Mkata mauno wa Koffi akanusha kupigwa na Papaa Mopao

Mkata mauno wa Koffi akanusha kupigwa na Papaa Mopao

Kofi imemkosti kama ilivyomkosti Chriss Brown.

Ila naona kama hawa kina Mama tu ndio wanaoonewa huruma....Jay Z amedundwa na Solange wala hakuna aliyehoji zaidi ya Jay Z kukebehiwa na kila mtu...na Solange anadunda tu kwa raha zake.
 
Kwa ile video nna uhakika wa 100% Koffie alimpga teke.Japo sijaona vizur
ile video kama una macho mawili haionyeshi sura ya mtu aliepigwa ilo teke inawezekana ni shabiki alievamia
 
Nakufuata PM sweet darling,ndio maana nakupenda ujue?
[emoji23][emoji23][emoji23] umbea kazi na wenye kazi ndio sisi.
Karibu dear, uliposemaga huna mzuka na JF ulinisononesha uje, looh, mpaka na mimi nikahamia zaidi siasani huko kubonda watu madongo na kijani zao maana hasira zilinipanda haswa. Umbea mtamu jamani, nimemisije Da jane!
 
ile video kama una macho mawili haionyeshi sura ya mtu aliepigwa ilo teke inawezekana ni shabiki alievamia
Da! na wewe umekuwa kama huyo mnenguaji aiseee! alipigwa "mateke" wala sio teke mpaka askari aliekuwa pale anakuja kushtuka ndio kumamata Kofii ili asiendelee kumpiga na wale madansa wengine wakabaki wamebutwaa kwa huzuni wanaangalia kwa woga sana. Aliekuwa anapigwa nae alikuwa anaonekana anayakwepa. Citizen TV walilioneshwa kwa muda sana ili watu wajionee.
 
Kilichotokea ni madhara ya bosi kuwa na mahusiano na mfanyakazi wake na hatimaye kuoa mfanyakazi huyo na kumuacha akiendelea kufanya kazi ofisi hiyo hiyo na wafanyakazi wenzake wale wale.....

Chanzo cha Ugomvi kimeanzia mbali sana hata kabla hawajatua Kenya na aliyesababisha sekeseke lile litokee ni mrembo Cindy ambae Alikuwa ni mcheza shoo wa Koffi akaja akawa mpenzi wake na hatimaye mkewe.....Baada ya Cindy kuwa mke wa Koffi hali kwenye band ilibadilika....

Cindy alipandishwa cheo na kuwa kiongozi wa choreography ambaye Alikuwa na jukumu la kuongoza mazoezi ya kudance kubuni staili mbalimbali na mitindo kadha wa kadha ya kudance...Hilo halikuwapendeza waliokuwa wacheza shoo wenzake waliokuwa wanaamini nafasi aliyopewa hakustahili hata kama ni mke wa bosi kwani kulikuwa na wacheza shoo kibao wenye uwezo kumzidi na wazoefu na wako kwenye kundi kwa muda mrefu kuliko yeye,hao ndo wangepaswa kupewa nafasi hiyo...

Hali hiyo ikazua bifu kati ya Cindy na madensa hao wengine hususani wa kike...Sasaaaa Cindy hutumia madaraka yake kuwaadhibu hao mahasimu wake na huwaadhibu kwa kutowajumuisha kwenye tripu za kusafiri nje ya nchi.....Kwenye safari ya kuja Kenya kuna madada hatari sana na wakali wa kudance waliachwa kitendo kilichowakera dancers wengine akiwemo Pamela yule aliyepigwa teke.....

Pamela yeye bwana ni mropokaji hasa na hakusita kuzinguana na Cindy .......Pale airport sasaaaaa Cindy si akamfuata Pamela na kumuambia amsaidie kubeba begi, Pamela akachomoa kisha akamuongelea shombo Cindy na si unajua wale wanawake tena,basi walirushiana maneno kiasi cha kuchapana makofi,hali iliyofanya Koffi afikishiwe taarifa......Uamuzi wa Koffi ulikuwa mmoja tu,kumfuata Pamela kumsema na inasemekana Pamela aliambiwa baada ya kumalizika kwa tamasha lile yeye kazi basi.....Kama kawaida Pamela hakai na neno kifuani akaongea mbovu kwa Koffi....Unajua kilichofuata...NDO LILE TEKE.....

