shikamkono01
JF-Expert Member
- Mar 26, 2016
- 685
- 2,055
- Thread starter
- #481
Ishi sana mwanangu Fei na i dedicate to u FEI song by Fid Q!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ishi sana mwanangu Fei na i dedicate to u FEI song by Fid Q!
Kuna nyingie naiandaa cuzo ni MOTO nipo katika kuisikiliza kwanza then niianze mdogo mdogoKwenda kwa mganga fake kuliharibu kila kitu kikubwa kumrudia Mungu
Asante sana shikamkono ukipata story nyingine tuletee barikiwa sanaa
Tubarikiwe sote ndugu yangublessed humble Man, ubarikiwe hadi ushangae
Hata Yesu walimkataa itakua story?ulitaka ukajibie mtihani wa necta?Hii stori ni nzuri ila inaonyesha si stori yenye uhalisia Bali ni hadithi iliyotungwa vizuri. Iweje hao jamaa walipomkamata bwana Rojaz wamwache aende kirahisi hivyo Tena Kwa kumpiga ngumi mbili tu na kukanyagwa mgongoni ilihali waliyekuwa wanamtafuta hawajampata? Kuna vingi vinaonyesha ni fabric ila Hilo ni mojawapo. Baada ya kusoma hizo sehemu 2 basi imenitosha
Kulikoni Tena mbona makasiriko!?Hata Yesu walimkataa itakua story?ulitaka ukajibie mtihani wa necta?
Boss asante tag haijanipa notification kumwa mwamba amenipa link kwenye uzi fulani hivi ndio nikaja kusoma.Karibuni wapendwa story.
,Antonnia ,Bantu Lady ,Kalpana ,Gily ,kaburungu ,Kibunango ,Lastmost ,wao ni wao ,Mpetde ,Santos06 ,To yeye ,niachiemimi ,JBourne59 ,harakati za siri ,Aaliyyah ,Lovelovie ,Semere92 ,mludego ,mwonge ,Smart AJ ,Mwana ,Mwanga Mkali ,sumbai Zeus1, Rashidi Jololo ,barakalyimo ,Iceberg9 ,ERoni ,Dahan ,Mwananchi B ,Watu8 ,liwaya ,Ushimen ,madindigwa ,The email ,Gamaha ,IBRA wa PILI ,Kaka yake ,shetaniKoffi Annan[/USERmacho_mdilikopremji canoonhamachoachila ceez
na ukubwa wa yale matranka na idadi yake kiukweli hofu ilinivaa sana,nayatoaje haya hadi kuweza kuyafikisha mjini? Inaonekana huu
Mkuu umetisha sana,barikiwa sana kwa kutoa muda wako kuandika kisa kirefu namna hii. Hakika unastahili tuzoSHUKRANI SANA:
Ndugu zangu nawashukuru nyote kwa kutumia muda wenu kusoma mkasa huu wa Rojas na hapa ndio hitimisho lake,tukutane tena katika mkasa mwingine siku nyingine kwani haikuwa jambo rahisi ukizingatia kutoa maneno katika mfumo wa sauti kuleta katika mfumo wa maandishi kulileta changamoto kidogo ili kuweza kuifanya hadithi ibaki na mvuto wake ule ule,kuna baadhi ya maeneo ilinilazimu kuongeza nyama ili kuweza kuleta muunganiko kwani upande wa audio kulikuwa ama kukatikakatika,kukosekana kipande kirefu au episode kutosikika kwa zaidi ya dakika 10 hapo ikanibidi nijiongeze.
Mkasa huu umenipa mzuka wa kufanya kazi nyingine na nyingine na kama kuna mtu kati yetu anakifahamu kisa chochote kilicho katika mfumo wa sauti na akapendezwa tukilete jukwaani asiwe mchoyo aniPM nami ntatimiza wajibu wangu kama mwana jukwaa,mbarikiwe sana!
