Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Sitasahau’ cha Radio Free Africa​



Sehemu ya 15


Mimi nikawa nimepata mwanzo mpya wa maisha,kitendo ambacho kimetokea siku yajana,juzi,siku za nyuma,ikazaa tabia mpya katika maisha yangu kwani mimi nilikuwa ni kijana wa kitaa,nilipata pesa kwa ghafla lakini nilistuka nilipoziona pesa na najua hizi ni za kwangu lakini ndani yangu niliamini katika kujisimamia kwamba mimi hii pesa kwa sababu ni ya kwangu haitanibadilisha kwa chochote,mimi nitabaki vile vile kama nilivyo,wav wanasema watu wanabadilishwa na pesa nami nikasema pesa haitanibadilisha lakini nguvu sasa imenishinda,pesa imenishinda nguvu na tabia zangu zikaanza kubadilika kwani kwa masuala ya wanawake ikawa kama nimefungua mlango na hata kama leo utaniuliza mlango wa kuhusudu wanawake,kupenda wanawake kiwango kisicho kawaida ilianza lini? Ni usiku ule mtoto wetu kupata graduation na mimi baada ya kuambatana na huyu msichana baada ya kutumia kilevi na kupata matamanio kwani tangu hapo ni kama ukurasa mpya ulifunguliwa maishani mwangu.

Hatia ya kujisikia vibaya kwa kutembea na yule msichana ilidumu kwa muda mfupi sana na hata kaka yangu aliniuliza "hivi Rojas wewe unaweza ukaona maisha ya furaha ni yapi,maisha ya furaha kwa mwanaume ni yapi,ni kuwa na vitu anavyovitaka, sasa hivi unaweza kuwa na mwanamke yoyote unayemtaka,kuna furaha gani zaidi ya hiyo? Huyu ni kaka yangu alinambia maneno hayo,sitaki kumuhukumu kusema maneno yake pia yalichangia mimi kuwa hivi,siwezi kusema hivyo lakini mimi nilibadilishwa kwani Rojas mimi niliyekuwa sipendi wanawake nikaanza kupenda wanawake na hasa nnapotumia kilevi,nnapotumia kilevi matamanio kwangu yanakuwa makubwa kuliko kawaida,nikaanza kuishi maisha ambayo mwanzo sikuwa nayo,pesa ikaanza kunipeleka puta na hata nikawa muhudhuriaji mzuri kwenye hizi bendi za muziki na nikifika pale lazima niwe na kampani kubwa na hizo kampani hata ukiniuliza zimetokea wapi nakuwa sina jibu,mimi na kampani yangu nikawa ni mtu wakubadili viwanja mara tupo hapa,mara hapa panaboa twende huku mara kule, katika gari yangu nyuma ya gari nakuwa na briefcase yenye hela yaani hizi ni kwa matumizi yangu ya kuwel heshima bar!

Mwenendo wangu ulibadirika na nikisema niseme jinsi ulivyobadilika yaani ni kwa kiwango kikubwa sana tena kwa muda mfupi sana,mabadiliko yangu yalifikia kiwango cha hadi kuwa natmwanamke mmoja haitoshi kwani si pesa ndio inayoongea na wanawake wanataka nini,wanawake wanataka pesa na pesa ipo kiasi nikawa hata kulala na wanawake wawili kwa pamoja kwangu haikuwa ishu,yaani pesa ilinibadilisha kwa kiwango kikubwa sana,nakumbuka hatua za mwanzo nikiwa na ujasiri wakujiambia kuwa pesa haitanipeleka,pesa haitaniharibu na nitabbki **** Rojas yuleyule na nitaendelea kufanya majukumu yangu kama kawaida lakini pesa inayo nguvu kuliko vile watu tunawaza,pesa ina macho,pesa ina mdomo,pesa ina masikio,pesa ina miguu yaani kuliko vile tunawaza,niliwaza hivyo lakini kumbe pesa inaenda kunifanyia vitu vipya kwenye maisha yangu.

Nakumbuka siku moja hapo nikiwa nimeishi katika mifumo hiyo hata mwaka ulipita,mwaka ulipita mimi nikiwa ni mtu wa starehe tu ingawa napata muda natizama maendeleo ya biashara lakini nilikuwa nimetawaliwa na starehe kwa kiwango kikubwa ikawa hata nikitumia kilevi nakuwa sitoshelezeki nacho nakuwa nasaka kilevi kipya almradi kujaribu kila aina ya ulevi nikapelekea hadi katika uvutaji wa sigara huku shauku ya kufanya tena na tena ikinijia,kuna mshkaji wangu miongoni mwa vijana ambao nimewakabidhi taxi ninazozimiliki aliniomba kuzungumza nami,ni mmoja kati ya watu waaminifu na uko nyuma yeye alikuwa akinipa mimi deiwaka katika gari lake nami ndio nilipopata pesa na kununua zangu sasa nimekuwa bosi wake,alinambia maneno haya "yaani Rojas kila siku ninapokuona naona sio Rojas ninayekufahamu" nikamwambia "kwanini unasema hivyo" akasema "wewe ni mdogo wangu,wewe ni mshkaji nimesena nikutafute siku ambayo naamini utakuwa hauna hang over,naamini huu muda uko fresh kabisa,Rojas kuna kitu kwako hakiko sawa" nikamwambia "kwanini,kwanini unasema hivyo" akasema "hapana,mshkaji unakunywa sana ,unakunywa sana Rojas alafu wanawake,sikwambii kwa ubaya wewe ni kama mdogo wangu alafu tena mshkaji alafu tena ni bosi wangu nakwambia tu katika roho nzuri kaka yako anakuharibu,kaka yako haiwezekani akawa anakutafutia wanawake akutegee wakati huo huo anakusifia na wakati huo huo anataka akuchume wewe pesa,mimi sizungumzi kwa ubaya yule ni kaka yako lakini Rojas kuna kitu kwako hakiko sawa"

