Mkasa wa Nabii Ann Wanyoro na vifo vya ajabu vya watu watano kutoka familia moja

Mkasa wa Nabii Ann Wanyoro na vifo vya ajabu vya watu watano kutoka familia moja

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177
Vuta kiti, uketi. Kisha agiza popcorn ya kutosha ukipitia mkasa huu wa ajabu.

Ndani ya siku mbili tu, tarehe 25 na 26 ya mwezi November, miili miwili ya mume na mke iliokotwa sehemu tofauti ikiwa haina uhai na haifai kwa majeraha makubwa. Mume alikuwa ni Paul Magu na mke ni Lydia Wangui.

f94ffbfa269a2673bfe8e8cad872e12b.png

Mume yeye aliokotwa kwenye barabara kubwa huku mke akiokotwa vichakani akiwa na alama za kuungua.

Baada ya miili hii kupatikana, ilibainika watoto watatu wa mume na mke huyu (msichana mmoja na wavulana wawili) hawakuwepo nyumbani na haijulikani wako wapi, achilia mbali kama huko walipo wako hai ama wafu.

Screenshot_20240717-204753.png

Kule nyumbani ilipokuwa inaishi familia hii kubwa, sasa alikuwa amebaki mtu mmoja tu, naye ni mfanyakazi wa ndani, jina lake Magreth Njoki.

Siku nne mbele, tarehe 1 December, baada ya msako mkali wa polisi, mtoto mmoja wa kike alipatikana akiwa amekufa na ametupiwa vichakani kama mama yake. Msako ukaendelea kutafuta watoto wawili waliobakia.

Baada ya siku mbili, tarehe 3 December, Polisi wakishirikiana na ndugu wa familia, waliwapata watoto wakiwa wamekufa na miili yao imetupiwa huko vichakani. Vilevile kama dada na mama yao.

Screenshot_20240717-205608.png

Hapa ndo' taharuki ikazuka. Familia hii ikashika vyombo vya habari. Watu walitaka kujua nini kilichowakumba watu hawa kiasi cha kupukutika wote katika mazingira haya ya kutatanisha?

Screenshot_20240717-205511.png

Mbele ya macho ya watu, familia ya Paul Magu ilikuwa ni familia ya kuigwa kwa wivu mkubwa kwani ni familia tulivu yenye hofu ya Mungu. Familia imara inayojiweza kiuchumi.

Na wivu huu haukuanzia hapa majuzi tu, ulianzia na Paul akiwa masomoni kwani alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora darasani.

Alifaulu vema primary na secondary kisha chuoni akafaulu vema taaluma ya sheria kabla ya kujiunga na Kenya School of Law. Hapo alitoka na marks nzuri zilizomfanya awe wakili ambaye hakuchukua muda mrefu kujipata.

Mwaka 2005, Paul alifunga ndoa na bi. Lydia Wangui wakaweka makazi yao eneo la Pipeline Estate, si mbali sana na barabara kubwa ya Thika.

Screenshot_20240717-201006.png

Haikuchukua muda, familia hii ilibarikiwa mtoto wa kiume aitwaye Allen, kisha mtoto wa pili wa kiume aitwaye Ryan na mtoto wa kike aitwaye Tiffany.

Kwasababu hii, waliona busara kuwa na dada wa kazi wa kuwasaidia majukumu, ndo' wakamleta dada, Magreth Njoki, hapa nyumbani kwa kazi ya kumsaidia Lydia kuangalia watoto.

Maisha yalikuwa ya kawaida kama familia nyingine.

Pengine yapo yalokuwa yanaendelea kwenye familia hii lakini sio kwa kiasi cha kunyooshewa vidole.

Asubuhi ya Jumapili, tarehe 23 November 2014, ndo' mambo yalipoanza kuwa meusi. Mambo yalipoanza kwenda kombo ambayo ilikuja kushtua kila mtu.

Screenshot_20240717-200915.png

Asubuhi hiyo, familia ya Paul Magu walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa kwa pamoja. Baada ya kumaliza, bwana Paul alimuagiza Magreth dukani kununua soda. Magreth alipokwenda na kurejea, alishangaa anaagizwa tena dukani. Mara hii alitumwa akalete unga.

