Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba. Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake. Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China. Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe. Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi. Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka. Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni. Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika. Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni. Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia. Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari. Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe. Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji. Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani. Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini. Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje. Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari. Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza. Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia. Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio. Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo. Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania. Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem. Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani. Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini. Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi. Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi. Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar. Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi. Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza. Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani. Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani. Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine. Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote. Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo. Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote. Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari. Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake. Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli. Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa. Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi. Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo? Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi. Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe. Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti. Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema. Mijicho yao imelenga mbali. Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM. Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao. Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini. Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. Ana shahada ya Falsafa kutoka Birkbeck, Chuo Kikuu cha London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

View attachment 2656186
Sawa shekhe DP world watawapa tende za bure Kila mfungo
 
Alert❗❗❗🚫

T h i s i s s m t h n g w r i t t e n t o d i s t r u c t t h e s e d e c e n c y s o u l w i t h a b i l i t y t o q u e s t i o n.

Be warned ❗
You Tanzanian don't be fooled and this article there is high possibility that it has been written to neutralize the indecent and decisive immoral action

I leave you with one powerful single question

What else DP world can do that we can't if we dedicate our efforts to achieve it regardless how wrong it will take us❓

If we don't sign the contract what else we got to loose ❓
 
acha ujinga dada. siku hizi hakuna ma eunuch, walikuwepo zamani enzi Yesu alipokuwepo hapa duniani. tafsiri ya enzi hizo ilikuwa ni watu wanaohasiwa ili wawe walizi wa royal family na lengo ili wasifanye nao ngono. mfalme alikuwa na amani walizi wa mabinti zake au wake zake wakiwa wanmehasiwa. hivyo tafsiri ilikuwa ni watu wasiokuwa na nguvu za kiume. sasa Yesu alikuwa anawaeleza watu kwamba, kuna watu wengine wanazaliwa wakiwa mahanith. katika yoote hayo, hakuna sehemu ilimaanisha watu wanazaliwa wakiwa mashoga. najua unatamani iwe hivyo lakini sivyo ilivyo. mistari ya Biblia nimekuwekeeni hapo juu ukiisoma utaelewa.

Mtume Paulo hajawahi kuoa, na alisema yeye ana tatizo mwilini mwake ambalo hakulifafanua na inasemekana yaweza kuwa alikuwa hana nguvu. lakini pamoja na yote, ukisoma Warumi 1:26 amepinga na kulaani ushoga na usagani. Biblia tangu agano la kale kipindi cha sodoma na gomora MUngu amepinga sana ushoga na aliadhibu, hadi Yesu alipokuja na wafuasi wake wote wamepinga ushoga hadi mwisho. ila sina uhakika kama vitabu vingine vinavyoruhusu sunna kama vinapinga ushoga. na huwa sielewi kwanini maeneo yenye imani sana kama zanzibar, tanga na mombasa, au niseme uarabuni yote na waarabu wote wanaogopwa kwa kuingilia kinyume na maumbile. jibu utakuwa nalo wewe mwenyewe kama upo fair katika huu mjadala.

10 The disciples said to him, “If this is the situation between a husband and wife, it is better not to marry.”

11 Jesus replied, “Not everyone can accept this word, but only those to whom it has been given.

12

A.

For there are eunuchs who were born that way,

Kumbe kuna watu huzaliwa katika hali hii , Jee siku hizi hawazaliwi tena ??

B.

and there are eunuchs who have been made eunuchs by others

Watu wanaofanywa kuwa eunuch na watu wengine , na Nabii wa kanisa lako Nabii Tito

—and there are those who choose to live like eunuchs for the sake of the kingdom of heaven.

Hawa waliojichagulia kuishi kama eunuch , nitajie ni nani katika kanisa lenu ??

Sasa niwekee wapi bwana Yesu alisema alituwekea haya maneno uliyoandika ??

Tafsiri ya enzi hizo ilikuwa ni watu wanaohasiwa ili wawe walizi wa royal family na lengo ili wasifanye nao ngono

Ningalikushauri ukasoma hivi vitabu

1. “The Secret Love Letters of Saint Paul” by Bern Callahan. (Booklocker, 2016)

2.“Damascus” by Christos Tsiolkas (Atlantic Books, 2019)

Utamjua Paulo alikuwa mtu gani wakati anaongea maneno haya

“Love is patient and kind; love does not envy or boast; it is not arrogant or rude. It does not insist on its own way; it is not irritable or resentful; it does not rejoice at wrongdoing, but rejoices with the truth. Love bears all things, believes all things, hopes all things, endures all things. Love never ends.”
— I Corinthians 13:4-8 (ESV)