nikamwambia "wewe unanionaje yaani kitu gani kwangu kimebadilika " akanambia "Rojas pesa zisije zikawa zinakutumikisha katika mambo ya uovu,yaani mimi nakujua Rojas ingekuwa mtu mwingine tu baki mimi hata nisingezungumza hivyo,mimi nazungumza hivyo kwa sababu nakujua" nikamwambia "kwahiyo unataka nifanyaje sasa" akanambia "unajua Rojas unatakiwa upate muda wewe mwenyewe ujitathmini na kujiuliza wewe ndio Rojas au kuna mtu mwingine amezaliwa ndani yako" mtu huyu alizungumza na mimi,ni mshkaji ni mkubwa kwangu pia,alizungumza na mimi maneno ambayo pengine ni nadra kukutana na mtu kwani hata kaka yangu mimi haniambii hata washkaji ambao tunakutana nao kula bata,tunatega mingo tumpate msichana gani mfano kuna msichana huyo ndio mwenyewe mwenyewe yaani mtaa flani ndio funga kazi lakini mgumu kweli kweli nasema "nileteeni huyo,nileteeni huyo mimi huyo nampata" wapo washkaji ambao tunajadiliana hayo na jana ilikuwaje? Demu wa jana ilikuwa moja,mbili,tatu,nilikuwa na watu wengi wakujadiliana nayo hayo na nilikuwa nasikia raha kunapokuwa na stori za muundo huo,nasikia furaha,kwahiyo mtu anaponiambia mambo haya kwa kukuface na kukwambia ukweli kwamba bwana umebadilika,nikamind kiukweli maana niliona kama anataka kuniambia jambo la maana alafu kumbe jambo lenyewe la kipuuzi,akanambia "hapana Rojas sio jambo la kipuuzi,mimi ingawa ni mkubwa lakini naweza kuwa sina chochote ambacho naweza nikakwambia lakini naweza nikakushauri,wewe ni mdogo wangu alafu sipendi kukuona unaharibikiwa,Rojas hauwezi kumaliza wanawake wa dunia nzima,hauwezi,yaani wanazaliwa kila siku na wana urembo wa kila aina lazima urudi ujijue ujirudishe wewe kama Rojas,wewe Rojas uliyekuwa na displine yako wewe mwenyewe binafsi" mazungumzo ya deep sana alinambia,deep sana na sikuwa nimelewa kabisa nilikuwa niko fresh kabisa.

Nakumbuka katika mengi tulizungumza kwakuwa ni mtu ninayemheshimu sana nikamwambia sentensi moja nikamwambia "sijui,sijui hata nimepatwa na nini kwani muda wote najisikia kufanya starehe,nasikia kusukumwa kufanya starehe yaani" akanambia Rojas hauko sawa,kuna kitu kwako hakiko sawa Rojas,unajua pesa na hasa kwa sisi ambao tumezaliwa katika familia maskini tukipata pesa lazima pesa zinaweza zikatupeleka kama tutakosa ushauri mzuri tukakosa watu sahihi ambao watatuambia ukweli na kuturudisha kwenye mstari pale tunapokuwa tunakosea tofauti na yule aliyezaliwa katika mazingira ya umiliki wa pesa,kwao wana pesa,hizo pesa zipo,wanapata mahitaji yote kwahiyo eneo la mwanamke anaweza kumpata mwanamke yoyote kwa sababu pesa ipo yaani hashoboki na vitu lakini sisi ambao tumezaliwa katika familia maskini tunapopata nafasi kama hivi unaweza kuta ile hali ya uhalisia wako sasa inaanza kutumikishwa kwa sababu kuna hali inazaliwa ndani yako ya kujiamini,ya kumiliki kila kitu,ya kujitukuza unajikuta unafanya vitu ambavyo awali haukuwa unavifanya lakini Rojas haimaanishi kila mtu anayepata pesa anatakiwa abadilishwe na pesa,pesa inatakiwa wewe ndio uicontrow na sio yenyewe pesa ikucontrow wewe,Rojas sasa hivi pesa inakucontrow wewe,unaweza kuwa katika mambo yako muhimu lakini washkaji zako ambao wamezaliwa baada ya wewe kupata pesa hata wakikwambia njoo unaenda,wakikwambia tunakuja wanakubeba,unaharibu mipango yako,ratiba zako,unaharibu vitu vyako kwa sababu tu umeshaingia katika utumwa" alinambia maneno mengi mengi sana mpaka nikawa nasikia kuchanganyikiwa kuendelea kuyasikia,nikamwambia "naomba uniache,naomba uniache" akanambia "Rojas naomba yafikirie haya pia nafikiri unahitaji msaada Rojas angalau wa kuongea na watu wanaokupenda pia,mimi nasikitika (akawa ananitajia msichana mmoja ambaye mimi nimetoka nae )wewe Rojas wakutoka na msichana kama yule kweli? Wasichana ambao wana sifa mbaya kwelikweli unafanya kwa mashindano ili uonekane nawe umepita pale,wewe sio Rojas bwana,wewe sio Rojas ninayemjua mimi ambaye anajipenda,anayejiamini"

Yote haya alinambia kwa uchungu na kaka yangu hajawahi kuniusia kuhusu haya mambo ya wanawake yaani yeye ananambia sifa ya mwanaume na hasa mwanaume aliyebarikiwa uchumi miliki mwanamke ambaye moyo wako unasikia una washawasha,unasikia furaha nae,kwahiyo leo nikisikia furaha na huyu niwe nae,kesho nikisikia furaha na yule kwahiyo kwa mapana kabisa pesa ikanibadilisha nikawa mtu mbaya,mtu ambaye sikujali tena hisia za mwanamke yoyote,mimi nikipita napita na za kwangu yeye kama ataona mimi nadumu hapo kumbe mimi ni msafiri tu bado nasafari sijafika hata yule mwanamke wa mshkaji ambaye nasema mwanzo ilikuwa bahati mbaya nilimjeruhi kwa sababu nilimwambia "hapana,hapana usinicontrow hapana ilitokea bahati mbaya lakini inaonekana ni mtu aliyeniamini kwa sentensi zangu za mwanzo katika ulevi lakini kote uko mimi niliendelea kupita,naendelea kupita,nikaja kugundua kitu pesa kinabadilisha watu wengi sana,watu wengi walio katika hali ya umaskini walipopata pesa nyingi asilimia kubwa wanabadilika,uhalisia ule wandani ambao uwa hauonekani majira akiwa hana pesa ndio unaonekana sasa,kitu ambacho sikuweza kusahau katika starehe zangu zote ni kwenda kuwatizama wale watoto wa mshkaji kwa sababu yule mama alipambana (yule mama niliyempa mtaji wa biashara ya vinywaji)huyu mama kweli alikuwa mpambanaji kama kweli alivyosema kwamba mimi sitahangaika tena na wanaume,sitahangaika tena mbdam nimepata kitu changu cha kuniingizia shilingi mbili tatu nitasimama nacho hiki,kwahiyo mara nyingi akawa ananipigia simu "watoto wanakusalimia" kwahiyo yeye hata katika mabadiliko yangu,hata katika hali ya ulevi niwe naenda pia kuwatizama wale watoto na kuwapa mahitaji mbalimbali kwa hao watu sikusahau lakini kwa yule nilikuwa ni mtu wa kukata kamba labda anikumbuke yeye tu na kama akinikumbuka akinifosi hivyo yaani sina ile mambo yakusema nikae nitulie,nikaanza mambo ya kuhangaika kuhangaika ndio kama nilivyoelezea kwa mapana katika eneo hilo.

