Likwanda
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 3,922
- 1,149
Yanga wapo makini kama chadema
Mkuu, hata mimi nimeona mantiki ya malalamiko yao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yanga wapo makini kama chadema
Kweli na sawa na Man U kuonyesha EPL
hivi arsenal wanaweza kukubali mechi zao zionyeshwe man utd tv?
Tatizo kubwa hapa ni je tendering process ilifanyika? Kulikuwa na tangazo la kuzitaka tv icluding dstv kuleta quotation ili washindane? Kama jibu ni hapana, hao azam tv wamepewaje hiyo nafasi? Ni kigezo gani kimetumika?
Tibaa
Mbona watu wengi,tulilitegemea hili kuwa litajitokeza,Na hapa tatizo kubwa ni maslahi ya kibiashara ya MANJI,hakuna kitu kingine,ameona anayetoa udhamini huo ni mfanya biashara mwenzake,na ki2 kingine hawa wakina manji,wanapoona kuwa mtu anakuja na mipango ya kusaidia timu zote ili ligi iwe na ushindani,na kuzifanya timu zianze kujitegemea,hawapendi wanataka kila siku waonekane Miungu watu.shame on u.
Tatizo hapa ni migongano ya kimaslahi na chuki binafsi. Mfano swala la Ngasa lina uhusiano gani na haki ya kuonyesha mechi...!?Na kuhusu kutotangazwa kwa tender eti ndo sababu nakataa kwasababu Tff na vilabu vyetu havina utamaduni wa kutangaza tenda. Mikataba mingi tunashtukizwa wakati wa kusaini tu kama huu wa Azam tv. Labda kama wewe mkuu ulishawahi kuona tender zozote kwenye vyombo vya habari unaweza kuviweka hapa ili niibatilishe hii kauli yangu. Vinginevyo kwenye suala la tender hawana hoja wana lazimisha tu.
mbona timu za Afrika Kusini zimekubali zionyeshwe na SuperSport huku wakijua kuwa supersport wana timu yao kwenye ligi...?Acha akili za kushikiwa mkuu, usifuate mkumbo.
Tatizo hapa ni migongano ya kimaslahi na chuki binafsi. Mfano swala la Ngasa lina uhusiano gani na haki ya kuonyesha mechi...!?Na kuhusu kutotangazwa kwa tender eti ndo sababu nakataa kwasababu Tff na vilabu vyetu havina utamaduni wa kutangaza tenda. Mikataba mingi tunashtukizwa wakati wa kusaini tu kama huu wa Azam tv. Labda kama wewe mkuu ulishawahi kuona tender zozote kwenye vyombo vya habari unaweza kuviweka hapa ili niibatilishe hii kauli yangu. Vinginevyo kwenye suala la tender hawana hoja wana lazimisha tu.
Kama vipi basi dili apewe DSTV ili mgeni ale mema ya nchi, maana uchoyo mwengine hauna mashiko. AZAM TV wala haimilikiwi na Bakhresa na wala haina uhusiano wa kimapato na AZAM FC, sana sana Bakhresa atakua kama mdau tu na facilitator. Watu wakiona jina AZAM tu basi ishakua shida.
Swala la msingi zaidi ni: iko wapi hiyo Azam Tv?
(Answer)Hapo kuna ujanja kibiashara nahisi hiyo imesajiriwa ndani ya azam as group of company.
Inakuwaje kwa kituo ambacho hata hakijaanza kazi au angalau kusajiliwa rasmi, kanze kufanya biashara tena isiyo na ushindani wa kisheria,
(Answer)Ndo mgongano wa kimaslahi anauzungumzia manji kuna deal imepigwa hapo bila shaka.
au ni kwa ajili ya iina la anayekimiliki?
Sababu walizoeleza Yanga kwa nini hawataki kulipwa sawa na vilabu vingine ni za kitoto, ni kweli wao ni klabu kubwa ni sawa na Simba lakini lazima wakumbuke Azam Media group hawadhamini vilabu wao wanadhamini ligi sasa labda watuambie hao vilabu vikubwa kama wanaweza kucheza ligi bila hivyo vilabu vingine wanavyoviita vidogo.