Nimepata hasira kuna mijitu ina wivu na roho mbaya sana. Kaka mtu kashapata tamaa ya pesa.Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
Sehemu ya 11
Moyo wangu unatunza siri na moja kati ya vitu nilimuahidi huyu kaka kule gerezani ni kuhusiana na kutunza siri,niliifanya siri hii kuwa ya sisi wawili peke yetu na yeye akiniambia "nimekupa siri ya maisha yangu sijawahi kumpa mtu yoyote hii siri mahali nimetunza pesa sikuwahi kumwambia mtu na ndio maana kile kijumba watu hupita na pengine wengine uenda kufanya shughuli zao uko na hawajawahi kujua chini ya ardhi ziko pesa nyingi,mimi nikamuahidi ya kwamba nitaitunza siri hii lakini kaka amezungumza nami katika lugha ya urafikiya undugu kabisa,nasikia moyoni mwangu angalau niweze kusema nae jambo,nikamwambia kaka "kuna vitu ni vigumu sana hata kusema,naogopa hata kusema" kaka akanambia "ni kitu gani mdogo wangu kama ni cha hatari niko tayari hata mimi kuingia kukusaidia sitamani kukuona unapata matatizo,unajua" nikamwambia "kaka najua" nikaketi na kaka na nikamwambia "hii ni siri,ni siri ambayo sijawahi kutaka kumwambia mtu yoyote yule" kaka akanambia "hata mimi ntaifanya kuwa siri kwa sababu wewe mdogo wangu umetaka iwe siri,niambie" ndipo nilipoanza kumwambia kaka ila nilimwambia kwa uchache sikumueleza kwa upana kama safari ya huyo mtu na mimi ilipoanzia,nilimwambia "kaka ni kweli nina pesa,unaona nafanya maendeleo haya unaona ninavyoagiza magari,unaona jinsi nimefungua biashara yaani kufungua duka la jumla na nimeweka pale kiasi cha milioni ishirini,ni kweli nina pesa lakini kaka hizo pesa si zangu,ni pesa za mtu na huyo mtu amekuwa anatamani kufanya makubwa sana lakini yeye amekosa hiyo bahati ya kuishi maisha ambayo mimi naishi ya uhuru" kaka anakanambia "una maanisha nini,ni nini ambacho unamaanisha? Ni mtu gani ambaye kakosa uhuru,ni vitu gani unazungumza,nikamwambia "kuna mtu amenipa majukumu ya kumfanyia vitu vyake kwakuwa yeye hawezi kufanya hivyo" akanambia "ni nani huyo na kiasi gani cha pesa akupe hata uweze kuagiza magari mengi kiasi hiki na hizo pesa unaweka wapi mwisho wa siku uweze utahatarisha maisha yako na hizo pesa unazijua amezitoa wapi? Kaka alinihoji kwa kuonesha kunijali sana na ni kweli kaka ananijali sana,nikamwambia "mtu huyu yuko gerezani kaka" kaka akashangaa sana "yupo gerezani? Sasa mtu yupo gerezani anawezaje kukupa wewe pesa? Nikamwambia "kaka ni stori ndefu sana ila elewa niko na pesa ila si za kwangu,mtu huyo yuko gerezani anatumikia kifungo na ameniomba nimsaidie kufanya hivi vitu nikiwa uraiani,kwahiyo nimechukua majukumu yake nafanya vitu ambavyo yeye alitamani kuvifanya ili siku moja akitoka gerezani aone hatua ameshaipiga kuliko pesa kuendelea kukaa sehemu bila kuzalishwa" nakumbuka kaka alinambia "kwahiyo umekaa chini na kunitungia kastori,umenitungia kasimulizi kakusadikika flani hivi,iko kitu kinawezekanaje? Hakuna kitu kama iko unanidanganya" nikamwambia "kaka nilihisi hata nikikwambia hautaweza kuniamini" akanambia "ni nani uko gerezani,ni nani ambaye awe na pesa hizi akupe wewe,hana ndugu? Hana watu wa karibu akupe wewe?