Kuna biashara mwanzo ambayo nilitamani sana kuifanya,nilitamani kufanya na nilipata watu ambao niliamini nimepata watu sahihi kwenye eneo la madini,kuna eneo mwanzo nilifanya niliona kama kuna matunda mazuri,eneo hili kunahitaji umakini na kunahitaji watu sahihi kwa sababu kuna nyakati nilipigwa yaani niliingia mkenge watu waliamua kunitengeneza na kunipiga masuala mazima ya utapeli kwahiyo ikanijeruhi sana hiyo kwa sababu ni harakati ambazo naendelea kupamcna nazo lakini sikurudi tena kule gerezani nyakati hizo zote sikuwahi kurudi gerezani,mimi ulipita mwaka mmoja mzima sikukanyaga gerezani,ukafika mwaka mmoja na nusu sikufika gerezani mpaka ikafika miaka miwili sikurudi gerezani,maisha yananipeleka resi sana lakini uzuri pia zile biashara ambazo nilizidi kuwekeza ziliendelea kuzalisha.

Kuna mambo uwa hatupendi kuyasikia kwa sababu yanakera sana kwa sababu mimi huyu aliyekuwa dereva wangu hakuacha kuniusia,hakuacha kuniusia kutokana na tabia yangu,nakumbuka siku hiyo alinambia "vipi bosi leo nina shida nawe nataka tuonane,natamani hata twende nyumbani kwangu tuandae chakula,tupate chakula pamoja" nikamwambia "kuna nini" kumbuka huyu mtu tuna mahusiano mazuri toka siku za nyuma,akanambia "kuna vitu tu vya msingi sana natamani tuongee" nikamwambia "yaani wewe hubadilishagi mada zako kila siku ni hizo hizo" akanambia "Rojas ni kitu muhimu sana nataka tuongee,hatuwezi kungea kwenye gari,hatuwezi kuongea kwenye mahoteli yako uko unakokuwa na wanawake zako mimi nataka tuongee hili jambo nyumbani kwangu" nikamwambia "poa basi tutacheki muda siku nikiwa free" akanisumbua akanambia "iwe leo leo bwana,iwe leo leo" nikamwambia "nina ratiba nyingine" lakini akanisihi sana,nikamwambia "nitakuja mida ya usiku" akanambia "mida ya usiku siwezi kukupata Rojas washkaji zako watakuwa wameshakudaka Rojas" nikamwambia "hamna nitakuja,nitakuja alafu ndio nitaendelea na mambo mengine" kwa sababu alinisumbua sana na mpaka akanifata mahali nilipo na mahali nilipo nilishaanza kunywa pombe.alinichukua na nikamwambia "si tuongee hapa hapa" akasema "hapana mimi twende tu nyumbani kwanza mimi nasimamisha kila kitu kwa sababu mke wangu kaandaa chakula" kweli tukaenda hadi kwake na nikamwambia "yaani hata sijui unachoniitia mimi muhimu hivyo mi najua utanikwaza tu pale ntakapojua ni habari zako zisizobadilika"

Nilifika na kumkuta mke wake na alifurahi sana kuniona na kwa sababu ananifahamu kwa sababu anajua mimi nilikuwa kijiweni tu sema nimepata pesa nimetoboa kwahiyo kimaisha hatufanani lakini ni mwanamke anayenifahamu basi nami nilitamani kujua nini hasa hadi wameniita mpaka huku na huyu mama aliandaa chakula lakini mimi niliwaambia nimeshiba lakini yule mama akasema "hiki ni chakula maalum kwa ajili yako maana nimemwambia mume wangu natamani kumuona Rojas angalau tule nae chakula akanambia ratiba zako zimekuwa ngumu ,ninamshukuru Mungu sana angalau leo umekuja asante sana shemeji yangu yaani nimefurahi sana" nikasema "asante"

Tukala pale na kiukweli chakula kilikuwa kitamu sana,huyu shemeji yangu alikuwa mahiri katika mapishi,baada ya kula na kupumzika kidogo kupisha chakula kishuke tumboni yule shemeji yangu alinambia "Rojas nimekwita,naomba unisamehe mimi ndiye nilikwita baada ya kuzungumza na mume wangu nikaona nimshirikishe kiundani ili akuambie tuonane lakini mimi ningesema nije pengine usingeweza kunielewa lakini kwa sababu najua unamheshimu ndugu yako huyu nikasema ngoja nimtumie huyu huyu angalau tuzungumze,nikawa najiuliza sasa huyu mama anataka kuniambia nini? Akaniambia "Rojas wewe ni ndugu yetu kabisa,sisi tunakuhesabu ni ndugu yetu lakini pia wewe ni bosi wetu,utanisamehe kwa maneno ambayo nitazungumza lakini nayazungumza haya yanatoka ndani ya moyo wangu,moyo wangu unaugua sana juu ya maisha yako,moyo wangu unajeruhika kuhusu maisha yako,najua sitakiwi kuzungumza chochote kwa habari ya maisha yako lakini mara zote nimekuwa nikimwambia mume wangu Rojas kila ninapomtizama usoni nikipata nafasi simuoni Rojas katika macho yake,simuoni Rojas hata nikimtazama naona mtu mwingine na sio Rojas" mimi nikacheka na nikamwambia "kwanini unasema hivyo shemeji yangu,kwanini useme hivyo? Akasema "ni kweli,samahani kwa kukwambia haya pengine nakosea lakini Rojas umebadilika sana na mabadiliko yako sio mazuri sana" wakati ananielezea haya maneno hasira zikawa zinajijenga kichwani mwangu na kujiuliza huyu ananifatilia maisha yangu kama nani.