Na kingine watwambie mgawo wanaopata kutoka Vodacom je ni tofauti na mgawo wanaopata vilabu vingine? Je vipi kuhusu gate collection wanapocheza na hivyo vilabu vidogo wanagawana sawa au Yanga kwa sababu ni klabu kubwa wao wanapata zaidi? Na kama wanapata sawa kote huko kwa nini hizi za Azam wanataka wapewe tofauti na wengine?
Wao kama ni klabu kubwa na wanaamini wanaweza kuingiza hela kutokana na ukubwa wao si watafute wadhamini wengine kama vile walivyopata kutoka TBL. Yanga wanatakiwa wakubali hicho kiasi ili Azam waonyeshe hiyo ligi na timu ndogo kama ndugu zao Toto wasiwe wanawagharamia siku wanacheza na Simba.
Suala la kwamba tenda haikuwa wazi mimi sina uhakika nalo lakini TFF wenyewe wanasema dau la Azam ndo lilikuwa kubwa zaidi kuliko la supersport sasa wao walitaka supersport wapewe eti tu kwa sababu wanaonekana
sehemu kubwa Afrika kwani Yanga wanafanya biashara gani nje ya Tanzania wanataka waonekana nje? Wao si ni wa hapa hapa tu.
Kusema kwamba wana ugomvi na Azam wa kimchezo na wanatolea suala la Mrisho Ngasa kama mfano sio sawa, labda Yanga wangeweka wazi kwamba ugomvi wao na Azam ulianza lini? Je ulianza kipindi kile Yanga wanafungwa mfululizo au ulianza tu baada ya wao kumuuza Ngasa kwa Azam? Au ulianza pale Azam walipotaka kumuuza Ngasa kwa utovu wa nidhamu alivyoibusu jezi ya Yanga huku akijua yeye ni mchezaji wa Azam? Ieleweke Yanga walitamka wazi kabisa kupitia kwa aliyekuwa katibu wao (Mwesiga) Ngasa hakuwa na thamani ya zaidi ya TZS.20M kwa hiyo wao wasingeweza kutoa zaidi ya hapo, sasa wanapotaka kutuaminisha kwamba Azam hawakutaka kuwauzia Yanga si kweli ila wao walitaka wampate kwa bei chee sababu Ngasa anaipenda Yanga.
Ninachoona hapa kwa sababu ni ngumu kutofautisha Azam FC na makampuni mengine ya Bakhresa na Bakhresa mwenyewe kama ilivyo ngumu (kwa sasa) kutofautisha Yanga na Manji, nalazimika kuamini Manji na Bakhresa watakuwa na msuguano wao wa kibiashara, nalazimika kuamini hivyo kwa sababu makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga na katibu mkuu Mwalusako walishiriki vikao vyote na hoja zao zilijibiwa na wenyewe wakaondoka kwenye vikao wameridhika iweje leo wageuke, je ni shinikizo la mwenyekiti Manji au ni shinikizo la wajumbe wengine wa kamati ya utendaji? Kwa vyovyote vile mwenyekiti Manji ni kila kitu kwa Yanga (kwa sasa) hivyo lazima atakuwa yeye ndo aliyebatilisha waliyokubaliana kina Sanga kwenye vikao.
Hoja ya kwamba Azam Media Group hawawezi kudhamini kwa haki kwa sababu nao ni washiriki kwenye ligi haina uzito kwa sababu kuna mifano ya makampuni yanayodhamini ligi za nchi mbali mbali na yenyewe yakiwa na timu inayoshiriki kwenye ligi hiyo; mfano: Supersport wana timu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika kusini na wao ni wadhamini wa ligi hiyo; EABL wanadhamini ligi kuu ya Kenya na wao wana timu inayoshiriki hiyo ligi; Mashindano ya vilabu ya CECAFA yanadhaminiwa na Rais wa Rwanda ambaye ndo Amiri jeshi mkuu wao na mara nyingi timu ya APR ambayo ni timu ya jeshi inashiriki haya mashindano, kama haitoshi Manji aliongeza udhamini wa mashindano ya CECAFA ya vilabu huku akijua kwamba yeye ni mwenyekiti wa Yanga na timu yake mara nyingi inashiriki kwenye hayo mashindano.