahi kwa pamoja,siku njema tunafurahi na nini na kulikuwa na vilevi vya aina mbalimbali vilikuwa vimenunuliwa basi na mimi nikatumia kile ambacho kwa wakati huu nikikitumia nakuwa najiona napata stimu zaidi yaani najisikia furaha,kwahiyo ni siku ambayo nimejikuta nimekunywa,nimekunywa,nimekunywa zaidi tofautitna siku za nyuma hapa kidogo nilikuwa nakunywa kiasi flani,tulikuwa na kaka na rafiki zake na washkaji zangu pia ambao mimi nilikuwa nimewakaribisha na vitu kama hivyo,yaani ni pati ya furaha,nakumbukaka kaka alinambia "naona umechangamka mdogo wangu,haya sasa ndio maisha mdogo wangu unayotakiwa kuishi,unatakiwa kuishi kwa furaha,acha kujitenga,mambo ya kujitenga sio mazuri mimi najua hupendi vitu gani nimeshakuelewa,tuishi kwa amani sasa usianze kunikwepakwepa" ujue ukiwa katika hali umelewa unaweza ukazungumza vitu ambavyo katika hali ya kawaida unakuwa huwezi ukavizungumza,nikawa namwambia "kaka mimi unaniboa bwana,unaniboa sana" akanambia "mdogo wangu basi yaishe toa iko kinyongo moyoni tuishi kama zamani,mimi ni kaka yako na yote hayo ni kwa upendo wangu tu wa dhati lakini kama nilikuwa nakukosea nisamehe,angalia shughuli hii yote umeibeba wewe leo mimi hapa nasifiwa,napata heshima,watoto wangu wanaendelea vizuri,mahitaji mbalimbali naweza kuyafanya,nayafanya lakini sio mimi bali ni wewe ndio unawezesha hayo,sasa hivi familia yetu imekuwa bora,maisha yamekuwa mazuri na yote ni wewe ndio unayeyafanya hayo kwahiyo siko tayari kuona nagombana nawe mdogo wangu" hayo maneno kaka aliniambia nami nikawa nafuraha kwa sababu sisi ni ndugu unajua pamoja na yote yanayoweza kutokea na kukosa kuelewana,kiukweli nilifurahi sana.
Nikiwa hapa kwenye pati nilipigiwa simu,aliyenipigia simu alikuwa ni yule msicpgana wa yule kaka kule gerezani na sio mtu ambaye uwa ananipigia pigiaa simu kwani sijaweka mazoea hayo ya yeye kunipigia simu,nilipokea nakatika hali niliyonayo kichwani (kilevi) niliipokea ile simu kwa uchangamfu sana,akanambia "uko wapi? Nikamwambia mahali niliko,akanambia "natamani hata nije sijisikii hata vizuri" hii sentensi naikumbuka alinambia,sasa namimi tena nina kilevi,nikamwambia "njoo,uko wapi? Uko wapi nimwambie dereva akufate hapa kuna pati hapa tunafurahi yaani tunaweza tukakesha mpaka asubuhi"akanambia "sawa basi nifanyie mpango niweze kuja" nikamkodi mshkaji palepale ambaye ni dereva amfate alipo.
Sherehe ilikuwa kubwa kwani ilianza toka asubuhi kwa kuchoma nyama na watu kunywa supu yaani ni furaha na vinywaji vipo vya kutosha,nikiwa nimekaa hapa kweli yule msichana akaja na akanambia "yaani hata umejuaje hadi umeniita hapa,yaani hata sijui ingekuwa ni siku ngumu kiasi gani kwangu ,natamani hata nitumie wine yoyote sweet nami palepale nikatoa maagizo aletewe chaguo lake naye aweze kuenjoy,nikawa nimekaa nae kwa karibu nikawa nazungumza nae na akanambia "yaani nina msongo wa mawazo usio wa kawaida" nami nikamwambia "basi leo msongo wa mawazo unaisha hapa kwa sababu leo utafurahi na mastress yote utayaacha hapa"akanambia "kweli? Unanambia kweli,ntafurahi sana" namimi nikawa ni mwenye furaha,huyu msichana ni mkubwa,huyu msichana kwangu mimi ni mkubwa lakini kutokana na mazingira tuliyokuta kabla ni tunaheshimiana tu hatujawahi kuvunjiana heshima tukawa tunapiga stori za hapa na pale,muda ukasogea na kadri muda unavyosogea nami nikawa najikuta nalewa zaidi,pombe kadri muda unavyoenda ndio nami najisikia kutaka kuchangamka zaidi,nakumbuka huyu dada aliomba aende maliwato,aliposimama kuelekea maliwato yaani nilipomuangalia niliona ni msichana mwenye shepu nzuri ajabu wakati sijawahi katika hali ya kawaida kufeel kitu kama iko,yaani sijawahi kumtizama kabla huyu msichana na kupata matamanio yoyote,ni mwanamke ambaye mshkaji wangu wa gerezani alimpenda,alinipa maelekezo na moja kati ya ahadi niliapia ni nisimguse mwanamke anayempenda bali nimsaidie,nilikuwa sijawahi kuwaza lakini leo nilisikia hiyo kitu ndani yangu hata nikasema imekuwaje leo tena?