Unajua ukiwa na pesa kuna watu wakiongea unakuwa unawaona kama sijui wanaongea nini au waongee haraka haraka amalize na unaona kama anakupotezea muda ndio mimi kwa huyu mama nilikuwa nataka kusikia haraka haraka kwa sababu mume wake kanitoa sehemu napata moja mbili nimfanya heshima nimekuja huku alafu huyu mtu anakuja kama kunisema,kama maonyo flani alafu yeye kama nani kwangu yaani ila nikajitahidi kujicontrow hasira zangu,akanambia "nimemwambia mume wangu na mimi nakuambia wewe unahitaji msaada na msaada unaohitaji wewe ni msaada wa kumruhusu Mungu aingilie kati kwenye pesa zako,pesa zako zinamhitaji Mungu Rojas,pasipo Mungu utajiri wote si kitu maana utajiri huo utakupeleka kaburini mapema kabla ya wakati,Mungu anataka wewe uishi miaka mingi na mpaka amekupa hizo pesa ina maana ana mpango mzuri sana wakuwasaidia watu ambao ni wahitaji,kuwatia moyo wengine pia na kufanya vitu vikubwa ambapo utaajiri watu zaidi ya mume wangu ambaye umempa ajira kwahiyo Mungu anategemea wewe utafungua miradi mikubwa na hiyo miradi utaajiri watu lakini shetani amedaka pesa zako,amedaka umiliki wa pesa zako,sasa hivi shetani ndio anatumia pesa zako kwa sababu wewe haujamruhusu Mungu yeye ndio atawale hizo pesa zako" maneno haya nayakumbuka mpaka kesho katika safari ya maisha yangu,mpaka kesho na nafikiri ntaendelea kuyakumbuka,nilimuangalia huyu mama na kumwambia "kwanini unaniambia hivyo? Akanambia "kwa sababu nakujua Rojas,nakujua Rojas,najua harakati zako,najua mapambano yako,najua hata changamoto ulipitia kipindi kile ambapo tulilia na kukuombea sana ili usiendelee kubaki kwenye matatizo lakini Mungu leo amekupa pesa na mimi naaminini ni Mungu ndio kakupa pesa lakini pesa leo zimegeuka zimekufanya wewe umekuwa mtumwa,Rojas umekuwa mtumwa,wewe sio Rojas mwenye sifa mbaya,sio Rojas wakuumiza mioyo ya wanawake,wewe ni Rojas mtu mwenye busara tena ni mtu mwenye upendo sana,ni mtu ambaye unajituma sana,ni mtu ambaye ni mfano wa kuigwa,mimi nimekuita kwa sababu nataka tuombe pamoja tumruhusu huyu Mungu atawale pesa zako,unatakiwa uwe unamtolea Mungu,ukimtolea Mungu,Mungu atalinda pesa zako,sasa hii ni elimu pana sana kwa sababu utajiri unalindwa wenzako unaowaona wanamiliki utajiri na utajiri unadumu wana njia zao ambazo wanalinda pesa zao,wengine pesa zao si pesa za kawaida ni pesa za sadaka,wanatolea sadaka pesa zao,utajiri wao sasa wewe umezipata pesa je uko upande gani? Uko upande wa shetani? Mi naamini Rojas hauko upande wa shetani kwa sababu nakujua wewe,nakujua wewe kuwa moyo wako hauko uko kwenye kutumika na mashetani kwa ajili ya kupata pesa,pesa hizi umezipata kwa njia halali Mungu amekupa wewe ndio unajua lakini basi mpendeze Mungu kwa pesa hizi alizokupa,zilinde hizi pesa ili ziendelee kudumu na wewe,unajua kwanini watu uwa wanatajirika alafu wanakuja kufirisika kabisa? Pengine wamesahau sijui wewe katika utajiri wako kwa nafasi ya utandawazi sasa hivi pengine unaweza kupata hiyo nafasi" lakini mimi watu wengi wanajipendekeza kwangu,watu wengi wananiambia mazuri ninayopenda kuyasikia mabaya hawanambii kwa sababu ukinikorofisha wanahisi pengine sitakupa nafasi,ukiniomba kitu labda nitakunyima lakini huyu mama alinieleza haya mambo ambayo sijawahi kuelezwa na mtu.

Tuliongea kwa kirefu pale na yule rafiki pamoja na shemeji yangu na akajaribu kunipa njia tofauti tofauti ya namna gani naweza kutoa sadaka ya shukrani na ya kuweza kupata ulinzi wa Mungu kwa pesa zangu na katika mapendekezo aliyonipa kulikuwa na pendekezo la kuhudumia kituo cha watoto yatima nami bila kusita nikakubaliana na kuamua kubeba jukumu la kukihudumia kituo flani na kwa kuanza siku iliyofuata tukaelekea pale kituoni kuona mazingira yake,mahitaji yake na mengineyo,kiukweli niliumia na hali niliyoikuta pale kituoni na nikaamua mara moja kufanya ukarabati wa miundombinu na pia kuongeza fungu la chakula na mahitaji mengine ya lazima,niliwaunganisha wahusika wa kituo na mhasibu wangu endapo kama kutakuwa na changamoto yoyote basi wanaweza kumtafuta huyo kwa haraka kuweza kukamilisha kwa wakati na tukajumuika na watoto wale mimi,shemeji yangu pamoja na watu kadhaa waliofika na tukapata chakula cha pamoja na watoto walishukuru sana wao na walezi wao kwa ujumla,baada ya zoezi na wenzangu tuliaga na kuahidi muda si mrefu nitafika tena kuja kuwatembelea hawa vijana.


ITAENDELEA!
 
1.John yupo wapi
2.Bosi wa John kwanini hafuatilii juu ya gari yake?
3.Yule binti wa bosi wa John alikatatamaa juu ya rojaz?
4.kule kijijini rojaz aliwapotezea??
5.ni kweli yule abiria aliuwawa? Na je aliuwawa na akina Nani?

Naona kwenye hii stori kivuli Cha John ndio starling wa stori
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha ‘Sitasahau’ cha Radio Free Africa​



Sehemu ya 16



Baada ya kuhasi kwa muda mrefu kwa kutokwenda gerezani kumuona yule ndugu yangu kwani ilishapita miaka miwili na siku kadhaa toka mara ya mwisho niende kumtembelea yule ndugu leo nikaamua kwenda uko kumtembelea,kiukweli moyo wangu ulijaa usaliti sana kwa haya yote ninayoyafanya juu ya huyu ndugu kwani Rojas huyu wa leo asingekuwa Rojas kama sio fadhila za huyu ndugu na nikajiuliza sana hivi amewaacha watu wangapi na hadi kuja kwangu na kunipa yote haya leo ninayotamba nayo,ni huzuni sana!

