Mkataba na Shetani ni kitu kipo?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Mkataba na Shetani(Deal with the devil) inasemwa ni kitendo cha mtu kuingia mkataba na Shetani apewe umaarufu, pesa, mamlaka, afya njema nk, kisha yeye anampa Shetani nafsi yake(yaani anajitoa kuwa mali ya Shetani. . . ?)

Mfano mmoja ni kitendo cha Shetani kumshawishi Yesu amsujudie, na yeye Shetani kumuahidi kumpatia Yesu utajiri na mamlaka, akidai hivyo vyote ni vyake anaweza kumpa yeyote anpendaye.

Mifano mingine ni wasanii wengi maarufu. Kuna msanii kama Jimi Hendrix. Huyu anachukuliwa kama mpiga gitaa nguli wa muda wote. Lakini umaarufu wake uliibuka ghafla, ukadumu kwa miaka mitatu na akafariki hata miaka 30 hajafika. Wanasema aliuza roho yake kwa Shetani. Akapewa umaarufu na baada ya miaka mitatu Shetani akaja kuchukua malipo yake.

Msanii mwingine ni Leroy Johnson. Huyu naye aliibuka ghafla kuwa nguli wa gitaa. Kafa na miaka 27 tu. Zaidi ni kuwa aliimba sana nyimbo kuhusu mkataba wake na Shetani. Mmoja aliuita Me and The Devil. Akizungumzia Shetani kumtembelea na kumuambia kuwa muda wa kuondoka umefika.

Kuna ushahidi wowote wa kuonyesha kuwa mkataba na Shetani upo?
 
Kwanza shetani hayupo.

Hao wanaokuingiza na kukusainisha mkataba ni binadamu kama wewe.

Sio shetani.

Sasa wewe umepewa masharti na binadamu halafu unasema ni shetani?

Au unafikiri hao binadamu wanaokupa hizo mali wao hawataki kuwa nazo?

Wakupe burebure tu bila masharti?
 
Hakuna. Japo kama wewe ni mtu wa dini, kuna uwezekano mkubwa utashindwa kuniamini.

Wasanii wengi wa muziki wa rap, rock na metal huko marekani wamekuwa wakitumia taswira za kishetani kama njia ya kushangaza watu, au kuonyesha uasi dhidi ya mamlaka za kijamii...

Wapo wanaomuabudu shetani(satanists) lakini hawa ni atheists wanaopenda kufuatilia mambo ya kichawi tu...
 
Satan
 
Kuna mashetani wanadamu kwahiyo ushetani ni cheo
 
Shetani ni Roho, je unawezaje kuingia mkataba na kitu kisicho na mwili?
 
Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo shetani.

Unacheka halafu huna uthibitisho wa uwepo wa huyo shetani!

Unataka kuleta stori za vijiweni mnazo pumbazana huko kwenye kahawa zenu.
Unataka nikuletee udhibitisho hapa Jamii Forum? nafikiri tafurta maarifa zaidi uache hekaya hizo za Vijweni
 
Hata na ninyi kusema kuna mkataba na shetani ni mitazamo yenu tu.

Hakuna kiumbe kiitwacho shetani unachoweza kufanya mkataba nacho.
wewe unaamini kile kinachoonekana tu, kisichoonekana hukiamini kabisa.

Unajua tu mambo ya ulimwengu wa mwili, lakini ulimwengu wa roho hakuna ukijuacho kabisa..

Au upo hapa kupotosha tu kumbe wewe ndio kachawi kakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…