“Faith, hope, and love abide, these three; and the greatest of these is love.”
— I Corinthians 13:13
 
Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba. Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake. Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China. Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe. Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi. Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka. Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni. Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika. Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni. Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia. Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari. Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe. Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji. Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani. Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini. Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje. Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari. Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza. Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia. Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio. Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo. Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania. Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem. Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani. Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini. Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi. Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi. Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar. Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi. Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza. Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani. Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani. Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine. Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote. Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo. Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote. Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari. Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake. Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli. Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa. Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi. Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo? Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi. Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe. Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti. Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema. Mijicho yao imelenga mbali. Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM. Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao. Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini. Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. Ana shahada ya Falsafa kutoka Birkbeck, Chuo Kikuu cha London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

View attachment 2656186
 
Attachments

  • BF2D3224-92D6-48AF-BDFE-2453E4C239C2.jpeg
    BF2D3224-92D6-48AF-BDFE-2453E4C239C2.jpeg
    51.3 KB · Views: 5
10 The disciples said to him, “If this is the situation between a husband and wife, it is better not to marry.”

11 Jesus replied, “Not everyone can accept this word, but only those to whom it has been given.

12

A.

For there are eunuchs who were born that way,

Kumbe kuna watu huzaliwa katika hali hii , Jee siku hizi hawazaliwi tena ??

B.

and there are eunuchs who have been made eunuchs by others

Watu wanaofanywa kuwa eunuch na watu wengine , na Nabii wa kanisa lako Nabii Tito

—and there are those who choose to live like eunuchs for the sake of the kingdom of heaven.

Hawa waliojichagulia kuishi kama eunuch , nitajie ni nani katika kanisa lenu ??

Sasa niwekee wapi bwana Yesu alisema alituwekea haya maneno uliyoandika ??

Ningalikushauri ukasoma hivi vitabu

1. “The Secret Love Letters of Saint Paul” by Bern Callahan. (Booklocker, 2016)

2.“Damascus” by Christos Tsiolkas (Atlantic Books, 2019)

Utamjua Paulo alikuwa mtu gani wakati anaongea maneno haya

“Love is patient and kind; love does not envy or boast; it is not arrogant or rude. It does not insist on its own way; it is not irritable or resentful; it does not rejoice at wrongdoing, but rejoices with the truth. Love bears all things, believes all things, hopes all things, endures all things. Love never ends.”
— I Corinthians 13:4-8 (ESV)

“Faith, hope, and love abide, these three; and the greatest of these is love.”
— I Corinthians 13:13
aisee ndugu kapuku, kwa mistari hiyo ya love, kwako umeelewa ni ngono? does love ngono pekee according to your religion? hapo alikuwa anaongelea upendo wa ndugu. ndio maana hata sehemu zingine ameongelea upendo kwa wake zetu. ila wewe kwasababu akili yako yote imejaa shahawa umeshafika kusikofikika.

waliojichagulia kuishi hivyo ni kama hao mapadri na masista, ila waliozaliwa hivyo ni mahanith kama wewe. Jesus or anyone in the bible hajawahi kumaanisha au kubariki ushoga. ni dhambi na itabaki dhambi milele.
 
Tafsiri hiyo umeitoa kitabu gani ??

Umesema waliozaliwa ni mahanithi nimekuuliza mara nyingi nitajie huyo towashi mmoja aliyezaliwa na kubaki kanisani akifanya kazi za kanisa lenu , unakimbia , au ni Wewe ???

Nilikuwekea vitabu usome kuhusu Paulo kuwa mwenyewe alikuwa shoga hutaki kusoma

Both Paul’s sense of unworthiness and his appreciation for God’s grace may have the same unexpected cause: Some scholars believe that Paul was a celibate homosexual man trying to reconcile faith and sexuality in a culture that condemned same-sex attraction. This may have been the “thorn in the flesh” that God refused to remove despite his prayers.
 
shoga ni baba yako na sio paulo. kama familia yenu mnaliwa usifikiri kila mtu analiwa. angalia Warumi 1:26 hadi 27 halafu uje na huo ubwabwa wako kuwa paulo alikuwa shoda.
 
Some facts suggest Paul was gay​

The modern concept of homosexuality did not exist in Biblical times. But Spong and others point out that a sexual attraction to men would explain some mysteries about Paul’s life:

* Paul never married, which was unusual for a first-century Jew, but had a series of younger men as companions.

* He sometimes expressed negativity toward women and homosexual exploitation.