Nikiwa nimenunua vitu ambavyo niliamini kwa mazingira ya gerezani vinahitajika na nikafika pale na kufanya kama utaratibu wa mtu anayekwenda kumtembelea mfungwa ufanyika na nilipotaja la mfungwa ninayekwenda kumuona nikaelezwa kuwa yule ndugu ameamishwa gereza na nikatajiwa gereza ambalo yupo kwa wakati huu,nikaondoka pale gerezani nikiwa na sononeko kubwa moyoni kwa haya yote ninayomtendea huyu ndugu,hivi ni kweli nimekuwa busy kiasi cha kufikia kusahau chanzo cha huo ubusy wangu kimeletwa na nani? Nilijihisi hatia kuawa ndani yangu na nikajiapiza iwe itakavyokuwa lazima nifike katika hilo gereza alilohamishiwa huyu ndugu mara moja,siku ya pili nikafika uko na kweli nilifanikiwa kumuona,hali yake niliyomkuta nayo iliniumiza sana,sana,sana kwani alikuwa amekuwa dhohofu sana,amepungua mwili,hali ya kukata tamaa ilikuwa inajionesha katika uso wake na machozi yalinidondoka kwa yale yote niliyoyafanya na nikikumbuka maneno yake,matumaini yake kwangu je imekuwaje leo namtenda kinyume mwokozi wangu huyu? Naye alinishangaa kwakuwa nilikuwa nimebadilika sana nimekuwa mnene kwa sababu maisha ambayo nimekuwa nikiishi mimi kwa pesa nilizopata mifumo ilikuwa imebadilika,starehe ambazo nilikuwa nafanya na utumiaji wa vilevi,kupenda kula kula nyama nyama na vyakula tofauti tofauti vyakupendeza machoni pangu vikanifanya kuwa na mwili mkubwa,nikawa na kitambi yaani nimeshiba kweli kweli na nimependeza sana kwahiyo wote tukashangaana lakini nakumbuka sentensi alinambia "nilijua tu,nilijua tu hauwezi kuwa vile vile kama ambavyo nilikuona lakini siwezi kuilaumu nafsi yangu kwa sababu niliyafanya kwa mapenzi mema sana lakini hofu yangu ni hii pesa kukumaliza mapema wewe"

Hii ni sentensi aliyonambia mara tu tulipoanza mazungumzo" nikamwambia "unapenda sana lawama,unajua umekuwa mtu wa kunipa sana msongo wa mawazo kwa sababu ya pesa,sikuwa naishi na msongo wa mawazo nikaona sasa bora nitulie nipunguze kuja ili niishi maisha ya amani kwa sababu kila nikija kuna kitisho kipya unanipa sasa kwanini niishi maisha ya vitisho? Tazama nimekuja tu unaanza kuniattack moja kwa moja kwa maneno ya vitisho,akanambia "haya nakusikiliza maana najua umefunga safari ukaenda pale na ukaambiwa sipo nimehamishwa na ukaja mpaka huku naamini kuna jambo ambalo limekuleta huku" nikamwambia "nimekuja kukuona na pia kukujulisha kuhusu hali ya watoto wako" akasema "ni muda sana na nilishapoteza hata matumaini,mimi ni mtu ambaye nimeshasahaulika kama wewe ndio ulikuwa unakuja na nilibakiza tumaini pekee wewe na wewe tena ukaingia mitini basi nikapoteza tumaini,lakini nafurahi nimekuona na naona sasa umeingia katika muonekano mpya,naona umenenepa sana,pesa zangu zimekunenepesha sana,naona pesa zangu zimekupa kitambi lakini haukutakiwa kutumia hivyo pesa,pesa zina kanuni zake kwani haiwezekani kwa sababu una pesa ukawa una kulakula tu unakulakula tu,unatakiwa unakula na pia unatenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa imara kiafya kwa sababu mwisho wa siku wewe utapata magonjwa na ukipata magonjwa ni hatari kwa sababu unaweza kufa cha ghafla" alinambia maneno hayo sikuyapenda nikachukizwa nayo sana,nikamwambia "kwahiyo ni hayo tu baada ya kutokuonana kwa muda mrefu" akanambia "naweza nikakwambia kipi ambacho kinaweza kukurudisha katika uhalisia ule wa Rojas ninayemfahamu mimi ambaye ni kijana aliyekuja gerezani akiwa amesingiziwa kesi,amekuja akiwa amechoka,ni kijana ambaye hana chochote aliyeshindwa kujipigania ili atoke mapema kwa kesi ndogo iliyokuwa inamkabili lakini akajikuta anakaa mwaka unakaribia lakini leo ni mtu mwingine,leo ni mtu mwingine naona hata kuongea kwako kumebadilika kabisa,ni masikitiko yangu kwa sababu pesa niliyoitafuta kwa bidii yote inaenda kunaliza kijana ambaye familia ilikuwa inamtegemea sana" nikamwambia "tuzungumze mambo mengine,tuzungumze mambo mengine"

Akanambia "nimejua wapi tatizo lilipoanzia" nikamuliza "kwanini unasema hivyo" akasema "kwa sababu uliitoa siri yetu kwa watu na baada ya kuitoa siri yetu watu wamekuharibu kiakili ili wakutumie,ili uwanufaishe na wamefanikiwa kukutumia sana tazama nikikutazama machoni mwako hata sio wewe unayezungumza sasa ni mtu mpya kabisa ambaye amezaliwa ndani yako,utaisingizia pesa ni kweli pesa inabadilisha watu lakini niamini mimi kuwa watu wa karibu wameshaiharibu saikolojia yako wameshakutumbukiza katika mambo ya uovu ili waendelee kujinufaisha na mwisho wa siku watakumaliza,kwani wewe haujaanza kutumia madawa ya kulevya? Nikashtuka na nikamuuliza "kwanini unaniambia hivyo? Akanambia "moja kati ya uteja mbaya kabisa ni huo watu wengi ambao ni wajanja hapa mjini uwafata watu ambao wana uwezo kifedha au wao kama hawawezi kufanikiwa basi watoto wao uwaingiza katika magenge ya madawa ya kulevya maana wanajua pesa za kuchuma mahali zipo basi watu hawa utumika sana kwa sababu arosto uwa zinawasumbuawatajikuta wanamaliza pesa zao zote mpaka wanabaki masikini, lakini ni akina nani wanafanya hayo? Wala si watu wa mbali na wewe,ni walewale unaotoka nao,ni walewale unaowapenda,ni walewale unaokula nao bata,ni walewale ukipata tatizo unawapigia simu kuomba ushauri hawa ndio maadui zako"

Mpaka sasa hivi nikikwambia mengi nimefanya kama kufanya starehe ninao washkaji ambao wameniambia "Rojas unatakiwa upate kitu ambacho unatakiwa ufeel vizuri yaani unajisikia vizuri na gharama hata sio kubwa kwahiyo nimeshaingia katika huo ulimwengu yaani anazungumza hapa kuhusu hilo jambo mimi nimeshajiconnect umo ni katika mazingira hata nikikueleza niliingiaje mpaka kufikia kutumia hivyo vitu sijui hata lakini tu katika mambo ya starehe starehe nikajikuta na mimi nimeingia na wao wananiambia hii ndio the best zaidi kwahiyo nimejikuta pia naweka pesa uko kwa ajili ya kupata hizo feelings ambazo nimeanza kuzipata baada ya kutumia iko kitu kwahiyo mtu huyu anazungumza kana kwamba yuko nje,yaani anavyozungumza kana kwamba anajua hatua zangu,anajua mimi nimefikia wapi yaani anajua mpaka sasa hivi nipo katika mazingira gani kwamba hujaanza kutumia hiki kitu,akanambia "Rojas ukiwa na pesa alafu ukawa mpumbavu pesa zako zitatumika na wajanja wenye akili nyingi mjini,unataka kutajirisha watu,wakati unatajirisha watu huku unaathirisha afya yako,ungekuwa na watoto wakati wewe ni mtu mzima wangekuwa wanatumia mbinu kuwaattack watoto wako ili wajiingize katika hayo magenge,unajua huo mtandao ni mkubwa kiasi gani?

