Mkasa!

sasa ukute huyo jamaa ni mjeshi utasingizia mwanafunzi gani?
Kama huyo jamaa yako kazi yake inahusiana na taaluma katika ngazi yoyote aseme tu kuwa ni matokeo ya mwanafunzi wake mengine yatajulikana baadaye.Tofauti na hapo mh......
 

Skulmeti @ work!
 
kila lifanywalo gizani kuna siku litakuwa mwangani,hakuna refu lisilokuwa na mwisho na mwisho wa ubaya ni aibu,aseme ukweli na kutubu.
 
Ningekuwa mimi hapo ningeruka futi 100 namwambia nimefanyiwa hujuma tu kwenye daladala
Kwanini wewe?...
There must be a story behind!...lazima agundue kuna kitu anafichwa!
 
Mungu ameamua kumuweka wazi mkewe ili ajue mumewe anachokifanya!hakuna haja ya kumfundisha uongo huyo,heri kuwa na hofu ya Mungu siku zote jamani mambo haya hayatatupata.
 
KAka PJ mfano huu unatuonyesha wazi kuwa siku MUNGU akiamua kukuumbua atakuumbua tu?? Hivi ulimwuliza sababu ya yeye kukiweka kidhibiti A ndani ya suruali kama police wa mashtaka ilikuwa ni nini? Nina uhakika atakujibu hata haelewi ilikuwaje: Hiyo ni kazi ya MUNGU kaamua kumpatiliza kwa maovu yake.

Hata akikana kuwa hafahamu bado haisaidii kwani ndio atakuwa ameanza maisha ya Web of Lies' maana imagine haya kafanikiwa kumtia changa la macho mkewe juu ya kipimo ambacho kimeonyesha positive. Mtoto akizaliwa kuna mauongo mengine yatafuata - kugawa kupato cha familia kuitunza familia mpya lazima atadanganya, siku mtoto akiumwa lazima atadanganya ili amuhudumie, siku akienda shule lazima atadanganya ili amlipie ada, mpaka siku anaoa au kuolewa pia atadanganya ili ahudhurie harusi ile peke yake yaani kila siku itakuwa lies, lies and more lies. Taabu yote hiyo ya nini kama si kuuchosha tu ubongo kwa sababu ukiwa mwongo lazima uwe na kumbukumbu kwa hiyo yeye atakuwa anafanya kazi kubwa ya kuupdate ubongo wake kila siku ili asichemshe eh!! atajikuta anazeeka hadi maini kabla ya kufa.

Wakati hata yote yangezuiliwa na tendo moja tu- KUKIRI kwa kupiga magoti na kukamua machozi
"Mke wangu nisamehe, huyu mwanamke nilipitiwa tu siku moja ndo amekuja anadai ana mimba yangu ndo nikawa siamini ndo nikamwambie nikampime ndo majibu ndo haya mke wangu. Lakini hata hivyo sweetheart siamini kabisa najutia sana kosa hili na ninamwomba MUNGU anisaidie isiwe mimba yangu.......Hivi darling unafahamu sehemu wanayopima DNA? Nakuomba unisaidie kunipeleka mke wangu please"

Hata awe na moyo mgumu kiasi gani, huruma ya kike itamwingia atamwelewa na kumshika mkono ili amprovie mwanamke mwenzake kuwa hafai. Na hata ikikutwa ni kweli ya kwake basi mke atalipokea ----- wanawake tunabeba mengi!! Tuoneni tu tukitembea na kunyongesha nyonga. Moyoni yametujaa

Ah am out of here. Mbarikiwe
 
ushauri wa kipumbavu huo sitoi...
kama anajua ameiba, ajue kuna kukamatwa pia!
 
Huenda hii ikafanya kazi!..Kumbe kweli mAmbo yanayofanyika gizani yatadhihirika hadharani kwenye Nuru!
 
.........................................:juggle:Mshahara wa dhambi ni mauti, Na mauti ikishafika hakuna nafasi ya kutubu..........
 
Anatakiwa amweliza mkewe ukweli tena kwa utaratibu aombe msamaha
akisema afiche haitasaidia sababu kuna mtoto anakuja
maji yameshamwagika hana la kufanya
baada ya kumweleza ukweli mkewe aonyeshe kweli kubadilika kitabia
 

We Babu unatafuta kesi juu ya kesi wewe.....haya umesema ni ya Housegelo we ni nani uamue kumpima pasipo kunijulisha mie mama mwenye nyumba?? AU MIMBA HIYO NI YAKO?

Binti yako - the same swali ah usimpotoshe mwanaume mwenzio akiri tu ukweli.

Labda kama ni daktari kwa sababu hata akiwa mwalimu labda awe wa nidhamu au msaidizi wa Mwalimu Mkuu kusema kuwa ameweka ushahidi kwa ajili ya kumfukuzwa huyo mwenye mimba.
 
jamani mlio oa mjifunze mkitoka nje mvae condom kuondoa utata huu au kama mnataka watoto basi muende wakavuwakavu tuu lakini pia ukimwi upo jamani licha dawa ipo kwa babu loliondo
 
Kyabu naona umesahau kuwa hao hao wanawake wa 'kisasa' kama ulivyowaita ndio wale wasiopenda kuburuzwa kama watoto wadogo........kwa usasa wao wanataka hata hayo maamuzi ya mume yajengewe hoja inayoeleweka mezani na si kudictate otherwise unajichimbia moto wa makaa ya mawe usiozimika.
 

Kwa uzoefu wangu - Wanaume wote wanaozaa nje ya ndoa uhalalisha watoto na maisha yanaendelea - Mwanaume kuzaa nje ya ndoa haiwezi kusababisha ndoa kuvunjika - Unless kuna kitu kingine tofauti..

Kwa sisi ambao tuko-binded na imani za kidini ni vigumu kuoa mke wa pili, lakini had it been "legal" ungeshangaa watoto wangapi wamezaliwa nje ya ndoa!
 

kazi ipo, kumbe ndio inachowapa kichwa cha kufanya maovu huko nje? hapo ujue tayari familia imeingia dosari kubwa, mama nae akiwa na roho ndogo ataishilia kutafuta wa kumpooza machungu, tit 4 tat...mijanaume inapenda matatizo kweli...mxsii
 
Huenda hii ikafanya kazi!..Kumbe kweli mAmbo yanayofanyika gizani yatadhihirika hadharani kwenye Nuru!

PJ, bila shaka kulikua na 'initial reaction' ya huyo jamaa yako kwa mkewe....
Kwamba alifumwa na ushahidi alisema....ni masaa mengi yashapita....what did he do/say to his wife??
 
kazi ipo, kumbe ndio inachowapa kichwa cha kufanya maovu huko nje? hapo ujue tayari familia imeingia dosari kubwa, mama nae akiwa na roho ndogo ataishilia kutafuta wa kumpooza machungu, tit 4 tat...mijanaume inapenda matatizo kweli...mxsii

Ukweli ndo huo mama akipigwa na out moja ya nguvu kisha tenge la wax toka Congo biashara imeisha huku nyumba ndogo anatoa singo basi maisha yanasonga Nyamayao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…