Mkataba Barabara ya Mafinga - Mgololo (KM 81) Kusainiwa Kesho Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BARABARA YA MAFINGA - MGOLOLO (KM 81) MKABATA KUSAINIWA KESHO DODOMA

Mikataba ya ujenzi wa barabara saba (07) ambazo zimekuwa zikiongelewa kwa muda mrefu katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakwenda kusainiwa hapo kesho Juni 16, 2023 tukio ambalo litashuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo itafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo barabara zote hizo zitajengwa kwa kiwango cha lami kupitia utaratibu wa EPC+ F (wa ujenzi wa manunuzi ya uhandisi pamoja na fedha).

Moja ya mkataba ambao utakwenda kusainiwa hapo kesho ni pamoja na mkataba wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mafinga hadi Mgololo yenye urefu wa kilometa 81 ambayo itakwenda kujengwa kwa lami.

Hayo yamesemwa leo Juni 15, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akijibu swali la mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mheshimiwa David Kihenzile aliyetaka kujua ni lini barabara hiyo itaanza kujengwa.

Aidha, Mheshimiwa Kihenzile ameishukuru serikali ya awamu sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali barabara hizo kujengwa kwa kupitia utaratibu wa EPC+F ambapo amesema italeta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii katika jimbo la Mufindi Kusini na majimbo jirani barabara hiyo inapopita.

Miradi ya ujenzi wa barabara hizo ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi ambao barabara hizo zinapita pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.
 
Attachments

  • E1LRNM3WUAMCxgz.jpg
    E1LRNM3WUAMCxgz.jpg
    76.9 KB · Views: 19
  • UntitledSAWE.jpg
    UntitledSAWE.jpg
    7.9 KB · Views: 20
Hii barabara wameichelewesha sana..
 
Hii barabara wameichelewesha sana..
Hii barabara inaenda kwa muwekezaji. Walimuuzia kiwanda, mji wenye nyumba zaidi ya 300, wafanyakazi 1000 na hekari 10000 na vingine tusivyo vijua kwa bilioni 1 tuu leo wanamjengea na barabara.

Ahsanteni.... mtukumbuke na mgololo kwenda makambako.
 
Yeah sure,umeme Kijiji Cha isaula tunahitaji pia
 
BARABARA YA MAFINGA - MGOLOLO (KM 81) MKABATA KUSAINIWA KESHO DODOMA

Mikataba ya ujenzi wa barabara saba (07) ambazo zimekuwa zikiongelewa kwa muda mrefu katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakwenda kusainiwa hapo kesho Juni 16, 2023 tukio ambalo litashuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo itafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo barabara zote hizo zitajengwa kwa kiwango cha lami kupitia utaratibu wa EPC+ F (wa ujenzi wa manunuzi ya uhandisi pamoja na fedha).

Moja ya mkataba ambao utakwenda kusainiwa hapo kesho ni pamoja na mkataba wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mafinga hadi Mgololo yenye urefu wa kilometa 81 ambayo itakwenda kujengwa kwa lami.

Hayo yamesemwa leo Juni 15, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akijibu swali la mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mheshimiwa David Kihenzile aliyetaka kujua ni lini barabara hiyo itaanza kujengwa.

Aidha, Mheshimiwa Kihenzile ameishukuru serikali ya awamu sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali barabara hizo kujengwa kwa kupitia utaratibu wa EPC+F ambapo amesema italeta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii katika jimbo la Mufindi Kusini na majimbo jirani barabara hiyo inapopita.

Miradi ya ujenzi wa barabara hizo ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi ambao barabara hizo zinapita pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.
Vipi walisaini yako wapi mbona hawajengi sasa
 
Back
Top Bottom