Huo mtandao ni mkubwa kwani leo hii unaweza kuwa hapa Tanzania unafanya biashara zako,unainvest katika vitu vyako wewe hawajakunasa lakini una mtoto wako umempeleka mahali flani,umempeleka nchi flani wao kwa sababu wanajua pesa zinaweza kuchumwa wanaweza kutuma mtu wao,wanaweza wakacreate mtu wao uko watahakikisha anakuwa close na mtoto wako na mwisho wa siku mtoto wako anaingia katika 18 na akishaingia katika 18 basi pesa za wewe zitakuwa zinanyonywa kupitia mtoto wako maana watamuharibu kabisa na mtoto wako hataweza kustahimili bila ya kupata chochote cha kumpa starehe hiyo ambayo itakuwa imeshamuhathiri,wewe unaingia umo katika magenge hayo,mtu ambaye umeishi katika maisha ya umaskini ukiwa mtaani,umehustle hata kupata elfu kumi kwa siku,leo umepata pesa unaenda kuwatajirisha watu?"

Nilisikia maneno yamepenya kabisa yaani yameingia ndani katika moyo wangu na nikajisikia vibaya sana,akanambia "Rojas mimi nakupenda,mimi nakupenda upendo wangu kwako mimi ni mkubwa toka siku nimekupokea kama mdogo wangu gerezani Mungu ni shahidi katika hilo,sijawahi hata siku moja kukutoa katika maisha yangu hata pamoja na wewe kunitelekeza,sijawahi kumshirikisha mtu mwingine siri hii ili aje akufanyie ubaya ili ile pesa mimi niichukue nimpatie mtu mwingine kwa sababu nilikuamini toka siku ya kwanza na wewe Rojas ni mtu mzuri ila umeruhusu watu wabaya wameharibu moyo wako,wameharibu uhalisia wako,wamepanda mapando mabaya ndani yako,Rojas hivi pesa unataka ikuzike,yaani kwakuwa umekuwa tajiri pesa unataka ikuzike yaani unafikiri unaweza kumaliza wanawake wote yaani wanawake wote,kuna wanawake wazuri ajabu yaani unazungumza wanawake wa nchi moja ambayo umeishi labda na hizo umeenda lakini Rojas kuna wanawake wazuri wana muonekano wa kuvutia unaweza kumuangalia muda wote lakini wazuri hawaishi wanazaliwa kila siku,huwezi ukawamaliza wewe ndio utamalizwa" maneno yake yalinichoma sana nikajikuta nasema "sielewi,mimi sielewi nahisi kuchanganyikiwa mimi sielewi (nikitaja jina lake),akanambia "najua,najua Rojas pesa ambavyo zinaweza zikambadilisha mtu hasa watu wabaya wanavyoingia" nikawa mpole sana kwakuwa maneno yalikuwa yamenigusa sana,akanambia "Rojas hata siku moja mimi siwezi kukunyang'anya hizo pesa lakini sio furaha yangu pesa hizi zikuzike mapema hata kabla yangu mimi,natamani uishi,uoe mke sahihi upate familia,familia yako inufaike na mali ambazo umezipata,unataka uishie bila familia?

Nikamwambia "hata sielewi,sielewi,sielewi" akanambia "bado haujachelewa wameshatumia pesa yako sasa hivi inatosha bado haujachelewa waweza kubadilisha njia ambayo ulikuwa unapita na ukaenda katika njia nzuri" nami nikamwambia "kama unajua yote haya kwanini bado unaongea na mimi vizuri,kwanini haujachukia?" Akasema "wewe ni mdogo wangu Rojas,wewe ni mdogo wangu" maneno ambayo yalinigusa sana kweli,kiukweli nimemkosea mtu huyu,ahadi nilizompa sijafanya lakini hajaanza kunifokea na kunisema kwa mabaya ila ameniambia ukweli ili niweze kubadilika na akanambia "sasa hivi niko mbali na mahali uliko lakini unapopata nafasi usiache kuja kunitembelea afya yangu imekuwa dhaifu pengine siku utakuja na ukakuta mimi siko tena" nikamwambia "nini shida,nini shida" akanambia "maradhi tu" nikamwambia "niambie" akaniambia "naumwa sana,naumwa sana,afya yangu imekuwa dhaifu figo yangu moja imefeli kabisa na unajua tuliko huku tupo tu"

Niliguswa sana kwa sababu huyu mtu sikumtembelea muda sikujua hata mapito anayopitia nikajisikia kujihukumu sana katika haya,naikumbuka sana siku hiyo,naikumbuka sana siku hiyo kwa sababu ilizaa jambo jipya katika maisha yangu,inawezekana,inawezekana ni pesa imenibadilisha mimi,inawezekana ni watu wamenibadilisha,inawezekana nimebadilishwa na maneno ya watu ambayo yamekuwa yakipandwa kwangu yaani kile nimekuwa nikikipokea ndani ya moyo wangu kuhusiana na mtu mwenye pesa "mbona unakaakaa tu kama mtu ambaye hauna pesa bwana" labda hayo yamepandwa sana ndani yangu au inawezekana mimi nachezewa,labda nalogwa yaani mbona sijielewi yaani.

Aliendelea kuniambia "Rojas hizi pesa nikikuambia mimi nilipozitoa,nikikwambia pesa hizi nilikozitoa hukutakiwa kutumia hata senti moja kwakuiteketeza tu,Mungu anisamehe,lakini pesa hii ambayo wewe unaiteketeza leo hii ilitakiwa ilipe gharama ya mengi ambayo mimi nilifanya katika nyakati za utafutaji wangu na nilipanga nikiwa uraiani nitayafanya hayo lakini naona mwenzangu umeshindwa,umeshindwa lakini kama nilivyokwambia waweza kurudi katika maisha yako na ukafanya vizuri tu,mimi nakuamini unaweza" nikaachana na mtu huyu na hayo ndio maneno aliyoniambia.