Nikamwambia "kaka huyu ni mtu ambaye yuko gerezani ana muda kidogo lakini ndugu zake walimtelekeza uko gerezani,hakuna watu wamekuwa wakienda kumwangalia hata kumtia moyo,hakumuona mv wa kumpa hilo jukumu,kipindi mimi naenda gerezani na nikaanza kuwa na urafiki naye ndio kipindi aliniamini nakuniona ni mtu mwema na akaniomba kama naweza kuwa mwaminifu kwake,ndicho kaka kilichotokea" kaka akaniuliza "ndio mwenye wale watoto uliokuwa ukijipa stress? Nikamwambia "ndio kaka" kaka akaanza kuamini katika nnachokisema baada ya kuendelea kumwambia lakini kaka aliyashangaa sana haya maelezo ambayo mimi namwambia nakumbuka sikutaka kumuweka kaka kiundani zaidi niliongea hayo tu kwa uchache,aliniuliza "pesa ziko wapi? Nikamwambia "kaka siwezi kukwambia" akasema "mimi ni kaka yako" nikamwambia "kaka naweza kukwambia vyote lakini nilimwambia mtu huyo sitasema kwa sababu ni maelekezo yake aliyonipa,kama nilivyokwambia kaka hizi pesa si za kwangu ila yeye aliniruhusu nifungue duka,lile duka la nafaka ni la kwangu lakini kuhusu magari sio ya kwangu,hivi vitu vingi sio vya kwangu"
Nilimueleza kaka yangu kwa upendo kabisa kwa sababu huyu ni kaka yangu na niko nae karibu sana katika mahangaiko yangu,katika mateso yangu kwa mfano kipindi kile nimekwenda gerezani ni kaka ndio alinipigania mpaka hatua ya mwisho akunyamaza,hakutulia mpaka alipoona mimi mdogo wake nimeachiwa huru kwahiyo yupo na mimi siku zote kwahiyo naamini nimemwambia kaka yangu naamini nimemwambia mtu sahihi,nilishea na kaka hayo na kaka alizidi kuniuliza maswali lakini sikujibu yote kwa sababu sikutaka kuzungumza kila kitu,aliniuliza "sasa ulipataje hizo pesa,alizihifadhi wapi?" Hayo yote aliniuliza lakini sikusema.
Baada ya kumwambia kaka hayo maneno nakumbuka niliporejea nyumbani nilisikia moyo wangu unauma sana,nilisikia moyo wangu unapatwa na uchungu kwanini nimesema,nilijilaumu kwanini kinywa changu kimezungumza siri ambayo nimeitunza kwa ahadi kuwa nitaitunza na sitaisema,mbona naumia hivi nami naona nimemwambia mtu sahihi,mbona nimemueleza kaka yangu kwanini nasikia hivi vibaya? Sikulala mpaka asubuhi,ushawahi kufanya jambo alafu ukawa unajilaumu kwanini unafanya? Mimi nilisikia hatia ndani yangu kwanini nimemwambia kaka,kama ningenyamaza kwani nini kingetokea,angenifanya nini? Niliona nimekosea,sikutakiwj kufanya hivyo.