KWAHIYO UKIANGALIA NA KUFUATILIA KWA MAKINI SANA TATIZO NI HILO KUJIHUSISHA NA MAPENZI NA MFANYAKAZI WAKO,UNAMPA CHEO ILI AWAONGOZE WALE WALE ALIOKUWA ANAFANYA NAO KAZI LINE MOJA,WENGINE WAKO JUU YAKE NA WENGINE WAKO CHINI YAKE....

NI JAMBO LA KAWAIDA KUWA KUNA WAFANYAKAZI WENZIE WALIKUWA WAKIMZIDI SANA KIUTENDAJI JE UNADHANI WATARIDHIKA????NI KAWAIDA KUWA WATAKUWA NA KINYONGO NA MAMBO KAMA TAFRANI LAZIMA ZITATOKEA....
Cindy siyo dancer,Cindy ni mwimbaji,tena nakumbuka kwa mara ya kwanza alitambulishwa pale Diamond Jubilee 2006 baada ya Fally kuhama bendi ya Koffi.
 
Cindy siyo dancer,Cindy ni mwimbaji,tena nakumbuka kwa mara ya kwanza alitambulishwa pale Diamond Jubilee 2006 baada ya Fally kuhama bendi ya Koffi.
Cindy ni kama Luiza Mbutu wa Twanga anaimba na kudance, Wacongo katika kitu walichotuzidi show zao wanamuziki wote wanajuwa kucheza, wakiwa kwenye stage ni kazi kszi tu.
 
Kuna wimbo anasifia pombe ya Skol ndiyo kale ka Dada alikoimba nako wimbo huo? Kana rangi flani chocolate kako natural.
Swadakta,ndiye Cindy yule,na kuna post mdau ameattach picha ya koffi anampa mike,ile ilikua dar ana sauti tamu sana.
 
Karibu dear, uliposemaga huna mzuka na JF ulinisononesha uje, looh, mpaka na mimi nikahamia zaidi siasani huko kubonda watu madongo na kijani zao maana hasira zilinipanda haswa. Umbea mtamu jamani, nimemisije Da jane!
Nilishakuomba msamaha mpenzi,na kukuahidi ndio nimerudi tena.
Huoni siku hizi hunikosi kama zamani?
Da Jane jamani sijui tukamfukue wapi!
Najuta ningejua ningechukuaga namba zake! [emoji22][emoji22]
 
Cindy ni kama Luiza Mbutu wa Twanga anaimba na kudance, Wacongo katika kitu walichotuzidi show zao wanamuziki wote wanajuwa kucheza, wakiwa kwenye stage ni kazi kszi tu.
Ni kweli unachosema hata Fally anaimba sana na kudance pia,nilielezea vile kwa kua mdau alieleta uzi alielezea kama vile Cindy ni kiongozi wa madancer tu.
 
Nilishakuomba msamaha mpenzi,na kukuahidi ndio nimerudi tena.
Huoni siku hizi hunikosi kama zamani?
Da Jane jamani sijui tukamfukue wapi!
Najuta ningejua ningechukuaga namba zake! [emoji22][emoji22]
Nilisha kusamehe wangu, shaka ondoa karibu tupunguze stress za maisha hapa. Da jane ban alokula la maisha haa kisa DIDA?! Mfyuuu, nilikuwa nasubirije ubuyu wa LULU?! Acha tu.
 
fb17301de959396664e3c9be4d41e4db.jpg
 
Nilisha kusamehe wangu, shaka ondoa karibu tupunguze stress za maisha hapa. Da jane ban alokula la maisha haa kisa DIDA?! Mfyuuu, nilikuwa nasubirije ubuyu wa LULU?! Acha tu.
Kumbe kapigwa ban LA maisha nime miss ubuyu na kichambo chake aisee mana jukwaa limepoa
 
Kumbe kapigwa ban LA maisha nime miss ubuyu na kichambo chake aisee mana jukwaa limepoa
Hapana sina uhakika kama kapigwa ban, niliuliza tu maana nimemis sana vichambo vya watu wa mjini.
 
Back
Top Bottom