Nilifunga safari na kurudi zangu nyumbani lakini nilikuwa ni mtu niliyeinama moyo wangu umekosa raha kabisa yaani sina raha,nilipigiwa simu na washkaji yaani ukiwa na pesa simu yako inapigiwa zaidi ya mtu asiye na pesa,ukiwa hauna pesa yaweza pita siku nzima haujapigiwa simu lakini mimi napigiwa simu mpaka naamua kuzima,nikifungua meseji nakuta meseji nyingi huyu anaomba hiki,huyu anataka hiki,huyu anataka urafiki,huyu anataka tutoke tena meseji za wanawake ndio nyingi lakini nilijikuta nimekuwa down kabisa,mimi ni mtumiaji wa kilevi sana lakini sikuwa hata na hamu yakusema nitoke nikapate hata kilevi najikuta niko ndani na moyo wangu unaugua sana.

Katika nyakati moyo wangu unaugua sana mke wa rafiji yangu ambaye huyu mama amekuwa akinishauri shauri mambo ambayo sijawahi kuyapokea,alikuwa akiniambia "pesa sio kila kitu katika maisha,waweza kuwa na pesa na ikakugeuza kuwa mtumwa,Mungu anapotawala pesa zako yeye atakupa amani ya moyo,unaweza kuwa na pesa lakini inaweza kukuondolea amani wewe mwenyewe ya moyo" sasa wakati niko katika mazingira kama hayo huyu mama alinipigia simu n huyu mama uwa akipiga simu unikumbusha majukumu ambayo napaswa kufanya katika kile kituo cha watoto yatima(wakati ule nilipoenda kwake alinishauri kutoa sadaka yangu ya shukrani kupitia kituo flani cha watoto yatima nami nikaafiki),nilipokea simu na huyu akanambia "shemeji unaendeleaje? Nikamwambia "naendelea vizuri""nimekukumbuka tu niko hapa nimekaa nikakukumbuka sana nikasema hata nisikie sauti ya shemeji yangu na siku mbili tatu hizi nilikuwa nasikia mzigo ndani yangu na najisikia kukuombea na sijui unaendeleaje" nikamwambia "naendelea vizuri" huyu mama akanambia "Rojas sadaka zako ambazo umekuwa ukitoa kwa yatima,sadaka zako ambazo umekuwa ukitoa kwa wahitaji tangu umeanza kutoa kwa moyo wako wa dhati kwa uaminifu naomba nikwambie umewaponya watu hawa kwenye mengi wanakuombea kila siku na wana ratiba za ibada na kwenye kila ibada zao wanataja jina lako Mungu akukumbuke katika kila jambo,naamini maombi ya wahitaji hawa,wasiojiweza yatima hawa Mungu atakugusa nawewe pia" sikuwa na mengi yakusema nikamwambia shemeji "niombee,niombee shemeji yangu" akanambia "ni nini mbona nasikia sauti yako iko down sana?" Nikamwambia "sina hata raha sijui kwanini sina hata amani,sina amani kabisa" akanambia "tunaweza tukaonana tukaongea" nikamwambia "labda twende tena kwa wale watoto,twende tukawatembelee labda tukaarrange tupate nao chakula pamoja" akasema "sawa basi mimi ntafanya hivyo" nikasema "sawa basi utatoa taarifa alafu utamcheki mhasibu na kila kitu aweke sawa.

Yaani nimetoka gerezani amani furaha imekata,yaani nilipokutana na yule kaka ambaye amenipa utajiri kila kitu kimekata,kama ambavyo tulikubaliana na huyu mama kweli nilipata muda na nikaenda kwa watoto hawa ambao nilipoenda kwa mara ya kwanza niliguswa sana na maisha ambayo wanaishi,niliguswa kufanya kitu kwani nimekuwa natumia pesa zangu kwa makahaba,nikitumia pesa zangu kwa starehe mbalimbali nikaona basi nifanye hata kwa ajili ya watu hawa lakini ni huyo mama ndio alinipa mwongozo kama nitakapoweka kwa watu wahitaji kama hawa basi ulinzi utaambatana pamoja na mimi na mimi sifanyi uchawi wowote,yaani mimi ukiniuliya kwa Mungu sipo kwa shetani sipo yaani mimi hizi pesa nimepata yaani sio kwa namna ya nguvu za giza za kishirikina kwamba kuna masharti ya kumwaga damu na nini,hizi pesa nimepata katika mazingira ambayo nilishayaeleza,nilienda kuzichimba mahali nikazimiliki zikawa za kwangu lakini kwa Mungu sipo yaani kwamba na muda nimetenga sijui msikitini,sijui kanisani yaani mimi ijumaa,jumapili ni siku za mishe zangu kama kawaida kwahiyo pesa zangu hakuna kitu ambacho kinakipa ulinzi na huyu mama ni moja ya kitu ambacho aliniambia "hayo ni maisha mabaya na hatari sana lazima uchague kati ya sehemu mbili ukiwa vuguvugu utapigwa,utaangamizwa" mengi aliniambia huyu mama kwahiyo tumekuja huku nilipata faraja,watoto hawa wanaimba kwahiyo tuliimba,tukapata chakula nikajikuta kama napata relief napata unafuu ndani yangu baada ya kukaa na hawa watoto kwa muda na nilikaa nao sana kwa muda mrefu na shemeji ameona jinsi nikifurahia maana nilikuwa mnyonge lakini nikafurahia kupata chakula na mengi yaliyofanyika pale na nikatoa ofa nikasema "na kitu kingine ambacho kitahitajika mimi hii ni familia yangu mimi niko na nyinyi kuhakikisha hii safari tunafika pamoja" kwahiyo nikajisikia kufanya vitu vingi nikiwa hapa lakini nilipata unafuu mkubwa na hata nilipata nafasi ya kuongea na shemeji nikamwambia "shemeji nasikia angalau nasikia kama moyo umetulia kidogo" akanambia "nini shemeji yangu,nini kinausonga moyo wako,nini kinakukosesha raha mimi niko hapa na mimi ni mtu sahihi sana kwako unajua nishirikishe hata kidogo" nikamwambia "ni mambo mengi,ni mambo mengi sana shemeji yangu,nakosa hata wapi nianze,wapi nianze kuzungumza na hata kinywa changu ni kizito kuweza kuzungumza" akanambia "sawa shemeji yangu kwani unaweza kuona ni ngumu kuzungumza na mwanadamu mwenzako lakini Rojas shemeji yangu yuko Mungu waweza kuzungumza nae,Mungu ni wa sisi sote haijalishi una dhambi kiasi gani,haijalishi watu wanakuona haustahili kwa kiasi gani lakini Mungu wetu ni Mungu wa rehema unapokwenda mbele zake na kumwambia Mungu mimi wewe ni baba yangu sina mwingine naweza nikazungumza nae,nimekuja mbele zako sikia haya ambayo yamejaa kwenye moyo wangu tamka kwa kinywa chako Mungu anasikia na Mungu atakupa majibu,unaweza kufanya hilo zoezi kuanzia leo unapofika nyumbani kabla ya kwenda kulala zungumza hayo maneno mwambie Mungu unanisikia uko karibu na mimi zaidi kuliko akili yangu inawaza hata hapa uko na mimi,mwambie Mungu vile unasikia moyoni mwako atakupa majibu" alirudia kunambia maneno hayo mara mbili na nilimwambia "sawa" na hakunilazimisha niseme kilicho ndani yangu kwa sababu nilimwambia mdomo wangu ni mzito akanambia "nenda kamwambie Mungu,usijihesabie kuwa wewe ni mchafu usiyestahili mbele ya Mungu,Mungu pia anawahitaji walio wachafu,anawahitaji pia na anawasikia pia"

