KAka PJ mfano huu unatuonyesha wazi kuwa siku MUNGU akiamua kukuumbua atakuumbua tu?? Hivi ulimwuliza sababu ya yeye kukiweka kidhibiti A ndani ya suruali kama police wa mashtaka ilikuwa ni nini? Nina uhakika atakujibu hata haelewi ilikuwaje: Hiyo ni kazi ya MUNGU kaamua kumpatiliza kwa maovu yake.
Hata akikana kuwa hafahamu bado haisaidii kwani ndio atakuwa ameanza maisha ya Web of Lies' maana imagine haya kafanikiwa kumtia changa la macho mkewe juu ya kipimo ambacho kimeonyesha positive. Mtoto akizaliwa kuna mauongo mengine yatafuata - kugawa kupato cha familia kuitunza familia mpya lazima atadanganya, siku mtoto akiumwa lazima atadanganya ili amuhudumie, siku akienda shule lazima atadanganya ili amlipie ada, mpaka siku anaoa au kuolewa pia atadanganya ili ahudhurie harusi ile peke yake yaani kila siku itakuwa lies, lies and more lies. Taabu yote hiyo ya nini kama si kuuchosha tu ubongo kwa sababu ukiwa mwongo lazima uwe na kumbukumbu kwa hiyo yeye atakuwa anafanya kazi kubwa ya kuupdate ubongo wake kila siku ili asichemshe eh!! atajikuta anazeeka hadi maini kabla ya kufa.
Wakati hata yote yangezuiliwa na tendo moja tu- KUKIRI kwa kupiga magoti na kukamua machozi
"Mke wangu nisamehe, huyu mwanamke nilipitiwa tu siku moja ndo amekuja anadai ana mimba yangu ndo nikawa siamini ndo nikamwambie nikampime ndo majibu ndo haya mke wangu. Lakini hata hivyo sweetheart siamini kabisa najutia sana kosa hili na ninamwomba MUNGU anisaidie isiwe mimba yangu.......Hivi darling unafahamu sehemu wanayopima DNA? Nakuomba unisaidie kunipeleka mke wangu please"
Hata awe na moyo mgumu kiasi gani, huruma ya kike itamwingia atamwelewa na kumshika mkono ili amprovie mwanamke mwenzake kuwa hafai. Na hata ikikutwa ni kweli ya kwake basi mke atalipokea ----- wanawake tunabeba mengi!! Tuoneni tu tukitembea na kunyongesha nyonga. Moyoni yametujaa
Ah am out of here. Mbarikiwe