Lakini unajua neno linapotamkwa linakuwa lishatamkwa unakuwa hauna namna yoyote yakuweza kulifuta tayari linakuwa lishatamkwa,nakumbuka kulipopambazuka na siku mpya kuingia kaka alinitumia meseji ikisema Rojas nataka tuongee,naomba nije nyumbani kwako tuzungumze,nilikuwa na ratiba za mishe zangu za hapa na pale lakini kaka yangu namheshimu sana na kama anasema ana jambo anataka kuja nyumbani litakuwa ni muhimu sana,nikamwambia kaka sawa na kaka alikuja nyumbani akanambia "mdogo wangu sijalala usiku kwa maneno uliyoniambia nimekosa usingizi,sijajua uko katika hatari kwa kiasi gani sijui lakini tu kwa experience yangu ya maisha,kwa maisha mimi nimeishi,mimi ni kaka yako najua vitu vingi,napata mashaka sana,nasikia kukosa amani sana kuhusiana na kile umenieleza jana lakini kuna kitu nimesikia amani nacho ndani ya moyo kwa sababu umesema huyo mtu yuko gerezani na hajawahi kumwambia mtu yoyote kuhusiana na hizo pesa,sasa mdogo wangu mimi najambo nataka kukwambia,mtu yupo gerezani na pesa unazo wewe uraiani unajua anatoka lini? Sikujua kaka kwanini ananiuliza maswali kama haya tena akiwa siriasi kweli amefunga safari tuje tuzungumze kuhusiana na hili na nikamwambia "kaka, sijui labda kuna neema itakuja ya yeye kutoka au pengine hiyo neema isipotokea uenda maisha yake yote akamaliza gerezani" "kwani amefungwa kifungo cha maisha? Nikamwambia "kaka kesi ya huyo mtu ilikuwa ngumu sana kwa maelezo ambayo nimepata,alinambia ni miaka 30 lakini nikaja nikagundua yule mtu amefungwa maisha" akasema "amewezaje kukudanganya wakati ni rahisi tu kujua miaka ya mtu" nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "mimi naweza kuifanya hiyo kazi nikajua miaka yake ambayo anatumikia uko gerezani,yaani tujue miaka yake ni mingapi,ni wa kutoka au siwakutoka kwa sababu hapo tupate uhakika" sasa nikawa najiuliza kwanini kaka azungumze hivyo,nikamwambia "yanini kuyajua hayo kwa sababu mimi nimemshauri kitu kwa sababu anazo pesa nyingi alizitafuta katika nafasi yake akiwa uraiani na pesa inanguvu nami nilimshauri ikiwezekana sehemu ya pesa yake ebu atumie uenda akaupata uhuru kwa nguvu akarudi huku uraiani kama ni rushwa au namna yoyote ile itakavyowezekana" nakumbuka kaka akanambia "wewe umshauri maneno kama hayo kwanini? Nikamwambia "kaka ni mtu mwema tu" akanambia "unajua hizi pesa amezitoa wapi? Nikamwambia "hajawahi kunieleza wapi alipozitoa" akanambia "hawa ndio watakuwa watu ambao ni wahujumu uchumi" nikamwambia "unamaanisha nini? Akanambia "kuna watu ambao walijilimbikizia pesa lakini kuna nyakati kuna msako uwa unapita na watu uhofia kuhusiana na hizo pesa kwa sababu hawaziweki benki wanaogopa,watu wengi kumekuwa na historia walikuwa wakichimbia pesa ardhini,vipi hizi pesa hakukwambia ukazichukue ardhini?
Nikashtuka,nikamwambia "kaka kwanini tunazungumza haya na wakati tulishazungumza jana na tumeshamaliza kwa sababu niliona nikushirikishe kaka yangu" akasema "ah umenishirikisha ila wewe bado mdogo hujui vitu vingi mimi ni kaka yako,sasa mimi ni kaka yako mimi najua maisha na najua vitu vingi,unajua ni kwanini huyu mtu kakutafuta wewe? Kwanini uwe wewe ushawahi kujiuliza? Hana watu ambao ameshawahi kufanya nao dili? Hawapo? Kwanini iwe wewe? Unajua kwanini? Nikamwambia "ndio najua" akaniuliza "unajua nini? Nikamwambia "najua kwakuwa tulikuwa marafiki,tuliishi kwa furaha na akaona mimi ni mtu ambaye sina shida yoyote" akasema "sio kweli,iko sababu nyuma ya huyo mtu kukutafuta wewe" sasa mimi kweli uenda kaka yangu ana upeo mpana na akili nyingi kuliko mimi siwezi kataa,sasa mimi namuuliza kaka "kwa sababu zipi? Anasema "si unaona hujajua kwanini akutafute wewe,ngoja nikwambie mdogo wangu mitego ya pesa ni mikubwa sana,waweza pesa itumia leo pesa isiyo halali inaweza ikakuletea shida hata baada ya miaka 10 baadae inaweza ikakuhukumu,ikawa kitanzi kwako,ikatesa moyo wako na maisha yako na ndugu zako" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "pesa hiyo siyo halali,hiyo pesa ni pesa haramu na amefanya hivyo ili siku hukumu ikija ikukute wewe na yeye akiwa pembeni ametulia" nikamwambia "sasa litampata vipi mtu aliye gerezani" nakumbuka kaka akanambia "ndio maana nakwambia wewe bado mdogo,uelewa wako bado mdogo haujajua kuchanganua mambo,usalama wako Rojas ni kukata kila connection ya wewe na huyo mtu wa gerezani na kukata connection na majukumu yote aliyokupatia na hizi pesa zisiwe chini yake,ziwe ni pesa zako sijui kama unanielewa? Kaka alinambia maneno hayo tena ni siku ya pili tu yaani nimemwambia jana na leo ananiamkia asubuhi kumepambazuka kaka anakuja na ujumbe kama huu,nikamwambia "kaka mimi Rojas siwezi kufanya kitu kama hicho,siwezi kufanya kama hivyo,siwezi kutumia pesa isiyo ya kwangu kuifanya ya kwangu siwezi,siwezi kaka kufanya hivyo,ahadi niliyompa mtu huyu nitaitimiza siku zote siwezi kuikengeuka hata kiku kimoja maana nimetafuta pesa katika nyakati zote sikuwahi kupata kwanini nimsaliti mtu ambaye amekuwa mwaminifu kwangu ambaye ameamua kunitunuku na kunitoa katika umaskini nakunipa maisha mengine,kwanini kaka unazungumza maisha ya ushetani hivyo" nakumbuka kaka akacheka na akasema "ushetani? Mdogo wangu kweli hauyajui maisha? Nazungumza mambo ya maana wewe unasema ushetani mimi nazungumza ushetani?" Kiukweli sikupenda kabisa kauli za kaka kabisa na nikamwambia "ndio maana moyo wangu umekosa amani kabisa kukushirikisha,hukustahili kunambia maneno haya tena ikiwa mapema kama hivi" akanambia "nakwambia mapema kwakuwa wewe hujui,wewe bado mdogo hujui kadri unavyozidi kwenda gerezani,wewe si kila siku uwa unaenda gerezani mwisho wa siku utastukiwa,huyu mtu bado anafatiliwa kule gerezani usihisi watu wametulia kumfatilia nisikilize mimi ninachosema" kaka akanambia "huyu ni mhujumu uchumi hawezi kukwambia na mimi ndio nakwambia sasa kwa sababu najua haya mambo ziko nyakati hata wewe ulikuwa bado mdogo kuna watu walifanya hujuma,walihujumu uchumi hawa watu walifanya namna nyingi hawajaacha kufatilia siku mpaka anapokufa ndio huyo mtu ndio wanaacha hivi ninakwambia we si uwa unaenda si una route za kwenda? Unavyoenda watu wameshachora ramani,kuna mtu ana dot dot alikuwa gerezani ametoka lakini anaendeleza ukaribu na huyu mtu,mdogo wangu sasa hivi unakamatwa,unakamatwa na unaniingiza kwenye matatizo kata hiyo connection haraka sana usiende gerezani unakamatwa na ninavyozungumza hivi na pengine si siku nyingi kutoka leo na umezungumza kwangu kwa sababu Mungu hataki upate matatizo"
Kaka anaendelea kunambia vitu yaani mimi naenda gerezani kila siku sikuwahi kuwaza hata siku moja kuwa hizi route za kwenda gerezani ninazofanya labda zinaweza zikawa na ishara yoyote lakini kaka anasema huyu mtu bado yuko kwenye uangalizi kwani amehukumiwa lakini haimaanishi kwamba ameachiwa,huyu bado anafatiliwa yuko kwenye uangalizi.