Sababu humu ndani kulikuwa na desturi ya mama kununua vitu, Magreth alitaka kumuuliza Lydia ni unga wa aina gani anunue lakini bwana Paul alimwambia Lydia ashaondoka kwenda kanisani. Hayupo tena nyumbani.

Hivyo alilazimika kwenda kununua unga kwa utashi wake mwenyewe. Baadae akiwa anaendelea na kazi zingine, alisikia watoto wakimuuliza baba yao, mama yuko wapi, baba akajibu ameongozana na mchungaji Ann kwenda kwenye maombi.

Mpaka kufikia usiku, mama hakuwa amerudi nyumbani. Bwana Paul aliwasihi watoto wakalale kwani mama amekawia kurejea ila wasijali, atakuja tu.

Lakini mpaka kufikia kesho yake asubuhi, mama hakurejea bado. Kwenye majira ya saa tatu, Paul alimwambia Magreth awaandae watoto kwani anataka kuwapeleka shopping. Baada ya kufanya hivyo, aliwapakia watoto kwenye gari na kuondoka nao.

Mchana wa siku hiyo, majira ya saa nane, Magreth alishangaa kumwona bwana Paul akirejea nyumbani peke yake asijue watoto kawaacha wapi.

Bwana huyo hakusema kitu. Aliingia chumbani kubadilisha nguo kisha akaondoka tena na gari. Na huo ndo' ulikuwa mwisho wa Magreth kuona mtu yoyote wa familia hii akiwa hai. Si baba, mama wala watoto.

Sababu ya mashaka alokuwa nayo, punde baada ya bwana Paul kuondoka, Magreth alienda chumbani kwa bwana huyo kukagua. Alihisi kuna kitu fulani hakipo sawa.

Chumbani alikuta kila kitu kikiwa safi na nadhifu, lakini alipotazama kwa umakini alibaini kuna madoa ya damu sakafuni na ukutani na pia kuna vipande kadhaa vya mifupa mithili ya meno hapo chini.

Hofu yake ikaongezeka zaidi. Gari la bwana Paul Magu lilienda kukomea kijiji cha nyumbani kwao huko Kiganjo ambapo bwana huyo alipokelewa na baba yake mzazi.

Screenshot_20240717-200856.png

Mama yake alikuwa ametoka siku hiyo kwenda kumtembelea dada yake. Alipofika hapo, na baada tu ya muda mchache, baba yake alitambua mwanae hayuko sawa. Alijaribu kumuuliza shida ni nini, akasema ni njaa tu kwani hajala tangu jana yake asubuhi.

Haikupita muda, Paul aliaga anatoka kidogo atarejea. Alitoka kwa miguu na baada ya masaa alirejea nyumbani akiwa amechafuka kwa vumbi na tope, akasema alivamiwa na wahuni akiwa njiani kurudi.

Baba yake alimuandalia chakula lakini aligoma kabisa kula. Akalala hivyohivyo. Usiku huo, baba anasema alikuwa anamsikia Paul akiongea mwenyewe chumbani kama mtu aliyepagawa.

Kesho yake palipokucha, siku ya tarehe 25 November, ndo' mambo yalizidi kuwa ya ajabu. Baba alimkuta Paul chumbani akiwa amevaa sketi na blauzi ya mama yake!

Jambo hili lilimshtua sana na kumwondolea mashaka yote kuwa Paul hakuwa mzima. Alimwamuru avue nguo hizo mara moja, Paul akabadilisha na kuondoka zake eneo hili pasipo kuaga.

Baba alikata shauri la kumpigia simu mkwe wake, yaani Lydia, kumuuliza nini kinaendelea? Mbona hamwelewi huyu bwana?

Simu haikupatikana. Hivyo akapata mashaka zaidi. Alimpigia kaka yake na Paul, bwana Andrew, ili amweleze mambo ya ndugu yake na kumbe wakati huo Andrew alikuwa ametoka kuiona habari ya kupatikana kwa mwili wa Lydia vichakani kando ya barabara ya Kiambu.

