Ebwana ee...
Salamu kwa Mods...
Poleni kwa kazi nzito...
Salamu kwa members...
Poleni kwa shughuli za kila siku...
Yaliyonikuta Chit Chat tangu Desember mwaka jana mpaka leo hii.
Fata stori hapo chini...
Ni katika thread za kuchangia nilizozikuta Chit Chat mwezi Jana Desember 2012.
Nikamwona huyu kiumbe kwa jina sitaki kumtaja..
Nilitupa nyavu zangu kwa mara ya kwanza hapa Chit Chat zikatoswaaa mbaaali kama Mbwa ukimnyima msosi ukamfukuza nikaficha mkia wangu nyuma nikaondoka.
Sikwenda mbali niliendelea kutupa japo ndoano butu kwa bahati nzuri au kama sio mbaya ikanasa.
Nilifatwa PM yaliyonenwa kule natamani kusema nasitaaa...
Nikaposti kua Mtoto wa kike enzi hizo namjua kwa jina lileee kuwa namchumbiaaa...
Hongera nyingii nikamwagiwaaa nyingine zikamwagikia chini...
Nikawa nasubiria kaka wakubwa wanisaidie kupeleka posa kwao ambapo niliambiwa Mamndenyi ndie mama mdogo wake.
Nadhani Kaka wakubwa Erickb52Arushaone na Mr Rocky walitambua ila hawakuniambiaaaaa...
To be continued...
Sehemu ya pili...
Nilikua najiuliza kwanini walikua nachelewaaa?? sikupata jibu...
Nilipokuwa jana nazungukaaa zunguka jukwaani nikareply moja ya thread za huyo kiumbe...
Nikafatwa PM tukaanza salamu na mambo kama hayo. Akasema anatoka Mji fulani anaelekea kwingineeee...
Leo nimeingia jamvini jioni hii nakuta malumbano niliyoshindwa kuelewa kabla sijakaa sawa nikapokea PM kutoka kwa Donn a.k.a shemeji kuwa umepata habari kwa yaliyotokea???
Nikamwambia sijapata. PM ya 1, 2, 3, ikanibidi nimtafute muhusika kwa njia ya chumbani a.k.a PM. Ile nafika chumbani kwangu nashangaa PM za watu wawili zimegeuka kuwa za mtu mmoja nikapata kizunguzungu. Ndipo nikaambiwa na Donn yaliyotukia.
Kufumba na kufumbua napewa pole na mwenyekiti Baba V...
Yamenikutaaaaa.
Jipange na wewe mwenzangu yasije yakakukuta...
Pole stevoh hii hata mimi nimejifunza kitu... But namshukuru Baba V kwa ushirikiano wake tangu mwanzo mpaka mwisho... Ila sasa tunaomba kwa moyo mmoja mjomba wangu kipenzi na ndugu pekee aliyebaki Chimbuvu afunguliwe toka kifungoni.
Pole stevoh hii hata mimi nimejifunza kitu... But namshukuru Baba V kwa ushirikiano wake tangu mwanzo mpaka mwisho... Ila sasa tunaomba kwa moyo mmoja mjomba wangu kipenzi na ndugu pekee aliyebaki Chimbuvu afunguliwe toka kifungoni.