Toka kaka amezungumza siku ile alinipa hofu,nilianza kuwa nahofu moyoni mwangu kwa maneno kaka aliyoniambia,nakumbuka kama baada ya siku mbili toka siku zile tumezungumza na nikamkatalia kaka akaja na akanambia kitu cha ajabu sana,mimi nilizungumza na kaka na sikuwa nimemtaja mtu kwa majina yake ambaye ndiye yuko gerezani,ambaye ndiye amenipa hili dili na mimi nafanya hivi katika mazingira na sikumuweka kaka kiuwazi sana,kaka alinijia na jina kamili,jina kamili la yule ndugu kule gerezani[emoji23] na akanambia alikuwa gereza flani na akapelekwa gereza flani,yaani amemjua sasa kuliko hata mimi,kuliko mimi ambaye nafanya nae kazi katika mfumo ambao nimekuambia na akanambia uwa naenda gerezani mara ngapi (akanipa idadi),niliogopa sana na nikamuuliza "kaka umeyajuaje yote haya" akasema "nimejua kwakuwa mimi ni mkubwa kwako,mimi ni kaka yako,najua mambo kuliko wewe,hivi unajua kuna watu pale gerezani kila unapoenda kumtembelea uwa wanarekodi? Unajua wewe mpaka sasa hivi inawezekana umeshaanza kufatiliwa mpaka unavyoondoka asubuhi mpaka jioni shughuli zako unavyofanya na watu unaoongea nao,unajua iko kitu?" Niliogopa sana na kaka akasema "uko unatazamwa mdogo wangu,watu wanakufatilia" nikamuuliza "kaka umejuaje,umeyajuaje haya?" Kwa sababu kaka yangu ni mtu wa kawaida tu,ni mtu wa kawaida kusema amjue hadi mfungwa hivyo mimi nilivyomueleza hadi apate connection na kujua mimi nilienda siku flani na siku flani huyo ni mtu wa namna gani,si unaona unaogopa,unajua hii sentensi ninayokwambia maana yake nini,maana yake yule mtu ni kweli siku zimepita ila bado anaendelea kufatiliwa na amemtafuta mtu mdhaifu mdogo ili isiwe rahisi mtu yoyote kujua lakini mambo yashajulikana,unajua uko katika hatari kwa kiasi gani? Unajua?
Niko hapa kaka yako nataka nikusaidie,nataka nikusaidie,utapata matatizo upigwe kifungo cha maisha,kwanini hajatumia ndugu zake,kwanini akutumie wewe? Maneno ya kaka yalizidi kuniogopesha na labda kutokana na umri wangu sielewi lakini niliogopa,naogopa kwenda gerezani,sitaki kwenda tena uko.
ITAENDELEA!
Naomba unitumie audio mkuuSHUKRANI SANA:
Ndugu zangu nawashukuru nyote kwa kutumia muda wenu kusoma mkasa huu wa Rojas na hapa ndio hitimisho lake,tukutane tena katika mkasa mwingine siku nyingine kwani haikuwa jambo rahisi ukizingatia kutoa maneno katika mfumo wa sauti kuleta katika mfumo wa maandishi kulileta changamoto kidogo ili kuweza kuifanya hadithi ibaki na mvuto wake ule ule,kuna baadhi ya maeneo ilinilazimu kuongeza nyama ili kuweza kuleta muunganiko kwani upande wa audio kulikuwa ama kukatikakatika,kukosekana kipande kirefu au episode kutosikika kwa zaidi ya dakika 10 hapo ikanibidi nijiongeze.
Mkasa huu umenipa mzuka wa kufanya kazi nyingine na nyingine na kama kuna mtu kati yetu anakifahamu kisa chochote kilicho katika mfumo wa sauti na akapendezwa tukilete jukwaani asiwe mchoyo aniPM nami ntatimiza wajibu wangu kama mwana jukwaa,mbarikiwe sana!
Tunajaribu nduguMkuu umetisha sana,barikiwa sana kwa kutoa muda wako kuandika kisa kirefu namna hii. Hakika unastahili tuzo
Salute kwako cuzo,ubarikiwe sanaCuzo asante sana na umemaliza, huwa huna longolongo kabisa, barikiwa sana.
Huwezi amini nilipokuwa naisoma, ni kama naisikia sauti ya Rojaz akisimulia na sijawahi isikia.
Imenihuzunisha baadhi ya vipande, mpaka nikawa naogopa kusoma, sababu ya kuumia. Kweli mwisho wa njia ni mzuri kuliko mwanzoni.
Hatimaye Rojaz ana familia na anaishi maisha yake.
Kuna mafunzo mengi sana nimeyapata humu.