Mkataba kati ya DP world na TPA hauna tatizo lolote ila kuna baadhi ya ibara zinatakiwa zifanyiwe mareboresho mfano ibara ya 23

Huo mkataba si ushaingiwa au?
IGA ndio imeisha sainiwa na kuridhiwa na Bunge, mkataba ni HGA ambao bado, na hauridhiwi na Bunge, ila wabunge wakiuhitaji wanaweza kuomba!.

Lazima tuboreshe sheria zetu, Bunge letu lisifanywe ni rubber stamp ya nyavu za kokoro, kupitisha kila kitu!.

Mikataba iletwe Bungeni kuidhinishwa na sio kuridhiwa!.
P
 
Mkataba upo sawa tatizo ni English naona.
Mkataba uko very clear kuwa IGA itakufa pale HGA itakufa....
IGA itabaki only kama HGA itakufa kinyume na makubaliano....
Mind you hiyo HGA hatujasaini bado ni miaka mingapi
Mkuu The Boss , tatizo sio lugha tuu!, Watanzania tunahitaji elimu ya uelewa wa mikataba ya kitaifa na kimataifa, International treaties, bilateral agreements na multilateral treaties, na the role ya Bunge letu kuridhia kwa rubber stamp badala ya kuidhinisha!.

Tunahitaji Bunge letu liidhinishe na sio hii ya rubber stamp!.
P
 
Kama wameweza kulidhia hats kuidhinisha hawashindwi.
 
Kuwa positive haimanishi kutokuwa na upeo wa kuona mambo yanayoweza kutokea.
Nakubaliana na wewe
Ni sawa na mtu anachukua ardhi, anaanza kulima kwa kutegemea mvua, amefanya projections za mapato, unamwuliza, itakuwaje kukiwa na ukame? Halafu akujibu kuwa uwe positive. Yaani usifikirie kabisa kunaweza kuwa na ukame. Huko itakuwa ni kujitia upofu.
Nakubaliana na wewe
Nakubaliana na kesi, issues ya Djibouti, ni issues ya kitu kinachoitwa a legitimate expectations baada ya kusainiana mkataba wenye monetary value. Ile IGA haina monetary value hivyo tukiivunja hakuna kushitakiana!. HGA itakuwa na monetary value na huu sasa ndio mkataba.

Japo Mkurugenzi Mkuu wa Bandari anadai wamewafanyia DPW a tharaly due diligence, I doubt kwasababu kama hii due diligence ilifanyika, haya madudu yasingetokea kwenye hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
P
 
Kama wameweza kulidhia hats kuidhinisha hawashindwi.
Tofauti ya kuridhia na kuidhinisha, kwenye kuridhia the role of Bunge ni Rubber stamp!, bunge letu linaletewa mkataba ulio sainiwa ili kuu domesticate na hakuna marekebisho yoyote!. Lakini kwenye kuidhinisha Bunge letu linakuwa na mamlaka ya kurekebisha kasoro na kutoa go ahead.
P
 
Wewe shida yako DP au uwekezaji? kwa jinsi unavyoandika shida yako yako ni DP na hoja yako wanachangamoto na nchi zingine mbona hujaongelea na mazuri yao umejikita na issue ya Djibout tu? sasa lini umesikia port ya Djibout imesimama sababu wana issue na DP? kama swali lako moja umeuliza. Hii ni business mwekezaji pia mkataba unamlinda hata hao kina Google, Siemens makumpuni makubwa duniani lakini wamewahi kuingia kwenye matatizo na baadhi ya nchi lakini haiondoi sifa ya hizi kampuni. Nadhani ungeweka wazi shida yako yako DP au uwekezaji. kuna uwekezaji mkubwa wa LNG kuwahi kutokea nchi hii hakuna mtu anajadili PSA watu wako busy bandarini sehemu tunajuwa wazi tunashida kubwa ya uendeshaji sio leo tu toka tupate uhuru. Ni wazi kuna watu wana agenda zao binafsi tu lakini uwekezaji ndio key wa maendeleo awe DP awe sijui DX sio muhimu.
 
Huu ndio uzalendo, ubarikiwe sana
P
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Mimi nadhani Article 23 (3) inajitosheleza, mengine yote yamemezwa na neno "reasonably". Kama kuna kipindupindu, it is reasonable. Kama kuna vita, it is reaonable. Kama hajalipa kodi, it us unreasonable. Kama kaja Rais mpya Mbowe kwa mabavu tu anataka mkataba ufe, it is unreasonable. Etc etc.
 
Hapa swala nikukaa chini na hao DP World tuandike vizuri vifungu vyenye shida. Tusitukanane tutaonekana hatuna hekima.
 
Ndugu yangu urudi darasani ujifunze Kiswahili. Unasema mkataba HAUNA TATIZO LOLOTE halafu unarudi tena kukosoa ibara ya 23, ndio nini sasa? Unajua maana na matumizi ya neno LOLOTE?
 
Ndugu yangu urudi darasani ujifunze Kiswahili. Unasema mkataba HAUNA TATIZO LOLOTE halafu unarudi tena kukosoa ibara ya 23, ndio nini sasa? Unajua maana na matumizi ya neno LOLOTE?
Haha boss hutoweza kunielewa hata siku moja. Kikubwa ujumbe wangu umefika kwamba ibara hiyo ina shida. Hivyo ndivyo narushaga mawe. Huwa sirushi jiwe likupige likuumize hapana. Nakuvuta nakuonyesha tatizo.
 
Sijauona mkataba baina ya DP World na TPA, kama unao uweke hapa tuuone. Niliouona ni ule wa makubaliano ya maendeleo baina ya Dubai na Tanzania "IGA". Bofya chini hapo uuone:

 

Ha ha 😂😂🤣 wabongo bwana Kwa sifa za kijinga

Kama hujui Jambo si ukae kimya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…