Aliporejea tukawa tunaendelea na vinywaji na maongezi na pombe zikawa zinanituma tuondoke eneo lile na kwenda eneo jingine tofauta na nikamwambia yule msichana "unaonaje tukahamia eneo jingine? Akanambia "mbona hapa pametulia tu,tukae hapahapa" nikamwambia "nimesikia sana makelele eneo hili,tukae kidogo alafu tutaenda uko" akasema "sawa" dada amechangamka nami nimechangamka yaani ilikuwa balaa,nakumbuka alinambia "leo imekuwa ni siku ya furaha sana kwangu" nikamwambia "kweli? Akanambia "kabisa,najisikia amani,najisikia amani kama nimetua mizigo" nikamwambia "kwanini? Akasema "hata sijui,nasikia tu hivyo" nikamwambia "vizuri,vipi changamoto zako" akanambia "yaani sitaki hata tuzungumzie kuhusu yule mtu,sitaki hata kumuona,mimi na yeye tumeshamalizana,sitaki tena" nikamwambia "kwanini mtu anakuumiza mwanamke mrembo kama wewe,ni mwanaume gani mwenye moyo mgumu kiasi hicho anakuumiza msichana kama wewe" akatabasamu,nikamwambia "unatabasamu vizuri sana" akatabasamu tena,nikamwambia "wewe ni msichana mzuri sana na hautakiwi kuumizwa" akanambia "unajua wewe umekuja kwenye maisha yangu na ukanipa tumaini jipya kabisa,sapoti ambayo umenipa nilikuwa sijawahi kuipata katika maisha yangu,yaani umenifanya sasa hivi nione kama naweza kusimama mwenyewe na kutokuhangaika kuhusu mambo ya mahusiano kwa sababu sasa hivi naweza kujipambania katika mwanzo mzuri ambao umenipa" msichana alinambia maneno mazuri sana,pombe ilinifanya nimuone huyu msichana ni mrembo isivyo kawaida lakini mimi mpaka kesho uamini ile haikuwa akili yangu.
Unajua waweza kumuona mtu tofauti kwa sababu ya pombe lakini pale akili yako inaporudi clear kabisa unashtuka sana,mimi nilishtuka kwanza nakutana na mwanga kukiwa kumeshapambazuka,akili yangu inajiuliza kwani uko wapi? Kwani niko wapi? Nafumbua macho naangalia najikuta niko kwenye room,hiki si chumba ambacho mimi uwa nalala,naangalia naangalia najikuta nimelala na msicpgana pembeni! Ndipo kumbukumbu zinanijia kwa haraka sana,wakati kumbukumbu zinanijia na huyu msichana alikuwa amegeuka upande mwingine akajigeuzia kwangu namuona sasa ana kwa ana! Dah nimevunja makubaliano na mtu ambaye niliapa mimi sitafanya iko kitendo,sijui kwanini alinambia ile sentensi nimuahidi kwamba nitamsaidia na sitakuwa nae katika ulimwengu wa mahusiano,sijui niyaite mahusiano au niyaiteje na sijazungumza na huyu msichana mimi mambo kuhusu kumpenda,sijazungumza,sijazungumza kabisa,ushawahi kusikia mtu anasema nimefanya jambo kwa bahati mbaya? Mimi kwangu niliona nimefanya kwa bahati mbaya,imeshatokea!