Screenshot_20240717-214028.png

Kwa pamoja walianza kumtafuta bwana Paul bila ya mafanikio, baadae wakatoa taarifa polisi ya kuwa wapotelewa na mwanafamilia mwenzao na kazi ya kumtafuta ikaanza huku na kule.

Kesho yake, tarehe 26 November, polisi walipata habari ya kutokea kwa ajali mbaya maeneo ya Ngoliba, barabara kuu ya Thika na Garissa. Walipofika huko walikuta gari imeegeshwa kando ya barabara huku ikiwa 'on' na dereva hayupo. Gari hii walikuja kulitambua baadae ni mali ya bwana Paul Magu.

Screenshot_20240717-214141.png

Mashuhuda wa ajali walisema, walimwona mtu wa gari hili akitoka na kujirushia barabarani mbele ya lori linalokimbia kwa kasi. Akakanyagwa na kufa papo hapo.

Baada ya hapa ndo' msako wa watoto ulifuata na wao wakaokotwa sehemu tofauti tofauti wakiwa wamekufa kwa vifo vya kutatanisha. Polisi walianza uchunguzi mara moja kujua nini kilichojiri nyuma ya vifo hivi.

Walienda kwenye makazi ya bwana Paul kufanya ukaguzi, ndani ya nyumba yake wakakutana na chumba kimoja chenye mafuta, vitabu, CD na kanda zenye mafundisho ya dini ambayo yalikuwa ni ya ajabu na tofauti.

Magreth, dada wa kazi, alisema chumba hicho kilikuwa kinatumika kama madhabahu ya ibada.

Bwana Paul na familia yake wangeingia humo chumbani kusali aidha wakiwa wenyewe ama wakiongozwa na mama mmoja aliyekuwa anakuja mara kwa mara hapo nyumbani, jina lake Ann Wanyoro.

Sasa Ann Wanyoro ni nani?

Screenshot_20240717-212018.png

Polisi walipochunguza na kuhoji, walibaini mwanamke huyo ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuonana na familia hii kabla ya mtu yeyote hajaanza kupotea.

Tena kwa siku nne mfululizo, Wanyoro alikuwa na familia hii wakiendesha ibada. Baada ya hapo ndo' mambo yalianza kubadilika kuwa majanga. Hii ikawa sababu nzuri kwa polisi kutaka kumjua mwanamke huyu kwa undani zaidi.

Kwa mara ya kwanza bwana Paul alikutana na Ann Wanyoro kwenye kanisa la Faith Evangelistic alikopelekwa kusali na mama yake mzazi. Ilikuwa ni mwaka 2005. Paul alitambulishwa hapo kanisani kama muumini na Ann akatambulishwa kama kiongozi wa kanisa, cheo cha unabii.

Nabii Ann Wanyoro.

Baada ya kusali kwa muda fulani hapo, mama yake Paul alikuja kuhama kanisa akisema aliona mambo fulani hayako sawa na nabii Ann Wanyoro, lakini kwa mwanae Paul, mambo yalikuwa tofauti.

Kadiri muda ulivyoenda, ndivyo alitengeneza ukaribu na nabii. Hata mama yake alipojaribu kumweleza mambo tofauti, hakutaka kusikia. Aliacha kumtembelea mama yake, akakaa naye mbali sana.

Alikuwa ni yeye kanisa, kanisa na yeye. Ndani ya miaka mitano, mwaka 2009 mpaka 2014, Paul alisafiri pamoja na Ann Wanyoro kwa zaidi ya mara ishirini wakienda Nigeria kwenye kanisa la TB Joshua.

fff88d1800ee621b506eb10d1b4d757d.png

Kanisa hilo lilikuwa na 'connection' na kanisa la Ann Wanyoro, Faith Evangelistic Ministry. Huko walipata huduma na 'mafuta ya upako' ambayo walirudi nayo nyumbani kwajili ya kuyatumia kwenye shughuli zao za maombi, ikiwemo kule chumbani kwenye nyumba ya Paul Magu.