Sina utaratibu wowote katika maisha yangu wa kuwa na muda kusema nitenge japo dakika ngapi niseme na Mungu ambaye simuoni yaani mimi naamini Mungu yupo lakini ule muda wa kutenga kuanza kujieleza yaani kwa njia hiyo ya maombi sasa hapo kwangu imekuwa ni kazi kweli kweli lakini kukosa amani na mashauri ambayo nilipewa na shemeji yangu niliona angalau nitoe hata dakika mbili nitoe labda naweza hata kupata nafuu,kuna vitu huwezi kuongea na mtu kwa sababu huwezi amini katika starehe zote ambazo nimefanya sijatoa siri zaidi ya kumueleza kaka,hakuna mtu anajua vingi zaidi,kijiji nilichoenda na mengi zaidi sijayazungumza haya,ndipo nilipopata muda wa dakika chache kusema na Mungu.




ITAENDELEA!
 
Huu mkasa umenikumbusha movie ya prison break, nimemkumbuka mfungwa mmoja John Abruuz(Mbabe gerezan na alikua na crew zake ndani gerezani za kibabe na nje ya gereza alikua na crew za kibabe ,,(business man)) na upande wa pili ni mfungwa wa muda mrefu dp cooper(Tajiri,humble down to earth,lakin pia mafia wa kichinichini, ukiingia kwenye anga zake kindez[emoji38]) ambaye alikuwa na hela ndefu sana, alizozichimbia mji fulan uraiani , kabla ya kuingia gerezani ,hivyo crew ya kina scolfied lilimuunga John Abruuz kwny mpango(msafara) wao wa kutoroka coz ndo aliepewa mchongo na db cooper,yaan aliujua mji zilipo hela na zilipochimbiwa,na alikua na raman,pia alikua na access ya kuagiza watu wake nje walete helikopta nje karibu na gereza usiku ,ili waitumie ku escape from the prison, ili iwe easy kuwachenga polisi japo walichemka, helikopta iliwaacha baada ya wao kuchelewa kufika eneo la tukio kwa sababu ya obstacles walizokua wakizipata wakati wa kutoroka zikala muda wao waliohadiana na watu wa helikopta,coz ile wanakimbilia helikopta na polisi hao nyuma yao,watu wa helikopta wakawa washasepa,wacha wakimbizwe na mijibwa ya polisi pori kwa pori,ndimi njee,daah, polisi nao nyuma yao full armed,, hivyo walivyotoroka gerezani scolfied na wenzie , moja kwa moja walikuwa wanazifata zile pesa,siunajua tena mtu akitoroka jela hana mishe wala nini, uhuru zero,kuishi kwa mashaka,pesa ndio kila kitu na ukizingatia kaka scolfied alikuwa na msala mkubwa,unaohitaji pesa kujificha na kuufanyia research kesi yake na kupata solutions,lakini bahat mbaya mfungwa mwenzao(walotoroka nae) mtukutu TBAG(alikua selfish Sana huyu jamaa) ,akaisoma Raman chap walipokua karibu na mji wenye ambao ndio tajiri dp cooper kafukia pesa zake ndani ya nyumba flan,baada ya kuisoma Raman chap kaimeza ili wenzie wasijue ni wap,akakimbia kwenda kufukua mwnyww ,alizifaid hela kidogo mtaan,kabla hajadabwa,ila kuna mahali alijikata mkono wake mwenyewe wenye pingu ,na kukimbia bila mkono kisa kuwakimbia polisi, very interesting story ,sema movie nimeona Zaman kidogo ,najaribu kuvuta kumbukumbu za kurelate na hii story. .wadau mnaoikumbuka hii movie mtanikosoa ni kitambo sana , naweza kuwa nimechanganya hapo kwenye mchongo wa hela ya dp cooper km alipewa scolfied basi John Abruuz alikua kwa ajili ya kufanikisha helikopta kufika eneo husika siku ya tukio. .anyways kumbe hayo mambo yanatokea kweli kwny jamii na si kwny movies tu.
Mzee mwenye hela ndani anaitwa dB cooper, na t_bag hakujikata,ila alijua jamaa watamuacha so ikabidi ajifunge pingu na michael, wakati wa kutoroka walimtumia John kupata ndege sio helicopter.

Ila kwenye season ya kwanza michael mwenyewe alimvuliaga kofia Alex mahone,nae alikuwa kichwa sana.
 
Mzee mwenye hela ndani anaitwa dB cooper, na t_bag hakujikata,ila alijua jamaa watamuacha so ikabidi ajifunge pingu na michael, wakati wa kutoroka walimtumia John kupata ndege sio helicopter.

Ila kwenye season ya kwanza michael mwenyewe alimvuliaga kofia Alex mahone,nae alikuwa kichwa sana.
Ww unaongelea kipindi wanatoroka ila huyo TBag alijikata mkono
 
Maisha ni fumbo kubwa sana,imagine jamaa alitakiwa aende jela ili akakutane na jamaa wa kumpa utajiri..so far nimejifunza yafuatayo..

1.maisha ni fumbo,kufanikiwa au kufeli ni siri.
2.Uaminifu ni silaha kubwa sana maishani.
3 Mungu akitaka kukupa lazima upitie shida,kiasi unaweza kuhisi kakuacha,kumbe yupo hapo hapo ulipo.
4.Wema ni akiba.
5.Mungu yupo.
Hapa ndo tunaungana na waliosema

"Everything happens for a reason"

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Story nzuri... Pesa zinabadilisha sana zisikie tu na bora pesa za kazi au shughuli Fulani rasmi... Ila less za deal na miujiza weeee zinabadilisha sana usiombe ninaexperience na mil 12 tu sio safi.
 
Back
Top Bottom