Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,205
- 5,121
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.
Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.
Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?
Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.
Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.
Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.
Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!
Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.
MALISA GJ