Kama haitoshi, Paul alikuja kuacha kazi alokuwa anafanya, akahamishia mawazo yake yote kanisani. Na si mawazo tu, bali pesa yote aliielekezea huko kwenye huduma. Inasemekana alikuwa analipia ada watoto wa Ann na pia alimnunulia gari ya kutembelea nabii huyo.

Lakini kitu kingine cha ziada na cha ajabu, muda mfupi kabla ya kifo chake, bwana Paul alihamisha umiliki wa mali zake nyingi kwenda kwa nabii Ann Wanyoro.

Kwanini alifanya hivi? Na kwanini muda huu? Hamna aliyejua lakini kwa polisi ilitosha kumweka Ann Wanyoro kwenye cheo cha mtuhumiwa mkuu. Wakamkamata na kumtia nguvuni kwa mahojiano.

Screenshot_20240717-211546.png

January 2016, mwanamke huyu alitoka kwa dhamana ya milioni mbili ksh. Baada ya miezi miwili mbele, alipandishwa tena mahakamani na kesi ikasikilizwa.

Magreth, dada wa kazi, alikuwa shahidi wa kwanza. Alisimama kizimbani akasema yote anayoyajua. Alielezea namna gani kwenda na kurudi dukani kulivyomfanya ampoteze Lydia mbele ya macho yake kisha baadae akaenda kukuta damu chumbani.

Wa pili akawa Mama yake na Paul (pichani). Alisimama na kusema yote anayoyafahamu kuhusu Ann Wanyoro na ukaribu wa ajabu wa Ann na marehemu mwanaye.

Screenshot_20240717-200844.png

Wa tatu akawa Baba yake Paul. Alisimama akaeleza hali ya ajabu ya Paul siku ile alipokuja nyumbani.

Wa nne ikawa jeshi la polisi. Maafisa walisimama wakaeleza waliyoyapata kule chumbani kwa Paul Magu. Walibeba CD, Casettes na vitabu vya mafundisho, wakaviwasilisha mbele ya hakimu.

Moja ya kitabu walichokiwasilisha kilikuwa ni 'MURDER MOST FOUL'. Kitabu kinachoongelea mambo ya ibada za damu na mauaji.

Screenshot_20240717-212939_1.jpg

Polisi waliamini huenda bwana Paul alikipitia kitabu hicho kabla ya kutokea kwa vifo vile vya ajabu.

Waliamini pia wakati Magreth alipoagizwa dukani, bwana Paul ndo' alitumia fursa hiyo kumshambulia mkewe huko chumbani kisha akamwingiza kwenye kiroba na kumpakiza kwenye gari kabla ya kesho yake kuondoka naye akiwa pamoja na watoto.

Lakini kwa muda wote huo wa matukio, kwa rekodi ya simu, bwana Paul alikuwa akiwasiliana sana na Ann Wanyoro.

Walikuwa wanaongea nini? Polisi walipata shaka mwanamke huyo atakuwa anahusika na matukio haya ya mauaji aidha direct ama indirect.

Kwa upande wa pili, Ann Wanyoro alisimama kizimbani akakana mashtaka yote akisema ahusiki nayo kwa vyovyote vile. Yeye kazi yake ni ya kiroho. Alitumia taaluma yake kumwongoza Paul na si kumpotosha kama watu wanavyosema.

2f0367a83717e87953730d9a6e8cc033.png

Wakati kesi hii ikiwa inaendelea kusikilizwa, mara kadhaa Ann alikuwa anaomba nafasi afanye maombi, tena muda mwingine baada ya kuulizwa maswali na mawakili. Na muda mwingine alikuwa analipuka kwa ukichaa, akisali na kukemea kwanguvu.

Mpaka muda huu unaposoma hapa ndugu yangu, ni miaka kumi imeshapita. Bado kesi hii inaendelea mahakamani pasipo kutolewa hukumu.

Bado haijulikani kwanini Paul alifanya mauaji na kisha kujiua yeye mwenyewe.

Na bado haijulikani aliyafanya mauaji haya yeye mwenyewe ama alisaidiana na mtu.