* Tormented by self-reproach, he pleaded with God three times in vain to remove an unspecified “thorn in my flesh” that troubled him. Some believe that “thorn” was attraction to other men. God’s answer, according to Paul, was to deny his request with the explanation, “My grace is sufficient for you, for my power is made perfect in weakness.”

* Homosexuality might even help explain Paul’s cataclysmic conversion experience. He went from intensely persecuting Christians to becoming the most articulate leader of the very movement that he had tried to destroy. His vision of Christ left him stunned by the revelation that nothing could separate him from God’s love.
 
shoga ni baba yako na sio paulo. kama familia yenu mnaliwa usifikiri kila mtu analiwa. angalia Warumi 1:26 hadi 27 halafu uje na huo ubwabwa wako kuwa paulo alikuwa shoda.
 
Umeongea saana ila ukweli unabaki kwamba na wewe umeingia kwenye list ya wachumia tumbo!

Umeingia kwenye list ya wadini watetea Samia muislamu kama ilivyo kwa Zitto kabwe na genge lote.

Umeongea saana kwa sababu huna uchungu na Tanganyika!

Nakuuliza jambo moja ili uwaulize wabunge....

Je!
Ni kwa nini walikwenda ziara ya wansyoiita ya mafunzo huko nyumbani kwa Dudu- World au DP World ambako ni Dubai....
Badala ya kutembelea nchi zenye migogoro na Deep World kama Djibout na hizi zifuatazo....msijione wajuaji kuliko watanzania wote...

Ebu tuanzie hapo
ahmed rajab

Ili kujifunza aina na sababu ya chimbuko la migogoro hiyo na kisha kuja kuwa na uwezo wa kulishauri bunge vizuri?

Here is a list of the latest 20 cases versus DP World in international arbitration court:

1. DP World v. Kenya (2022). The International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID) is currently hearing a case brought by DP World against Kenya. DP World is seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Kenya.

2. DP World v. Ethiopia (2022). The ICSID is also currently hearing a case brought by DP World against Ethiopia. DP World is seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Ethiopia.

3. DP World v. Djibouti (2021). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Djibouti. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Djibouti.

4. DP World v. Pakistan (2020). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Pakistan. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Pakistan.

5. DP World v. India (2019). The ICSID dismissed a case brought by DP World against India. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by India.

6. DP World v. Argentina (2018). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Argentina. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Argentina.

7. DP World v. Chile (2017). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Chile. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Chile.

8. DP World v. Uruguay (2016). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Uruguay. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Uruguay.

9. DP World v. Peru (2015). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Peru. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Peru.

10. DP World v. Brazil (2014). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Brazil. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Brazil.

It is important to note that these are just a few of the many cases that DP World has been involved in. DP World is a major player in the global port industry, and it has been involved in a number of disputes with governments around the world. These disputes have often been complex and have involved significant financial stakes.

The cases listed above are still ongoing, and it is not yet clear how they will be resolved. However, they provide a glimpse into the challenges that DP World faces as it operates in a number of different countries.
Hii zee ni ji-dini. Linaongozwa na udini hili. Hatari kwa nchi!
 
shoga ni baba yako na sio paulo. kama familia yenu mnaliwa usifikiri kila mtu analiwa. angalia Warumi 1:26 hadi 27 halafu uje na huo ubwabwa wako kuwa paulo alikuwa shoda.

Hawezi kukaa na dude lisilo na faida.mi naona wapewe tu
 
Unaweza ukawa unamheshimu MTU, ila siku atakapo toa mawazo take, utagundua kwamba ulikua unaheshimu kibudu.
 
Huyu mzee wa redio teherean kichwani kwake kumejaa ule uchafu tu

Hatutaki mkataba wa hawa majangili na waharibifu kutoka uarabuni
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Sasa hivi salama yako ni kuuvunja Muungano tu.

Wazanzibari wana nchi yao na wanuwezo wa kuifanya yote ile kuwa bandari huru kama ilivyokuwa kabla ya uvamizi wa 1963.

Sijuwi sisi huku nchi yetu iko wapi?
 
Zanzibar Ni mkoa Kama ulivyo mkoa wa Kigoma.
Zanzibar ingekua nchi rais wao asingeteuliwa Dodoma.
 
Sawa kabisa, kwa sasa anateuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Dodoma au siyo?

1688180702079.png

Nimeona kwenye mtandao kuwa hiyo ni bendera ya Zanzibar, sasa nikajaribu kutazama na mkoa wa Kilimanjaro, hola. Nikajaribu Mkoa wa Mwanza, hola. Kulikoni huu mkoa wa Zanzibar uwe na bendera yake?
 
Back
Top Bottom