Mkataba na DP World siyo miaka 100, bali ni MILELE

Hii nchi nashindwa kuelewa usalama wa Taifa upo wapi?Jeshi lipo wapi?Bunge lipo wapi?mpaka yanatokea haya?
 
Kwa Haya yanayoendelea kuhusu Taifa letu kwa sasa Yakiitishwa Maandamano Ntakuwa tayari tena ntakaa mstari wa mbele kabisaa
 
Je Wana JF mko tayari Kupinga yanayoendelea? Taifa letu linaenda pabaya kwa hii Mikataba wanayoingia!
 
Mlimnanga Ndugage aliposema nchi itauzwa....

Leo mnalalamika nini nyie wasaka tonge?
 
Termination clause Huwa Haina specific period for termination isipokuwa automatic termination.Nadhani tuletewe kifungu Cha Duration ya mkataba.
 
Eti umesainiwa 2022? Hata wana sheria wamekaa kimya?
 
Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.

MALISA GJ[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumepigwa kwa Fei,tukataletwa kwa Yanga kwenda Ikulu mixer vituko vya Morrison, tukaja mabehewa ya gorofa, mkeka wa DED ukabiduliwa then katikati ya haya matukio ndio wakapenyeza ya Bandari, kudadeki hapo ndipo ujue kuna mashivo walichora mchoro, haya wale wa Burundi mjiandae.
 
Ndio maana kule liberia walipomtoa yule mpuuz Samweli Doe madarakani walimsurubu mitaana bila hiyana hata ccm ni swala la muda tu narudia tena ccm ni swala la muda tu kisha cha moto mtakiona.
 
Kwa Haya yanayoendelea kuhusu Taifa letu kwa sasa Yakiitishwa Maandamano Ntakuwa tayari tena ntakaa mstari wa mbele kabisaa
Wavaa gwanda wanatazama hii comment huku wakicheka, jinsi watakavyokupa kilema cha ukubwani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wavaa gwanda wanatazama hii comment huku wakicheka, jinsi watakavyokupa kilema cha ukubwani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huwezi Jua
 
Mwamba umesoma kwa hamaki kubwa sana hapa, ebu shusha pumzi basi na angalia kama wewe ndio unawekeza kwa nchi hizi zetu maslahi yako yanalindwaje na kweli jamani tuna watu viazi wa kiasi hiko cha kuingia mkataba infinity!!!! Tusome tena na kiglass pembeni ndio tunaweza elewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…