Sikutaka hata kupoteza muda nakumbuka nilivaa nguo zangu kwa sababu mimi nashtuka nikiwa niko mtupu yaani sina nguo yoyote ile na kumbukumbu inaniambia yapo yameendelea mambo! Huyu dada aliamka kwa tabasamu,akijinyoosha akinambia ""Rojas mbona unaonekana kama unaondoka? Nilimwambia "tulipanga tuwe hapa? Tulipanga tuwe hapa?" Akanambia "unasema nini Rojas,mbona tuliongea na kwanini unaniuliza swali kama hilo,mbona ni mapema sana ebu njoo tupumzike zaidi" nikamwambia "hapana" akasema "kwanini? Nikamwambia "nina mambo mengi sana ya kufanya naona nimechelewa" akasema "sasa unaniacha hivi,unaniacha hivi kweli? Nikasikia kichwa kinaniwaka moto,najua hii hali haijawahi nikuta mimi peke yangu kwangu naamini hata wewe msomaji unaweza kujikuta katika hali kama hii yaani umejikuta na mtu pasipo katika mazingira yasiyoelezeka alafu unajikuta kumepambazuka umeshafanya vitu ambavyo haukuvitarajia,haukupanga hata kabla ya kuanza kutumia iko kilevi,unajikuta ushafanya na mshtuko wake uwa mkubwa.
Narudia tena,maisha ni safari ndefu sana,mwanamke huyu ananiambia "naondokaje sasa,yaani namuachaje hivyo?" Nina kikao muhimu sana na nimeshachelewa sana,akanambia "sawa sasa kwahiyo? Nikamwambia "wewe endelea kupumzika alafu tutaendelea kuwasiliana" akasema "sawa basi njoo hata uniage" nikamwambia "tutawasiliana" akasema "no bwana usifanye hivyo" nakumbuka yule msichana alikuwa kitandani ma akashuka,alishuka akiwa mtu kabisa akaja akanikumbatia,akanikiss na kunambia "umenipa tumaini jipya kabisa,naomba ahadi uliyonipa toka jana ya kuanza mahusiano na mimi naomba iwe kweli" yaani sikumbuki hata kama nilimwambia huyu msichana kama nampenda,sikumbuki kabisa na maneno haya anayoniambia nachanganyikiwa kabisa,akanambia "nakupenda na nimegundua wewe ni mtu wa tofauti sana,yaani umeufanya usiku wangu ni kama nazaliwa upya,naona mwanga mpya,naomba basi ukimaliza kikao unitafute" sina jingine ambalo nilimwambia zaidi ya kumwambia "basi baadae" niliwaza,niliwaza,nilijuta,nilikaa kwenye gari kwa muda mrefu nawaza nikijiuliza nimefanya nini mimi leo? Ilikuwaje? Ilikuwaje? Sikuwa na kikao wala nini ile ilikuwa ni njia yakuondokea tu pale,nilienda nyumbani na nikajimwagia maji yaani akili yangu hainipi,akili haitulii na nikaamua kukaa ili kutuliza akili na nikawa niko chumbani nimekaa,nimekaa tu mpaka ikafika majira ya saa saba hivi "bado haujamaliza kikao? Nikamwambia "bado,bado sijamaliza kikao" akanambia "basi nilikuwa nawaza nikutengenezee kitu uje ule maana jana umetumia vilevi sasa angalau upate chakula chenye nguvu" inamaana hapa anataka niende kule kwake sasa ndio kwenda kula hicho chakula kwani alishatoka kule hotelini tulipolala usiku uliopita,akanambia "nilipiga simu ukawa haupatikani" nikamwambia "nimewasha muda sio mrefu,nitakupigia,nitakupigia" akasema "kwahiyo nakusubiri,si utakuja jioni? Nikamwambia "nitakupigia" Yaani hata sijui nilimwambia nini huyu msichana lakini niliona ni vitu ambavyo nikaona vinanichanganya kichwani.Mchana nikasema ngoja nitoke nijinyooshe miguu kidogo na nilipokuwa njiani nikakutana na kaka naye baada ya salamu akaniambia "vipi mbona ukatokomea kimoja,lazima utakuwa ulikuwa na furaha sana na yule mtoto mrembo" nikamwambia "kaka acha tu,acha tu niko na maumivu sana ya moyoni" akanambia nini tena? Nikamwambia "hata hayaelezeki,achana nayo.
ITAENDELEA!