Tarehe 10 December 2014, Paul Magu na familia yake nzima walipumzishwa kwenye kaburi moja huko kijiji cha Kimuchu, kaunti ya Kiambu, kwenye msiba ambao ulibeba hisia kali za wanandugu.

  • e6631e9da574c270c3e761b9a26c5a60.png

Na leo hii, ijapo vidole vyetu na vya wanafamilia vinamnyooshea nabii Ann Wanyoro, ushahidi wa kumtia hatiani mwanamke huyu bado haujajitosheleza.
 

Attachments

  • 2e7aaa17629bf0e418f0a40c5d5dcf4e.png
    2e7aaa17629bf0e418f0a40c5d5dcf4e.png
    249.7 KB · Views: 20
  • e6631e9da574c270c3e761b9a26c5a60.png
    e6631e9da574c270c3e761b9a26c5a60.png
    236.4 KB · Views: 20
  • Screenshot_20240717-212939.png
    Screenshot_20240717-212939.png
    123.9 KB · Views: 14
Kilichofanyika kwa Paul ni 'Brainwashing'. Pamoja na elimu yake kubwa lakini hakufua dafu kwa Ann.
Hawa hata kama una degree kumi ukiwapa nafasi mkuu umekwishaaa wife alikua anataka kuleta hizo mambo za makanisa nikamwambia siku ukienda kwenye mkesha nenda na begi lako la nguo usirudi hapa mpaka Leo amerudi roma anasali fresh
 
Kilichowatokea hao wote kilianza na Baba wa familia alipojazwa mapepo ya kuzim na huyo nabii wa kike!!

Alipojazwa mapepo akawa yes man kwa Kila kitu!

Mhusika alianza kujazwa na kitu kama upepo kwenye moyo wake yaani ujazo wa roho was mapepo unaosababisha msukumo wa damu wa mawimbi ya ghafula ndani ya moyo na pumzi!!

Anajazwa na hayo madudu mhusika anakua controlled na roho ya huyo nabii,mchawi,mganga n.k,mara nyingi wanachukua majina ya mama na Babu wa mhusika Ili kumpiga pin kumloga kupitia jina la mama na Babu yake!!

Mhusika ataanza kufuata maelekezo kwa njia ya sms au kupigiwa sim mara Kwa mara na akili ya mhusika inakufa au haifanyi kazi tena Bali inategemea nabii mkuu,mchawi au mganga anaemuendesha kupitia roho wa mapepo!!

Mhusika ataelekezwa kutuma pesa,kumilikisha mali hasta kuua mtu ili kutimiza matakwa ya nabii ,mchawi au mganga huyo na Wala hatajua zaidi ya kufuata maelekezo na akili yake haitofanya kazi!!

mambo haya yanatokea sana hata hapa Bongo na huo uchawi au ulozi ni WA Hali ya juu hata baadhi ya watu wazito wa kwenye mfumo wa usalama wa nchi wanao ili kuwapumbaza na kuvuna Wanachotaka Toka kwa wahalifu au wanaowapeleleza!!!

Ulozi huu unatumika kuwafilisi watu ambao ni threat Kwa mfumo wa utawala au hata kuwaua Kwa mhusika kujiua mwenyewe Kwa kujazwa maroho machafu!!

itoshe kusema kwamba ujasusi na uchawi plus secret societies plus mashirika ya kijasusi duniani no wamoja !Hakuna Mfumo wa kimbingu kwa watu wa mfumo zaidi ya kuwa walozi wa kijasusi ndani ya secret societies!!

Refer mapesa meengi wanayotumia wanasiasa Ili washinde uchaguzi na hawashindi Huwa Wana. Be blackmailed kiakili na kiroho kuaminishwa mambo yasiyoaminika mwishowe hupata hasara na anguko la kiuchumi Hadi hupata kiharusi na kufa!!

RIP nywele nyeupe Hadi ikulu!!

Watch out mkojani team!

Kama akiukosa huo anaoupigania anaweza PATA kiharusi au kuparalyse na Sasa kajazwa maroho anajazwa upepo kuwa naweza kumbe hawezi kifupi analogwa kiakili na hey hajui kama anachezewa shere!!
 
Back
Top Bottom